MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA CRDB ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA

July 06, 2023

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto) akiwa ameambatana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd (kulia) pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo wakati wakitembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Mohamed (wapili kulia) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Sabasaba, Zoe Kafulusu.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaban akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipokutana katika ukumbi maalum wa wageni katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya Maafisa wa benki hiyo wanaotoa huduma za kibenki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa benki hiyo wanaotoa huduma za kibenki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo wakati alipotembelea maonyesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Lughano Nselu wakati alipotembelea Banda la benki hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo wakati alipotembelea maonyesho hayo.





WANACHAMA, WASTAAFU WAIMIMINIA SIFA PSSSF KWA HUDUMA BORA

July 06, 2023

 

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SABASABA

WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) hususan Wastaafu wameelezea kuridhishwa kwao na huduma wanazozipata hivi sasa kutoka kwenye Mfuko huo ambao Agosti Mosi, 2023 utatimiza miaka Mitano tangu uanzishwe baada ya Serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, LAPF NA GEPF.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walipofika kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 5, 2023 walisema kero zilizokuwepo miaka michache iliyopita kwa sasa hawakumbani nazo.

“Wakati nafuatilia Mafao yangu nilihudumiwa vizuri, ofisi hii imebadilika sana nawaombea kwa Mungu muendelee hivyo hivyo, nawapa hongera nyingi, nasema haya kutoka moyoni mwangu, nimefika hapa na kupata huduma kwa haraka.” Alisema Mstaafu Bw. Abdallah Mandwanga.

Bw. Amana Shomari, Mstaafu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) miaka 10 iliyopita alisema kwa upande wake huduma anazozipata kwa sasa kutoka PSSSF zimeboreka sana na zimekuwa za kutia moyo.

“Nikiwa kama Mstaafu, kilichonileta hapa sabasaba kwenye banda hili la PSSSF, ni kuhakiki taarifa zangu, nimetumia si zaidi ya dakika 5 kupata huduma, hakika nawapongeza sana, nitoe wito kwa wastaafu wenzangu zoezi la uhakiki ni muhimu kwani linaondoa ucheleweshaji wa malipo ya mafao, mimi sina tatizo na malipo yangu ya kila mwezi, napokea kwa wakati haivuki tarehe 25 pesa nakutana nayo kwenye akaunti yangu.” Alisema.

Naye Bw. Stanslaus Kagaruki ambaye naye alifika kwenye banda la PSSSF amewahamasisha wastaafu wenzake kuona umuhimu wa kuhakiki taarifa zao kwani licha ya kwamba ni takwa la kisheria lakini ni huduma inayotolewa kwa muda mfupi.

“Nimechukua muda mfupi sikutarajia, nilidhani itanichukua muda mrefu, kumbe ni dole gumba, sekunde tu nimekamilisha, hivyo nawasihi wenzangu wafike kuhakikiwa ili waendelee kupokea Pensheni bila ya kikwazo.” Alisema Bw. Kagaruki.

Akizungumzia hali ya Mfuko kwa sasa, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema Mfuko umeendelea kutekeleza majukumu yake kama yalivyo ainishwa katika sheria ya Mfuko kwa umahiri na umakini mkubwa ambapo aliyataja majukumu hayo kuwa ni Kuandikisha Wanachama, Kukusanya Michango na Kuwekeza Michango hiyo na Kulipa Mafao.

“Hadi sasa tuna wanachama 780,000 na tunakusanya Michango kwa mwaka shilingi trilioni 1.65, na tunalipa Mafao shilingi trilioni 1.6 kwa mwaka,” alifafanua CPA. Kashimba.

Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo Mkuu wa PSSSF alibainisha kuwa, kwa sasa kuna jumla ya wanufaika wa Mafao ya kila mwezi (Monthly Pension) wanaofikia 160,000 ambao wanaolipwa Pensheni ya jumla ya shilingi bilioni 65 kila mwezi.

“Hapa utaona jinsi Mfuko unavyochachua uchumi wa nchi kwani wazee wetu hawa wanapopokea Mafao haya wanakwenda kununua huduma na mahitaji yao mbalimbali na hivyo fedha nyingi zinawafikia wananchin huko mtaani.” Alifafanua.

Aidha Mkurugenzi huyo Mkuu wa PSSSF amedokeza kuwa, Mfuko uko mbioni kuzindua mfumo mpya wa Kidijitali utakaowezesha kushughulikia masuala yote ya mafao kwa njia ya mtandao.

