WAANDISHI WA HABARI WAPATA SEMINA KUHUSU MAHINDI YA GMO NA MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA KATIKA KILIMO

January 24, 2017
 Mshauri mstaafu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk.Nicholas Nyange, akitoa mada kwa waandishi wa habari kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika matumizi ya kilimo walipotembelea kituo cha utafiti wa kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma.
 Mshauri mstaafu wa mradi wa kuzalisha mahindi yanayostahimili ukame kupitia mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya akitoa mada kuhusu mahindi hayo yanayotokana na teknolojia uhandisi jeni (GMO) kuhusu mafanikio ya mradi huo na changamoto zake.
 Wanahabari wakiwa nje ya lango kuu la kuingia katika shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia ya GMO la Makutupora mkoani Dodoma wakisubiri taratibu za kuingia kwenye shamba hilo.
 Mtafiti Ismail Ngolinda wa Kituo hicho (kushoto), akitoa maelekezo kwa wanahabari kabla ya kuingia katika shamba hilo la majaribio.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
  Mtafiti Ismail Ngolinda akiwaonesha wanahabari mahindi yaliyooteshwa kutokana na teknolojia hiyo ya GMO.
Wanahabari kutoka mikoa 7 wakiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo mbele ya shamba hilo.

BIASHARA 5 UNAZOWEZA KUZIFANYA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUKUINGIZIA KIPATO

January 24, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Kuishi katika jiji kubwa kama vile Dar es Salaam kuna changamoto nyingi endapo hauna shughuli maalum ya kukuingizia kipato cha kila siku. Na ili kufanikiwa katika hilo basi huna budi kuwa mwerevu wa kugundua ni biashara ipi ukiifanya itakuwa inakuingizia kipato cha haraka.

KONGAMANO LA MAASKOFU WA JUMUIYA YA AGAPE WUEMA LAFANYIKA JIJINI MWANZA

January 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonald Masalle, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, akifungua Kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni Agape WUEMA kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika kwa siku mbili (leo na kesho) Jijini Mwanza.

Kongamano hilo limelenga kujadili na kuazimia mgawanyo wa ujenzi wa miradi ya jumuiya hiyo katika nchi sita za Afrika Mashariki na Kati (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Kongo) ambayo ni pamoja na Makanisa, Shule na Hospitali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mataifa husika.
Aliyesimama kulia ni Askofu Mkuu wa Agape WUEMA barani Afrika, Mande Wilson, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Tanzania, Martin Gwilla, akizungumza kwenye kongamano hilo
Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati
Binagi Media Group
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.

Hayo yamebainishwa katika risala yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masalle kwenye ufunguzi wa kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni AGAPE WUEMA kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika Jijini Mwanza.

Amesema serikali inaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na jumuiya hiyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi yake nchini ikiwemo ujenzi wa makanisa, shule pamoja na hospitali.

Askofu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Gwila, ameishukuru seikali kwa ushirikiano wake ikiwemo kuruhusu ujenzi wa miradi iliyokusudiwa ambapo ameomba ushirikiano huo kuwa endelevu kwani miradi hiyo itaongeza chachu ya maendeleo katika jamii.

Askofu Mkuu wa Jumuiya ya AGAPE WUEMA barani Afrika, Mande Wilsoni, amebainisha kwamba kongamano hilo lililowakutanisha zaidi ya Maaskofu 170 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati limenga kuhakikisha ugawaji na utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa unaanza mapema mwaka huu.

MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

January 24, 2017

Na Woinde Shizza,Arusha

Mfanya biashara maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance  Moshi
(30) amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi  inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesh mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa
yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya  .
Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa
mahakamani.

Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha . 

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february  6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.

Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNEP

January 24, 2017


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 2.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye ameongozana na ujumbe wake kwa ziara ya siku 2 wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Faustine Kamuzora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim na ujumbe wake .
Picha ya pamoja

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini ambao umepelekea mamia ya ekari za misitu kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo mpango wa upandaji wa miti kote nchini lakini bado msaada na nguvu zaidi inahitajika kutoka shirika la Mazingira la UNEP ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo nchini.

