MBUNGE MUSSA NA MKEWE WASHIRIKI ZOEZI LA MSARAGAMBO WA MTARO KATA YA MAWENI JIJINI TANGA

August 25, 2017
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akichukua sururu kwa ajiliu ya kushiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe hadi mtaani hapo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Tanga nae akishiriki zoezi la Uchimbaji wa mtaro huo
 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Tanga nae akishiriki zoezi la Uchimbaji wa mtaro huo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea na kushiriki nao uchimbaji wa mtaro wa kupitishia maji

MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.

August 25, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na  waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikagua kwa kujaribu kuziendesha Pikipiki  hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
.Muonekano wa pikipiki hizo.
 Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.

Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.

BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA

August 25, 2017
Na Lawrence Raphaely - Bunge.

Balozi wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai  Jijini Dar es Salaam mapema leo kumuaga baada ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.

Akizungumza na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda wake wa kutumikia kama Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi kuondoka ingawa angetamani kuendelea kubaki.Balozi huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika kipindi chake chote akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kukua.

“Ninafuraha kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa uhusiano wetu wa kihistoria umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa China hapa Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi mingi,” alieleza Balozi huyo.

Balozi huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya mwisho kuhudumu kama Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na akiwa huko ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na China.

“Tanzania ndiyo nchi yangu ya mwisho  kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea nyumbani (China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China,”  alisema Balozi Youqing.

Kutokana na hilo Balozi Youqing alisema kuwa ingawa  anarejea nchini China lakini yupo tayari kwa Tanzania kuendelea kumtumia kama Balozi wake katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakozosaidia katika kudumisha ushirikiano baina wa nchi zote mbili.

“Nipo tayari kwa Tanzania kuendelea kunitumia kama Balozi wake aliyepo Nchini China, ninawakaribisha kwa mikono yote miwili tuendelee kufanya kazi kwa pamoja,” alisema Balozi huyo.

Kwa upande wake Spika Ndugai alimshukuru  Balozi huyo kwa kazi kubwa ambayo ameifanya akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa daima Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.

“Mimi binafsi katika kipindi chako ukiwa kama Balozi nimeshuhudia ongezeko kubwa la watanzania wengi tena wa hali ya chini wakisaifiri kwenda China kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara,” alisema Spika Ndugai na kuonegeza kuwa; kupitia fursa hiyo Watanzania wengi wameweza kujiajiri kupitia biashara ya kununua bidhaa toka China na kuja kuuza hapa nchini.

Mhe Spika pia alimshukuru Balozi Youqing kwa uchakapakazi wake katika kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia wataalamu kutoka nchini China.

“Unaondoka lakini utakapojisikia kurudi, sisi kama Bunge na Serikali kwa ujumla tupo tayari kukupokea kwa mikono miwili na kuendelea kufanya kazi na wewe,” alisema Spika Ndugai.

Mbali na hayo Spika Ndugai pia alimuomba Balozi Youqing kuendelea kuwa Balozi wa Tanzania atakaporejea nchini China kwa kuendelea kufanya shughuli ambazo zitasaidia katika kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi  Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

UKAID NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WATUMISHI

August 25, 2017
Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa  lengo la kuongeza ujuzi na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na Gloria Mduda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy, kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), wakielekea katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa miaka mitano wa masomo ya juu kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza wenye thamani za shilingi bilioni 3.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Mkuu wa Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) nchini Tanzania Beth Arthy (wa pili kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) wakielekea katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo ya mafunzo ya juu kwa ngazi ya Shahada ya Uzalimili kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza kuhusu masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha umma na sheria kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango uliotolewa na Serikali ya Uingereza.
Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly, akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo ya juu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la UKAID-DFID utakaogharimu shilingi bilioni 3.6. British Council Tanzania ni waratibu wa mpango huo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la  UKAID-DFID, uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya ufadhili wa masomo ya Juu katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango katika ngazi ya shahada ya uzamili kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza UKAID-DFID wenye thamani ya shilingi bilioni 3.6, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)​

RAIS DKT. MAGUFULI AJICHANGANYA NA WANANCHI KUPANDA KIVUKO KWENDA KIGAMBONI NA KUFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM

August 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akichukua Tiketi zake pamoja na chenchi mara baada ya kulipia huduma ya Kivuko wakati akielekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Ndemango ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea  katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiingia katika kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine  wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili upande wa Kigamboni mara baada ya kushuka pamoja na abiria wengine kwenye pantoni la MV Kigamboni.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama mmoja mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

August 25, 2017
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017. Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka  wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.
Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.
“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.
Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.
TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.
“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo.

 Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
 Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.

MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA

August 25, 2017
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao. 
 Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati 


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.

Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.

Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.

Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.

