UWT YAUNGA MKONO UAMUZI YA RAIS KUHUSU MAKANIKIA NA MIKATABA YA MADINI

June 14, 2017
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) inaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na kupongeza jitihada zake za kupambana na aina zote za ubadhirifu, dhulma na unyonyaji uliobainika kwenye mikataba ya uchimbaji na usafirishaji madini, na hivyo kuhakikisha maliasili za Taifa zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote.
Pia, Umoja wa Wanawake Tanzania unatoa pongezi kwa wajumbe wa Kamati kwa weledi, uzalendo na ujasiri mkubwa wa kubainisha hasara kubwa iliyopatikana kwa Taifa letu kutokana na usafirishaji wa makanikia, na hivyo UWT inakubaliana na kuunga mkono mapendekezo yote ya Kamati na uamuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kutaka kurekebisha mikataba na sheria za usimamizi na uchimbaji wa madini nchini.
Aidha UWT inapongeza hatua za awali za mazungumzo yaliyofanywa leo tarehe 14/06/2017 baina ya Mhe Rais Dkt Magufuli na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambao ni wamiliki wa Kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuhusu malipo ya fedha zilizopotea na kushirikiana katika ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.
Kufanikiwa kwa mazungumzo hayo, na marekebisho ya sheria na mikataba ya madini kutawezesha Watanzania kupiga hatua ya kujikomboa na umasikini, hususani Wanawake ambao wameendelea kukosa huduma za msingi za kijamii ikiwemo afya, elimu, maji na malazi bora. Wanawake wengi wanahangaika kwa kukosa mitaji ya biashara na mikopo ya wajasiriamali wadogo huku wakisumbuliwa kulipa tozo, ushuru na kodi za kero.
UWT inatoa rai kwa wananchi wote kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujivunia utanzania wetu. Tunamuombea Mhe Magufuli, MwenyeziMungu azidi kumpa afya njema, moyo wa ujasiri, uzalendo na upendo kwa watanzania.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

AMINA MAKILAGI (MB)
KATIBU MKUU
JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA.
                                                               14/06/2017

Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo

June 14, 2017
[​IMG]

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr.Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyona ambayo inaiwezesha Kampuni kumilikiwa na Umma wa watanzania.
Akiongea na Wanahabari Dr. Ulomi amesema kwamba Kuanzia Sasa Kampuni ya Maxcom Africa itatambulika kwa Jina la Maxcom Africa Public Limited Company (Maxcom Africa PLC) .  Kampuni hii maarufu kwa jina la Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika mchakato wa kuanza  kuuza hisa zake kwenye soko la hisa.   Dr. Olumi amewaambia wanahabari kwamba wanasubiri kibali cha wasimamizi wa Soko la Hisa ili waweze Kuorodhesha Kampuni yao katika Soko hilo
             
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.

[​IMG]

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi (kulia ) akikata utepe wa kuzindua rasmi Jina Lipya la Kampuni ya  Maxcom Africa PLC anayeshuhudia ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.

[​IMG]

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia ) akionesha nembo ya jina jipya Maxcom Africa PLC na kushoto kwake ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi wa Jina jipya la Kampuni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam



[​IMG]

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC. 

[​IMG]

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC. 
SIKU YA KUCHANGIA DAMU DUNIANI

