AZAM FCYATUPWA NJE KAGAME CUP YALAZWA PENATI 4-3 NA EL MARREIKH YA SUDAN

August 20, 2014


Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la KagameAzam FC ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3 dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.

Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango  Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao. 

Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliaji Lionel Saint- Preux kutoka Haiti.
Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon Joseph Marious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mno kuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumo na aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.
Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penalti, lakini hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila shaka.
MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA MICHEZO ZANZIBAR.

MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA MICHEZO ZANZIBAR.

August 20, 2014


01
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akipokea saluti mara baada ya kuwasili kwenye  ufunguzi wa kiwanja kipya cha Michezo kilichopo Makao Makuu ya Brigedi ya Nyuki Migombani. 02
Jenerali Davis  Mwamunyange akifungua kiwanja kipya cha Michezo kitakachotumika kwa ajili ya michezo ya Majeshi ya Shirikisho la Jumuia ya Afrika Mashariki, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi na kushoto ni Mkuu wa Brigedi ya Nyuki, Brigedia Jenerali Sharif  Sheikh Othman. 03
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akimpongeza Mkandalasi wa kiwanja hicho kutoka Kampuni ya M. S Maya Heardwere ya Zanzibar Bw. Abdallah M. Salim. 04
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza na wanahabari mara baada ya ufunguzi wa kiwanja hicho Migombani Zanzibar jana Agosti 19. (Picha na Makame-Maelezo Zanzibar).
MAGAVANA WA BENKI YA PTA KUKUTANA TANZANIA

MAGAVANA WA BENKI YA PTA KUKUTANA TANZANIA

August 20, 2014

01 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (katikati) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma juu ya mkutano wa 30 utakaofanyika      nchini mwishoni wiki hii. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba. 02
03 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha nchi 18 za Afrika, mkutano huo utafanyika kesho jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Steven Wasira akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba. 04
05 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (kushoto) abibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA),  Admassu Tadesse mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
19/082014
Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) itakuwa mkutano wa mwaka utakaofanyikia nchini jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu.
 
Hayo yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mkutano huo utakaofanyika mwishoni wiki hii.
 
“Huu ni mkutano wa kawaida wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa nchi wanachama pamoja na Mawaziri wa Fedha, Tanzania ni mwanachama ndio maana mkutano wa 30 unafanyika hapa” alisema Wasira.
 
Wasira amesema kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo masuala ya fedha na uchumi, maendeleo ya benki ya PTA na mafanikio yake kwa nchi washirika.
 
Vile vile Wasira amesema kuwa PTA ni benki ya Kiafrika na inafanyakazi nzuri ambapo inaonesha inakua kwa zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka kwa miaka kadhaa hadi sasa na imekuwa na mizania ya Dola za Kimarekani mil. 2.8 ikiwa miongoni mwa benki za maendeleo zinazofanya vizuri katika bara la Afrika.
 
Aidha, Wasira ameongeza kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa Magavana hao ambapo Serikali itawakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
 
Kwa upande wake Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya PTA Admassu Tadesse amesema kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele na ni mwanachama hai ambapo imekuwa mfano mzuri kwa nchi wanachama kwa kutoa michango mbalimbali kwa wakati.
 
Zaidi ya hayo, Tadesse amesema kuwa benki hiyo mwaka huu inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu ili washerehekee na Watanzania.
 
Tadesse amesisitiza kuwa Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama ikiwa na lengo la kuwa tasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki.
 
Benki ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ambapo hadi sasa ina jumla ya wanachama 22 ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti Congo, Kenya na Malawi.
 
Nchi nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Mauritania, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania
 
Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika wengine ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.
 
Mkutano wa mwaka huu unafanyikia Tanzania ikiwa ni utaratibu wa benkiya PTA kufanya mikutano ya mwaka kwa mzunguko ambapo washiriki watakuwa Mawaziri wa Fedha, Magavana wa nchi wanachama, sekta binafsi, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini na Wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa.  

*MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA MJINI DODOMA JANA.

August 20, 2014
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga baada ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 9, 2014.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga baada ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 9, 2014.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga baada ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 9, 2014.
PICHA NA IKULU

HIVI NDIVYO COASTAL UNION ILIVYOONDOKA JANA MKOANI TANGA KUELEKEA PEMBA

August 20, 2014
KUSHOTO NI KATIBU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI,MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI NA MENEJA WA COASTAL UNION AKIDA MACHAI ,FIKIRINI SULEIMANI MAPARA NA MENAJA WA U -20 COASTAL UNION ABDUL UBINDE WAKATI KWENYE PICHA YA PAMOJA UWANJA WA NDEGE JANA

WACHEZAJI WA COASTAL UNION WAKIPANDA NDEGE KUELEKEA PEMBA JANA UWANJA WA NDEGE TANGA.


