MAFUNZO YA TABLE TENIS MKOA WA TANGA YALIVYOFANYIKA JIJINI TANGA.

August 20, 2013
KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,BENEDICT OLE KUYAN AKIZUNGUMZA JAMBO NA MCHEZAJI WA MCHEZO WA TENIS JANA KABLA YA KUANZA MAFUNZO YA MCHEZO HUO ENEO LA RASKAZONE JIJINI TANGA.







AFISA MICHEZO MKOA WA TANGA,DIGNA TESHA AKIZUNGUMZA NA MKUFUNZI WA MAFUNZO HAYO AMBAYO YALISHIRIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.

58 WAJITOSA UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI

58 WAJITOSA UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI

August 20, 2013
NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.
Jumla ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani,Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia.

Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii.

Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge.

Athuman Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.

Wengine ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.

Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).

Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

RAMBIRAMBI MSIBA WA BARAKA KITENGE

August 20, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74) kilichotokea leo mchana (Agosti 20 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Kitenge amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman Juma.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi. Amina

24 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA GAMBIA

August 20, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.

Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.

Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).

Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).