RAIS DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA BUKOBA MJINI, MULEBA NA MUGANZA MKOANI GEITA

RAIS DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA BUKOBA MJINI, MULEBA NA MUGANZA MKOANI GEITA

January 02, 2017
bk
bk-1
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Bukoba mjini mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera.
bk-2
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Muleba mkoani Kagera mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
bk-3
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Muganza Wilayani Chato mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
AZAM FC YAANZA VYEMA MAPINDUZI CUP YAILAZA ZIMAMOTO SC

AZAM FC YAANZA VYEMA MAPINDUZI CUP YAILAZA ZIMAMOTO SC

January 02, 2017
azam-vs-kagera-4
Timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam imeanza vyema michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuwanyuka wenyeji Zimamoto goli 1-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Amani na ukiwa mchezo wa kwanza wa Kundi B.
Kipindi cha kwanza hakuna aliyeweza kumtambia mwenzake baada ya kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa kutokana na timu hizo kucheza mchezo kwa kutegeana huku Zimamoto wakikosa nafasi nyingi za wazi.
Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikiamini kutoka na pointi tatu muhimu kutokana na kupewa maelezo toka kwa makocha wao na pia zikifanya mabadiliko ya kuongeza nguvu hata hivyo mabadiliko hayo yaliwasaidia Azam FC.
Akitokea benchi Mshambuliaji Kinda Shaaban Idd alifunga goli dakika ya 79 baada ya kumpiga kanzu mlinda mlango wa Zimamooto SC na kuiandika bao safi na kumnyanyua benchini kaimu kocha wa Azam FC Idd Nasor Cheche kwa furaha.
Dakika 87 Nyange Othumani aliinyima goli la wazi la kusawazisha Zimamoto baada ya kupokea safi huku akibaki yeye mwenyewe  Aishi Manula na kupiga shuti lake nje ya lango hadi mwamuzi anamaliza Mpira Azam Fc wameibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuongoza kundi B.
Huu ni ushindi wa pili kwa kaimu kocha wa Azam FC Idd Nasor Cheche baada ya kupokea mikoba toka kwa Wahispania ambao walitimuliwa na mchezo wake wa kwanza ulikuwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baina ya Tanzania Prisons ambapo Azam FC waliibuka na ushindi wa goli moja mfungaji akiwa ni John Bocco
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Visiwani humo ni ule wa usiku saa 2:30 ambapo bingwa Mtetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga watatupa karata yao ya kwanza kucheza na Jamhuri toka visiwani Pemba.
RAIS DKT MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI KAGERA

RAIS DKT MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI KAGERA

January 02, 2017
magu0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu  Januari mbili, 2017 amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundo mbinu iliyoathiriwa na tetemeko hilo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo  Omumwani iliyobomolewa na tetemeko la ardhi la Septemba 10,2016.
Mara baada ya ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ihungo na kuagiza kuvunjwa kwa kamati ya maafa ya Mkoa huo iliyokuwa ikiratibu utoaji wa misaaada na kufanya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.
”Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho wake ukiwa na harusi huwa kuna kamati ya harusi,ukishamaliza kufunga ndoa kamati ya harusi huwa inavunjwa,na ukiwa kwenye msiba huwa kuna kamati ya msiba na msiba  mkishazika kamati ya mazishi huvunjwa,kamati ya maafa ya Kagera huu ni mwezi wa tano na inawezekana hata kwenye kamati huwa wanalipana posho,sasa nataka hii kamati nayo iishe,yalishapita yamepita”
Aidha Dkt Magufuli amewataka wote walioahidi kuchangia katika kamati ya tetemeko la ardhi ya mkoa wa Kagera ambao bado hawajatekeleza ahadi zao ambazo ni jumla ya shilingi bilioni nne nukta tano wakamilishe ahadi hizo ili ziweze kumalizia miundombinu ya Serikali iliyoathiriwa na tetemeko hilo.
Ameongeza kuwa wale wote wanaoendelea kuguswa kusaidia wapeleke michango yao moja kwa moja kwa wananchi badala ya kuipeleka serikalini kwa kuwa hakuna mchango mwingine utakaopokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Pia Rais Dkt Magufuli ameagiza shule ya Sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na Jumuia ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imilikiwe na Serikali kutaka wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo kutolipa ada kama zilivyo shule nyingine za serikali.
Dkt Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kupunguza utitiri wa kodi katika zao la kahawa ili bei ya zao hilo ipande na kuwanufaisha wakulima
Balozi wa Uingereza hapa Nchini Bi Sarah Cooke ambaye nchi yake imechangia kiasi cha shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ihungo, amempongeza Rais Dkt Magufuli na serikali yake kwa jitihada za kupambana na rushwa suala ambalo nchi yake ya Uingereza inalipa kipaumbele sambamba na kutoa elimu bila malipo jambo linalowawezesha watoto wengi wa kitanzania kupata elimu bure
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
02 Januari, 2017
KOCHA SALUM MAYANGA