KOCHA WA MAKIPA RAZACK SIWA AKIWA ENEO LA UWANJA WA NDEGE TAYARI KUPANDA NDEGE KUELEKEA PEMBA KWA AJILI YA KUWEKA KAMBI YA MAZOEZI NA TIMU YA COASTAL UNION JANA.

RAZACK SIWA ATUA COASTAL UNION,AUNGANA NA TIMU KAMBINI PEMBA.

August 20, 2014
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union umeingia mkataba aliyekuwa Kocha wa Makipa Yanga Razack Siwa ili kuweza kukinoa kikosi hicho ambacho kinajiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania bara utakaoanza Mwezi ujao hapa nchini.
Siwa ameingia mkataba wa kuwanoa makipa wa timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa kuipa mafanikio makubwa timu hiyo msimu ujao.

Tayari Kocha Siwa aliungana na wachezaji wa timu hiyo jana kupanda ndege kuelekea Visiwani Pemba ambapo timu hiyo inakwenda kuweka kambi ya wiki nne ikijiwinda na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

Akizungumza jana ,Katibu Mkuu wa Coastal Union ,Kassim El Siagi alisema kuwa kocha huyo wa makipa anachukua nafasi iliyokuwa wazi kutokana na kutokuwa na mwalimu maalumu wa kuwafundisha walinda milango wa Coastal Union.

    “Sasa tutakuwa tumepata mwalimu maalumu ambayo atashughulika na walinda milango wa timu hii tunaaimani hili litatuwezesha kuwanoa vilivyo kwa ajili ya kuweza kuwa walinzi wazuri kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara “Alisema El Siagi.

Akizungumzia safari ya timu hiyo, El Siagi alisema kuwa safari ya timu hiyo jana ilikuwa na wachezaji 27 ambao wameondoka ambapo watakapofika pemba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa soka Gombani.

Safari hiyo imefadhiliwa na wadhamini wa timu hiyo kiwanda cha Pemba Floor Mils ambao wamedhamiria kuhakikisha wanaipa mafanikio timu hiyo.

Katibu huyo alisema wakiwa visiwani humo watacheza mechi nne za majaribio ambazo zilikwisha kutayarishwa na chama cha mpira wa miguu Pemba pamoja na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuacha kuwa na wasiwasi na timu hiyo kwa sababu wamefanya usajili wa nguvu .
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma Salamu za Rambirambi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma Salamu za Rambirambi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

August 20, 2014

jm1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.PICHA NA IKULU
jm2
Mama Salma Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
jm3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014
jm4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa marehemu pamoja na Jaji Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014
……………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia Taifa letu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu, bidii na umahiri mkubwa”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake.
Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi za uhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NEC ambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafu mwaka 2011. Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani, utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapya ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.
“Ni kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozi alichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis Makame, Taifa letu limepoteza mtu muhimu sana kwani hata baada ya kustaafu kwake alikuwa bado anahitajika sana kutokana na mchango wake wa ushauri katika mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu”, amesema Rais Kikwete na kuongeza,
“Kutokana na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza aliyekuwa Kiongozi Mahiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu kwa kumpoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Jaji Lewis Makame, Amina”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.
Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira Wanafamilia wote, ndugu na jamaa wa Marehemu, ili waweze kuhimili machungu ya kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Agosti, 2014
 MATUKIO YA PICHA KAMATI ZA BUNGE MAALUM LAKATIBA

MATUKIO YA PICHA KAMATI ZA BUNGE MAALUM LAKATIBA

August 20, 2014
DSC04200 - Copy
Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hamad Rashid (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mambo yaliyojiri katika Kamati yake jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wake Mhe. Assumpter Mshama.
  ???????????????????????????????
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hamad Rashid , ambaye hayupo pichani wakati  akizungumza mambo yaliyojiri katika Kamati yake akwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma.
IMG_9260
Mwenyekiti wa Kamati  Namba 12 ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Paul Kimiti(katikati) akijadiliana jambo  na baadhi ya wajumbe wa Kamati yake yake  kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma.
Picha na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba.
Serikali kulipia wanafunzi wa sayansi wapatao 5000 ngazi ya stashahada mwaka wa masomo 2014/15

Serikali kulipia wanafunzi wa sayansi wapatao 5000 ngazi ya stashahada mwaka wa masomo 2014/15

