RC TANGA ATOA NENO KWA WANUNUZI WA ZAO LA MWANI TANGA

April 24, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea wakulima wa zao hilo katika Mtaa wa Sahare Kijijini Kata ya Mzingani Jijini Tanga ambao pia alizungumza na wakulima wa zao hilo kwenye wilaya za Tanga,Mkinga ,Muheza na Pangani ikiwa ni kuelekea Shamrashamra za kuelekea miaka 60 ya Muungano.


MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akitoka kukagua zao la Mwani wakati wa ziara yake 






Na Oscar Assenga, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewataka wanunuzi wa zao la mwani mkoani humo kuheshimu mikataba wanayoingia na wakulima ili waweze kulima kwa tija na hivyo kuweza kujikwamua kimaendeleo.

Amesema kutokuheshimu mikataba hiyo hawatakubali kuona linatokea badala yake wataona namna ya kufatuta njia nyengine za kuwahudumia ikiwemo mabenki kwa ajili ya kuwawezesha kupata mikopo yenye riba ndogo na nafuu.

RC Batilda aliyasema hayo  wakati wa ziara ya kutembelea wakulima wa zao hilo katika Mtaa wa Sahare Kijijini Kata ya Mzingani Jijini Tanga ambao wametokea kwenye wilaya za Tanga,Mkinga ,Muheza na Pangani ikiwa ni kuelekea Shamrashamra za kuelekea miaka 60 ya Muungano.

Ambapo pia alitembelea shamba la wakulima wa Mwani pamoja na kugawa kofia,mabuti ,nyundo,kamba na taitai ili kuweza kuwawezesha wakulima hao wa mwani kutekeleza vema shughuli zao za kila siku .

Alisema kwasababu haiwezekani wanunuzi wa zao hilo wanaingia mikataba na wakulima lakini wanashindwa kutoa vifaa, kutokuwahudumia wala kutoa pembejeo kitendo ambacho kinapelekea wakulima kuhangaika bila kujua kamba wanatoa wapi.

“Hii haiwezekani mkulima wa mwani anakopa hii sio sawa unamuumiza mkulima kutokana na kwamba wanafanya kazi kubwa yenye tija lakini kama mkipata mwekezaji mzuri mtaweze kujikwamua kiuchumi nimewaelekeza Jiji na nitaongea na Waziri wa Uvuvi aweze kuona namna ya kuwasaidia tupate boti”Alisema

“lakini niwaambie wanunuzi kama hii kazi imewashinda tutavunja mikataba tuweze kujua wakulima wetu tunawahudumiaje tuwaitea mabenki waje watoe mikopo kama benki ya kilimo TIDB wanatoa mikopo yenye riba ndogo sana chini ya asilimia 4 mpaka 3waweze kuwakopesha waweze kununua kamba,taitai,troliki waweze kufanya kazi kwa tija yenye faida”Alisema

Aidha Mkuu huyo wa mkoa alisema Wizara ya Uvuvi watashirikiana nao kwenye suala la masoko huku akimpongeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ulega kwa kuanzisha stakabadhi ghalani kama ilivyo mazao mengine ya kilimo .

Alisema mfumo huo utawezesha za la Mwani kuwekwa kwenye stoo utapigwa mnada na watapata bei ya soko kuliko ilivyokuwa bei ya sasa ambao madalali wanapanga bei wanayotaka jambo ambalo linawaumiza wakulima wengi.

“Nimetembelea Shamba la Mwana nimeona changamoto hawana vifaa vya kubebea mwani kutoka baharini mpaka nchi kavu ,hawana chombo wanatumia kama boya mpaka kufika pwani hiyo ni kazi kubwa ina tija hivyo nimewaekeza jiji nitaongoea pia na Waziri wa Uvuvi awasaidie mpate (faiba) boti hata ndogo milioni 15”Alisema

“Ndugu zangu hapa nimesikia mnachangamoto ya Kamba kazi hii bila kuwa navyo itakuwa ni ngumu hivyo nitawasaidia milioni 3 (3000, 000) kwa ajili ya kununua kamba taitai ili msimu utaoanza mwezi wa saba usipite bila kuwa nazo”Alisema RC huyo.