SIKU YA KUCHANGIA DAMU DUNIANI

June 14, 2017
unnamed
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Njema akizungumza na Jonas Hans Atile (kushoto) ambaye amejitokeza kuchangia Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Leo.
1
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Praxeda Ogweyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani. Pia Dk. Ogweyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
2
Mmoja wa Wananchi akishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu duniani Leo katika hospitali hiyo.
3
Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchangia damu Leo katika jengo la Maabara kuu, hospitali ya Taifa Muhimbili
4
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Muhimbili wakiendelea na shughuli ya utoaji damu Leo.
……………………………….
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki katika madhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu duniani kwa kuendesha shughuli ya utoaji damu kwa watu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji.
Shughuli hiyo inaendelea katika hospitali hiyo kwenye Jengo la Maabara kuu ambako watu wamekusanyika kwa ajili ya kuchangia damu. Mmoja wa viongozi walishriki katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema pamoja na Watanzania mbalimbali.
Akizungumza katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wakiwamo kinamama na watoto wadogo.
“Nawapongeza wote walifika leo hapa Hospitali ya Muhimbili kuchangia damu, ni jambo la muhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema Mheshimiwa Mjema.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa hospitali hiyo, Dk Praxeda Ogweyo amewataka wananchi,mashirika  ya umma na yasiyo ya kiserikali, shule, vyuo mbalimbali na taasisi za dini  kujitokeza kuchangia damu hospitali hapo.
Dk Ogweyo amesema kuwa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 hadi 120 kwa siku na kwamba damu inayokusanywa ni kati ya chupa 50 hadi 60 na upungufu wa damu ni chupa 60 hadi  hadi 70, hivyo damu inahitajika zaidi.
“Kutokana na hali hii, naomba rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuokoa maisha ya wagonjwa. Hospitali imejipanga kupitia kitengo chake cha uchangiaji damu kilichopo maabara kuu hivyo karibuni mchangie damu,” amesema Dk Ogweyo.
 
PICHA NA  JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA

June 14, 2017
Katika kuhakikisha dhamira ya Serikali ya dhamira ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda wadau wa kilimo na viwanda wamekutana ili kuzungumzia nafasi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) katika  kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo nchini.

Wakizungumza katika Kikao hicho kilichoandaliwa na TADB ili kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.
Bw. Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo.
“Benki imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Bw. Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga kutoa elimu ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha  na kuchochea mabenki na taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani katika shughuli za kilimo.
TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza nafasi ya Benki yake katika kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

NIKOHUB TUNAFUTURISHA WATU 100 KILA SIKU KUANZIA LEO HADI SIKU KUMI

June 14, 2017

Mambo yanazidi kuwa mazuri kwa wanaoenda na wakati kadri siku zinavyo zidi kwenda kufuatia ukuaji wa kitekenolojia siku  hadi siku, hali hii inazidi kuleta manufaa na msukumo mkubwa wa kimaendeleo  Duniani hasa kwa kurahisisha vyanja za utendaji kazi katika biashara.

Dar es salaam  Kampuni ya Candy and Candy imekuja kivingine msimu huu wa Ramadhan kwa kutumia mfumo mpya tulio uanzisha wa kiteknolojia “Nikohub”tumeanza mchakato wa kufuturisha watu 100 kila siku kwa muda wa siku kumi.

Ili upate kushiriki Futari unatakiwa ku-download  Nikohub kwenye Play Store katika simu yako. Kisha jiunge ili tuweze kukuona kwenye mfumo wetu na uingie kwenye list ya watu 100 watakao kula futari leo.

Ukifanikiwa ku-downloda tutumie SMS au piga 0765802457 tukuelekeze sehemu ya kwenda kula futari maeneo ya huko uliko ni bure!.

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro azoa Milioni 20 za Biko

June 14, 2017

Balozi wa Biko Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, wakihakiki namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Sinyangwa na kumpigia ili kumjulisha juu ya ushindi wake.

RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA.

RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA.