"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti

Wenyeviti hao waliwataka viongozi wa Manispaa ya Iringa kutoa kwa haraka vibari vya ujenzi maana kumekuwa na ukilitimba mwingi kitu kinachosababisha ujenzi holela wa makazi kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa hivyo viongozi wanapaswa kuwa makini na mikakati madhubuti kwa kuwa wananchi wanataka kujenga nyumba zao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Sweetbert Maro alisema kuwa kweli posho wanazopewa wenyeviti wa mitaa ni ndogo hivyo uongozi wa halmashauri ya manispaa imejipanga kukaa pamoja wenyeviti kujadili jinsi gani ya kuongea posho hizo kulingana na majukumu wanayoyafanya kuiwakilisha serikali.

"Mnafanya kazi kubwa mno lakini mnapewa posho kiduchu hivyo tutakaa na kulijadili hili swala kwa kina kwa kuwa bila wenyeviti wa mitaa halmashauri haiwezi kupata maendeleo na kukuza mji kwa nguvu zote hivyo tunawaomba wenyeviti muendelee kufanya kazi wakati swala la posho linashughulikiwa"alisema Maro

Maro alisema kuwa atamshauri Mkurugenzi kutafuta muda muafaka wa kukaa pamoja wenyeviti wote wa mitaa 192 ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kuzijua changamoto na jinsi gani ya kuzitatua maana leo hii mkutano huu ulikuwa wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.

Aidha Maro aliwataka wenyeviti wa mitaa kuwabana maafisa watendaji wa mitaa maana uongozi wa halmashauri umekuwa ukitoa posho kwa wakati kulingana na agizo la serikali na kufuata sheria ya ugawaji wa posho  kwa walinzi wa amani kwenye mitaa yako.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa kuna kero nyingine atazipeleka bungeni ili kuweza kupatiwa ufumbuzi zaidi na kuzitafutia njia za kuzitatua maana kwa ngazi ya Manispaa wameshindwa kuzitatua.

Kabati aliwaahidi wenyeviti wote wenye kero za ngazi ya manispaa atahakikisha zinatatuliwa kwa wakati lakini amewahakikishia kuwa ataitembelea mitaa yenye kero ambazo zipo kwenye uwezo wake atazitatulia huko huko kwenye mitaa.

Wenyeviti hao walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kuwakutanisha na viongozi wa halmashauri na kusikiliza kero zao kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ambao utaongeza tija ya kuleta maendeleo kwenye mitaa hao.

WATOTO KUTOKA COMPASSION KUCHUANA VIKALI JIJINI MWANZA

August 25, 2017
BMG Habari, Pamoja Daima!
Fainali ya mashindano ya watoto kutoka Vituo vya Huduma ya Mtoto (Compassion) Kanda ya Mwanza, inatarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 26,2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi, Joram Samwel amesema mashindano hayo yalianza tangu Mei 25 mwaka huu kwa kuhusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete pamoja na riadha.

Amesema timu ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma itachuana na wenzao kutoka Moravian Kigoto kwenye mchezo wa fainali huku timu ya watoto wenye umri kama huo kutoka AIC Bujora ikichuana na wenzao timu ya PAG Mabatini ili kumsaka mshindi wa tatu.

Upande wa timu ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka minane hadi 12 ya EAGT Buzuruga itacheza wenzao kutoka AIC Buhongwa kwenye mchezo wa fainali huku.

Katika fainali ya mchezo wa mpira wa pete, timu ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma,itacheza na wenzao kutoka TAG Nyakato huku wale wenye kati ya miaka minane hadi 12 kutoka FPCT Pasiansi wakicheza na wenzao kutoka Moravian Kigoto.

Joram Samwel amesema lengo la michuano hiyo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto ambapo wamewasihi wazazi, walezi, watoto pamoja na wapenzi wa michezo Jijini Mwanza, kujitokeza kwa wingi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi ili kushuhudia fainali hiyo ambayo itakuwa na mvuto wa kipekee.
Tazama video hapo chini

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUSAFIRI NA MTOTO

August 25, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Sidhani kama kuna mtu hajawahi kukumbana na kadhia ya watoto kwenye chombo cha usafiri iwe ni basi, meli, ndege, treni au usafiri binafsi. Ni mara ngapi umewahi kusafiri halafu ukaketi pembeni na mtoto ambaye yeye analia tu safari nzima huku mzazi akiwa hana njia yoyote ile ya kumnyamazisha? Nadhani utakuwa una kumbukumbu nzuri tu ya namna ulivyokwazwa.

Zipo sababu nyingi ambazo husababisha watoto kuwa wasumbufu wakiwa njia na kwa kawaida hiyo ni asili yao kutokana na umri au udadisi walionao. Jumia Travel imemekukusanyia mbinu zifuatazo ili kuzuia hali hiyo kutojirudia tena pindi utakasafiri.      

PROFESA NDALICHAKO AVUTIWA NA KITUO CHA MAFUNZO KWA VITENDO CHA KIKULETWA WILAYANI HAI

August 25, 2017
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.Picha kwa hisani ya ATC

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akipewa maelezo na Mkuu wa Chuo chaUfundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakati ya ziara yake kwenye Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mhandisi Stella Manyanya.