“Lakini lazima tuhakikishe kwanza tunakwenda na kauli mbiu ya Rais Dkt Samia Suluhu na Rais za Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi ya uchumbi wa bluu kwa Mkoa wa Tanga tuliokuwa nao ni zao la mwani na ufungaji magongoo bahari na kwenda kwenye ufungaji wa pweza,kaa na majongoo bahari ,chaza,kamba”Alisema RC

Hata hivyo katika kuhakikisha analitilia mkazo zao hilo ,RC Batilda alisema kwamba Aprili 29 mwaka huu atakuwa na viongozi wa wavuvi na viongozi makampuni yanayonunua mwani ili kuweza kuweka mikakati ya namna ya kuweza kuhakikisha wakulima wanaendelea kupata tija. 

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa alitumia wasaa huo kueleza kwamba vitu ambayo atasimama navyo ni kuhakikisha wanavidhibiti uvuvi haramu huku akiwaonya wanaojihusisha na uvuvi haramu kuachana nao.

JOKAT E ATAJWA SHINDANO LA MISS TANGA 2024 LIKIZINDULIWA

April 24, 2024



Na Oscar Assenga, TANGA

SHINDANO la Miss Tanga 2024 limezinduliwa rasmi huku Mratibu wa Shindano la Miss Tanga 2024 Victoria Martin akisema suala warembo sio uhuni bali ni fursa ambayo inaweza kuwabadilishia watu maisha yao.

Katika kusisitiza umuhimu wa tasnia ya urembo kwamba sio uhuni alimtolea mfanoaliyewahi kuwa Miss Tanzania Jokati Mwogelo manufaa aliyokuwa nayo kupitia tasnia ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu UVCCM Taifa Bara.

Victoria ambaye aliwahi kuwa Miss Tanga 2007 aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Tanga Beach Resort Jijini Tanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na usajili wa warembo ambao watawania taji hilo huku akitoa wito kwamba usaili bado unaendelea kujitokeza kushiriki kwenye shindano hilo ambalo mwaka huu ltakuwa la aina yake.

Victoria alisema lengo la kuandaa shindano hilo ni aliona ni muda wa kurudi nyumbani ,kuridisha ari na thamani ya urembo ili kuhamasisha ushiriki kwenye shindano hilo ambalo limesheheni fursa mbalimbali.

“Kupitia urembo watu wanaweza kubadilisha maisha yao kwa mfano wapo watu wengi wamenufaika kupiti huku kama ilivyo kwa Jokate Mwegelo ambayo wa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara lakini wapo wengi wametoka kutokana na tasnia hiyo”Alisema

“Lakini kupitia Miss Tanga tunaweza kubadilisha maisha hivyo ni muhimu wadau kuendelee kuisapoti tasnia hiyo kutokana na kuwa sehemu ya ajira kwa vijana wanaoshiriki kutokana na baadhi yao kupata nafasi katika maeneo mbalimbali ambazo zinawakwamua kiuchumi na hivyo kuchochea maendeleo kwenye jamii zao”Alisema

“Tunaomba tujitokeze kwa wingi kusapoti urembo kwani sio uhuru bali ni ajira tumekuwa tukipigwa bunduki kubwa tukiambiwa kwamba urembo ni uhuni sio sahihi maana asilimia kubwa washiriki wanatokea vyuoni “Alisema Victoria

Aidha Mratibu huyo alisema kwamba warembo ambao wanawania taji hilo wanatarajia kuingia kambini Mei 2 mwaka huu Shindano hilo lilitarajiwa kufanyika Mei 11 mwaka huu katika Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini humo.

PROF. MKENDA AZIPONGEZA SHULE BINAFSI KUSITISHA MASOMO KUTOKANA NA HALI YA HEWA MBAYA

April 24, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewataka wazazi na walezi pindi wanapoona mvua kubwa zinanyesha kutowaruhusu watoto kwenda shule ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza kutoka na mafuriko na kuharibika kwa miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini.

Wito huo umetolewa leo Aprili 24,2024 jijini Dar es salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara baada ya kuharibika kwa miundombinu ya shule.

Amesema  walimu wakuu wanapaswa kuchukua hatua za haraka na kutoa maamuzi pindi wanapoona hali mbaya ya hali ya hewa aidha kwa kuwaruhusu watoto mapema na kufunga shule lakini pia kwa kuwasiliana na wazazi.

