RC SHIGELLA :SERIKALI ITAENDELEA KUNYAG'ANYA MASHAMBA NA VIWANDA AMBAVYO VIMESHINDWA KUENDELEZWA

October 31, 2017
 MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara kwenye shamba la mkonge la Mkumbara kulia ni Mmiliki wa Shamba hilo,Damian Ruhinda na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo D.D Ruhinda Deogratius Ruhinda

 MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella wa pili kutoka kushoto akiangalia maeneo mbalimbali kwenye shamba hilo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella wa pili kutoka kulia akiangalia bidhaa zinazozalishwa na shamba hilo kushoto ni
Mmiliki wa Shamba hilo,Damian Ruhinda
 MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiangalia namna mkonge unavyozalishwa kulia ni Mmiliki wa Shamba hilo,Damian Ruhinda kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo D.D Ruhinda Deogratius Ruhinda
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto aliyeshika zao la mkonge akimsikiliza kwa umakini Mmiliki wa Shamba la Mkonge la Mkumbara wilayani Korogwe Mkoani Tanga Damian Ruhindawakati alipofanya ziara ya kulitembelea

                               Yusuph Mussa,Korogwe.
 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema Serikali itaendelea kunyang'anya  mashamba na viwanda ambavyo vimeshindwa kuendelezwa na kupewa wawekezaji wengine kama walivyofanya kwa baadhi ya mashamba ya wilaya ya Muheza na sasa wamechukua Shamba la Mkonge Mnazi wilayani Lushoto.

Nia ya Serikali ni kuona wawekezaji wazawa na wageni wanawekeza kwa tija kwenye viwanda, makampuni na mashamba makubwa ili wao wanufaike kwa wananchi kupate ajira na serikali ipate kodi.

Aliyasema hayo  alipofanya ziara kwenye Kiwanda cha Mkonge Mkumbara kilichopo Kata ya Mkumbara, Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe chini ya Kampuni ya D.D. Ruhinda inayomilikiwa na Damian Ruhinda.

Shigela alisema uwekezaji aliouona kwenye kiwanda hicho ambacho kina shamba lenye ukubwa wa eneo la mraba la hekta 1,700, ni mkubwa na unatakiwa kuwa mfano kwa wawekezaji wengine hasa wazawa, ambapo kwa kiwanda hicho cha mkonge kuzalisha kwa tija, wananchi na Serikali wanapata.

"Uwejezaji unaofanywa na Ruhinda ndiyo unaotakiwa kuoneshwa na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Kwani tunachokitaka Serikali ni kuona wananchi wanaofanya kazi kwa mwekezaji huyo wanapata neema na sisi Serikali tunachukua kodi, na hilo ndilo linafanyika hapa, ambapo zaidi ya wafanyakazi 300 wameajiriwa.

"Tunapenda kutoa tahadhari kwa wawekezaji kuwa Serikali msimamo wake upo pale pale, kiwanda, kampuni au shamba lisiloendelezwa tunalichukua na kumpa mtu mwingine, kama tulivyofanya kwa Shamba la Mkonge Mnazi (lipo Wilaya ya Lushoto), ambapo baada ya mwekezaji kushindwa kuliendesha Serikali tumelichukua" alisema Shigela.

Shigela alisema shamba hilo lenye hekta 5,000, hawawezi kulibadilishia matumizi, bali litaendelea kuzalisha mkonge, kwani malighafi ya mkonge na mitambo yake vyote vipo, na amempa ofa Ruhinda aweze kwenda kununua shamba hilo na kuweza kuendeleza zao la mkonge.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayomiliki kiwanda na Shamba la Mkonge Mkumbara Deogratius Ruhinda alisema moja ya changamoto kwao ni mlolongo wa kodi ambazo zinashikwa na watu tofauti ikiwemo Taasisi ya Osha, ambayo ipo kwa ajili ya kuangalia usalama wa wafanyakazi kazini.

"Kodi nyingine inachukuliwa na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) na halmashauri. Kama tungepewa nafasi ya kutoa maoni yetu, ningeshauri kodi ikusanywe na mtu mmoja ambaye ni TRA. Hiyo ingetusaidia kupata unafuu mkubwa, na kuweza kupata faida kile tunachozalisha. Lakini pia tuwalipe vizuri wafanyakazi wetu na tuweze kulipa kodi serikalini" alisema Ruhinda.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni  ya D.D. Ruhinda, Damian Ruhinda, alimuomba Mkuu wa Mkoa amueleze Rais Dkt. John Magufuli aweze kufanya ziara ya kutembelea wadau wa mkonge mkoa wa Tanga, kwani kwa sasa wamebaki wawekezaji wazalendo tofauti na wale wa zamani maarufu kama mabepari.

