RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA LEO, KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MUSEVENI.

May 11, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya maua kama ishara ya Ukaribisho kutoka kwa mtoto katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda mara baada ya kuwasili kutokea Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa mbalimbali waku wa vyombo vya  Ulinzi wa Serikali ya nchini Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchini Uganda. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Pongezi wakati alipowasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Entebbe, nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni, kesho.


MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA.

May 11, 2016


Baadhi ya Wabunge wa Majimbo mbalimbali wakielekea katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma tayari kwa vikao vya asubuhi leo 11 Mei, 2016.

Mbunge Iringa Mjini, Mhe. Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari wakiwapungia mkono Wapiga picha (hawapo pichani wakati wakiingia Bungeni kwa ajili ya vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akifurahiua jambo pamoja na Wabunge wenzie nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira akiingia ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma.

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole-Nasha akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisoma bajeti ya Wizara yake mbele ya Wabunge leo 11 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Uutumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) Bungeni mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma)

BENKI YA CRDB WAELIMISHA WATEJA WAKE KUTUMIA INTANETI BENKI.

May 11, 2016


 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Vijana, Pales Fungo akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wa matawi matatu tofauti jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapa mafunzo ya benki kwa njia ya Mtandao(Internet Banking.)

Meneja wa njia mbadala wa Benki ya CRDB, Hamis Mhini akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wa matawi matatu tofauti jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapa mafunzo ya benki kwa njia ya Mtandao(Internet Banking.) katika mafunzo hayo yaliwashirikisha matawi matatu ya Benki ya CRDB ambayo ni Water Front, Vijana na Lumumba.

Kutoka kushoto ni Msimamizi wa benki ya CRDB kwa njia ya mtandao(Internet Banking), Sarah Nzowa, Meneja wa benki ya CRDB tawi la Water Front,Donath Shirima na Meneja wa njia mbadala wa Benki ya CRDB, Hamis Mhini  wakimsikiliza Meneja wa maswala ya mtandao(Internet Banking) wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda.Meneja wa maswala ya mtandao(Internet Banking) wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda (aliye simama) kifafanua jinsi ya kutumia mtandao wa intaneti  yaani (Internet Banking) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya CRDB wakisikiliza maada.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CRDB wakimsikiliza Meneja wa maswala ya mtandao(Internet Banking) wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda, jijini Dar es Salaam.

SERIKALI MKOANI MBEYA YAFUTA HATI YA KIWANJA CHA MAKAZI KILICHOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA.

May 11, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba)


Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu)
SERIKALI Mkoani Mbeya  imeagiza kufutwa kwa hati ya  kiwanja kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.

Agizo hilo, limetolwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kutembelea na kukagua chanzo kikuu cha maji cha Nzovwe, chenye uwezo wa kuzalisha mita 12 za ujazo kwa siku na kusambaza maji kwa asilimia 41 kwa wakazi wa jiji la Mbeya wapatao zaidi ya  200,000.

Kiwanja hicho ambacho kipo karibu na eneo la chanzo cha maji cha Nzovwe, kilitolewa na maafisa ardhi, idara ya mipango miji kwa ajili ya matumizi ya makazi na kumilikiwa na mtu binafsi aliyetajwa kwa jina moja la Mwakasala.

Makala amesema, chanzo hicho cha maji ndio tegemezi kwa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa Jiji la Mbeya, hivyo kama kitaachwa na kuharibiwa, wananchi zaidi ya 200,000 wapo hatarini kuikosa huduma hiyo ambayo ni haki yao ya msingi.

 Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali iliwaondoa wananchi wote waliokuwa wanaishi au kuendesha shughuli zao za kiuchumi ndani ya mita 60 na kuwalipa fidia zao hivyo hatua ya wananchi hao kuendelea kuishia mahali hapo ni kukaidi agizo la serikali.

 Amebainisha kuwa kiwango  kikubwa cha upotevu wa maji kwa asilimia 31  inatokana na baadhi ya vyanzo vya maji kuharibiwa kwa kufanyika kwa shughuli za kibinadamu, kulisha mifugo au kujenga nyumba za makazi pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.

Hata hivyo, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa mamlaka ya maji kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuhakikisha wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo ndani ya siku tatu.
“Wananchi wengine wameondoka tena kwa hiari yao wenyewe, sasa kwa nini huyu atuchezee mchezo mchafu?.. kwa hili sikubaliani nalo, huku akiwataka wananchi ambao ni vijana kulilinda eneo hilo na kuwaonya wale ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya fujo,”alisem

RAIS TFF AIPONGEZA YANGA

RAIS TFF AIPONGEZA YANGA

May 11, 2016
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ameipongeza timu ya soka ya Young Africans kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.

Hii ni mara ya 26 kwa Young Africans ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.

“Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambaz
o haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.