Aidha amesema endapo shule zimefungwa kutokana na mafuriko na familia zimehama hivyo kule wanapohamia watoto wanapaswa kupelekwa kwenye shule zilizokaribu ili kuendelea na masomo yao.

"Kama shule zimefungwa na maji yamejaa na familia zimehama kule wanapokwenda wapokelewe wakati maafisa elimu kata wakiwa wanashughulikia taratibu nyingine ikiwa kama mtoto ataendelea kwenye shule hiyo au atakuwepo kwa muda na shule yake ikakarabatiwa anarudi",Amesema.

Prof. Mkenda amesema kuwa Wizara inashirikiana na wazazi ambao watoto wao wanasoma kwenye shule binafsi kuhakikisha wanapata shule ambazo watazichagua wao kwa maelewano yao ili kuwapeleka watoto.

Sambamba na hayo ametoa onyo kwa madereva wa magari ya shule kutopitisha magar hayo kwenye mabwawa ya maji au sehemu yenye maji mengi ili kuepuka kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

"Kitu cha kwanza katika shule zetu ni usalama wa watoto wetu na usalama wa wafanyakazi katika taasisi zetu madereva kama wakiona dalili zozote za hatari waache wasije wakaingiza watoto wetu kwenye hatari",

Aidha ameongeza kuwa kamishna wa elimu atoatoa mongozo na kuruhusu mabadiliko katika kalenda ya ufundishaji ili kusaidia kwenye swala la mvua watoto wasiumie. 

Amezipongeza shule binafsi ambazo walipooana hali ya hewa mbaya wakaamua kusitisha kwa muda masomo kwenye shule zao ili kupisha hali hiyo.

Akizungumzia miundombinu iliyoharibika amesema serikali kupitia wizara wamesema wanafuatilia taarifa za hali ya hewa ili waweze kuirejesha miundombinu hiyo ambapo shule ambazo zilizokuwa mabondeni wataangali sehemu salama na kuzijenga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara baada ya kuharibika kwa miundombinu ya shule. Amezungumza leo Aprili 24,2024 katika Ofisi za Wizara jijini Dar es salaam 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara baada ya kuharibika kwa miundombinu ya shule. Amezungumza leo Aprili 24,2024 katika Ofisi za Wizara jijini Dar es salaam 




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara baada ya kuharibika kwa miundombinu ya shule. Amezungumza leo Aprili 24,2024 katika Ofisi za Wizara jijini Dar es salaam 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

TBS YATOA WITO KUPIMA UBORA NA USALAMA WA MAJI YA KISIMA KWA MATUMIZI YA NYUMBANI

April 24, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewashauri wenye visima vya maji kuhakikisha maji yanapimwa ili kukidhi ubora na kulinda usalama wa afya zao.

Hayo yamebainishwa Leo Aprili 24,2024 na Afisa udhibiti Ubora (TBS) Bw.Ibrahim Feruzi  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za TBS, Jijini Dar es Salaam.

Amesema wananchi wamekuwa na desturi ya kujitafutia vyanzo vya maji kutokana na uchache wa vyanzo vya maji salama ili kujipatia suluhisho endelevu ambapo changamoto inayojitokeza ni kutokuwa na uhakika wa ubora na usalama wa maji hayo.

Aidha Bw.Feruzi amesema kuwa TBS kupitia maabara zake inapima maji katika maeneo mawili ambayo ni Mikrobiolojia pamoja na kemikali ambapo maabara hizo zina ithibati hivyo majibu yake yanakubalika popote duniani.

Pamoja na hayo ameeleza umuhimu wa  wananchi kufahamu usalama na ubora wa maji  ili kuepuka maambukizi ya vimelea hatarishi.

"Kuna vimelea hatarishi kama aina mbalimbali za bakteria kama vile salmonella wanaosababisha ugonjwa wa typhoid ambao wengi mnaufahamu, kuna wadudu wanaitwa Vibrio wanaosababisha ugonjwa wa kipindupindu na wadudu wengine wanaoitwa shigella ambao wanasababisha matumbo ya kuhara, uwepo wa wadudu hao unatupatia kila sababu ya kuhakikisha maji yanapimwa na kutibiwa ili kuwa salama"Bw.Feruzi ameeleza.

