NYOMI KUBWA YA MASHABIKI WA ASERNAL YAJITOKEZA MITAANI KUSHANGILIA KOMBE LA FA

NYOMI KUBWA YA MASHABIKI WA ASERNAL YAJITOKEZA MITAANI KUSHANGILIA KOMBE LA FA

May 18, 2014

MAELFU ya mashabiki wa Asernal wamefurika katika mitaa ya London kaskazini kushangalia ubingwa wa FA waliotwaa jana kwa kuwafunga Hull City mabao 3-2 baada ya kukaa miaka 9 bila taji.


Wachezaji walikuwa katika basi la wazi lililoondoka Emirates majira 11:00 asubuhi na kuzunguka mjini Islington, mitaa ya juu ya mji wa London na kurudi uwanjani.
The wait is over! Arsenal players celebrate breaking their trophy drought by raising the FA Cup

Party time! Arsenal players, including Aaron Ramsey (R), lift the trophy in front of their fans
For the fans: Supporters wave and take pictures of the Arsenal victory bus on a good day to be a Gooner
French fancy: Goal scorer Laurent Koscielny lifts the cup during the  Victory Parade on Sunday
UFALME WA BARCELONA HISPANIA NA ULAYA UMEKWISHA, AMESEMA MASCHERANO

UFALME WA BARCELONA HISPANIA NA ULAYA UMEKWISHA, AMESEMA MASCHERANO

May 18, 2014
 Barca's cycle of dominance is over, says Mascherano
KIUNGO wa Barcelona, Javier Mascherano amekiri kuwa ufalme wa klabu hiyo katika soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla umefika kikomo.
Wakatalunya walishindwa kutetea ubingwa wao wa La Liga baada ya kushindwa kuwafunga Atletico Madrid kwenye uwanja wa Camp Nou jana usiku na kumpa nafasi Diego Simeone kunyakua `ndoo`.
Atletico Madrid licha ya kuwabania Barca kutetea taji lao, pia waliwatoa katika hatua ya robo fainali ya UEFA.
Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa Barca baada ya kufungwa na Real Madrid katika fainali ya Copa del Rey na sare ya jana imewafanya wamalize msimu bila kombe.
Mascherano anaamini kufanya vibaya msimu huu kunadhihirisha kuwa ufalme wa Barcelona umefikia kikomo na yanatakiwa mabadiliko makubwa, lakini alikaa kimya kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.
“Kuzungumzia hatima ya Mascherano ni jambo dogo sana, kinachotakiwa ni kuizungumzia Barcelona. Ufalme umekwisha.” Aliambia Barca TV.
“klabu itafanya maamuzi na mabadiliko, lakini lazima tukubali kuwa msimu huu haukuwa mzuri”.
Kocha Tata Martino amethibitisha kuondoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka huu, huku Luis Enrique akitarajiwa kurithi mikoba yake.
JOHN BOCCO ATIKISA NYAVU NA KUIPA TAIFA STARS USHINDI WA 1-0 DHIDI YA ZIMBABWE

JOHN BOCCO ATIKISA NYAVU NA KUIPA TAIFA STARS USHINDI WA 1-0 DHIDI YA ZIMBABWE

May 18, 2014
 DSC_45751
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAO pekee la mshambuliaji, John Raphael  Bocco `Adebayor` limeipa ushinda taifa Stars dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa raundi ya awali kabisa kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kushindania  tiketi za kushiriki kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Bocco alifunga bao hilo katika dakika ya 13 kwa kumalizia pasi nzuri ya Thomas Ulimwengu.
Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Taifa stars walionesha uwezo mzuri, lakini Zimbabwe nao hawakuwa wabaya.
Kukaa nyuma kwa wachezaji wa Zimbabwe kuliwasaidia kuokoa hatari nyingi langoni mwao.
Tatizo kubwa kwa stars lilikuwa ni viungo wake, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto  kushindwa kupiga pasi za kupenyeza, hivyo kuwalazimisha John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata kugeuka na kuchukua mipira kwa nyuma na kwenda mbele.
Aina hii ya mpira ilipunguza  kasi ya mashambulizi na kuwafanya Zimbabwe wacheze kwa kujiamini na kuona wanawaweza Taifa stars.
Sehemu ya ulinzi wa kati ya Taifa stars  ilikuwa nzuri, lakini beki wa kulia, Shomary Kapombe hakuwa katika kiwango chake na inawezekana ni kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu. Naye Oscar Joshua kwa upande wa kushoto alicheza vizuri , lakini alikuwa mzito kidogo.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya kwanza tu Taifa stars walikosa bao, nao Zimbabwe wakakosa goli.
Dakika moja baadaye John Bocco `Adebayor ` alikosa nafasi nyingine baada ya kushindwa kumalizia krosi ya chinichini.
Bado tatizo la Stars lilikuwa kukosa umakini wanapofika langoni mwa Zimbabwe.
Mbwana Samata na John Bocco kwa nyakati tofauti walishindwa kuzibadili nafasi muhimu kuwa magoli na kuipa Stars kazi ngumu katika mchezo wa marudiano mjini Harare nchini Zimbabwe.
Mzani wa mpira katika kipindi hiki cha pili ulikuwa sawa, lakini Zimbabwe walioneka kuwa na mipango mizuri zaidi.
Hawakujibana katika eneo lao kama kipindi cha kwanza, walifunguka na kwenda mbele na kuifanya Taifa stars ihangaike.
Kwa soka walilocheza Zimbabwe kipindi cha pili wameonesha kuwa wanao uwezo wa kubadilika na kucheza kulingana na mazingira.
Ni dhahiri kwa wiki mbili zinazokuja kabla ya kwenda Zimbabwe, kocha Mart Nooij anatakiwa kufanya maandilizi mazuri zaidi kwasababu inaonekana mechi itakuwa ngumu.
Zimbabwe hawatakuwa na sababu ya kujibana langoni mwao, watashambulia kwa muda wote ili kufuta matokeo ya leo.
Moja ya kanuni ya mpira ni kumfunga magoli mengi mpinzani wako ukiwa nyumbani kwani siku zote ugenini mchezo huwa ni mgumu.
Hata hivyo, Taifa stars wanastahili pongezi kwa matokeo ya leo kwani kimfaacho mtu chake.
Huwezi kujua nini kitatokea Harare kwasababu hata Stars wanaweza kushinda pia.