Kadhalika Rais Malinzi amezikumbusha na kuhamamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kutoa maoni, mapendekezo, marekebisho ya ili kuboresha kanuni za uendeshaji wa ligi hiyo kwa msimu ujao. Maoni hayo yapelekwe kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) au kwa njia ya barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Young Africans imefikia rekodi hiyo baada ya kutwaa ubingwa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006 na misimu ya 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013, 2014-15 na 2015-16.

Pamoja na kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2015/2016, kikosi cha timu ya Young Africans kwa sasa kimebakiza michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ndanda unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Mei 14, 2016 kadhalika dhidi ya Majimaji Mei 22 ambayo itakuwa ni siku ya kufunga pazia la Ligi Kuu msimu huu wa 2015/16.

TIGO YATOA MSAADA WA VYANDARUA KWA HOSPITALI YA UKEREWE

May 11, 2016
Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(fulana ya blue), akimkabidhi Vyandarua 80 Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe Dk Kaniki Titus,kwenye hafla ya Makabidhiano iliyofanyika Mwanza juzi.

Mkurugenzi wa Mikakati(Director of Strategy)wa tigo Kobbina Awuah(wa tatu kushoto) akimkabidhi Vyandarua 80 Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe Dk Kaniki Titus,kwenye hafla ya Makabidhiano iliyofanyika Mwanza juzi.



photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz IMAGINE INSPIRE INFLUENCE
Matukio bungeni Dodoma leo

Matukio bungeni Dodoma leo

May 11, 2016

umi1 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Mhe. Ummy Mwalimu (IMb) akisoma taarifa ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma, 11 Mei, 2016.
umi2 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni mjini Dodoma.
umi3 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akifurahi na Wabunge wenzie nje ya Bunge mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.
EU YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

EU YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

May 11, 2016
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer
Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali katika Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 66 ya EU duniani (Picha na Modewjiblog)
Umoja wa Ulaya (EU) umesema kuwa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika shughuli za maendeleo ikiwa kama ni moja ya kazi wanazozifanya kusaidia ukuaji wa maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani, kuwa kwa kipindi kirefu EU imekuwa ikifanya kazi nchini na hivyo wataendelea kukuza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya lakini pia kuisaidia Tanzania kuata maendeleo zaidi.
“Tutaendelea kusaidia Tanzania kukuza uchumi, kusaidia kuwepo na usalama na amani na hizo ni kazi ambazo tumekuwa tukizifanya hivyo tunaamini ushirikiano wa Tanzania na EU utaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu,” alisema Van de Geer.
Pia alisema wanatambua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere wakati akiwa madarakani na hata kasi iliyopo sasa katika kuleta maendeleo katika serikali ya Rais Magufuli hivyo wanaamini maendeleo yatapatikana kwa kasi.
Alisema kwa upande wa EU wataendelea kusaidia maendeleo ambapo kwa sasa watahakikisha mradi wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2020) utafanikiwa ili kuifanya Tanzania kufikia malengo ya kuwa moja ya nchi iliyo na maendeleo barani Afrika.
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiamkaribisha Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Roeland Van de Geer EU Tanzania
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akikaribisha wageni waalikwa kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hoyce Temu UN Tanzania
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
Felista Rugambwa
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale akisalimiana na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa anayeshughulikia dawati la Marekani na Ulaya Marekani, Felista Rugambwa huku Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiendelea kukaribisha wageni waalikwa.
Susanne Mbise
Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya, Susanne Mbise akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Balozi wa Umoja huo, Bw. Roeland Van De Geer kuzungumza na wageni waalikwa katika hafla mchapalo ya siku ya Umoja wa Ulaya iliyofanyika tarehe 9 Mei katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Roeland Van de Geer
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa Kiuchumi, Ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jiijini Dar es Salaam.
Awa Dabo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uswiss Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arthur Mattli katika hafla hiyo.
Balozi wa Ireland nchini Flonnuala Gilsenan
Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan akibadilishana mawazo na Balozi Liberata Mulamula (kushoto) halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
IMG_4676
Picha juu na chini ni wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo katika hafla hiyo.
IMG_4772
Stella Rwechungura
Stella Rwechungura wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania (wa pili kushoto), Clara Swai wa Ubalozi wa Uingereza (wa pili kulia) pamoja na Ameeta Mehta wa EU Tanzania (kulia) katika picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 tangu kuanzishwa kwake.
Hoyce Temu
Kutoka kushoto ni Afisa mshiriki anayeshuhghulikia Mawasiliano na Ushirikiano wa UN Tanzania, Didi Nafisa, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa anayeshughulikia dawati la Marekani na Ulaya Marekani, Felista Rugambwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 tangu kuzaliwa kwake.
IMG_4761
Pichani juu na chini ni baadhi ya mabalozi na wadau kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali, Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mbalimbali waliohudhuria hafla ya siku ya Umoja wa Ulaya nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
IMG_4755
IMG_4758
Liberata Mulamula
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula wakati halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya (EU) katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani tangu kuzaliwa kwa umoja huo.