RC CHALAMILA AHIMIZA MAZOEZI KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

July 16, 2023
p>
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aliwasihi wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya mwili hivyo kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. Chalamila aliyasema hayo alipozindua maandalizi ya CRDB Bank Marathon inayotarajiwa kufanyika Agosti 13 jijini Dar es Salaam ikiwashirikisha wakibiaji 7,000 kutoka kila pembe ya dunia.


“Mlio hapa naamini kabisa mnafahamu umuhimu wa mazoezi kwa afya zetu hasa katika kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.  Mimi binafsi nawasihi wana Dar es Salaam kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zetu. Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa akituasa sana juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi. Nimefurahi leo kuwa hapa kwani nimepata wasaa wa kuchangamsha damu kidogo,” amesema Chalamila. 

Mkuu huyo wa mkoa amesema kwa muda mrefu amekuwa akizisikia mbio za CRDB Bank Marathon na baada ya kuja mjini sasa amepata nafasi ya kushiriki maandalizi ya msimu wa nne wa mbio hizo za hisani za kimataifa.

Zilipoanzishwa mwaka 2019, mbio hizo zilikusudia kufanikisha matibabu ya watoto 100 wenye matatizo ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na mwaka uliofuata fedha zilizopatikana zikijenga kituo cha huduma katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kabla mwaka jana hazijawanufaisha wanawake wenye fistula na ujauzito hatarishi katika Hospitali ya CCBRT.
Kwenye mbio za mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema watafanikisha matibabu ya upasuaji wa moyo kwa Watoto, matibabu ya wanawake wenye ujauzito hatarishi na wale wenye fistula pamoja na kujenga kituo cha afya visiwani Zanzibar.

“Haya ni makundi muhimu katika jamii yetu na wana uhitaji wa kuwa na afya njema, ni nguvukazi ya kutosha kushiriki ujenzi wa Taifa letu. Fedha zote zinazopatikana kutoka kwa washiriki wa CRDB Bank Marathon zitatumiwa kwa malengo haya yaliyotajwa hivyo kila mshiriki anachangia upatikanaji wa huduma bora za afya. 
Nawasihi Watanzania wenzangu hasa kutoka Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla kujisajili ili kushiriki mbio hizi huku kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaweka tofauti katika jamii na kuacha alama chanya,” amesema Nsekela.

Kujiandikisha kwenye mbio hizi zitakazoishirikisha familia nzima zikiruhusu wakimbiaji wa kilomita tano, 10, 21 na 42, kwa mtu mmoja ni Sh45,000 tu lakini kwa kikundi chakuanzia watu 30 ni Sh40,000 kila mmoja.








--

MBUNGE UMMY MWALIMU ACHANGIA MILIONI SITA NA LAKI TATU (6,300,000) KUWEZESHA WAJASIRIAMALI NA VIJANA NGAMIANI KATI

July 16, 2023











Mbunge wa Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 16/07/2023 ametembelea Kata ya Ngamiani Kati ambapo pia amechangia kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000/-) kwa vikundi vitatu vya Wajasiriamali ambavyo ni Nguvu Kazi kilichopo barabara 12 Mnadani, Mtaa wa Makoko; Kikundi cha Kuonda Mai cha Wafanyabiashara wa kuku kilichopo Sokoni Ngamiani na Kikundi cha Wazee kilichopo mtaa wa Maua. Kila kikundi, kimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 2. 

Aidha, Mh Mbunge amechangia shilingi laki 3 kwa ajili ya kukarabati Sehemu ya kufanya mazoezi ya ngumi kwa vijana katika mtaa wa Karafuu.

Mhe Ummy ameeleza kuwa licha ys majukumu ya kitaifa aliyonayo ataendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga Mjini hususani kutatua kero za maendeleo ya wananchi kupitia fedha za Serikali Kuu, Fedha za Halmashauri pamoja na mshahara wake na posho. 

