LG YATOA PUNGUZO KABAMBE LA BEI YA BIDHAA ZAKE KIPINDI HIKI CHA RAMADHANI NA SABASABA

LG YATOA PUNGUZO KABAMBE LA BEI YA BIDHAA ZAKE KIPINDI HIKI CHA RAMADHANI NA SABASABA

July 01, 2015
IMG_5470
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer akipokea taarifa ya shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” kwa mmoja wa maafisa wa kampuni ya bidhaa za LG Tanzania ambapo kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish”.
2
Mmoja wa wakurugenzi wa LG toka Korea, Bw. Billy Kim (Kulia) akizindua rasmi friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish” katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” anayeshuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer.
IMG_5552
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG Tanzania, Bi. Elizabeth Morris (katikati) akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari hawapo pichani aina mpya ya friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish” wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya, katika viwanja vya maonyesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. Kulia ni Mkurugenzi wa LG, Mohan Kumar na mmoja wa wakurugenzi wakuu wa LG toka Korea Bw. Billy Kim pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer (wa pili kushoto).
Na Modewjiblog team
Kampuni ya LG Tanzania imetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei za bidhaa zake, itakayodumu katika kipindi chote cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ikiwa ni kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Meneja mwandamizi wa LG, Bw. Kim Taehoon amesema wateja watakaonunua bidhaa za LG katika kipindi hiki cha Ramadhani na Sabasaba watafurahia punguzo la bei la hadi asilimia 15, pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo zawadi za bure.
Bw. Kim pia ametumia fursa hiyo kuitambulisha friji mpya za LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia” na “Coral Irish” kwa mara ya kwanza kabisa katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini.
Amesema friji hizo zina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa kuzuia bakteria na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama wa kiafya.
Friji hizo zina makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, ambapo aina hiyo ya milango huja pamoja na kioo imara.
Amesema friji hizo zinatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter Compressor” ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Bw. Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hizo mpya zilizoingia sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na uwezo wa friji hizo,
Amesema kuwa Friji hizo pia zitapatikana katika maduka mengine yote yanayouza vifaa vya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani, watu wengi hutunza vyakula vyao kwenye friji na ni hulka ya wengi kuamka usiku kwa ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa na manufaa sana kwao, kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia kutunza chakula katika hali ya usalama.
Ofa hizi zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na Sabasaba, hii ni katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia bidhaa za LG zenye punguzo la bei
Bw. Kim Taehoon amesisitiza kuwa kampuni ya LG Electronics daima inaendelea kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa zenye ubora na muonekano yakinifu, ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa.
Amesema toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya sokoni ni muendelezo wa matoleo ya teknolojia, ambayo yanatengenezwa na kuboreshwa kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja.
IMG_5580
5
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ubora wa kompresa za friji za kampuni ya LG ambazo ni imara na zinahimili hali ya hewa ya mazingira yoyote wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya katika viwanja vya maonyesho vya sabasaba.
IMG_5657
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) bidhaa nyingine za LG ambazo zipo kwenye ofa ya punguzo la bei la asilimia 15 katika msimu huu wa sabasaba na Ramadhani ndani ya banda la MeTL Group.
IMG_5663
Waandishi wa habari wakiangali moja ubora wa TV za LG kwa kutumia miwani ya 3D inapoivaa inakuonyesha uhalisia wa picha unayoitaza kwa ukaribu zaidi wakati uzinduzi wa moja ya bidhaa za LG katika banda la kampuni ya MeTL Group kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5610
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akimkabidhi zawadi kutoka MeTL, Mkurugenzi wa kampuni ya LG toka Korea, Bw. Billy Kim mara baada ya uzinduzi huo katika banda la MeTL Group.
IMG_5618
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akiendelea na zoezi la kukabidhi zawadi kwa maafisa wa kampuni ya LG Tanzania.
IMG_5647
Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kutembelea banda la LG na kununua bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali juu na zipo katika punguzo la bei la asilimia 15 ya kila bidhaa katika kipindi hichi cha sabasaba na mwezi huu wa Ramadhani.
IMG_5620
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo. Wa tatu kulia ni Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi.
IMG_5468
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya LG Tanzania na MeTL Group wanaotoa huduma kwenye cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

TEMBELEA OFISI YA GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) ILIYOPO SABA SABA UJIPATIE NAFASI YA KUSOMA CHUO NJE YA NCHI

July 01, 2015
Muonekano wa Ofisi ya Global Education Link iliyopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Haroun Weggoro akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Makungu Joseph akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao  iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Kantante Cornerio akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (Kushoto) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, David Nsimba (katikati) wakizungumza na mteja aliyewatembelea ofisini kwao katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wafanyakazi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Doreen Luzuki akiwakaribusha wateja walitembelea ofisini kwao katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Global Education Link wakiwa na nyuso za furaha kusubiri wageni.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI NDANI YA SABASABA, KARUME HALL

UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI NDANI YA SABASABA, KARUME HALL

July 01, 2015
IMG_5730
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_5736
IMG_5779
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyetembelea la Umoja huo jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania.
IMG_5793
Laurean Kiiza (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akimsimia Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige kuwasilisha maoni (GeoPoll) yake moja kwa moja kwenye simu ya kiganjani, alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5772
Mdau wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Lemmy Hipolite (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, jinsi alivyowezeshwa na Umoja huo kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5710
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akionyesha baadhi ya kazi zake kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5764
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali yaliyofanikiwa katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDAP) kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa na kutaka kufahamu shughuli mbalimbali za UN Tanzania.
IMG_5744
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimkabidhi makabrasha na vipeperushi mbalimbali vya Umoja Mataifa, Mwandishi wa Michuzi blog, Chalila Kibuda aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesha ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5701
Sophia Mataro (wapili kushoto) kutoka Shirika la UNESCO Tanzania, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa mmoja wa wananchi alitembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5717
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na kituo cha Televisheni cha Channel Ten kilichotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5802
Timu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa "Delivering as One" wanaotoa huduma kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama “Sabasaba” yanayoendelea kurindima jijini Dar es Salaam.
IMG_5738
Muonekano wa nje wa banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Modewji blog team
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28, huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Aidha, katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha, maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.

LOWASSA ARUDISHA FOMU LEO MJINI DODOMA, ATEMA CHECHE KWA WANAOMTUHUMU

July 01, 2015

WAZIRI Mkuu Mstafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

 Mh. Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya saa 8:30 mchana wa leo Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi. 

Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni  kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.

 "Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.  Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini.

 Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akizipanga vyema fomu zake ili azikabidhi kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi (kushoto), wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amerudisha fomu hizo, baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, ambapo jumla ya WanaCCM 874,297 walimdhamini.Kushoto kwa Mh. Lowassa ni Mkewe, Mama Regina Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi fomu za wanaCCM waliomdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kurudisha fomu za wanaCCM waliomdhamini ili apare baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

NYUMBA YATEKETEA TANGA BARABARA YA 13

July 01, 2015


 Wakazi wa Ngamiani kati Tanga, wakishuhudia uzimaji moto wa  nyumba  barabara ya 13 mtaa wa makoko iliyoungua na kuteketeza mali zote za ndani na chanzo kudaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.