Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Pili

February 20, 2018

Picha/Makala na Josephat Lukaza
Siku ya Leo tutaangalia Makundi mawili yaliyobaki katika makundi mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa, Siku zilizopita Katika makala ya Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanza tuliweza kuangalia Makundi mawili ambayo ni Viral Infections pamoja na Bacterial Infections. Leo tutaangalia makundi mengine mawili ya mwisho ambapo tutapata nafasi ya kuangalia ni magonjwa gani yapo katika Makundi hayo mawili yaliyosalia.
Yes Let's Back to Class kama wasemavyo Wazungu, Leo tutaangalia Makundi Mengine Mawili ambayo ni Kama Ifuatavyo
1: Fungal Infections
Fungal infections ni magonjwa ambayo  husababishwa na fangasi magonjwa haya yanaathiri binadamu pamoja na mbwa japokuwa Mbwa hushambuliwa mara kumi zaidi ya binadamu kwa magonjwa yasababishwyo na fangasi. Magonjwa yasababishwayo na fangasi kwa Mbwa yanaweza kuleta madhara katika Macho, Ubongo, ngozi nk. Katika Kundi hili la magonjwa yasababishwayo na fangasi Ni kama vile Blastomycosis, Histoplasmosis,>>>>KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
-- Josephat Lukaza B.A Sociology - The University Of Dodoma (UDOM) - 2012 Sociologist | Photographer | Mentor | Social Media Influencer | Blogger Founder & Chief Editor - Lukaza Blog - http://www.josephatlukaza.com Phone: +255 712 390 200 E-mail: Josephat.lukaza@gmail.com

"NAJIVUNIA KUFANYA KAZI CHINI YA RAIS MAGUFULI ANAYEFANYA MAAMUZI KWA WAKATI" MHE BITEKO

February 20, 2018

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WazoHuru Blog
 Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili mgodini
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya mitambo tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya magari tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amebainisha kuwa anajivunia kufanya kazi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Kwani amekuwa ni kiongozi anayefanya maamuzi kwa wakati pasina kuchelewa.

Mhe Biteko ameyasema hayo Leo 12 Februari 2018 wakati akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje.

Alisema kuwa Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya dhati ya kuepuka michakato ya kuchelewesha maendelo kwa maamuzi ya busara na haraka anayoyafanya huku akieleza kufurahishwa na maamuzi ya kujengwa ukuta katika machimbo ya Tanzanite yaliyopo katika eneo la Merelani Wilaya ya Simajiro Mkoani Arusha.

Mhe Biteko akiwa ziarani Mkoani Songwe amemtaja Rais Magufuli kama kiongozi mpenda haki, na msimizi madhubuti wa rasilimali za umma hivyo maamuzi yake yamepelekea Taifa kwa sasa kufikia hatua ya kuheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Hata hivyo alisema kuwa ili kuitafsiri vyema ndoto ya Rais Magufuli ya kuwanufaisha wananchi kupitia sekta ya Madini amekusudia kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na tija kwa kukuza uchangiaji wa pato la Taifa.

Akizungumza kwa msisitizo juu ya kusudio la serikali kuhakikisha Mgodi wa Kiwira unaanza uzalishaji ili kuchochea ajira kwa wananchi aliutaka uongozi wa Wilaya ya Ileje na Kyela kuketi mezani kwa ajili ya mazungumzo ya makubaliano ya namna bora ya kumaliza sintofahamu ya namna ya ukusanyaji mapato kutokana na mgodi huo kuwa Wilaya ya Ileje lakini baadhi ya huduma zingine zikipatikana Wilaya ya Kyela zikiwemo makazi ya wafanyakazi wa mgodi.

Aidha, alisema kuwa viongozi hao pindi watakapokuwa na makubaliano mazuri wanapaswa kutumia fedha watakazokuwa wanakusanya kwa kuzielekeza katika miradi inayoonekana.

Sambamba na hayo pia Mhe Biteko alielekeza Wakurugenzi kutotoza ushuru usiokuwa na tija ambao utawafanya wawekezaji na wachimbaji kushindwa kumudu jambo litakalopelekea kudumaa kwa faida wanayopata na hatimaye kushindwa kuwekeza.

MASOKO YASIYO RAMSI MGANDINI YADAIWA KULIKOSESHA SOKO MAPATO

February 20, 2018
MASOKO yasiyokuwa rasmi yanayolizunguka soko la Mgandani Jijini Tanga yanadaiwa kusababisha upatikanaji wa mapato kuwa madogo.

Hatua hiyo imepelekea uongozi wa soko hilo kuiomba Halmashauri ya Jiji hilo kuingilia kati kutumia nguvu za ziada ili kuweza kuwaondoa wafanyabiashara hao ambao wanauza bidhaa zao kwenye mazingira hatarishi.

Akizungumza na Tovuti hii mwishoni mwa wiki Katibu wa Soko hilo, Ridhiwani Mwinyiheri alisema licha ya hivyo lakini pia wafanyabiashara hao wamepelekea biashara kwa walipoo kwenye vizimba ndani ya soko hilo kukosa wateja.