“Hakutakuwa na sababu ya mstaafu kuzunguka ofisini kufuatilia mafao, mstaafu mtarajiwa atajaza maombi akiwa kwenye meza yake ofisini na taarifa atakuwa anazipata kwenye simu yake ya mkononi.

“Hii yote inafanyika katika kuhakikisha tunasogeza huduma karibu kwa wanachama wetu na wastaafu kwa ujumla ili kuwaondolea adha ya kuzunguka huku na kule kufuatilia mafao yao, tunaamini kupitia mfumo huu ndani ya muda mfupi baada ya kujaza taarifa zao zitachakatwa na muhusika atakutana na fedha zake benki,” amesema Kashimba.

CPA. Kashimba amesema kupitia mfumo huo mfanyakazi anayekaribia kustaafu ataweza kujaza taarifa zake akiwa ofisini na zikachakatwa kwenye mfumo kisha kukutana na fedha zake benki. 

Alisema mafanikio yanayoonekana hivi sasa kwa sehemu kubwa yamechangiwa na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye tangu ameingia madarakani Serikali imeongeza ajira kwa kiwango cha juu.

Wanachama wa PSSSF ni watumishi wote wa Umma, kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ambayo Serikali inamiliki Hisa zaidi ya asilimia 30%, alifafanua.

“Kwa kasi hii ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuongeza ajira nchini, Mfuko unatarajia ongezeko la wanachama na kufikia elfu 40 kwa mwaka.” Alifafanua.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akizungumza na Wanachama waliotembelea banda la Mfuko huo kupata huduma Julai 5, 2023.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye leo ameyafungua rasmi Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi
Mwanachama wa PSSSF (kushoto) akihudumiwa 
Mwanachama wa PSSSF (kulia) akihudumiwa 


-- Khalfan Said

RC KINDAMBA AVITAKA VYOMBO VYA SERIKALI NA TAASISI ZA UMMA KULIPA MADENI HARAKA TANGA UWASA

July 06, 2023
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati  ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa ziara yake wa pili kushoto katika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe 
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Goefrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa kwanza kushoto wakati wa ziara hiyo katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya ziara hiyo 
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akimueleza jambo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara yake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliyesimama katikati wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga
Eneo la Mowe ambapo maji husafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji

Na Oscar Assenga, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala watakatiwa huduma hiyo.

Kindamba aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba pamoja na kwamba Tanga Uwasa wamekuwa wakishirikiana na vyombo hivyo lazima wahakikishe wanalipa haraka madeni hayo kwa wale ambao ni wadaiwa sugu ambao hawaonyeshi jitihada za kuyalipa.

“Niwapongeze Tanga Uwasa kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa huduma lakini nivitake amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala mtasitishiwa huduma hii”Alisema RC Kindamba.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyoendelea kugusa maisha ya wananchi wa kawaida kwa maana ukienda kwenye maji,afya na elimu utamkuta walichokwenda kushuhudia ni kitu kikubwa sana ambapo Tanga Uwasa wameweza kuongeza uwezo wa kusambaza maji kutoka lita Milioni 30,000,000 mpaka lita milioni 45,000,000.

Hata hivyo alisema mpango wa muda ujao na muda wa kati ni kupanua uwezo wa kuzalisha lita milioni 60 na hilo litawezekana kutokana na mipango waliojiwekea watakuja kutangaza kwenye masuala la hati fungani ambazo zitasaidia kupatikana mtaji wa kuweza kupanua zaidi mradi wa maji kwenye mkoa na Jiji la Tanga.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama kutoa huduma zao kwani wao wanatoa huduma kwao.

Mhandisi Hilly alisema wakati mwengine kutokana na sababu mbalimbali kuna kukwama kwenye malipo na kwa sasa wanazidai taasisi hizo takribani Bilioni 1.8 wanashuruku wameanza kupunguza kidogo.

“Kama mlisikiliza Bunge mara ya mwisho tulikuwa tunadai Bilioni 2.4 hivyo wamejitahidi kupunguza Milioni 400 karibia 500 hivyo tunaomba wapunguze deni hilo kutokana na deni ni kubwa na linatukwamisha mambo mengi ya utoaji huduma,ununuaji madawa na ulipaji umeme”Alisema Mkurugenzi huyo.

Naye kwa upande wake Mwenyekiit wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kwamba madeni yamekuwa yakiwasumbua sana hususani vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma.

“Kwa kweli ni wateja wetu wazuri lakini madeni yamekaa muda mrefu na tuliona tukushirikishe ili uweze kutusaidia Mkuu wa Mkoa na uwasaidia wenzetu wanadai wanapodai walipwe ili waweze kutulipa”Alisema Dkt Fungo..