MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

June 30, 2016


C1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva   katika mazungumzo kati yake na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  yaliyofanyika kwenye  makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
C2 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika  kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
C3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa 2015 kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni30, 2016.
C4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Tume ya taifa ya Uchaguzi kwenye Makazi yake  mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.
C5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damiana Lubuva.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50

June 30, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.


Na EmanuelMadafa,Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa  mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa  kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

Awali, akitoa malalamiko  hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.

Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata mkandarasi huyo.

Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa ushindi mfuko huo..
Mwisho.



Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja, akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya kiutendaji katika kikao  hicho.

Baadhi ya wananchi waliofika kutoa kero na malalamiko katika kikao hicho.

Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 mwaka huu.

Baadhi ya wananchi wakitoa malalamiko na kero zao katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 -2016 ambapo MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ndiye aliyepokea kero hizo sanjali na watendaji wa serikali na taasisi  mbalimbali za serikali .

Kikao kikiendelea.(Picha E.Madafa)

TAASISI YA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WA MAZINGIRA

June 30, 2016
Jimmy Luhende, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini (ADLG), akizungumza katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo Jijini Mwanza. 

Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.

Katika mjada huo, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini.
Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.

Amesema tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mdau wa Mazingira, Sheikh Saad Rwekaka ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA mkoani Mwanza, akitoa maoni yake. Anasema ni vyema wachimbaji wadogo wadogo wakashirikishwa ipasavyo ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira katika shughuli zao.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Mijadala ikiendelea
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Ashraph Omary (katikati) ambae ni mdau wa Mazingira kutoka taasisi ya MEDTO (Mining and Environmental Transformation for Development Organisation), akifanyiwa mahojiano na mwanahabari. 
Imeandaliwa na BMG

SENDOFF YA BINTI WA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA YAFANA. KIFUATACHO NI NDOA TAKATIFU

June 30, 2016
June 30, 2016 Usiku wa kuamkia leo Julai Mosi, 2016, ilikuwa siku ye furaha kwa Bi.Happness Daniel Kulola (kushoto), ambapo ilikuwa ni siku ya sherehe yake ya "Send Off" iliyotoa fursa kwa Wazazi,Walezi, ndugu jamaa na marafiki zake kujumuika pamoja Jijini Mwanza na kumuaga rasmi kabla ya kufunga pingu za maisha.

Happyness anatarajia kufunga pingu za maisha na mchumba wake, Richard Jeremia,  kesho kutwa jumapili Julai 03,2016 katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.
Wasimamizi/wapambe wa maharusi
Bibi harusi mtarajiwa akiingia Ukumbini
Bibi harusi mtarajiwa akikata keki
Bibi harusi mtarajiwa akimlisha keki msimamizi wake, ishara ya upendo
Bibi harusi mtarajiwa akilishwa keki na msimamizi wake
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake upande wa mwanaume
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake wa kumzaa
Wasaa wa kufungua Shampeini
Furaha ikiendelea Ukumbini
Mwenyekiti wa Kamati ya SendOff akijimwayamwaya Ukumbini kabla ya kutoa salamu za kamati
Matukio yakiendelea kunaswa Ukumbini
BMG
Bibi harusi mtarajiwa, Happness Daniel Kulola (wa pili kushoto), akiwa na bwana harusi mtarajiwa, Richard Jeremia (wa pili kulia). Wengine ni wasimamizi/wapambe wa maharusi.
Bibi harusi mtarajiwa, Happness Daniel Kulola (kushoto) akiwa na bwana harusi mtarajiwa, Richard Jeremia (kulia)
Mapema Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akifungua sherehe kwa maombi.
Ujumbe
Nyumba na Mali ni Urithi apatao mtu kwa babae, bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana. Mithali 19:14
USAJILI WA MAGULI ‘OMAN PROFESSIONAL LEAGUE’ UTAIMARISHA ZAIDI STARS

USAJILI WA MAGULI ‘OMAN PROFESSIONAL LEAGUE’ UTAIMARISHA ZAIDI STARS

June 30, 2016
Maguli-uarabuni 1
Na Baraka Mbolembole
MSHAMBULIZI wa Taifa Stars, Elius Maguli amekamilisha usajili wake kutoka Stand United ya Shinyanga kama mchezaji huru na kujiunga katika klabu ya Dhofar SC ya Oman Professional League.
Kila mmoja anakumbuka namna mchezaji huyo alivyopitia kipindi kigumu msimu wa 2014/15 akiwa na kikosi cha Simba SC ambacho kabla ya kuanza kwa msimu wa 2015/16 kocha aliyepita wa kikosi hicho, Dylan Kerr alitangaza kutomuhitaji na uongozi ukavunja mkataba wake akiwa bado na mwaka mmoja zaidi.
Kitendo cha kujiunga na kocha Mfaransa, Patrick Liewig katika timu ya Stand kabla ya kuanza kwa msimu uliopita hakikuonekana kuwastua wengi lakini game 9 za mwanzo wa msimu ziliambatana na magoli 9 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Ruvu Shooting, pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika VPL na kujumuhishwa katika timu ya Taifa kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu.
Kujiunga na Dhofar timu iliyomaliza katika nafasi ya tano katika ligi ya kulipwa mwaka mmoja uliopita ni hatua kubwa kwa mchezaji kijana kama Maguli ambaye ameondoka VPL akiwa amefunga jumla ya magoli 33 katika misimu yake mitatu aliyocheza kama mchezaji wa vilabu vya Shooting, Simba na Stand United.
Ameruka vikwazo vingi katika ‘soka lenye fitna’ na matatizo mengi ya watendaji. Mfano, katika misimu yake miwili ya mwisho VPL (Simba na Stand) timu hizo zote mbili zimejaa migogoro ya kiutendaji kati ya viongozi na wachezaji au viongozi kwa viongozi.
Katika mazingira hayo si rahisi kwa mchezaji kutimiza malengo yake na inapotokea nafasi kama hii ya Maguli-Kusajiliwa moja kwa moja na timu ya kulipwa ukiwa U25 ni jambo la kumshukuru Mungu na pengine ni sehemu ya kufanya kazi nzuri zaidi kwa jitihada ili kuthibitisha kwa wale waliokusaini kuwa hawakufanya makosa.
Maguli ni mshambuliaji wa kikosi cha kwanza katika timu ya Taifa ya Tanzania kwa mwaka mmoja sasa akicheza sambamba na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta katika safu ya mashambulizi kwa maana hiyo, kocha Charles Mkwassa ataendelea kufurahia vijana wake watatu wakiwa ng’ambo ya nchi kuendeleza vipaji vyao na kudumisha viwango vyao vya kiuchezaji.
Kama Hamis Mroki anayecheza Thailand, huyu ni nahodha wa kikosi cha vijana kilichokuwa kikiwajumuhisha kina Ulimwengu, Himid Mao na wengine ni zao la TSA, Samatta, Tom, Maguli, Mrisho Ngassa watatupiwa jicho la 3 bila shaka timu ya Taifa Stars itaimarika licha ya kwamba bado hatuna ligi makini ya ndani.
Dhofar ni timu iliyoanzishwa miaka 44 iliyopita, na Oman kuna mishahara mikubwa hadi kufikia dola 30,000 kwa mchezaji wa kiwango cha Maguli. Mchezaji wa kikosi cha kwanza wa timu ya Taifa. Sasa mastaa watatu wa Stars katika kikosi cha mashambulizi wapo ng’ambo. Kila la heri Elius Maguli.

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA

June 30, 2016


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia)
mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba  wakati wa tafrija
ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima  iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.