KOCHA SALUM MAYANGA

January 02, 2017
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda  (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MAJIMAREFU KAIRUKI HOSPITALI

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MAJIMAREFU KAIRUKI HOSPITALI

January 02, 2017
maji-mare
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini  Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.

RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA MAENEO YALIOATHIRIKA NA TETEMEKO NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO MKOANI KAGERA

January 02, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

SERIKALI KULIPA DENI LA WALIOTHIRIKA NA WANYAMAPORI - MHANDISI MAKANI

January 02, 2017


Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akikagua moja ya shamba la mahindi lililoharibiwa na tembo katika kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda Mkoani Mara jana  wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda, mkoani Mara jana alipotembelea moja ya shamba la mahindi lilioharibiwa na tembo wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.


NA HAMZA TEMBA - WMU
.......................................................
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema italipa madeni yote ya miaka ya nyuma ya vifuta jasho na vifuta machozi ambayo inadaiwa na wananchi waliokubwa na vitendo vya uharibifu wa wanyamapori nchini kabla ya bunge lijalo la bajeti, madeni hayo ni yale ambayo yameshaifikia wizara hiyo na kuhakikiwa. 

Akizungumza jana na uongozi wa wilaya ya Bunda wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku moja ya kufuatilia changamoto za uhifadhi wilayani humo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema uamuzi huo wa Serikali utaondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamepata madhara mbalimbali ya wanyamapori ikiwemo vifo, majeruhi, kuliwa mazao na kuharibiwa mashamba yao. 

"Serikali ya awamu ya tano imeshakamilisha takwimu za madai, yale yote tunayodaiwa huko nyuma, yaliyoifikia Wizara yakafanyiwa uhakiki na nimesema kwenye uhakiki huo ndani ya kipindi cha miaka kumi, kwa wilaya zaidi kidogo ya 80 ambazo ndizo zina changamoto hizi kwa kiwango kikuu, deni jumla ni shilingi 2,081,532,700 (bil. 2.9)", amesema. 

Amesema wilaya ambazo zimeathirika zaidi na vitendo hivyo na ambazo madai yao ni makubwa zaidi ya Wilaya zingine ni Serengeti na Bunda ambazo ziko mkoani Mara na zinapakana na Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Ziwa Victoria, Pori la Akiba Grumeti na Ikorongo. "Serengeti ndiyo inayoongooza kwa madai hayo, shilingi milioni 408,547,600 alafu Bunda shilingi milioni 265,969,750",. 

Pamoja na Serikali kujiwekea utaratibu huo na wananchi wa kulipa vifuta jasho na vifuta machozi kwa waathirika, amesema ipo haja ya kutafuta njia endelevu ya kukabiliana na changamoto hizo na fedha ambayo ingetumika kulipia fidia hizo ikatumika kuwezesha mpango huo endelevu. Amesema mpango huo utawezekana kwa kuwashirikisha wananchi.

"Mpango endelevu wa kukabiliana na changamoto hiyo ni ule wa ushiriki wa pamoja wa Serikali na wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uharibifu dhidi ya wanyamapori", amesema. 

Ili kufanikisha mpango huo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Bunda na Serengeti kuratibu ushiriki wa wananchi wao katika zoezi hilo kwa kuunda vikundi shirikishi katika kila kijiji, kubaini mahitaji yake ikiwemo vifaa na kuwasilisha taarifa hiyo wizarani kabla ya tarehe 15 januari mwaka huu, kwa ajili ya hatua zaidi za kufanikisha mpango huo. 

