UTT-AMIS YASHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

August 30, 2016

Ofisa Mafunzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Ashura Kassim (kulia) akimuandikisha Bi. Azina Ramadhani mmoja wa watu waliofika katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mafuzo Idara ya Uendeshaji, Doris Mlenge na wa pili kulia ni Ofisa Masoko na Uhusiano, Waziri Ramadhani.


Ofisa Masoko na Uhusiano, Waziri Ramadhani (kushoto), akitoa elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa mmoja wa watu waliotembelea banda lao.
Wananchi wakijiandikisha katika Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS.
Ofisa Mafunzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Ashura Kassim akitoa maelekezo kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la UTT-AMIS.
Bi. Azina Ramadhani akijiandikisha.

Ofisa Masoko na Uhusiano, Waziri Ramadhani (kushoto), akitoa elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa mmoja wa watu waliotembelea banda lao.

Baadhi ya watu waliofika katika banda la UTT-AMIS wakipata maelezo kuhusu Uwekezaji wa Pamoja.

KAGERA SUGAR WAFURAHIA KURUDI NYUMBANI, WAJIFUA KWA MARA YA KWANZA KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOGA

August 30, 2016


Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye Uwanja wa Kaitaba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo ambao umemalizika kwa kusuasua.
Mecky Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.
Kwa Makini Wachezaji wa Kagera Sugar wakisikiliza Viongozi wao
Wachezaji wa Kagera Suga wakijifua leo hii hioni kwenye Uwanja wa Kaitaba
Kocha mpya wa Kagera Sugar Mecky Mexime

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA

August 30, 2016


Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa madawati 235 kwa mkoa wa Kagera toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande jana kwenye shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini  Deodatus Kinawiro akihutubia wakazi wa Bukoba baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi Kagera makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba 


 Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande  akitoa hotuba kwa wageni waalikwa na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi za mkoa wa  Kagera ,katika hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano  ya madawati 235 kwa shule za msingi mkoani Kagera   toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.

photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com

DC NDEJEMBI AJIONEA KITUO CHA AFYA KILICHOJENGWA CHINI YA KIWANGO

August 30, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali

RC SINGIDA AKABIDHI MADAWATI 630 KWA WAKURUGENZI WA WILAYA NA MANISPAA

August 30, 2016
Na Mathias Canal, Singida

Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.


Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe amesema kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500 hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika Halmashauri za Singida na Manyoni.