Akiongea baada ya kupokea mchango huo kwa niaba ya vikundi vingine, Ndugu Sadik Ali Mwenyekiti wa Kikundi cha Nguvukazi alimshukuru Mhe Mbunge kwa kuendelea kuwajali wananchi wake.

Katika ziara hii, Mhe Ummy aliongozana na Mhe Habibu Mpa, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kati, Mhe Fatuma Kitogo, Diwani wa Viti Maalum pamoja na Viongozi wa CCM ngazi ya Kata na matawi.

Imetolewa na;-
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini
16/07/2023

BENKI YA CRDB SASA KUTOA MIKOPO NAFUU KWA WASANII

July 16, 2023
Baada ya miezi sita ya uzoefu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa kutoa mikopo kwa wasanii nchini, umeingia mkataba na Benki ya CRDB kutanua wigo wa fursa hizo ili ziwanufaishe wananchi wengi zaidi kupitia mtandao wake mpana wa matawina mawakala.

Mpaka sasa, mfuko huo uliozinduliwa Desemba 2022 umeshakopesha shilingi bilioni 1.077 kwa miradi 45 ikiwamo 29 inayomilikiwa na kuendeshwa na wanaume, 12 ya wanawake na kikundi kimoja.
 
Akizungumza kwenye hafla ya kuingia makubaliano ya mkataba huo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Pindi Chana amesema kwa muda mfupi ambao mfuko huo umetoa fedha hizo, Serikali imeona mahitaji makubwa yaliyopo hivyo kuamua kuipeleka jirani na wananchi.

“Benki ya CRDB ina matawi nchini kote. Tunataka mikopo hii ipatikane kila mahali alipo msanii ili kukuza kipaji chake kwani sasa hivi jamii imeiona faida ya sanaa na wazazi wengi wapo tayari kuwaruhusu watoto wao kuingia kwenye usanii. Kwa mikopo hii kupatikana kwenye matawi ya benki, itawapunguzia wanufaika gharama za kuifuata Dar es Salaam,” amesema Waziri Pindi.

Licha ya kuwapa mikopo, waziri amesema wizara imeanza kuwatafutia wasanii fursa za nje ya nchi ambako wakishiriki matamasha hayo wanajiongezea mtandao wa washirika hivyo kutanua fursa za kipato zaidi. 

“Mikopo hii itapatikana kwa riba ya asilimia tisa tu. Hiki ni kiwango cha chini kikilinganishwa na riba zilizopo sokoni kwa sababu Serikali imeweka mkono wake. Nawasihi wasanii popote walipo nchini wajitokeze kunufaika na fursa hii,” amesisitiza waziri. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Abdulmajid Nsekela amesema wanafanya kila wawezalo kuinua ubora wa kazi za utamaduni na sanaa ili ziweze kujiendesha kibiashara na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana nchini kwa kuwapa mikopo na mafunzo tangu uliposajiliwa mwaka 2020.

“Kati ya mikopo tuliyoitoa, metoa wanaume wamepokea shilingi milioni 737 huku wanawake wakichukua shilingi milioni 275. Kikundi kimoja kilichojitokeza kimekopeshwa shilingi 10 pamoja na kampuni tatu zilizowezeshwa shilingi milioni 55. Kiwango cha marejesho kinaridhisha kwani ni asilimia 88 na tutazidi kusimamia ipasavyo ili kifikie asilimia 95 inayotakiwa,” amesema Nsekela.

Ili kuwawezesha wanufaika kuzitumia fedha za mikopo inayotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa, Nsekela amesema mfuko umetoa mafunzo kwa wadau 7,216 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Morogoro, Tanga na Pwani na kufanikisha ununuzi wa vitendea kazi kwa vyuo vitano ambavyo ni Simba Scratch Academy, Koshuma Training Institute, Mwanamboka Ujuzi-Hub, Dage School of Dressing na AM Fashion.

“Naomba kuwafahamisha wadau kuwa, mpango huu watakaoushuhudia leo utakuwa suluhisho la changamoto zilizokuwa zinawakumbuka wasanii hivyo nitaomba tuuamini, tuupokee na kutoa ushirikiano ili kutimiza ndoto za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Nsekela ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB.