Amesema ushirikiano huo pekee hautoshi kukabiliana na changamoto hizo kama wananchi nao hawataipunguzia mzigo serikali wa kupambana na vitendo vyao viovu dhidi ya uhifadhi, ili nguvu hiyo itumike katika kushirikiana nao kwenye ulinzi dhidi ya wanyama waharibifu. "Wananchi waache vitendo viovu dhidi ya uhifadhi, ujangili, kuua wanyamapori",. 

Ameeleza kuwa miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa changamoto hizo ni matokeo ya tabia za wananchi kusogelea maeneo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu, jambo ambalo lina athari kubwa katika uhifadhi na usalama wa wananchi wenyewe, hivyo ni lazima liepukwe.

"Njia ambayo tembo alikua akipita miaka 20, 30, 40 ndo anapita kila siku, sisi tumeenda kujenga, tumeenda kulima mashamba, sasa tembo wao na wenyewe wana ownership (umiliki), ile njia wao wanaona ni ya kwao tu, kwahiyo akikutana na wewe anafanya hayo anayoyafanya, hata kwenda kukaa kufanya shughuli za kibinaadamu ikiwemo kujenga na kulima jirani kabisa na kwenye mpaka ya hifadhi na yenyewe ni tatizo". 

Naibu Waziri Makani amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mara jana ambapo alitembelea vijiji kadhaa wilayani Bunda na Serengeti na kushudia athari mbalimbali za uharibifu wa wanyamapori pamoja na kupokea malalamiko mbalimbali ya uharibifu huo kutoka kwa wananchi. Alishuhudia mashamba kadhaa ya mahindi yaliyokuwa karibu na maeneo ya hifadhi yakiwa yameharibiwa na tembo.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA KABYAILE MISENYI MKOANI KAGERA

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA KABYAILE MISENYI MKOANI KAGERA

January 02, 2017


kag1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
kag2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
kag3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
kag4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag7 kag8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
kag11
Taaswira ya moja ya jengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumapili Januari Mosi, 2017 ameendelea na ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Kabyaile kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera
Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo hicho cha Afya Rais Dkt Magufuli amesema serikali kwa sasa imeweka nguvu kubwa katika kurejesha miundo mbinu ya huduma za jamii iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10,2016 Mkoani humo badala ya kujenga nyumba ya mwananchi mmoja mmoja.
”Na ndio maana nimeona leo hapa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2017 niwaeleze ukweli maana kuna watu wanapitapita huko na wapo wengine nyumba zao zilibomoka kidogo wakadanganywa wakaambiwa kuwa serikali itakuja kuwajengea nyumba wakazibomoa zote ”waafwa” kama ulitegemea ukiibomoa utalipwa fidia,hakuna”
Aidha Dkt Magufuli amemwagiza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupeleka huduma ya umeme katika kituo hicho cha afya alichokiwekea jiwe la msingi,ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa ajili kutengeneza barabara inayoelekea kituoni hapo kwa kiwango cha lami.
Pia ameuagiza uongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaojenga kituo hicho cha afya kuharakisha ujenzi wake na kukamilika kabla ya mwezi februari badala ya Machi mwaka huu.
Dkt Magufuli ameutaka uongozi na wananchi wa Wilaya ya Misenyi na maeneo mengine nchini kutumia vyema mvua chache zinazonyesha mkoani humo kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ili kuepukana na baa la njaa na kwamba serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
01 Januari, 2017

MAVAZI YA KHANGA YALIVYO SHINE KWENYE KHANGA PARTY MKESHA WA MWAKA MPYA

January 02, 2017
dq
Usiku wa 31,December 2016 kuamkia mwaka mpya 2017 ndipo wanamitindo mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa Khanga yaani “Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyo kuwa limetaarifiwa awali limefanyika Regency  Park Hotel.  Design mbalimbali za vazi la Khanga kutoka kwa wanamitindo zilioneshwa kwenye stage na kuzikonga mioyo za wadau pamoja na wahudhuriaji  usiku huo.
 
Kumbuka Party hii imeandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, mbali na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu. Tunawatakia mwendelezo mwema na wenye baraka wadau na wanamitindo kutoka hapa Tanzania. (Cheers 2017)