Amesema Tanzania ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Shirika la UNEP ambapo shirika hilo limeweza kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya kuhifadhi mazingira hivyo mahusiano hayo mazuri ni muhimu yakaja na mbinu bora na nzuri za kuhifadhi mazingira ili kuokoa Taifa lisigeuke jangwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini.

Makamu wa Rais pia amehimiza wataalamu wa mazingira wajikite zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi watumie nishati mbadala kama gesi na makaa ya mawe ili kudhibiti tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ERIC SOLHEIM amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kusisitiza kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali Tanzania katika Uhifadhi wa mazingira nchini.

Mkurugenzi huyo amesema suala la kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira sio la Serikali pekee hivyo ni muhimu kwa Serikali kushirikiana ipasavyo na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na tatizo ili kupata suluhu ya kudumu.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa UNEP hapa nchini ni fursa ya kipekee ya kufungua na kuimarisha ukurasa mpya wa mahusiano kati ya Tanzania na UNEP.

Makamba amesema kuwa Serikali imetengeneza programu mpya Tano za mazingira ikiwemo kupunguza matumizi ya mkaa ili kuhifadhi misitu,vyanzo vya maji,kushughulikia taka na kujenga uwezo kama hatua mpya kabisa ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.
MECHI ZA KESHO AZAM SPORTS FEDERATION CUP

MECHI ZA KESHO AZAM SPORTS FEDERATION CUP

January 24, 2017
Mechi za raundi ya tano ya mechi za Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), zitaendelea kesho Jamatano Januari 25, 2017 kwa timu za Singida United na Kagera Sugar kucheza kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za The Mighty Elephant ya Songea na Mashujaa ya Kigoma katika mchezo utakaofanyika Uwanja Majimaji mjini Songea.
Katika mchezo huo ambao uliahirishwa Jumatano iliyopita, mshindi wa kesho ndiye atacheza na Majimaji katika tarehe mpya itakayotangazwa hapo baadaye kama ilivyo kwa mechi kati ya African Lyon na Mshikamano.
Leo Jumanne Januari 24, mwaka huu kuna mechi kati ya Mtibwa Sugar na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Pia Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

WANAHABARI WATEMBELEA SHAMBA LA ZABIBU KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO MAKUTUPORA DODOMA

January 24, 2017
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la utafiti wa zabibu katika Kituo cha Utafiti  wa Kilimo Makutupora mkoani Dodoma leo.
 safari kuelekea shamba la zabibu ikiendelea.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zabibu kwa wanahabari. Kushoto Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle na kulia ni Mtafiti Andekelile Mwamahonje.
 Wanahabari wakiwa katika shamba hilo.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akionesha mche wa zabibu uliostawi vizuri.
 Wanahabari wakiangalia shamba hilo.
Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zao la zabibu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na Dotto Mwaibale, Dodoma

VIJANA wametakiwa wajiunge kwenye vikundi na kuanzisha mashamba ya kilimo cha zabibu ili wajipatie kipato badala ya kukaa vijiweni.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso wakati akizungumza na wanahabari waliotembelea shamba la zabibu katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.


"Mwito wangu kwa vijana waanzishe vikundi vitakavyoweza kuwasaidia kuanzisha mashamba ya zabibu ili wajiongezee kipato mikopo ya kuwezeshwa ipo" alisema Mroso.

Alisema mtaji wa kuanzisha shamba la zabibu ni kuanzia sh. milioni tatu hadi nne ambapo baada ya miaka mitatu au minne mkulima anaanza kunufaika na kilimo hicho.

Alisema katika kuinua pato la taifa na la mtu mmoja mmoja serikali imeaanzisha mashamba ya zabibu maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino kuna shamba la ekari 296, katika Kijiji cha Kamaiti wilayani Bahi kuna shamba la ekari 170 na Manispaa ya Dodoma katika Kijiji cha Gawaye kuna ekari 100 ambapo kila mwananchi hasa vijana wamepatiwa ekari moja kuziendeleza.

