TANGA UWASA YAPATA TUZO

September 07, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipokea tuzo ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ya ubora wa kimataifa,kupitia hati ya ISO 9001:2015 ulitokana na ushindi wa kuwa mamlaka bora ya hduuma za Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini kwa Mwaka 2014/2015 wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella walioipata mamlaka hiyo ushindi wa kuwa mamlaka bora ya huduma za maji na usafi wa mazingira nchini mwaka 2014/2015

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiwa na kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi ambapo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mpya wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Salum Shamte,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji

 Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji ikiwemo wafanyakazi wa Mamlaka hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) na wafanyakazi wa mamlaka hiyo

MKUU wa Kitengo cha Uzalishaji Maji katika kituo cha Kusafishia Maji Mabayani Jijini Tanga,Faraji Nyoni akimueleza mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella namna uzalishaji wa maji uzalishaji unavyofanyika na usafishaji wake kabla ya kuwafikia wananchi.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeweza kuwa mamlaka ya kwanza nchini kufikia vigezo vya kupewa leseni ya EWURA ya Daraja la kwanza (Class 1Lesence).

Leseni hiyo ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa kuzindua ripoti ya mwaka 2014/2015 ya mamlaka za maji uliofanyika Mjini Dodoma.

Akizungumza mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Felix Ngamlagosi  alisema kuwa leseni hiyo ilitolewa kwa Tanga Uwasa na kwa sasa ndio mamlaka ya maji pekee nchini iliyo na leseni ya EWURA ya daraja la kwanza nchini.

Alisema kuwa leseni hiyo ya daraja la kwanza imetolewa baada ya EWURA kupitia utendaji kazi wa Tanga Uwasa na kutadhimini viwango vilivyowekwa ili mamlaka ya maji kuweza kupata daraja la kwanza na kujiridhisha kuwa vimefikiwa.

Aidha alisema vigezo ambavyo vimeangaliwa kuwa mamkala bora ni kugharamia uendeshaji wa mamlaka,kugharamia uchakavu wa miundombinu na kuweza kulipia riba za mikopo ya uwekezaji.

  "Lakini pia uwezo wa Mamlaka hiyo kujitegemea kiufundi na kiuendeshaji"

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo imeweza kuwa ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo miongoni mwa mamlaka kubwa 25 za maji zinazotoa huduma katika makao makuu ya mikoa Tanzania bara.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema wao kama mamlaka wataendelea kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendena na viwango vikubwa ili kuendelea kuwa mamlaka bora nchini.

Alisema pamoja na changamoto walizokuwa nazo lakini wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanakabiliana nazo kwa kuwawezesha wananchi waweze kunufaika ana huduma ya Maji kwa kiwango kikubwa .

"Lakini pia sisi kama mamlaka tumejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha huduma za maji zinaimarika sambamba na kujiandaa na fursa ya ujio wa bomba la mafuta utakaoanzia nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ili changamoto ya maji isiwepo wakati wa ujio wa fursa hiyo.

Nusu ya malighafi inayozalisha bia Serengeti ni ya ndani

September 07, 2016

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha,akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusu mpango wa kampuni hiyo kuwawezesha wakulima wa hapa nchi wanaozalisha malighafi zinazotumika kiwandani kwao,ambapo wakulima wapatao 100 wamenufaika katika mkutano uliofanyika mapema leo katika kiwanda cha SBL Mwanza.





Waandihsi wa habari wakifuatilia kwa makin maelezo toka kwa Mkurungezi wa mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha mapema leo katika kiwanda cha SBL Mwanza.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha,akiongoza waandishi wa habari kutembelea baadhi ya maeneo ya kiwanda cha SBL Mwanza.



Meneja wa upishi wa bia wa Kiwanda cha Serengeti Rolinda Samson(Brewing Manager) akitoa ufafanuzi wa jambo jinsi utengenezaji wa bia unavyofanyika kwa  waandishi wa habari jijini Mwanza mapema leo.


Mwanza, Septemba 07, 2016 - Hamasa inayotokana na mradi wa kilimo biashara wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuwawezesha wakulima wa mahindi, mtama  na shayiri katika maeneo mbalimbali nchini  imewezesha kampuni hiyo ya bia kuongeza kiwango cha malighafi  inayotumika  kutoka ndani ya nchi kufikia  tano 10,000 sawa na asilimia 60  ya malighafi yote inayotumia  kuzalisha bia kwa mwaka.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika katika kiwanda cha SBL  Mwanza leo,  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, John Wanyancha  alisema  aina  sita za bia zinazozalishwa na kampuni hiyo zina asilimia 100  ya malighafi inayoizalishwa  ndani  ikiwa ni matokeo ya mradi wa kilimo biashara  ambao ulianza  miaka mitatu iliyopita.

Aina hizo za bia ni pamoja na Pilsner, Kibo Gold, Kick, Uhuru na Senator Lager.  Kwa mujibu wa Wanyancha  bia mbili za Pilsner na Kibo Gold  zimeshinda tuzo  za kimataifa mwaka huu ikiwa ni kielelezo cha ubora wa hali ya juu wa bidhaa hizo..

