KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI KUVISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA MKOA WA DAR ES SALAM

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI KUVISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA MKOA WA DAR ES SALAM

March 19, 2015
unnamed
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015
kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 157.
Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
                       Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
                       DAR ES SALAAM
                       19 Machi, 2015.

MWAKILISHI WA BALOZI WA NEWZLAND NCHINI TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI KAMANI OFISINI KWAKE

March 19, 2015


 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwa na Mwakilishi wa Balozi wa Newzland Hatim Amir Karimjee alipomtembelea ofisini kwake
.

Mwakilishi wa Balozi wa Newzland Nchini Tanzania Hatim Amir Karimjee alipomtembelea Waziri Kamani ofisini kwake
 





















Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania awasilisha mada kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

March 19, 2015

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akiwasilisha mada kuhusu  "Exchange Rate Developments in Tanzania and Implications for the Economy"  kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa Semina fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam tarehe 18 Machi, 2015.  Katika mada yake Prof. Ndulu  alielezea pamoja na mambo mengine umuhimu wa Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nje ili kudhibiti mfumuko wa bei na kuipandisha thamani  Sarafu ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine hususan Dola ya Marekani, kuimarisha upatikanaji wa fedha za nje kama dola na kuvutia zaidi wawekezaji nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akifuatilia uwasilishwaji wa mada kutoka kwa Prof. Ndulu (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Irene Kasyanju na kulia ni Balozi Mstaafu Elly Mtango.    
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na  Katibu wa Waziri Membe, Bw. Thobias Makoba  wakimsikiliza Prof. Ndulu ambaye hayupo nchini.
Waziri Membe akielezea jambo mara baada ya Gavana kumaliza kutoa mada 
 Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy (katikati), akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika,  Balozi Joseph Sokoine na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,  Bi Mindi Kasiga wakati wa Semina hiyo.
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia Semina iliyokuwa ikiendeshwa na Prof.  Ndulu.
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia (CFR), Balozi. Omary Mohamed Maundi akiuliza swali kwa Prof. Ndulu wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.
Prof. Ndulu akifafanua jambo
Wakurugenzi kutoka Chuo cha Diplomasia wakisikiliza semina iliyokuwa ikitolewa na Prof. Ndulu. Mwenye tai nyeusi ni Dr. Watengere Kitojo  na kulia ni Dr. Bernard Archiula.
Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Joseph Mwasota akiomba ufafanuzi wa hoja kutoka  kwa Prof. Ndulu ambaye hayupo pichani.
Prof. Ndulu akiendelea kutoa majibu yaliyokuwa yakiulizwa katika semina hiyo.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Paul Kabale (kushoto) akiwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani,  Bw. Mathias Abisai pamoja na  Mkurugenzi wa Idara ya Ununuzi, Bw. Elias Suka wakati wa semina hiyo.
Sehemu nyingine ya washiriki katika Semina hiyo
Prof. Benno Ndulu akibadilshana mawazo na Mkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Watengere Kitojo.  
Waziri Membe akizungumza na  na Waandishi wa Habari 
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Semina. Picha na Reginald Philip na Reuben Mchome

WATOTO ZAIDI YA ELFU KUMI HUZALIWA NA SIKO SELI KILA MWAKA NCHINI

March 19, 2015

Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Robert Mongi (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waliofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa simu 150 aina ya ZTE zitakazotumiwa na wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kulia) akimfungulia boksi lenye moja ya simu kati ya 150 aina ya ZTE, Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Robert Mongi wakati wa makadhiano ya msaada wa simu hizo zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kushoto) akimkabidhi boksi lenye simu 150 aina ya ZTE, Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Robert Mongi, Kwa niaba ya wagonjwa wa sikoseli msaada wa simu hizo zilizotolewa na mfuko (Vodacom Foundation) kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Mtoto Nira Khamis (12) anayesumbuliwa na Ugonjwa wa Siko Seli akionesha simu aina ya ZTE ambayo atatumia kwa ajili ya kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa. Jumla ya simu 150 zimetolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo. Wanaoshuhudia katika picha ni mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kushoto) na Mratibu wa matibabu kwa njia ya teknolojia Dkt . Deogratius Soka.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kushoto)akimkabidhi moja ya simu kati ya simu 150 aina ya ZTE, Mtoto Nira Khamis(12) anayesumbuliwa na ugonjwa wa Siko Seli ambayo atatumia kwa ajili ya kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa. Jumla ya simu 150 zimetolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba maboksi yenye simu aina ya ZTE walipofika kukabidhi msaada wa simu 150 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya kukabidhi msaada wa simu 150 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.

Tatizo la Ugonjwa wa Siko Seli ni kubwa nchini na limekuwa likiongezeka kila mwaka ambapo hadi kufikia sasa watoto wapatao 11,000 nchini wanazaliwa wakiwa na ugonjwa huu hatari ambao husababisha upungufu wa damu mwilini.

Hayo yamebainishwa na Dk Robert Mongi ambaye ni mratibu wa kitengo cha Siko Seli kwa watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa kupokea msaada wa simu 150 za mkononi kwa ajili ya  kuratibu matibabu ya wagonjwa wanaotibiwa kwenye kitengo hicho zilizotolewa na kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya  jamii ya Vodacom Foundation.

Dk. Mongi alisema tatizo la ugonjwa huu ni kubwa na unatibika iwapo mgonjwa atapima na kuanza kutumia madawa mapema ikiwemo kuzingatia masharti anayopaswa kufuata mgonjwa.

Alisema hivi sasa vipimo vya ugonjwa huu vinapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tu ,hali ambayo inasababisha waathirika wa ugonjwa huu wanaoishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuchelewa kupata vipimo na wengi wao kupoteza maisha.”Kutokuwepo na mashine za kufanyia kipimo cha ugonjwa huu za kutosha ni moja ya changamoto kubwa inayokwamisha kuutokomeza kwa kuwa kuna idadi kubwa ya wagonjwa sehemu mbalimbali za nchi wanashindwa kufanya vipimo na kuugundua ugonjwa mapema ili waanze kutumia dawa”.Alisema

Aliishukuru Vodacom Foundation kwa msaada huo wa simu  ambao alisema utawafikia walengwa ambao ni wagonjwa wanaotumia dawa na zitasaidia kuratibu matibabu yao kwa  kupigwa picha  wanapokuwa wanameza dawa wakiwa  majumbani kwao na picha hizo kuwasilishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuwekwa kwenye  mfumo wa kumbukumbu za matibabu ya wagonjwa.

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi msaada huo Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza ambaye aliambatana na baadhi ya wafanyakazi  wa Vodacom alisema kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imeona kuna  umuhimu wa kuwapatia wagonjwa simu ili ziwasaidie wakati wa matibabu yao.

“Tunajua kuwa kuna makundi mengi ya wahitaji katika jamii hivyo tumeona safari hii tuangalie kundi la wagonjwa  wanaotibiwa Siko Seli kwa kuwa ugonjwa huu unazidi kuongezeka na unahitaji jitihada za ziada kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuutokomeza”.Alisema Rwehikiza.


Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imekuwa ikitoa  misaada mbalimbali ya kuleta mabadiliko kwenye jamii hususan katika sekta ya elimu na Afya bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA WASHIRIKA MAJENZI YA KIJANI WA AFRIKA MASHARIKI, JIJINI ARUSHA

March 19, 2015



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, PSPF, Adam Mayingu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi mkutano huo kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo Machi 19, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washirika waliopata tuzo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, kuhusu miradi kadhaa inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa, NHC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Picha na OMR.