KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAUNGA MKONO KUFUTWA KWA KITONGOJI KILICHOANZISHWA KINYUME CHA SHERIA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SAADAN

September 03, 2017
NA HAMZA TEMBA - WMU.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.

Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria. 

"Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama" alisema Ndetiye.

Aliongeza, "tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali ifanye uwekezaji wa kueleweka"

Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza mgogoro huo. Alisema, "Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo".

Awali akielezea kuhusu mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga alisema baada ya maazimio ya kamati iliyoundwa na Serikali ya wilaya kumaliza mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali maazimio yaliyowekwa ya kulipwa fidia huku wengine wakikaidi kuondoka akiwemo muwekezaji aliyeshikilia sehemu ya eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa bila kuwekeza mradi uliokusudiwa ambapo wamepewa kipindi cha mwezi mmoja waondoke kwa hiari kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uvinje,  Hussein Akida alisema kitongoji hicho kilianzishwa ndani ya kijiji cha Saadan katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kikiwa na ukubwa hekta 3,000 na mpaka sasa Kitongoji hicho kina wakazi wasiopungua 72. Aliiomba Serikali kutambua mipaka ya kitongoji hicho pamoja na kuwasogezea wananchi  huduma za kijamii.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walitilia mashaka uwiano wa kimahesabu wa taarifa hiyo na uhalisia ambapo walihoji iweje kitongoji chenye miaka mingi kiasi hicho kiwe bado hakijapewa hati ya kuwa kijiji kamili pamoja na idadi ndogo ya wananchi wasiongezeka ndani ya muda mrefu wa miaka zaidi ya 100 toka kuanzishwa kwa Kitongoji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema, mgogoro huo uko wazi na unapaswa kumalizika mara moja kwa kuwa Serikali ya Wilaya kupitia kamati iliyoundwa imeshafikia maazimio ya kuwaondoa wananchi walioanzisha makazi ndani ya eneo la hifadhi kinyume cha Sheria. Alitoa wito kwa wananchi kutii sheria za hifadhi na kuheshimu mipaka iliyowekwa kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina ya Serikali na wananchi.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto) akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa pili kushoto).
Wajumbe wa kamati hiyo wakijadili baadhi ya mambo waliyoyaona katika eneo hilo lenye mgogoro.
 Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo  akiwasilisha taarifa ya Shirika hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan jana wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu mgogoro baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan.
Wajumbe wa kamati wakikagua eneo hilo la mgogoro.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),ambaye alikuwa Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Dkt. James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi kandokando ya fukwe  za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
 Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (kushoto) na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Gerald Magiri wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo jana.
TGNP yaweka wazi malengo ya Tamasha la Jinsia 2017

TGNP yaweka wazi malengo ya Tamasha la Jinsia 2017

September 03, 2017
[ 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuzungumzia Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi Septemba 5 hadi 8 ya mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa FemAct, .Abdulla Othman 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule (katikati) akijibu maswali anuai ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi na Mwenyekiti wa FemAct, Abdulla Othman. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano na vyombo vya habari kuzungumzia Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi Septemba 5 hadi 8 ya mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule pamoja na wanaharakati wengine.
  MTANDAO ya Jinsia Tanzania (TGNP) leo imeweka hadharani malengo makuu ya Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi Septemba 5 hadi 8 ya mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule alisema tamasha la mwaka huu litakuwa na malengo manne na lengo la kwanza ni kutafakari na kusherehekea mafanikio, changamoto zilizopo katika kuendeleza usawa wa kijinsia. Alisema hili ni kuzingatia utekelezaji wa mikataba, maazimio, sera na mikakati mbalimbali ya kimataifa. Alisema lengo la pili ni kutathmini ushiriki wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi katika uongozi, hususan uongozi wa kisiasa kwenye Serikali za mitaa. Lengo la tatu ni pamoja na kufuatilia kuhifadhi, kutambua na kusherehekea viongozi wanawake wenye michango ya kuigwa juu ya usawa wa kijinsia na uwezo wa wanawake, hususan mapambano dhidi ya mfumo dume na uliberali mamboleo. Akifafanua kuhusiana na lengo la tatu, Bi. Vicensia Shule alisema katika lengo hili TGNP itawatambua na kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu, Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda, Mbunge wa Bunda Mjini, Estar Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester Mwaikambo, na Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada walizozionesha katika uongozi. Aidha alisema lengo la nne itakuwa kuhimarisha harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi kupitia ujenzi wa nguvu za pamoja. "...Tamasha la Jinsia la mwaka huu litaongozwa na mada kuu isemayo 'Mageuzi ya mifumo kandamizi kwa usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu'" alisema Bi. Vicensia Shule.    
Mwenyekiti wa asasi ya WAJIKI, Janeth Mawinza (katikati) pamoja na wanaharakati wengine akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo.  
Mwanaharakati, Seleman Bishagazi (katikati) pamoja na wanaharakati wengine akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo. 
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo.

