"WAZIRI UMMY AIPIGA TAFU KLABU YA AFRICAN SPORTS"

January 25, 2018
Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kushoto akimkabidhi unga nahodha wa timu ya African Sports ambapo kiongozi huyo alitoa mchele kg100,unga wa sembe kg 100,Ngano kg 50,maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi ,sabuni na dawa za meno
Sehemu ya vitu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
 Katibu wa Klabu ya African Sports,Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi
 Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga aliyevaa kofia kushoto akiteta jambo na viongozi wa klabu ya African Sports mara baada ya kukabidhi msaada huo
 Katibu wa Klabu ya African Sports Ismail Mosoud kulia akimshukuru Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kwa msaada waliotoa
Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi salehe mara baada ta kukabidhi msaada huo
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MBUNGE wa Viti Maalumu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu leo amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.

Msaada huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika ndani ya wiki mbili.

Miongoni mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg 50,Unga wa sembe kg 100,Maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy ,Kilenga aliwaambia wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.

Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .

Naye kwa upande wake,Katibu wa timu ya African Sports,Ismail Masoud alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.

Alisema mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu hiyo kwani ni ya wananchi.

"Tanga ina enye ,na enye ni sisi,Shime wana Tanga'Tanga Kwanza.

Waziri Ummy Mwalimu azindua jengo la Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania

Waziri Ummy Mwalimu azindua jengo la Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania

January 25, 2018
index
Kibaha. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu amesema serikali inafanyia kazi mkakati mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa kada ya afya wanaosoma katika ngazi ya cheti na astashahada.
Waziri Ummy ameyasema hayo jana wakati akizindua jengo la Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania lililopo Halmashauri ya mji Kibaha, mkoani Pwani.
Alisema kundi hilo ni muhimu linalopaswa kuangaliwa kwa jicho la pili, kwani ndilo linalotoa huduma kwa ukubwa wake katika sekta ya afya.
“Nipo katika mazungumzo ya awali na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kuangalia ni namna gani tutaiwezesha tasnia hii ikue ili tupate watumishi wengi zaidi wenye viwango, maana mzazi ataweza kulipa ada litakapofikia suala la chakula na mengineyo inakuwa shida,” alisema.
Alisema watumishi wa ngazi za uuguzi na ukunga wenye ujuzi na weledi wa kutosha pekee wanachukia takribani asilimia afya 60 ya watumishi wote wa afya nchini.
“Shirika la Afya duniani (WHO)  linasema kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya huduma zote za afya hutolewa na wauguzi na wakunga, hivyo mimi binafsi, Wizara yangu na Serikali kwa ujumla tunaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha huduma za uuguzi na ukunga nchini zinaimarika vya kutosha,” alisema.

MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA MAZISHI

January 25, 2018

Waombolezaji wakiwa wamebeba  jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018.

 Marehemu Lulu  Sylvester Mattunda Lema.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


 Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Barabara ya Tanga






 




Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
 Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo

 Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza  jambo baada ya mwili wa  marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi yanayofanyika leo  Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza, Profesa Lema
pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana, wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu
wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba

kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani
pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali  afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.

-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

DC MJEMA, AKAGUA UKARABATI MAJENGO SHULE ZA JANGWANI NA AZANIA, LEO. WALIMU NA WANAFUNZI WAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI, WASEMA AKIAHIDI ANATEKELEZA