RADIO OFFICER WA FARM RADIO INTERNATIONAL ALIPOMTEMBELEA MKURUGENZI WA MWAMBAO FM OFISINI KWAKE LEO

May 18, 2014
MKURUGENZI MTENDEJI WA RADIO MWAMBAO YA TANGA,AHMED SIMBA KUSHOTO AKISALIMIA NA RADIO OFFICER WA FARM RADIO INTERNATIONAL WAKATI ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE KWA AJILI YA MAZUNGUMZO 

KUSHOTO NI MKURUGENZI MTENDAJI  WA MWAMBAO FM,AHMED SIMBA AKIBADILISHANA MAWAZO NA RADIO OFFICER WA FARM RADIO ALIYEMTEMBELEA OFISINI KWAKE LEO

HAPA WAKISISITIZA JAMBO.



MKURUGENZI MTENDEJI WA RADIO MWAMBAO YA TANGA,AHMED SIMBA KULIA  AKIMSIKILIZA NA RADIO OFFICER WA FARM RADIO INTERNATIONAL WAKATI ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE KWA AJILI YA MAZUNGUMZO  LEO



BAADA YA MAZUNGUMZO HAPO WANAAGANA

NSSF WAUSHAURIWA KUANZISHA MFUKO MAALUM WA KUWASOMESHA WATOTO WANAOZALIWA NJE YA NDOA

NSSF WAUSHAURIWA KUANZISHA MFUKO MAALUM WA KUWASOMESHA WATOTO WANAOZALIWA NJE YA NDOA

May 18, 2014

Social-Security-Fund-NSSF(1)(1)MFUKO  wa hifadhi ya jamii( NSSF) umeshauriwa  kuanzisha mfuko maalum  wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kwa kuwa hadi sasa mfuko huo unatoa mafao kwa watoto walioko ndani ya ndoa huku wanaozaliwa nje wakiwa hawapati mafao kutokana na kutelekezwa na baba zao.
Aidha kwa kipindi hiki cha miaka 50 toka kuanzishwa kwa mfuko kuna wanachama wengi wenye watoto wengi walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa huku watoto hao wan je wakiwa wanaachwa wakiteseka pamoja na mamazao.
Akizungumza jana mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa mfuko huo  uliokuwa ukifanyika mjini hapa mratibu wa dangote Esta Baruti alisema kuwa watoto wengi walioko nje ya ndoa hawapatiwi mafao hivyo ni vema mfuko huo ukaangalia namna ya kusaidia watoto hao.
 Alieleza kuwa wanachama wengii wa mfuko huo wana  watoto walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa na kwamba wanaopatiwa mafao ni wale tu walioko ndani ya ndoa jambo linalowafanya watoto hao wan je kukosa haki zao za msingi kama elimu na mengineo.
Alifafanua kuwa watoto hao wan je wanaponyimwa mafao kwa kuwa wamezaliwa nje kunawaathiri kisaikolojia kwa kuwa wao hawana  makosa na  sio wao waliochagua kuzaliwa na wazazi walioko nje ya ndoa.
“mimi nilishaona sana hili tatizo ni kubwa sana na hasa kwa akina mama wanaoachiwa wale watoto kwa kuwa baba zao hawawashirikishi mafao yao kwa hawa bali ni wale tu watoto wao walioko ndani  ya nyumba zao hili jambo naomba lifikiriwe sana na huu mfuko”aliongeza Baruti.
Aidha alieleza kuwa ni vema mfuko huo ukafikiria namna ya kuwasaida watoto hao pamoja na wakina mama kwa kuwatafutia njia mbadala  kwa kuwa wao ndio wanaobaki njia panda bila kujua wawafanyeje hao watoto hao na hivyo kuwafanya waishi katika mazingira magumu.
Wakati huo huo baadhi ya wadau wa mfuko huo waliutaka mfuko huo kuangalia maeneo ya kuwekeza maabara haswa katika shule za kata ili kuwasaidia wanafunzi kupata tekenolojia mbali mbali.
Mmoja wa wadau hao Said Habibu alisema kuwa mfuko huo umekuwa ukisaidia jamii sana hasa kati ka uwekazaji na hivyo endapo utawekaza zaidi katika maabara kwa shule za kata kutasaidia sana taifa kupata wanasanyansi wengi kwani shule za kata zina upungufu mkubwa wa maabara jambo linalowanyima wanafunzi kujifunza kwa vitendo.