June 14, 2017
pic+ukawa
Jovina Bujulu-MAELEZO.
Baadhi ya wasomi wameonyesha kuridhishwa na kuunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi.
Akiongea na Idara ya Habari (Maelezo) Dk Benson Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kitendo kilichofanywa na Rais Magufuli kimewafungua macho viongozi wengi wa Afrika na dunia na kitakuwa ni mfano wa kuigwa kwa Serikali nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla
“Ningefurahi kama tungetenga siku maalumu kuandamana kwa nia ya kuunga mkono nia njema ya Rais ya kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii hazitumiwi hovyo hovyo” amesema Dk Bana.
Aliongeza kusema kuwa kitendo cha kutafuta ukweli katika makinikia na biashara ya madini na kuweka wazi taarifa hiyo kwa umma  na kusema wahusika wa sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria kimeonyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake.
Aidha aliunga mkono kitendo cha Rais kukubali kufanyia kazi mapendekezo yote 21 yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi, kwani yataweka wazi mwenendo mzima wa biashara ya madini na kuziba mianya ya wizi wa madini.
Dk. Bana alimpongeza pia Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba kwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwazuia kusafiri nje ya nchi watuhumiwa wa sakata hilo.
Alisema wale wote waliotajwa kuhusika na suala hilo kukaa nje ya utumishi wa umma kwa muda wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea na  endapo watabainika kuwa hawana hatia warudishwe kazini na ikibainika kuwa walihusika wachukuliwe hatua stahiki.
Alitoa wito kwa Watanzania kuuunga mkono  nia njema ya Rais Magufuli kwa sababu hatua hiyo ni harakati za kuweka sawa uchumi wa nchi ili kuboresha maisha ya Watanzania.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 47 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO JUNE 14, 2017

June 14, 2017
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza Kikao cha 47 cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akijibu maswali mbalimbali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akijibu maswali mbalimbali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani akijibu maswali mbalimbali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge wa Ileje (CCM) Mhe. Janeth Mbene akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge Viti Maalum (CCM) Mhe. Mwantumu Haji akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge Kyerwa (CCM) Mhe. Innocent Bilakwate akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge Mdaba (CCM) Mhe. Joseph Mhagama akiuliza swali i katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge Tunduru Kusini (CCM) Mhe. Daimu Mpakate akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Mbunge Viti Maalum (CCM) Mhe. Angelina Malembeka akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Buyungu Mhe.Kasuku Bilago katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasili Bungeni kuhudhulia Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma. Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOWE

June 14, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai katika lango la kuingilia katika shamba la Kilimo cha Kisasa la Mboga Mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd lililopo Nshara Machame.
Mkuu wa wilaya ya Hai,akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Hai ,pamoja na askari Mgambo wakiingia katika shamba la Kilimo cha Kisasa cha Mboga mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Shamba la Kilimo cha Kisasa,(Green House) lililopo Nshara Machame wilaya ya Hai la Kilimanjaro Vegees Ltd .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai,wakiwa katika moja ya shamba hilo pamoja na asakari polisi wenye silaha wakiondoa miundo mbinu ya umwagiliaji pamoja na unyunyiziaji wa dawa .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza katika eneo hilo wakati zoezi la kuondoa miundo mbinu katika eneo hilo ikiendelea.Zoezi hilo limefanyika kwa kile kinachodaiwa shughuli za kilimo kufanyika kando ya mto kinyume cha sharia.
Sehemu ya Shamba la Strawberry kabla ya kuondolewa miundo mbinu.
Askari Mgambo wakiondoa miundo mbinu ya umwailiaji katika shamba la Kilimoa cha Kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wajimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Mipira maalumu iliyokuwa ikitumika katika umwagiliaji ikiwa imekatwa katwa .
Asakari Mgambo wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu.
Mkuu  wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akifuatilia zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akisaidia katika uondoshaji wa miondo mbinu katika shamba la kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Askari Mgambo wa kikata mipira kwa panga .
Zao la Strawberry ni moja wapo ya mazao yanyolimwa kisasa katika shmaba hilo.
Sehemu ya Mazao ambayo tayari yameanza kukomaa katika shamba hilo.
Kilimo cha kisasa cha zao la Nyanya pia kimekuwa kikifanyika katika shamba hilo.
Baadhi ya Green House zikiwa zimeondolewa wavu maalumu wa kuzuia wadudu kuingia ndani.

Na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.