Dk. Kigwangalla azindua zoezi la Uchunguzi wa Saratani ya matiti na shingo ya kikzazi Mkoani Ruvuma

August 25, 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla mapema jana Agosti 24,2017, amezindua rasmi zoezi la upimaji  wa Afya bure  kwa akina mama linalofanyika kwa siku tatu kwenye uwanja wa Majimaji  na maeneo mengine ya Songea  Mkoani Ruvuma.
 Zoezi hilo linaratibiwa na Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma. Kampeni itahusisha upimaji wa Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kisukari, Shinikizo la damu (Hypertension), Magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza na Ugonjwa mengine yakiwemo ya kuambukiza (Kifua Kikuu).
Dk. Kigwangalla  aliwashukuru MEWATA, kwakuwezesha zoezi hilola upimaji Afya bure  ambapo zoezi hilo linaonyesha dhamira ya kuhakikisha kwamba jamii ya Kitanzania inahamasika katika kupunguza tatizo la saratani kwa ujumla, hususani saratani ya matiti na mlango wa kizazi na matiti.
“Nilipopata mwaliko huu wa kuwa mgeni rasmi katika zoezi hili wala sikusita kabisa, nilikubali kwa vile ninafahamu tatizo la saratani kwa wanawake nchini, na mimi pamoja na Waziri wangu Mhe. Ummy Mwalimu ni wakereketwa wakubwa wa Afya ya mama na mtoto, hivi hatutasita kushirikiana na mtu yeyote mwenye nia njema hususan kwenye eneo hili, hapa Nchini kwetu, kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto na vitokanavyo na saratani.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla amebainisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwamo saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa, magonjwa ya figo, seli mundu, na magonjwa ya akili, kwa sasa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa duniani kote na hapa nchini pia. Magonjwa haya huchangia zaidi ya asilimia hamsini ya mzigo wa magonjwa duniani kwa vile husababisha gharama kubwa za matibabu, ulemavu na hata vifo.
“ Tanzania na nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara zina viwango vya juu vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi. Nchini Tanzania, katika saratani zinazo wapata zaidi wakina mama, saratani ya mlango wa kizazi inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti. Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakina mama vitokanavyo na saratani.
 Takwimu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kuwa saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa asilimia 36% (zaidi ya theluthi moja) ya wagonjwa wote wanaohudhuria katika taasisi. Aidha, mnamo mwaka 2005, kulikuwa na wagonjwa wapya 2500, ukilinganisha na wagonjwa wapya 5200 mwaka 2016. Hii inaonyesha dhahiri kuwa wagonjwa wameongezeka kwa asilimia 100% kwa kipindi cha miaka 10. Idadi hii ni kubwa sana, hivyo juhudi na ushirikiano zaidi zinahitajika katika kupunguza vifo hivi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika binafsi kama MEWATA na wengine katika kutoa huduma za uchunguzi wa awali na matibabu.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati akihutibia wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Akielezea kuhusiana na tatizo la kisukari, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, tafiti za ugonjwa wa kisukari zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani. Takwimu za mwaka 2015 kutoka kwenye Atlas ya kimataifa ya Kisukari, zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa milioni 415 duniani kote.  Ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa na wagonjwa milioni 642.
“Katika bara la Afrika kulikuwa na wagonjwa wa kisukari milioni 14.2 mwaka 2015 na idadi hii itaongezeka na kufikia milioni 34.2. Kwa Tanzania mpaka mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 822,880 wa kisukari. Utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini Tanzania ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25-64 wana ugonjwa wa kisukari. Hii inaonyesha ni jinsi gani ugonjwa wa kisukari unavyoongezeka, na namna amabvyo mazoezi haya yatasaidia kwenye juhudi za Serikali za kupambana na magonjwa haya.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wake, Rais wa MEWATA,  Dkt Serafina Baptist Mkuwa, amewataka wanawake mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi  kwenye zoezi hilo ili kubaini tatizo mapema ili kuweza kuchukua hatua.
“Wananchi wa mkoa wa Ruvuma na mikoa yote ya jirani, ni wakati mzuri wa  kuitumia vyema fursa hii muhimu, kuja kujichunguza afya zenu, na zoezi hili ni bure kwa watu wote” alieleza Dk. Mkuwa.
Katika tukio hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Ruvuma Dkt Gosbert Mutayabarwa  Wakuu wa Wilaya za Songea Mjini na vijijini, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mbunge wa Songea Mh, Gama, pamoja na madiwani wote.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi hilo
Rais wa MEWATA,  Dkt Serafina Baptist Mkuwa akimpa maelezo Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati akizunguka kukagua maeneo ya ukaguzi wa upimaji huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi hilo
 
Zoezi hilo likiendelea
Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Madaktari wa MEWATA katika tukio hilo
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha zoezi hilo la upimaji wa Afya bure linaloendelea katika Hospitali ya Peramiho.
 
Dk. Kigwangalla akitoa maelezo wakati wa ukaguzi wa zoezi hilo kwa kituo cha Hospitali ya Paramio