"Pamoja na mafanikio yetu tangu tuliponunua haya mashamba ya mkonge kutoka serikalini, bado tuna changamoto nyingi, hivyo Mkuu wa Mkoa tunakuomba mueleze Rais aweze kutembelea mashamba na viwanda vyetu... sisi tunamuunga mkono kwa asilimia 100 nchi hii kuwa ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025" alisema Ruhinda.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI JIJINI MWANZA.

October 31, 2017
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.
 Wananchi wa Butimba na Mkuyuni wakifurahi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

October 31, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikaribishwa na viongozi wa jeshi wakati alipokwenda kukabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.

Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 hadi 120 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

Amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya Mkuu wa Mkoa mwenye kuwapenda na kuwajali.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James ambapo wote kwa pamoja wamempongeza mkuu wa mkoa kwa hatua kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa wakishuhudiwa na  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James.
MAVUNDE ASISITIZA KUWA NA NGUVU KAZI YA VIJANA WENYE UJUZI KATIKA UJENZI WA UCHUMI WA TAIFA

MAVUNDE ASISITIZA KUWA NA NGUVU KAZI YA VIJANA WENYE UJUZI KATIKA UJENZI WA UCHUMI WA TAIFA

October 31, 2017

mavunde (1)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akizungumza na vijana katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro
mavunde (2)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akikagua maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa na Serikali kupitia mpango wa Ukuzaji Ujuzi Nchini katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro. 
…………….
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde leo ametembelea Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro na kukagua maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa hapo na Serikali kupitia mpango wa Ukuzaji Ujuzi Nchini.

Akizungumza na Vijana hao ambao wanasomea masomo ya Komputa,Mavunde amewataka Vijana hao kuutumia ujuzi watakaoupata hapo chuoni kujiajiri kwa  kuunda vikundi na Makampuni ili wapate nafasi ya kuwezeshwa kupitia mifuko ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi nchini na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa Vijana.

Mavunde pia amewaeleza Vijana hao kwamba watambue siku zote wao ndio moyo wa Taifa  na hivyo ndio nguvu kazi inayotegemewa kwa kiasi kikubwa ndio maana Serikali inaona umuhimu wa kuwekeza katika Mpango huu wa ukuzaji Ujuzi ili kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye ujuzi stahiki katika kuelekea nchi Uchumi wa Viwanda na ya kipato cha kati.

Kwa upande wao Vijana hao wanufaika na Mpango huu wameishukuru serikali kwa kutekeleza mpango huu wa ukuzaji ujuzi ambao utawasaidia kupata ujuzi na baadaye kuweza kujiajiri na Kuajiri Vijana wengine.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGA UWEZO KWA TAASISI KATIKA UDHIBITI WA KEMIKALI NA TAKA SUMU

October 31, 2017
 Mgeni Rasmi katika warsha ya uzinduzi wa Mradi wa kujenga uwezo kwa Tasisi katika udhibiti wa kemikali na taka sumu , Bwana Richard Muyungi ambaye ni Mkurugenzi idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akiongeakatika uzinduzi wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga akiongea wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira.
 Sehemu ya Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mwakilishi wa UNEP  Bibi Nalimi Sharma akiongea katika warsha hiyo, pembeni yake Mkurugenzi wa Mazingira Ofsis Ya Makamu wa Raisambaye  ni Mgeni Rasmi Bwana Richard Muyungi
 Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali.

Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Taka sumu nyingi zimekua tishio kwa Wananchi hasa Wanawake na Watoto. 

RC Rukwa aahidi kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Rukwa katika Sekta zote

October 31, 2017
​ Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo amewatahadharisha watumishi kutobweteka baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kustaafu na kumkabidhi yeye kijiti cha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya mkoa.

Amesema kuwa hatomwangusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumkabidhi madaraka hayo na kuahidi kuwa ataimarisha elimu inayoonekana bado ipo chini kwa ufaulu lakini pia kuendeleza kasi ya uzalishaji katika kilimo.

“Baada ya kusoma kabrasha hili la kukabidhiana ofisi kuna mambo mengi ya kuyazingatia ikiwemo, elimu, kilimo, ulinzi na usalama, utunzaji wa mazingira, uvuvi na uwekezaji katika viwanda. Hasa katika elimu maana mimba ni nyingi, kuna upungufu wa madawati, upungufu wa vyumba vya madarasa lakini pia kiwango cha ufaulu hakijafikia kile kilichopo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo ni asilimia 80 kwa darasa la saba,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mapema leo hii tarehe 31/10/2017 katika ukumbi wa ofisi hiyo, jambo lililoshuhudiwa na watumishi wa sekretariet ya Mkoa pamoja na baadha ya Halamashauri.