“BANDARI YA TANGA YANG’ARA KILIMANJARO CUP”

September 03, 2017


Mchezaji wa timu ya Bandari Tanga akiruka juu kuwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist  ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57
Wachezaji  wa timu za Bandari Tanga na Baptist wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist  ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57

Kocha wa timu ya Bandari Tanga Mohamed Fazal akitoa maelekezo kwa timu hiyo wakati wa mapumzikokulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Kocha wa timu ya Bandari Tanga,Mohamed Fazal  akitoa mawaidha kwa timu hiyo wakati wa mapumziko kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Kikosi cha timu ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga
TIMU ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga ambayo inashikilia Ubingwa wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup mwaka jana inashiriki tena Mashindano hayo kutetea ubingwa huo mwaka huu katika mashindano yanayoendelea kwenye viwanja KCMC mjini Moshi.


Kitendo cha timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa mara nyengine kinaonyesha namna kinavyotumia vema fursa hiyo kuitangaza Bandari ya Tanga.


Katika kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa vitendo leo timu ya Bandari Tanga wameibuka na ushindi wa vikapu 64-57 dhidi ya timu ya Baptist katika mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa huku Bandari Tanga ikipambana ili kuhakikisha inatetea Ubingwa wake na kuondoka na ushindi huo.


Awali akizungumza wakati akizundua mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira amezitaka timu shiriki kutumia fursa ya mashindano hayo kutangaza utalii wa nchi ikiwemo mlima Kilimanjaro.


“Baada ya mashindano haya timu zote shiriki zitakwenda kupanda mlima Kilimanjaro ili kuweza kuhamasisha wanamichezo na wananchi wengine kuweza kutalii mlima huo “Alisema Mkuu huyo wa mkoa.


Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuchangia damu kwa wahitaji ambapo katika viwanja hivyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiari.

Mashindano hayo yanaendelea kwa wiki nzima katika viwanja vya Baptist na KCMC Mkoani Kilimanjaro.


RITTA KABATI AICHANGIA TIMU YA LIPULI SH 700,000/= NA AHADI RUKUKI

September 03, 2017
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akimkabidhi pesa makamu Mwenyekiti wa timu ya lipuli Ayoub nyezi kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki ligi kui Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018
 Kocha Mkuu wa timu ya lipuli Suleiman matola akitoa shukrani kwa mbunge huyu Ritta Kabati kwa kuichangia timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya lipuli wakiwa wanasikiliza kinachojili wakati walipotembelewa na mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati

Na fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameichangia timu ya lipuli jumla ya shilingi lakini saba kwa ajili ya matumizi ya timu ili kuisaidia timu kufanya vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara ambapo inaonekana kuwa ligi hiyo mwaka huu inaonekana kuwa ngumu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi pesa hizo Kabati alisema kuwa ameamua kuchangia timu kwa kuwa anapenda michezo hivyo akiona timu ya inateteleka mara nyingi husaidia pale kwenye uwezo wake.

"Mimi ni muumini sana wa michezo hivyo nimekuwa nikijitolea sana kusaidia michezo mbalimbali ndio maana umekuwa mkisikia nikifanya mambo mengi kwenye sekta hii ya michezo,hivi karibuni nilikuwa nianzisha Mashindano ya Ritta Kabati challenge cup ambayo imesaidia kuinua soka la mkoa wa Iringa "alisema

Kabati alisema kuwa ataendelea kuisaidia timu kadili awezavyo kwa kuwa anaipenda timu ya lipuli hivyo hata akienda china ataitafutia timu ya lipuli jezi ambazo zitawasaidia katika ligi kuu na michuano mingine atayokuwa inaendelea hapo baadae.