Akisaini mkataba huo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa amesema leo ni siku ya kihistoria kuona mkakati wa unatafsiriwa kwa vitendo kwa kuishirikisha sekta binafsi ili kuwafikia wasanii wengi kadriiwezekanavyo.

“Benki ya CRDB imeingia katika mpango huu kuhakikisha malengo ya mfuko yanafikiwa. Tuna imani kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na taasisi za serikali, tutafanikisha kuyafikia malengo ya mfuko huu. Tumekuwa tukiona jitihada za serikali kujenga mazingira rafiki kwa wadau wa utamaduni, sanaa na michezo ili kuwawezesha kupata matunda ya kazi zao kupitia vipaji walivyonavyo kwa manufaa yao binafsi, familia zao hata jamii na Taifa kwa ujumla,” amesema Raballa.

Ili msanii apate mkopo ambao ni kuanzia shilingi 200,000 mpaka shilingi milioni 100, Raballa amesemaa atatakiwa kupeleka maombi yake ofisi za mfuko huo zinazopatikana nchi nzima ili kufanya uhakiki wa awali kisha kupendekeza maombi hayo yaende Benki ya CRDB. Ombi likikidhi vigezo, mfuko utalipeleka kwenye tawi la Benki ya CRDB lililo Jirani na msanii husika.

Kwa kukamilisha utaratibu huo, Raballa amesema wasanii wanaojishughulisha na kazi za sanaa na utamaduni waliosajiliwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bodi ya Filamu na namlaka nyingine za serikali watakuwa wamejihakikishia kupata mkopo wanaoulenga.

Hata waliomo kwenye vikundi, vyama vya utamaduni na sanaa, vituo vya elimu na mafunzo yanayohusiana na utamaduni na sanaa pamoja na asasi za kiraia zinazojihusisha na utamaduni na sanaa zinaweza kunufaika hivyo wasanii wa filamu, muziki, sanaa za ufundi na maonyesho, lugha na fasii na fani nyingine zenye mlengo wa utamaduni na sanaa.

CHATANDA-RAIS DKT SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA MAGEUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI

July 16, 2023
MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda  akizungumza katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo
MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda  akizungumza katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo
MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda  akizungumza katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo




Na Mwandishi Wetu,Mtwara


MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda  ameshiriki Mkutano wa Hadhara ulioandaliwa n Katibu Mkuu wa CCM, Cde Daniel Chongolo huku akiutumia kuwaeleza wananchi wa mkoa wa Mtwara  kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu.

Chatanda alisema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho amefanya kazi kubwa ya maendeleo hapa nchini ikiwemo mkoani Mtwara kwa kuwapelekea maendeleo wananchi na kuifungua nchi kiuchumi.

Mwenyekiti huyo alitumia mkutano huo kuwataka wananchi wa Mtwara na Tanzania  kwa ujumla kutembea kifua mbele maana Rais wao ni makini, msikivu na amedhamiria kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo nchini Tanzania.


Uwanja wa Nangwanda Sijaona: Mkoani Mtwara (16/7/2023)

JUMUIYA YA WAZAZI TANGA YAUNGA MKONO SERA YA RAIS DKT SAMIA YA KUTUNZA MAZINGIRA

July 16, 2023



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga wa pili kutoka kushoto akiwa ameshikilia mti mara baada ya kuzindua kampeni ya tembea na kivuli na kuimarisha lishe kwenye shule za Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiendeshwa na Taasisi ya Tanzania Environmental Agro Smart(T.E.A). wa kwanza kulia ni Katibu wa Wazazi wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro na kushoto Mjumbe wa Baraza la Wazazi wilaya ya Tanga Pamela Chaula



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga  akipanda mti mara baada ya kuzindua kampeni hiyo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga  akipanda mti mara baada ya kuzindua kampeni hiyo


shughuli za usafi ikiendelea kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga
usafi ukiendelea



Katribu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro kulia akiwa na Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga wakifanya usafi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Hamza Bwanga kulia akiwa na Katibu wa Jumuiya hiyo wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro na Mjumbe wa Jumuiya hiyo Pamela Chaula mara baada ya kumalizika kampeni ya upandaji wa miti








Na Oscar Assenga, TANGA.