“Jambo hilo tukilifumbia macho linaweza kukwamisha mipango yetu hivyo tunaiomba Halmashauri ya Jiji la Tanga kuangalia namna mzuri ya kuhakikisha wafanyabiashara hao wanaondoka kwenye maeneo hatarishi ya barabarani “Alisema

“Lakini pia kuwepo kwao nje ya soko kumepelekea hata biashara kuwa ngumu kwani baadhi ya wateja wanaofika hapa huishia nje hivyo kwa wale wanaouzia ndani wanakuwa wakikosa wateja”Alisema.

Hata hivyo aliopngeza hivi sasa soko hilo limekuwa na msongamano mkubwa wa wafanyabiashara ambao wengine wanalazimika kupanga bidhaa zao chini kutokana na ongezeko ambalo limesababisha kwa asilimia kubwa na vijana waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne.

“Licha ya hivyo lakini pia hali hiyo imesababishwa na wafanyabiashara wenyewe kwa sababu anamuingiza msaidizi wake sokoni hapo baadae anamtafutia sehemu ya kupanga bidhaa zake”Alisema.

BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS

February 20, 2018
 Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
BENKI ya Equity imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao  ambapo wateja wao sasa watapata huduma mahali popote kupitia  simu za mkononi, tablets na kompyuta za mezani na mpakato.

Huduma hizo watazipata kupitia Eazzy Banking kwa kufanya miamala  kirahisi iwe usiku au mchana, wakiwa nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa watakuwa na nafasi ya kuokoa muda na gharama.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Eazzy Banking,  Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Joseph Iha amesema kuwa huduma  hizo mpya zitatoa fursa kwa wateja kufanya miala mahali popote.

"Huduma za Eazzy Banking zitaambana na EazzyBanking App, app ya  kimataifa ya masuala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo na wakati wowote.

"EazzyBanking ni rahisi kuianzisha na hutoa huduma za kipekee kama  kutuma fedha kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo , kulipia bili(ankara) na aina ya huduma za malipo," amesema Iha.

Amefafanua kwa wale wenye simu za kawaida, kuna suluhisho kwao  ambalo linajukulikana kama Eazzy24/7. Huduma hiyo ambayo  imeboreshwa inawezesha watumiaji kupata huduma zilezile kama za EazzyBanking App kwa kupigiga *150*07# kupitia simu zao.

Ameongeza ndani ya huduma hiyo kuna kipengele cha huduma  ambacho mtandaoni unaweza kufanya manunuzi ya rejareja ambapo wateja wataendesha akaunti zao na hiyo inajulikana kama EazzyNet;  huduma ya malipo mbalimbali inayoitwa EazzyPay ambayo huwezesha  kufanya malipo ya bili kama ving'amuzi, Tanesco,Luku na Dawasco.

Pia amesema inawezesha kununua na kulipia bidhaa na huduma  kupitia kwa wauzaji waliosajiliwa kama Supermarket na hoteli kwa pale unapoona bango au stika ya "EazzyPay inakubalika hapa".

"Huduma ya mkopo kwa njia ya simu inayoitwa EazzyLoan pamoja na  uvumbuzi na usimamizi wa fedha kwa SMEs /wafanyabiashara wa kati na wateja wakubwa, kampuni kubwa au Wizara kwa kupata huduma  kupitia EazzyBiz.

"Pia kuna EazzyKikundi ambayo hiyo inatoa nafasi ya kusaidia Saccos,  Viccoba , vikundi vya kiuchumi na uwekezaji na utunzaji kumbukumbu za biashara,"amesema na kusisitiza kupitia EazzyBanking wateja watapata huduma za kibenki kirahisi , salama na bila stress,"amesema Iha.

Akifafanua zaidi amesema uzinduzi wa huduma hiyo ya kibunifu unaongozwa na huduma mama ya EazzyBanking App ambayo itaimarisha mbinu mkakati za kibenki katika kuwahudumia wateja kimtandao kutokana na mabadiliko ya mahitaji yao.

"Hii imejulikana  kutokana na mienendo ya kibenki ya wateja ambayo imeonesha kukua kwa huduma binafsi zinazowezesha kubenki popote na muda wowote.Mteja anachotakiwa kufanya ni kupakua tu EazzyBanking App na apate urahisi wa kubenki," amesema.

Amewahakikisha Watanzania kuwa benki hiyo ipo makini katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuomba wale ambao hawajajiunga na benki hiyo huu ndio wakati sahihi kwani mambo yote ya kibenki unayafanya bila Stress.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha akizungumza na wageni waalikwa na wanahabari waliofika katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Joseph Iha akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni ni wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.

DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BODI YA UTALII (TTB)

February 20, 2018
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
...........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Februari 20, 2018, amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu zaidi.

Akizungumza na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha mbalimbali za Kimataifa.

Aidha,amewataka kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA).

Hata hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara.

Pamoja na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.