August 20, 2014

Mkurugenzi-Msaidizi-wa-Habari-Elimu-na-Mawasiliano-wa-Bodi-ya-mikopo-Tanzania-Cosmas-Mwaisobwa.
NA SULEIMAN MSUYA
KATIKA juhudi za Serikali za kukabiliana na upungufu wa uchache wa waalimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwenye shule mbalimbali za msingi na sekondari hapa nchini imesema italipia wanafunzi wapatao 5000 wa ngazi ya stashahada katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mwaka wa masomo 2014/15.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo Tanzania Cosmas Mwaisobwa wakati akiongea na mwandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema uamuzi huo unakuja kutokana na ukweli kuwa waalimu wa masomo hayo wamekuwa wachache jambo ambalo linakwamisha juhudi za serikali katika kukuza sekta hiyo kwa siku za karibuni na zijazo.
Mwaisobwa alisema mpango huo utakuwa endelevu hadi hapo ambapo tatizo hilo litakapokwisha ili kuhakisha kuwa shule zote za serikali ziweze kukidhi mahitaji hayo.
Mkurugenzi huyo wa Habari, Elimu na Mawasiliano alisema serikali imekichagua chuo kikuu cha Dodoma kutokana na kuwepo na nafasi ambayo inaweza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi.
“Nadhani kila mtu ni shahidi kuwa waalimu wa sayansi na hisabati wapo wachache sana hivyo tumeamua kuwakopesha wanafunzi wa stashahada ili waweze kuziba pengo kubwa lililopo”, alisema.
Akizungumzia juu ya mwitikio wa wafaidika na mikopo kurejesha mikopo waliyokopeshwa na Bodi hiyo alisema ni mkubwa ambapo kwa mwezi zaidi ya shilingi bilioni 3 hurejeshwa.
Mwaisobwa alisema mrejesho huo ni mzuri ila bado wanatoa rai kwa wafaidika wote kuendelelea kurejesha ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wengine wanafaidika na mkopo ili waweze kusoma elimu ya juu.
Alisema pamoja na mwitikio huo bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wafaidika ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano mzuri jambo ambalo linakwamisha juhudi zao za kukusanya fedha hizo.
Mkurugenzi huyo wa Habari, Elimu na Mawasiliano alisema katika kuhakikisha kuwa wanakabiliana na changamoto hiyo wameingia mikataba na wakala mbalimbali katika kanda tofauti ili kusaidia ukusanyaji wa madeni.
Alisema zoezi hilo la ukusanyaji limekuwa rahisi kutokana na uwepo wa mfumo ambao unaonyesha wahusika wote ambao wamefaidika na wanaofaidika kwa sasa.
Kuhusiana na wanafunzi ambao walichelewa kupata fedha za mafunzo alisema bodi inafanyia kazi na matarajio yao ni kwamba mwishoni mwa wiki hii watakuwa wamepata fedha hizo.
Alivitaja vyuo ambavyo wanafunzi wake wamechelewa kupata mikopo ni St. Augustine, Stephano Memorial, IFM, Teofelo Kisanji

MICHUANO YA COPA COCA COLA MKOA WA KILIMANJARO KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 23,2014

August 20, 2014
Michuano ya Copa Coca cola ya vijana chini ya miaka 15 kwa mkoa wa Kilimanjaro yanatarajiwa kupigwa Agosti 23 na 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) , Yusuph Mazimu, michuano hiyo itashirikisha kombaini za wilaya zote sita za mkoa huo, 
zilizogawanywa katika makundi mawili, huku wilaya ya Moshi ikiwa na timu mbili .
Kundi la kwanza litakuwa na timu 3 za Wilaya ya Mwanga, Same na Rombo , litakalotumia uwanja wa David Cleopa Msuya uliopo wilayani Mwanga, wakati kundi la pili litakuwa na timu za wilaya ya Moshi Manispaa, Moshi vijijini, Siha na Hai.

Kundi la kwanza litaanza mechi zake Agosti  23, ambapo Mwanga itaanza na Rombo saa 3 asuhubi, baadae saa 6 Mwanga watakipiga na Same, saa 9 alasiri  Same itawavaa Rombo.

Agost 24, vijana wa Moshi Manispaa wataanza kukipiga na Siha saa 3asubuhi, saa 5 Hai na Moshi vijijini, washindi wa mechi hizo watakutana katika mchezo utakaopigwa saa 9 alasiri siku hiyo hiyo.

“Michuano hii inalenga kuunda timu ya mkoa kwa vijana chini ya miaka 15, kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Tanga septemba 9 mwaka huu, tutakapoanzia ugenini, ni muhimu kwa kila wilaya kutumia wachezaji wenye umri unaotakiwa, tutakuwa wakali”, alisema Mazimu.

Mshindi wa jumla kati ya Kilimanjaro na Tanga baada ya kurudiana septemba 13, atafuzu kucheza fainali za copacola taifa zitakazofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Septemba 20 mwaka huu.