JUMUIYA ya Wazazi wilaya ya Tanga imesema kwamba wataendelea kuunga mkono sera ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na taasisi ambazo zinajihusisha na kampeni hizo ili kuleta manufaa kwa jamii.

Sambamba na hilo wataendelea kuhamasisha upandaji wa miti ya matunda katika maeneo mbalimbali ya Tanga ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha mazingira yanatunzwa na baadae kuleta faida.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Hamza Bwanga wakati akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya tembea na kivuli na kuimarisha lishe kwenye shule za Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiendeshwa na Taasisi ya Tanzania Environmental Agro Smart(T.E.A).

Alisema kwamba jambo la mazingira ni muhimu sana na moja ya jukumu lao kusimamia na wapo tayari muda wowote kushirikiana na taasisi ambazo zinatunza mazingira kwa kuleta manufaa.

“Niwapongeze Taasisi ya TEA mlilolifanya hapa ni jambo nzuri niwaombe tuendelea kuhirikiana nanyi kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema kwamba wataendelea kusimamia suala la utunzaji wa mazingira ikiwemo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kuonyesha wanaunga mkono sera hiyo ambayo itasaidia kuzibiti uharibifu wake.

“Lakini niwaambie kwamba TEA mmetuwahi sisi tulishapanga na kuweka kwenye mipango yetu suala la uhamasishaji wa jamii kupanda miti katika maeneo mbalimbali katika wilaya ya Tanga “Alisema

Alisema pia miti yenye matunda ina faidi kubwa sana kwa jamii kwani ikitumiwa vizuri inaweza kuwa chanzo cha wao kuweza kupata kipato lakini kuwapa afya bora.

Hata hivyo alisema kwamba wanahaidi kwamba hawatachoka wakati wowote watapokwenda mahali popote watakuwa wakitoa ushauri juu ya kampeni ya tembea na kivuli kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga wapo vizuri chini ya CCM huku akimpongeza Diwani wa Kata ya Majengo kwa kuunga mkono jambo hilo akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo alisema kwamba wataendelea kushirikiana kwenye kampeni hiyo kuelimisha ili jamii iweze kuwa na uelewa mzuri wa upandaji wa miti hususani ya matunda na kivuli.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Sosiya – aliishukuru Shirika la TEA kuichangua Jiji la Tanga kwenye kampeni hiyo ya uzinduzi ambayo ina umuhimu mkubwa .

Alisema kwani hilo jambo ni maagizo ya kisera na kanuni kila Halmashauri nchini inatakiwa kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka na kwa takwimu hadi mwezi Mei 30 mwaka huu mkoa wa Tanga wamefanikiwa kupanda zaidi ya miti milioni 11 kat iya miti milioni 16.5 .

“Leo tunayofuraha kwamba Shirika la TEA limekuja kutushika mkono katika utekeleza kampeni hiyo kwa asilimia 100 hivyo viongozi a wananchi wakiande kuupokea mradi huo kwani utakuwa na manufaa makubwa sana “Alisema

Katibu wa Wazazi wilaya ya Tanga Urassa alilipongeza Shirika l;a TEA kwa jambo hilo ambalo wamelifanya huku akieleza kwamba CCM ndio iliyopewa dhamana kwenye ilani ya Uchaguzi 2020/2025 kusimamia eneo la elimu na mazingira .

Alisema kwamba wanapoona wanaungwa mkono kwenye utekelezaji wa ilani ya CCM kuhusu mazingira wanafarijika huku akiwapongeza viongozi wa Kata ya Majengo kwa kulisimamia zoezi hilo ipasavyo.

Mwisho.