Katika kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufanisi Mh. Wangabo amesema kuwa hupemda kusikiliza mipango ya watendaji inayotekelezeka ili waweze kuitekeleza kama walivyoipanga nay eye ataisimamia na kutoa ushauri wa kuongeza kasi ya utekelezaji pale inapobidi ili kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa wakati.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewashukuru watumishi wote wa serikali katika Mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wa mkoa kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote alichokuwepo na kuwaomba waendeleze kumpa ushirikiano huo huo Mkuu wa Mkoa mpya ili naye aweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
 Mkuu nwa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Leonard Wangabo akisalimiana na Meneja wa PS3 Mkoa wa Rukwa Bi. Rose wakati wa kumkaribisha Mh. Wangabo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwaajili ya Kuanza kazi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo. katika makabidhiano ya ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. JAPHET HASUNGA KATIKA SHAMBA LA MITI SAO HILL NA KITUO CHA MALIKALE CHA ISMILA NA KALENGA MKOANI IRINGA

October 31, 2017

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua baadhi ya vifungashio vya asali alipotembelea shamba la miti Sao Hill kwa ajili ya kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni. Asali inayozalishwa na shamba hilo imefanyiwa vipimo nchini Ujerumani na kugundulika kuwa ni bidhaa bora isiyo na viambata vya kemikali ya aina yeyote. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na Afisa Ufugaji Nyuki wa shamba hilo, Said Abubakar. 
Meneja wa shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akimueleza Mhe. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) kuhusu moto uliovamia hekta 77 za shamba hilo na hatua zilizochukuliwa kuudhibiti alipotembelea  kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni, alisema moto huo uliozuka hivi karibuni ulianzia kwenye mashamba ya wananchi haukuwa na madhara makubwa. 
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga kuhusu utafiti unaofanywa na shamba hilo kwa kushirikiana na Kampuni ya Art International kuhusu uvunaji wa utomvu kwa ajili ya kutengeneza madawa mbalimbali, bazooka (chewing gums) na ‘gel’ kwa ajili ya kujiongezea kipato alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mhe. Jamhuri David. 
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani) kuhusu njia mpya ya kuzalisha mbegu za miti kwa njia ya vikonyo ili kuongeza zaidi uzalishaji alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (wa pili kulia) alipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Ismila kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho mkoani Iringa hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela. 

HII SI AKAUNTI YA RAIS KARIA

October 31, 2017
Kuna Akaunti mpya wa Twitter inazunguka katika mitandao ya kijamii.
Akaunti hiyo yenye jina la Rais wa Shirikisho l Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeanza kutoa taarifa mbalimbali na kuchangia maoni kunakoelezwa kufanywa na Wallace Karia.
TFF tunatangaza kuwa hatuitambui akaunti hiyo. Rais Karia hajafungua akaunti ya Twitter.
Tunaomba wananchi wote hususani wanafamilia wa mpira wa miguu, kutoitambua akaunti hiyo kwa sababu si ridhaa ya Rais Karia wala Kitengo cha Habari TFF kilichofungua akaunti hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI JIJINI MWANZA.

October 31, 2017
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.
 Wananchi wa Butimba na Mkuyuni wakifurahi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia utengenezaji wa viti vya plastiki katika kiwanda cha Victoria molders and polybags katika eneo la Igogo jijini Mwanza.

UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA

October 31, 2017
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele), akitoka kuangalia ukarabati wa meli ya Mv.  Clarius, katika Bandari ya Mwanza, leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa vilivyo kwenye ziwa Victoria.
 Muonekano wa Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo inasafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port Bell” Uganda.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa nne kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, alipofika Bandari ya Mwanza leo kujionea maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV. Clarias katika Bandari hiyo.
 Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa meli katika Bandari ya Mwanza, leo.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), hatua zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv. Clarius na Mv. Umoja katika Bandari ya Mwanza.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa meli ya Mv. Clarius leo katika Bandari ya Mwanza. Kukamilika kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika visiwa vilivyo katika ziwa Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji na abiria katika visiwa hivyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za usafirishaji katika  Ziwa Victoria.

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa, amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.

“Mkandarasi ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi”, amesema Profesa Mbarawa.Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv. Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari  ya “Port Bell”, nchini Uganda.

“Kukamilika kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye biashara wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Naye, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, amemhakikishia Profesa Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika ziwa Victoria na Tanganyika.

KIKOSI KAZI SEKTA YA ARDHI CHAKUTANA KUREJEA MWONGOZO NA KUKAMILISHA MKAKATI,MOROGORO

October 31, 2017
Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta kuu za matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili kuendelea kurejea Mwongozo wa ushirikishaji katika kupanga mipango ya matumizi ya Ardhi pamoja na kukamilisha kazi ya rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo kuutafsiri kwa lugha ya kiswahili.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na kupongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia swala la mipango miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi utakaozingatia mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi kazi ya kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya kingeleza ili lipate kusomwa na wafadhiri pia wadau wengine.
Afisa Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile (wa kwanza kulia) akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa kutatua changamoto za matumizi ya Ardhi nchini.
Afisa Tawala wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona Rajabu akitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa anakabidhiwa Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi cha tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
Wanakikosi kazi wakiwa katika makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja kulibadili andiko la mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze kuja kusomwa na wafadhili pamoja na wadau wengine mbalimbali.