NHIF YATOA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA WA MRADI WA KFW

November 16, 2015
MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU AKIZUNGUMZA WAKATI WA SEMINA YA WATOA HUDUMA KUHUSU NAMNA YA KUWAANDIKISHA WAKINA MAMA WAJAWAZITO KUPITIA SIMU WANAOJIUNGA NA MRADI WA KFW

 













MSAADA WA WASAMARIA WEMA WA MATIBABU UNAHITAJIKA KWA DADA HUYU

November 16, 2015


Ndugu Wasamaria wema
Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital  hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.

JE,UMEJARIBU#RECRUIT ME UNAPOTAFUTA AJIRA TANZANIA?

November 16, 2015

Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi, amani na utulivu.Tanzania, miongoni mwa nchi za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na uwezo wao.

Kutokana na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini.  Matokeo yake ni; kiwango cha umasikini kimeongezeka.

Sababu kuu zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
·         Kutokuwa na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
·         Vijana kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao, hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.
·         Elimu duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweza kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi. Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani katika soko la ajira.
Kutokana na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii wanayoishi.

Kwa hiyo, #RecruitMe kwa makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua fursa mpya zilizopo katika soko la ajira. Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.

Lengo kuu la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli. #RecruitMe itakupatia ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.

Ili kupata huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu. Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA YA CRDB

November 16, 2015

 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja.
 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja
Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki leo sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.

 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto
 Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.
BENKI  ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali yachini, kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.

Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani
Arusha  Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.

Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.

Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo
imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaa karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .

“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons.

Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu. 

Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo
zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .

VIJANA WA TANGA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASILIAMALI KUPITIA AIRTEL FURSA

November 16, 2015


Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga,Hassani Juma Hassani akitoa mada wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.

 Wafanyabishara wadogo na wa kati zaidi ya 300 waliopo katika wilaya mbali mbali mkoani Tanga wameongezewa ujuzi wa elimu ya biashara ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuweza kuongezaza kipato chao na kuchangia pato la taifa.
Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mpango wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo ya ujasiriamali vijana wa manispaa ya Tanga kwa lengo la kuwawezesha kuboresha uendeshaji biashara na kukuza mitaji yao katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP uliopo mkoani hapo.
Akifungua warsha hiyo, meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Tanga Aluta Kweka katika alisema, “lengo letu hasa ni kuwapatia ujuzi vijana wajasiriamali wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ili waweze kufanya biashara kwa tija badala ya kufanya kwa mazoea. Mafunzo haya tunataraji yataongeza tija ya kibiasha ku kuwawezesha Vijana hawa kujenga ajira kwa vijana wengine huku wakichochea upatikanaji wa bidhaa na huduma katika jamii inayowazunguka.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria warsha hiyo wameishukuru Airtel kwa mchakato huo na wameiomba Airtel kuendelea na zoezi hilo kwa wafanyabishara nchi nzima ili waweze kufahamu umuhimu wa kufanya biashara kwa malengo zaidi.
Aisha Mtangi ni mfanyabiashara mdogo anayejihusisha na biashara ya kuuza matunda aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye alisema, “kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi”
“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa Tanga” Alisema Aisha.
Airtel imejipanga kufikia mikoa 10 kote Tanzania hadi kufikia December mwaka huu. Vijana wa mikoa hii watanufaika na mafunzo ya Ujasiriamali na vitendeakazi kwaajili ya kukuza biashara zao.
 Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga, Aluta Kweka akizungumza na wauzaji wa bidhaa za kampuni hiyo wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga,Aluta Kweka akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu semina ya Airtel Fursa iliyofanyika kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.

RC KILIMANJARO,AMOSI MAKALA ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI.

November 16, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Amos Makala akisalimiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akitia saini katika kitabu cha wageni maara baada ya kuwasili katika hosptali ya Rufaa ya Mawenzi mkaoni Kilimanjaro.
Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Hajati, Dkt Mtumwa Mwako akifanya utamburisho wa watumishi wa hosptali hiyo katika ukumbi mdogo wa mikutano hospitalini hapo.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ya mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akizungumza jambo katika kikao cha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala na watumishi wa Hopstali ya rufaa ya Mawenzi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mawenzi Dkt ,Bingilaki Rwezaula (kushoto) akiwa na watumsihi wengine wa hospitali hiyo. 
Katibu wa Hosptali ya Rufaa ya Mawenzi ,Boniface Lyimo akisoma taarifa ya hospitali hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala (hayupo pichani)
Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ,mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na watumishi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea hosptali hiyo.
Badhi ya watumishi katika hospitali hiyo.
RC Makala akizunguza na watumishi.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wzee waliofikisha wagonjwa wao katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo,kushoto ni mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Hajati,Dkt Mtumwa Mwako.
RC Makala akiwajulia hali wagonjwa waliofika katika hospitali hiyo kujipatia huduma ya matibabu.
Mganga Mfawidhi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi,Dkt Bingilaki Rwezaula akimuelekeza maeneo mbalimbali mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala alipotembelea hospitalini hapo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wazee waliofika katika hospitali hiyo kupata matibabu.
RC Makala akitizama hali ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.
RC Makala akitembelea kitengo kinachoshughulika na bima ya afya.
RC Makala akizungumza jambo na mkuu wa idara ya Bima ,Dkt Saganda katika hospitali hiyo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.
Wodi ya kina mama.
RC Makala akisalimiana na mmoja wa wauguzi wa zamu katika hospitali hiyo.
RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya kina baba.
RC Makala akizungumza na madkarai wa zamu katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Majeruhi katika hospitai hiyo.
RC Makala akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Makunga baada ya kupata maelezo toka kwa mmoja wa wagonjwa katika hospitali hiyo namna alivyojeruhiwa .
RC Makala akitoka katika wodi ya wagonjwa wa akili hosptalini hapo.
RC Makala akiwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Mawenzi.
RC Makala akitembelea jengo jipya la wodi ya wazazi linalojengwa katika hospitali hiyo.
RC Makala akiondoka katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo kujionea namna huduma zinavyotolewa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.