Alitaja aina za zabibu zinazolimwa katika maeneo hayo kuwa ni za mezani, mvinyo na kukausha ambazo soko lake linapatikana wakati wote.


MATUKIO MBALIMBALI YA LIGI KUU YA VODACOM

MATUKIO MBALIMBALI YA LIGI KUU YA VODACOM

January 24, 2017
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemwondoa Mwamuzi Hussein Athuman kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) baada ya kupata alama za chini ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha Ligi hiyo.
Mwamuzi Hussein Athuman kutoka Mkoa wa Katavi alichezesha mchezo namba 150 uliozikutanisha timu za Majimaji ya Songea na Young Africans ya Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika Young Africans imepigwa faini ya jumla ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yao kutoingia vyumbani, na pia kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14 (13) na (14) ya Ligi Kuu. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
Mwamuzi Ngole Mwangole: Mwamuzi huyo wa kati, Ngole Mwangole wa Mbeya amepewa barua ya onyo kali na kumtaka aongeze umakini wakati akichezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Licha ya kujitetea, lakini kamati haikuridhika na maelezo yake. Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa Bw. Mwangole alikuwa Mwamuzi Bora wa msimu uliopita (2015/2016) na hiyo ndiyo mara yake ya kwanza kuonekana kufanya uamuzi uliokosa umakini wakati akichezesha, TFF imeamua kumpa onyo.
Mechi namba 141 (Mwadui FC vs Kagera Sugar). Beki wa Kagera Sugar, Godfrey Taita anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kuwavamia waamuzi baada ya mechi na kuwatolea lugha chafu na vitisho kabla ya benchi la ufundi la timu yake pamoja na askari polisi kuingilia kati na kudhibiti kadhia hiyo.
Mechi namba 151 (Mtibwa Sugar vs Simba). Baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari. Pia kamera ya Azam Tv upande wa goli la Kusini iliangushwa na washabiki hao.

Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia

January 24, 2017


Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
WATANZANIA waishio nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamoja na kuangalia namna ya kutekeleza kiu ya nchi ya viwanda kama ilivyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, mwenye suti nyeusi, akifurahia jambo ofisini kwa Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten, alipofika ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo hija ya mwaka huu wa 2017.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, hayupo pichani walipokutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuangalia fursa za kimaendeleo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mjini Jeddah, Saudi Arabia na Balozi wa Tanzania nchini hapa, H.E Hemedi Mgaza, alipofanya kikao na Watanzania waishio nchini hapa kama njia za kushirikiana na wadau hao kwa ajili ya kupeleka maendeleo ya uhakika nchini Tanzania na kuisimamia kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Akizungumzia juu ya fursa ya uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Mgaza alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa nafasi yake kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao. Alisema mbali na Watanzania hao kuwekeza kwao kama uwezo wanao, pia wanaweza kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa ajili ya kuchangia fursa hiyo ya watalii inayolipa duniani kote.
Kikao kinaendelea.

Kikao kinaendelea.
“Tukitoka hapa kila mmoja awe balozi shupavu wa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania ili pamoja na mambo mengine, tuwe tumechangia ukuzaji wa uchumi wetu kulingana na uwezo wetu kwa kupitia sekta nyeti ya utalii, ambapo pia kama sehemu ya serikali nilisikiliza maoni na ushauri wao ili tusonge mbele..

“Tuonyeshe mazuri ya nchi yetu pamoja na sisi wenyewe kushiriki katika fursa za kiuchumi kuliko kusubiri wengine wafanye wakati tunajua fika kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuiletea maendeleo nchi yetu,” alisema Balozi Mgaza.

Kabla ya kikao hicho na Watanzania, Balozi Mgaza pia alifanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo, H.E Mgaza alijadiliana na Dr. Benten masuala mbalimbali yanayohusu maandalizi ya ibada ya Hijja ya mwaka 2017 na fursa kwa mahujaji wa Tanzania.