Vilevile Bw.Feruzi  amesema kupimwa kwa maji kunajumuisha vigezo mbalimbali kama kuangalia kiwango cha Oksijeni,kiwango cha tope,tindikali ya madini mbalimbali hasa metali nzito ambapo inasaidia  kufanya tathmini ya ubora na usalama wa maji.

"Viwango vya juu vya metali nzito mfano zebaki (Mercury) vinaweza kusababisha athari kubwa za kiafya kama kansa za ngozi,matatizo ya figo,matatizo ya maini na mengineyo"Bw.Feruzi amesema.

Bw.Feruzi amebainisha kuwa Shughuli za kibinadamu katika rasilimali maji zinanaweza kuchangia uchafuzi wa maji ambayo awali yalikuwa salama hivyo ni vema kufanya upimaji mara kwa mara ili kubaini  mapema aina ya uchafuzi na kuitatua mapema ili kulinda mifumo ya ikolojia.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Masoko , Bi. Gladness Kaseka amesema upimaji wa maji ya kisima kwa matumizi binafsi ni wa hiari ila  kwa wale wanaotaka kusambaza kwa ajili ya matumizi ya watu wengi upimaji ni wa lazima ili kulinda afya za watumiaji.

Kaseka ametoa rai kwa wenye visima binafsi na wale wanaosambaza maji kupima  kama biashara kuwa na tamaduni za kupima kujihakikisha usalama na ubora wa maji husika ili kuepuka changamoto zozote zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji, na muda wa upimaji hadi kupata majibu ni siku 14.


KATIBU MKUU WAZAZI HAPI AMETEMBELEA TRENI YA MWENDOKASI DODOMA

April 24, 2024

 KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Ally Salum Hapi (MNEC) ametembelea na kuona treni mpya ya kisasa ya mwendokasi iliyowasili, Jijini Dodoma jana usiku ikitokea Jijini Dar Es Salaam iliyokuja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Ndg.Masanja Kadogosa, pamoja na waandishi kwa ajili ya kuahiriki Dua Maalumu ya Kuliombea Taifa iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, leo, ambapo Mgeni Rasmi Alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Phillip Isdor Mpango.


Akizungumza baada ya kutembelea na kuona ubora, uzuri na utendaji kazi wa treni hiyo, Katibu Mkuu Wazazi, Ndg.Hapi, aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 - 2024 kwa vitendo na kusema anastahili kuongezewa hali, morali na moyo wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

"Kwa niaba ya viongozi, wanachama na wapenzi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM nichukue fursa hii adhimu kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma imekamilika kwa asilimia kubwa pamoja na majaribio ya treni ya mwendokasi na mabehewa yake kuletwa nchini na kuanza kufanyia majaribio yanayotoa matokeo chanya;

"Ama kwa hakika hii ni furaha na faraja kubwa sana kwetu sisi wamiliki wa duka kuona muuza duka wetu anaiendesha vizuri biashara yetu na matokeo chanya yanaonekana, lakini pia nitoe pongezi kwa watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa usimamizi bora wa fedha za mradi huu ambao ni Tshs.Bilioni 23.5 ni fedha nyingi mnoo ila ndugu zetu hawa wanastahili pongezi kwa kusimamia vyema fedha hizo" alisema Hapi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa TRC, Ndg.Masanja Kadogosa, alitoa shukurani kwa viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kwa kutembelea mradi huo kwa kusema kwao watumishi wa Shirika la Reli Tanzania hujisikia ufahari wa hali ya juu inapotokea nafasi ya viongozi wa CCM na Jumuiya zake wanapotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi na kusifia kwa kile kilichofanyika inawatia moyo na morali wa kuendelea kutumikia shirika na serikali kwa maslahi mapana ya nchi.

Katika msafara wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Ndg.Hapi, aliongozana na Naibu Katibu Mkuu Wazazi Bara, Ndg.Joshua Mirumbe Chacha, viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma, Wilaya pamoja na kata husika kwa kujitoa kuungana nao kutembelea na kutazama mradi huo.






RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALIMBALI

April 24, 2024

 RAIS Samia Suluhu Hassan Atunuku Nishani Viongozi Mbalimbali katika shamrashamra za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Fredrick kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.