January 25, 2018

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekonari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
 Mkuu wa shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akimpokea DC Mjema kuka alipowasili kwenye shule hiyo. 
 Mkuu wa Shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akieleza taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo ulipofikia sasa ambapo amesema umekamilika kwa kiasi cha asilimia 90. Kulia ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo na katikati DC Mjema
Ofisa wa Wakala wa majengo akimpatia maelezo DC Mjema kuhusu mradi huo wa ukarabati wa vyoo kwenye majengo ya shule ya jangwani. Kulia ni Edward Mpogolo
Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema (kushoto) akizunguma alipokuwa akikagua chumba cha darasa kilichokarabatiwa
Mwalimu wa somo la fizikia wa kidato cha nne Felix Sameli akifundisha darasani muda mfupi kabla ya DC Mjema kuingia katika darasa la kidato hicho.
DC Mjema (kulia) akisalimiana na wanafunzinwa Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Jangwani akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya ukaranbati wa majengo
DC Mjengwa akiwa na mwanafunzi wa kidato hicho  sabrina Saidi ambaye alikuta anakaa kwenye dawati alilokuwa akitumia wakati wakisoma katika shule ya Jangwani zaidi ya miaka 30 iliyopita.
DC Mjema akiwaonya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Jangwani kutojiingiza katika mambo ya utukutu ikiwemo kupata mimba wakiwa bado masomoni na badala yake wazingatie masomo kwa bidii.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa shule hiyo kukagua mabweni ya wasichana yaliyokarabatiwa.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekonari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
DC Mjema akihoji jambo alipokagua vyoo ambavyo ukarabati wake unaendelea katika shule hiyo.
"Hivi hii milango metengenezwa kwa mbao aina gani?" DC Mjema akahoji alipokagua ukarabati wa vyoo katika shule hiyo.
DC Mjema akijaribu kuhakikisha kama maji yanatoka kwenye bafu alipokagua ukarabati wa vyoo kwenye eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akionyeshwa sehemu ya wanafunzi kulia chakula ambayo bado ukarabati wake haujakamilika katika shule hiyo ya Jangwani.
baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wakiwa darasani katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema kabla ya kuondoka akakagua ukarabati wa chumba cha maabara katika shule hiyo
"Sasa chumba kama hiki cha maabara kinatakiwa kuwa na umeme muda wote" akasema DC Mjema.
DC Mjema akisonga mbele na msafara wake.
Ofisa wa wakala wa Majengo akitoa maelezo ya mwisho kabla ya kuondoka DC Mjema kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akizungumza na waandishi wa habari alichoshuhudia na maoni yake baada ya kukagua ukarabati wa majengo kwenye shule hiyo ya Jangwani. " Nimerishwa sana na ukarabati uliofanyika, Walimu, wafanyakazi wa kawaida na wanafunzi hakikisheni mnaitunza miundo mbinu hii ilivyokarabatiwa na kuwa mizuri. namshukuru na kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake wa kuielekeza serikali kukarabati shule hizi" Alisema DC Mjengwa.
DC Mjengwa akizungumza na wanafunzi aliowakuta wakijisomea kwenye viwanja vya shule ya Jangwani wakati akienda shule ya Azania kuendelea na ukaguzi wa ukarabati wa majengo pia katika shule hiyo.
DC Mjema akizungumza na wanafunzi katika shule ya Azania.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa Shue ya Azania Erasto Gwimile (kushoto), kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati katika shule hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (katikati) akiinama wakati wakienda kukagua ukarabati katika moja ya madarasa ya shule hiyo ya Azania.
DC Mjema akikagua vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shue hiyo ya Azania.
DC Mjema akizungumza wakati akikagua mabweni katika shule hiyi=o ya Azania. Alishauri kuwekwa milango ya dharula kuwezesha wanafunzi kutoka kwa urahisi wakati wa majanga kama ya moto, badala ya kutegemea kutoka katka milango yenye vizuizi vingi kama mageti.
DC Mjema akimpa pole mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Azania Enock Michael ambaye alimkuta amelala bwenini kutokana na kuwa na homa.
Mkuu wa shule ya Azania akitoa maelezo kuhusu ukarabati wa moja ya vyumba vya madarasa.
DC Mjema na msafara wake wakiendelea na ukaguzi
DC Mjema (kulia) akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya Azania aliowakuta wakifanya kazi zao nje kutokana na ofisi zao kuwa katika ukarabati.
DC Mjema akiwa katika chumba cha darasa kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Azania. Kulia ni Edward Mpologo na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Erasto Gwamile.
Wanafunzi wakiwa wamesimama kumlaki DC Mjema
Wakishangilia baada ya kuambiwa wakae.
DC Mjema akizungumza nao
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Azania Goodlove Kapufi akizungumzia ukarabati wa majengo ya shule yao. " kwa niaba ya wenzangu tunamshukuru sana Rais Dk Magufuli kwa kuelekeza ukarabati huu ufanyike, tunasema asante sana," alisema. Makamu huyo wa Rais.
Katibu Tawala wa Ilala akimsalimia Makamu huyo wa Rais wa Serikali ya Wafnafunzi wa shule ya Azabia
Mkuu wa Shule ya Azania Erasto Gwimile akisoma taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule, alisema ukarabati ulichelewa kukamilika kwa wakati hivyo kusababisha shule kuhelewa kufunguliwa.
DAS wa Ilala Mpogolo akiwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania.
Mkuu wa Shule ya Azania akimshukuru DC Mjema kwa kutembelea shule yao
DC Mjema akizungumza na baadhi ya wanafunzi za shule ya zanaki wakati ameketi nao kwenye dawati