Akiwa katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

MZUNGUKO WA NNE WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUANZA KESHO

February 20, 2018
MZUNGUKO WA NNE WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUANZA KESHO
Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inatarajia kuanza kesho Jumatano Februari 21, 2018.
Kwenye Uwanja wa Sabasaba Njombe kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha mwenyeji Njombe Mji atakayecheza dhidi ya Mbao  FC kutoka Mwanza saa 10 jioni.
Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea Jumamosi Februari 24,wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku Azam Complex.
Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro,Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.
Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
NDANDA VS YANGA SASA KUCHEZWA MWISHO WA MWEZI
Mchezo namba 152 wa mzunguko wa 19 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umepangiwa tarehe ya kuchezwa.
Bodi ya Ligi imetaja tarehe hiyo baada ya awali mchezo tajwa kutokuwa umepangiwa tarehe kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu.
Mchezo huo sasa utachezwa Jumatano Februari 28, 2018 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mkoani Mtwara.
Timu zote tayari zimejulishwa kuhusu tarehe ya kuchezwa mchezo huo.
FIFA WAONGEZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA KWA TANZANIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeongeza tiketi kwa Tanzania kwaajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Russia mwaka huu.
Kwa shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu wa namna ya kupata tiketi hizo.
Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018.
Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

SIMBA CEMENT YATOA MIFUKO 3000 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA

February 20, 2018
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akitokea mifuko 3000  ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi leo katika anayeshughudia ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Mashariki leo katika anayeshughudia ni kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akimkabidhi Msaidizi wake,Abdallah Salimu mifuko hiyo mara baada ya kukabidhiwa anayeshughudia katikati nyuma ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea sehemu ya mifuko ya Saruji 3000 kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi katika kulia anaye shughudia ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akieleza mikakati ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye hayupo pichani ambaye alikwenda kiwanda hapo kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya Elimu Jimboni kwake Iramba Magharibi
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na vyombo vya habari mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya saruji ambapo alikishukuru kiwanda cha Simba Cement kwa kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake kuli ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swat
 Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement  Reinhardt Swat mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya Saruji kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya Elimu Jimboni Kwake

Sehemu ya Saruji mifuko 3000 aliyokabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba 
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Simba Cement Reinhardt Swat wakitembelea kiwanda hicho kabla ya kukabidhiwa mifuko 3000 ya Saruji

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat kulia akimuonyesha eneo ambalo wanalotumia kwa shughuli za kiwanda Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema katika ambaye alitembelea kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho,Beny Lema 
Meneja wa Kiwanda cha Simba Cement Beny Lema akimuogoza Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kushuka ngazi mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kulia akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa ajili ya kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu kwenye Jimbo lake la Iramba Magharibi
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Jijini Tanga wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema kushoto akiwa na wafanyakazi wengine wa kiwanda hicho wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba katika akiwa na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia kushoto ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim wakiongia ukumbini kwa ajili ya kupata taarifa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga ambao nao waliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani katika makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdallah

MBUNGE MGIMWA AMETOA BATI 590 NA MIFUKO YA SARUJI 220 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MADARASA KATA YA IHALIMBA

February 20, 2018
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi  na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wanaofundisha katika kata ya Ihalimba katika jimbo la
Mufindi Kaskazini 

 Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi  na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alieleza maeneo ambayo ametoa bati na mifuko ya saruji kuwa ni shule ya msingi Nundwe Bati 160 kwaajili ya nyumba ya walimu 60 na ukarabati wa paa la madarasa, bati 100. shule ya msingi Vikula bati 100 na saruji 50, shule ya msingi Mong'a bati 50,Zahanati ya Ugesa bati 30 na saruji 40 kwaajili ya nyumba ya mganga wa kijiji cha Wami, ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Mbalwe bati 100 na saruji 20,Ihalimba sekondari nyumba ya mganga bati 50 na fedha tshs 1,100,000 kwaajili ya dari jengo la maabara na kununua pampu ya maji.

“Hizi ni gharama ni kata moja tu ya Ihalimba ambazo nimezitafuta nako kujua mimi hivyo lazima walimu mjue kuwa kuwa mbunge ni kazi kubwa sana na lengo la kuwa mbunge nikuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo ambayo yanatakiwa kwa wakati sahihi hivyo napenda kuwapa habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kata ya Ihalimba kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa

Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.

Aidha Mgimwa aliwataka walimu kumwambia changamoto ambazo wanakumbana nazo ili kuzitatua na kuhakikisha walimu wanafundisha katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ihalimba wilayani Mufindi mkoani Iringa Award Mahanga  amempongeza mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa kwa kuendelea kutatua changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu kwa kuchangia saruji mifuko 200 na bati 590 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule za msingi na sekondari za kata hiyo.
Mahanga aliesema kuwa mbunge Mgimwa amekuwa akijitoa kwa kutatua changamoto za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika.
Aidha Mahanga alisema kuwa mbunge huyo amechangia kwenye sekta ya afya ambapo amefanikisha ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji cha kata hii ya Ihalimba

Lakini pia Mahanga alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kuahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneno ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.

“Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Mahanga