MHANDISI MTIGUMWE AITAKA BODI YA KAHAWA KUONGEZA UZALISHAJI

November 12, 2017

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maelezo ya kitaalamu kuhusu mchakato mzima wa kupaki kahawa na soko lake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alipotembelea chumba cha kuchotea Sampuli zinazopelekwa ambazo ni kilo 8 na kuchotea Gramu 300 kwa Loti.
Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo
Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe katika Ukumbi wa Bodi hiyo.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia sekta ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Kahawa nchini kwani  Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele.

Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani 100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo kuongeza uzalishaji linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.

Katibu Mkuu Alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini nini chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kufahamu umuhimu wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na Biashara ikiwemo zao la Kahawa.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema miongoni mwa sababu ambazo huchangia uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali nchini huwa ni pamoja na Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo ambalo sio rafiki sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche na mche.

Mhandisi Mtigumwe aliitaka Bodi ya Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa inastawi kwa wingi ili kuongeza sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Hata hivyo amesema kuwa atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za Uzalishaji, Changamoto za Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na Changamoto za Sekta.

Majukumu ya Bodi ya Kahawa ni pamoja na usimamizi wa sheria namba 23 ya marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za Kahawa 2013 sambamba na kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina ya serikali na wadau.
Mkutano mkuu wa 44 wa wanahisa wa TBL wafanyika Dar es salaam

Mkutano mkuu wa 44 wa wanahisa wa TBL wafanyika Dar es salaam

November 12, 2017

TBL wanahisa 3
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL,Mh.Cleopa Msuya (katikati) akiendesha mkutano mkuu wa 44 wa  mwaka  wa wanahisa. wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa AB-InBev Afrika Mashariki Bruno Zambrano, Mkurugenzi wa Tbl Group ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Biashara Afrika Mashariki  AB-InBev,Roberto Jarrin, Mkurugenzi wa bodi ya TBL Group    Balozi Ami Mpungwe  na  Katibu wa TBL Group,Huruma Ntahena (wa pili kulia)
TBL wanahisa 1
Baadhi ya wanahisa  wa Tbl Group  wakiwa katika mkutano mkuu wa 44 wa mwaka uliofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa   Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
TBL wanahisa 2
Mkurugenzi wa bodi ya TBL Group ,Balozi Ami Mpungwe (kulia) Katibu na Mwanasheria wa Tbl Group,Huruma Ntahena (katikati)  wakibadilishana  mawazo.(Kushoto) ni Mwenyekiti wa bodi  wa TBL Group,Cleopa Msuya.
TBL wanahisa 5
Mkurugenzi wa TBL na Rais wa ABINBEV Afrika Mashariki,Roberto Jarrin, akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
TBL wanahisa 8
Watendaji wa Bodi ya TBL katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahisa waliohudhuria

Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

November 12, 2017
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo zilizochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji iliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili na mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Pemba pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za polisi katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema wadau wamemchangia shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 12 za Jeshi la Polisi ili kukabiliana na ukosefu wa nyumba za polisi katika mikoa hiyo. Awamu ya ujenzi wa nyumba hizo ni ya kwanza, na awamu ya pili itakua mikoa ya mipya nchini ambayo ni Geita, Simiyu, Katavi na Songwe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Mwajuma Majid Abdalla, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.

TPB BANK NA SHIRIKA LA WE CARE TANZANIA WAFANIKISHA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU JIJINI MBEYA

November 12, 2017
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya TPB wakichangia damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Nov 11 mwaka huu .

MHANDISI MTIGUMWE ATEMBELEA KITUO CHA UKAGUZI WA MAZAO MPAKA WA HOLILI NA TARAKEA

November 12, 2017

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akifungua bomba ili kuona kama maji yanatoka wakati akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA.
 
Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11, 2017 ametembelea Vituo vya ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ili kujionea ufanisi wa utendaji kazi sambamba na kubaini Changamoto zinazowakabili ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa ushuru.

Katika ziara hiyo ya kikazi Mhandisi Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na TARAKEA ambavyo vipo upande wa Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.

HOLILI ni moja ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa takribani Kilomita 25 Kutokea Himo Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea Himo Njiapanda.

Miongoni mwa Changamoto alizozibaini katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili ni pamoja na uduni wa vifaa vya kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya kufanya kazi ya kupimia Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi wanaosimamia ukaguzi wa mazao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika kufanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.

Aidha, Alisema serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za panya zote ili kubaini kila aina ya uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo yanayopitishwa kinyemela.