Kupitia programu hiyo kampuni ya Bia ya Serengeti  inatoa mbegu zilizo na ubora  kwa wakulima bure, kuwaunganisha na taasisi za kifedha  ili kupata mitaji  inayohitajika  kwa ajili ya kilimo  cha mashamba makubwa  hali kadhalika  kuwaunganisha na wasambazi wa mbolea na dhana nyninginezo za kilimo. Kwa upande wake SBL imekuwa ikinunua  mazao yote  kutoka kwa wakulima hawa na hivyo kuwawezesha kulipa mikopo ya mitaji pamoja na kuboresha hali zao za kiuchumi.

“Hadi sasa  mradi huu umeshawanufaisha  wakulima zaidi ya 100 kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Arusha, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Shinyanga na  Dododoma ambao kwa pamoja wanalima takribani ekari 20,000,”  alisema mkurugenzi huyo.

Wanyancha alisema  kwamba kampuni hiyo  imepanga kuendelea kupanua programu hiyo  ili kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kufikia lengo  la kuongeza upatikanaji wa malighafi kutoka ndani hadi asilimia 80 kwa mwaka huu. Mbali na manufaa mbalimbali ya kichumi kwa wakulima, bali zitokanazo na malighafi zinazozalishwa nchini  ni za bei nafuu ikilinganishwa na zile zinazotengeneza na malighafi kutoka nje ya nchi.

MUWSA YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MANDELA MJINI MOSHI.

September 07, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.Said Mecky Saidiq akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ,Joyce Msiru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msing Mandela.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq Madawati kwa ajili ya shule ya Msingi Mandela iliyopo Manispaa ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq (katikati) akiwa ameketi kwenye Dawati na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru pamoja na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela.
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandea wakiwa wameketi katika madawti yaliyotolewa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikabidhi madawati kwa mkuu wa shule ya msingi Mandela ,Pegi Michael.

Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Source East Africa B2B Trade platform for craft products in offing

September 07, 2016
Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....


Mratibu wa Maonyesho ya Sanaa za Mikono kwa Afrika Mashariki Bi. Nakaaya Sumari akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) na baadhi ya wadau waliokuja kwenye uzinduzi wa Maonyesho hayo kwa vyombo vya habari, vinavyotarajiwa kufanyika mwezi septemba 23 hadi 25 2016, Jijini Arusha



Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....














Ramadhani Mvungi (Star Tv ) na Ihucha Adam (EABC-PR)wakiteta jambo....
Mpiga Picha Kapigwa Picha Akionyesha Picha kwa wapigwa picha na mpiga Picha...
Mtangazaji Maarufu wa AZAM TV (Idd Uwesu ) katika Ubora wake....

ADAM IHUCHA,


CRAFTS producers in East Africa will soon be able to sell their products to international markets following the plans to establish an annual professional for Business-to-Business (B2B) trade fair for Home Décor, Fashion Accessories and Lifestyle products in the region.

Currently, there is no B2B trade platform for the crafts sector in the whole of East African region.

The Africa and Middle East World Fair Trade Organization (WFTO) regional director, Mr Bernard Outah said there is need to establish B2B so that producers could easily sell their products to any country of their choice without problem.
He said, at the moment, the only option for producers to reach regional or international buyers is to travel around the region in search of potential buyers or to participate in trade fairs in South Africa, West Africa or International trade fairs in Europe or the US. He said the high cost of participation fails most of African crafts producers from attending international trade fairs.
“Failure to access market opportunities is one of the key challenges that face most of African crafts producers in East African region,” he said. According to Mr Outah, the establishment of B2B will enable East African crafts producers to excel in the area and boost their businesses at both local and international levels.
Meanwhile, the public has been urged to recognize the crafts sector as a key economic sector in the region and offer required support so that it can unfold its potentiality. CBI programme manager for the export coaching programme in East Africa Ms Heiydy van der Ploeg said there is need to promote and give support to craft sector so that it could help in building up East African countries economies.
According to UNESCO, the crafts sector is the second largest employer in the developing world behind agriculture. Most of those engaged in crafts are majority women with little or no education.
The global crafts sector is valued at USD 34bn/- per annum and 65 percent of global crafts exports come from developing countries. East Africa is one of the most important crafts producing regions on the African continent.
Its geographical location has made it a melting pot of different cultures, resulting in a rich diversity of crafts skills and products.
The Chief Executive Officer (CEO) for TradeMark East Africa (TMEA), Mr Frank Matseart said crafts are important part of the East African trade story but it receives little input from various stakeholders.
He added that a growing tourism sector in the region offers the potential to sell products to tourists through souvenir and gift shops.
“Many hotels and lodges, besides sourcing products for their own in-house gift shops also look for interior decoration products to decorate their houses,” he said.
For the first time, professional craft trade fair is scheduled to take place in the country from September 23rd to 25th, this year.