PANONE FC MWENYEJI WA TIMU YA NYOTA WA ZAMANI WA REAL MADRID KILIMANJARO

August 20, 2014
Timu ya Panone FC ya Mkoa Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la Kwanza taifa, imeteuliwa kuwa mwenyeji  wa timu ya nyota wa zamani wa Real Madrid inayotarajiwa kuwasili nchini Agost 22 mwaka huu.

Panone FC watakuwa mwenyeji wa timu hiyo kutoka Hispania, itakapowasili mkoani Kilimanjaro Jumapili ya Agost 24, mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya wadau wa soka mkoani humo, kuwapokea magwiji hao waliowahi kuichezea Real Madrid miaka ya nyuma wakiongozwa na Zinedine Zidane.  

Nyota hao wanatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) saa 5 asbuhi na kuelekea moja kwa moja katika geti la kupandia mlima Kilimanjaro (Marangu Gate) kwa ajili ya kutalii na kupata maelezo mafupi kuhusu mlima huo mrefu kuliko yote Afrika.

Chama Cha soka Mkoa Kilimanjaro (KRFA) kiko katika mchakato wa kuandaa mechi moja kati ya Bingwa wa mkoa wa Kilimanjaro msimu huu, Panone Fc na bingwa wa msimu uliopita Machava, ili ishuhudiwe na magwiji hao.

Msemaji wa KRFA, Yusuph Mazimu alisema mchezo huo wa kirafiki unalenga kuwapa nafasi nyota wao wa Madridi kushuhudia vipaji vya soka mkoani humo.

“ tunajua wana ratiba ngumu sana, wanapaswa kwenda kulala Arusha siku hiyo hiyo, kwa hiyo hata ikikubalika, hawatashuhudia mchezo mzima, labda dakika 10 au 15 ila uwepo wao utaleta hamasa kwa vijana wetu na ligi yetu ya mkoa”.

Nyota hao wa Madrid kabla ya kuja Kilimanjaro, Agost 24 watakipiga na  nyota wa TSN Tanzania Eleven katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, watakaokuwa chini ya makocha Charles Boniface Mkwassa, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ na Fred Felix Minziro.

Mratibu wa ziara ya nyota hao wa Real Madrid, Denis Ssebo, alisema, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.

LIGI DARAJA LA TATU KILIMANJARO KUANZA AGOSTI 23

August 20, 2014
Ligi Daraja la tatu ngazi ya mkoa kwa mkoa wa Kilimanjaro, inatarajiwa kuanza agost 23, mwaka huu.

Ligi hiyo itakayoshirikisha timu 19, itaendeshwa kwa hatua mbili, hatua ya makundi na hatua ya fainali itakayokuwa na timu tano, nne ni zile zilizoongoza kundi na moja ni ile itakayokuwa na matokeo mazuri (best looser). 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), timu hizo zimegawanywa katika makundi manne, makundi matatu yakiwa na timu tano tano na kundi moja likiwa na timu nne.

Kundi A litakuwa na timu za Afro Boys, Reli, KIA, Soweto na Kilototoni wakati kundi B linaundwa na timu za New generation, Sango, Kilimanjaro Fc, Hai City na Lang’ata.

Timu za Polisi Kilimanjaro , Kilimanjaro Rangers, Kagongo, Magadini na Boda zinaunda kundi C na kundi D litakuwa na timu nne za Forest, Polisi Mwanga, Kitayosce na Machava ambaye ni bingwa wa misimu miwili iliyopita kabla ya kupokwa ubingwa na Panone FC katika msimu uliopita.

Pazia la ligi hiyo linatarajiwa kufunguliwa kwa mechi tatu ambapo timu za Afro boys itakipiga na Reli katika uwanja wa Magereza mjini Moshi, New Generation itakutana na Sango FC katika uwanja wa Memorial uliopo Soweto na Polisi Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa Kilimanjaro Rangers katika dimba la Mandela uliopo Pasua Moshi.

Akizungumzia maandalizi ya ligi hiyo, msemaji wa KRFA, Yusuph Mazimu alisema kila kitu kimekamilika ikiwa ni pamoja na maandalizi ya viwanja na waamuzi.

“tunataka ligi ya msimu huu iwe bora zaidi ya misimu mingine, ndio maana tumejitahidi kuandaa kila kitu mapema ili kutoa nafasi ya watu wa soka kufurahia michuano hii itakayokuwa na hatua mbili, ya awali na baadae hatua ya fainali itkayoshirikisha timu tano, nne zilizoongoaza makundi na moja itakayokuwa na matokea mazuri yaani besti looser”.