BONDIA ALLAN KAMOTE WA TANGA. |
BONDIA DEO NJIKU WA MOROGORO |
ALLAN KAMOTE AKIPIMA UZITO JANA. |
DEO NJIKU NAE AKIPIMA UZITO. |
HAPO KAMOTE NA NJIKU WAKITAMBIANA. |
MRATIBU WA PAMBANO HILO,ABASI MWAZOA. |
BONDIA Allen Kamote wa Tanga ametamba kumtwanga vibaya mpinzani wake Deo Njiku wa Morogoro kwenye raundi ya pili ya pambano lao la kuwania ubingwa wa Dunia WBF litakalokuwa la raundi kumi na mbili lenye uzito wa kg 61 ambalo litafanyika katika uwanja wa Mkwakwani leo.
Pambano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa kumi jioni leo octoba 16 katika uwanja huo ambapo pia kutakuwa na mapambano nane ya utangulizi.
Kamote alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kumaliza kupima uzito katika ukumbi wa CCM Hall jijini hapa na kueleza kutokana na maandalizi ambayo ameyafanya upo uwezekano mkubwa wa kuibuka na ushindi katika pambano hilo ambalo litakuwa na upinzani.
"Njiku namfahamu vizuri sana niliwahi kupambana naye na kumchapa vibaya na hii itakuwa ni mara ya pili kucheza nae,natamka kumwambie nilichokifanya kwenye pambano lililopita kitakuwa zaidi yake "alisema Kamote.
Kwa upande wake,Bondia Deo Njiku alisema atamkalisha chini mpinzani wake huyo katika raundi ya pili katika pambano hilo kutokana na umahiri aliokuwa nao.
“Ninachoweza kusema nimetoka Morogoro kwa lengo moja tu la kuhakikisha nachukua mkanda huo ili kuwapa heshima watu wa mkoa wangu “Alisema Njiku.
Mratibu wa Pambano hilo,Abasi Mwazoa alisema maandalizi yake yanaendelea vizuri na kuyataja mapambano ya utangulzi kuwa ni bondia Rajabu Mahoja wa Tanga ambaye atapanda ulingoni kuzichapa na J.J Ngotiko wa Tanga watakaocheza pambano la raundi kumi lenye uzito wa kg 57.
Mwazoa aliongeza kuwa bondia Khamis Mwakinyo wa Tanga atazichapa na Haruna Magali wa Morogoro katika pambano la raundi sita lenye uzito wa kg 64 wakati Saimon Zabron na Mohamed Kibari wote wa Tanga watachuana kwenye pambano la raundi sita lenye uzito wa kg 61.
Aliyataja mapambano mengine kuwa ni bondia Said Mundi wa Tanga atazichapa na David Maina wa Kenya katika pambano la raundi sita lenye uzito wa kg 61 ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Pambano mengine yatakuwa ni bondia Zuberi Kitandula wa Tanga atazichapa na Hajji Juma wa Tanga katika mpambano utakaokuwa wa raundi nane lenye uzito wa kg 55 huku Jumanne Mohamed wa Tanga atapanda ulingoni kuzichapa na Obote Ameme wa Dsm wataocheza pambano la raundi nne lenye uzito wa kg 57.
Mratibu huyo alilitaja pambano la mwisho la utangulizi litakuwa ni kati ya bondia Alli Boznia wa Kenya ambaye atazichapa na Jacob Maganga wa Tanzania litakalokuwa la raundi nne lenye uzito wa kg 69.