NAPE AANZA ZIARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

February 05, 2015

  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali,  Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki ( wa pili kutoka kushoto) akielezea masuala mbali mbali yanayohusu tasinia ya habari wakati wa mkutano na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye uliofanyika kwenye ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali,Tazara jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa kikao chake na Viongozi na waandishi wa Magazeti ya Serikali alipowatebelea leo ikiwa sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa Magazeti ya Serikali.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali,  Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimina na Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania kwenye ofisi za magazeti hayo mtaa wa Mwinyijuma,Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyeshwa sehemu ya waandishi wanapoandaa habari na Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na baadhi ya viongozi na wahariri wa gazeti la Raia Tanzania na Raia Mwema.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania.
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN.

February 05, 2015

she`1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
shei2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] shei3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (kulia kwa Rais ) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
 MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO

February 05, 2015
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Februari, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamedkay2 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Februari 5, 2015 unnamedkay4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wananchi kutoka wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe waliotembelea Bunge mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wao wa jimbo la Njombe Magharibi, Gerson Lwenge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Februari 5, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)pinda 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimaa John Kwegyir, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Februari 5, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONGOZA SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA

February 05, 2015


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akihutubia katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini Mkoni Rukwa leo tarehe 04/02/2015 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga. Kaulimbiu ya maaadhimisho hayo ikiwa “Fursa ya kupata haki: Wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau”. Katika hotuba yake hiyo alisema ipo haja kubwa kwa Serikali kubadili sheria zake ili lugha ya mahakamani na hukumu ziandikwe kwa kiswahili. Kwa upande wa wananchi aliwaasa kujiepusha na tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kudumisha amani nchini.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha Jeshi la Polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoani Rukwa leo tarehe 04/02/2015.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo katikati akisoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya sheria Mkoani Rukwa ambapo aliwataka mahakimu wote Mkoani Rukwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu miongozo ya mahakama ili kusaidia uharakishwaji wa utoaji haki kwa wananchi kwa wakati. Aliwaeleza pia wadau wote wa sheria wakiwepo mawakili wa kujitegemea kuwa mashauri yote ya kesi yatakua yakisimamiwa na kutolewa maamuzi na mahakama na sio mawakili kutaka kuingilia utendaji wa mahakama.
Baadhi ya wadau na viongozi wa Sheria na Serikali katika meza kuu.
Sehemu ya mahakimu, mawakili, wanasheria na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)

KIZUGUTO AULA TFF,SASA AWA OFISA HABARI MPYA

February 05, 2015
TFF YAPATA OFISA HABARI MPYA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto kuwa Ofisa Habari kuanzia Februari 1 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Kizuguto alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Young Africans, nafasi aliyoitumikia kwa miaka miwili.

Kizuguto ana Stashahada ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha LEARN IT cha Dar es Salaam. Pia ana ujuzi wa kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta na uchambuzi wa mifumo ya kompyuta.

Mei mwaka jana, Kizuguto aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhudhuria mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao (TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.

TFF inamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.

KAMATI YA NIDHAMU YAADHIBU TISA
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kinidhamu.

Katika kikao chake kilichofanyika juzi (Februari 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Kamati hiyo imewafungia mwaka mmoja viongozi wawili wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza kwa kuwashawishi wachezaji wa Mwanza Queens kugomea uamuzi halali.

Sophia Tigalyoma (Mwenyekiti) na Katibu wake Hawa Bajanguo walitiwa hatiani kwa kuwashawishi wachezaji kugomea uamuzi wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF kutupa rufani yao dhidi ya Kigoma.

Kocha wa Polisi Tabora, Eliakim Christopher amefungiwa mechi kumi na kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 39(2) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kutiwa hatiani kwa kumtukana refa wakati wa mechi kati ya timu yake na Panone FC iliyochezwa mjini Moshi.

Wachezaji wa JKT Oljoro FC, Dihe Makonga, Swaleh Idd Hussein, Ramadhan Mnyambegu na nahodha Shaibu Nayopa wamefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 300,000 kila mmoja kwa kuzingatia kanuni ya 36(10) ya FDL kutokana na kufanya vurugu kwenye mechi kati yao na Burkina Faso iliyochezwa mjini Morogoro.

Mtunza Vifaa (Kit Man) wa JKT Oljoro FC, Eliud Mjarifu amefungiwa miezi sita na kupigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumpiga Kocha wa Burkina Faso, CR Mwakambaya kwenye mechi kati ya timu hizo iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pia Mjarifu amepewa onyo kali na kutakiwa kutorudia tena kutenda kosa, kwani hata mwenendo wake wakati wa shauri hilo ulionyesha utovu wa nidhamu mbele ya Kamati.

Naye Mtunza Vifaa wa Rhino Rangers FC, Albert Mbuji amefungiwa miezi sita na faini ya sh. 200,000 kwa kupatikana na hatia ya kuwatukana na kugomea uamuzi wa marefa kwenye mechi dhidi ya Polisi Dodoma. Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya FDL.

Kamati hiyo imeondoa malalamiko dhidi ya Ofisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire kwa vile refa Israel Mujuni Nkongo ambaye ni mlalamikaji hakufika kwenye shauri hilo.

Nkongo alimlalamikia Bwire akidai alitoa maneno yenye kuweza kuchochea chuki dhidi yake kwa waamuzi, kwani kupitia redio 100.5 Times FM, Bwire alidai refa huyo ndiye aliyeshinikiza kuondolewa kwa refa Mohamed Theofil kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Pia Kamati hiyo imemkuta bila hatia Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda ambaye TFF ilimlalamikia kuwa akiwa mtendaji mkuu wa chama hicho alishindwa kuhakikisha timu ya Singida inaingia uwanjani kucheza na Dodoma kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake.

Kamati ilikubaliana na utetezi wa Gunda kuwa, jukumu la timu hiyo lilikuwa mikononi mwa viongozi wa TWFA Singida, na tayari SIREFA kupitia Kamati yake ya Nidhamu ilishatoa adhabu kwa viongozi wa timu hiyo kutokana na kitendo hicho.

Nayo malalamiko ya Polisi Tabora FC kutaka mechi yao dhidi ya Toto Africans FC irudiwe kwenye uwanja huru (neutral ground) kwa madai ya kuchezeshwa zaidi ya muda unaotakiwa, na kutokuwepo ulinzi wa kutosha kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekataliwa.

Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu za Mwadui FC na Polisi Mara FC dhidi ya Toto Africans kwa kumchezesha mchezaji Ladislaus Mbogo bila kuonyesha leseni yake yasikilizwe haraka na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa vile si ya kinidhamu.

Wakati huo huo, Kamati ya Nidhamu inaendelea na kikao chake leo (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko mengine ya kinidhamu yaliyofikishwa mbele yake.

TFF YAONYA KUHUSU UENDESHAJI MPIRA WA MIGUU
Kutokana na matatizo mbalimbali ya kiutendaji yaliyojitokeza kwenye uendeshaji, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa hadhari kuwa shughuli zote za mpira wa miguu zinazohusu mkoa wowote wa Tanzania Bara zitasimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa husika, yakiwemo mashindano ya Kombe la Taifa la Wanawake.
  
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Tanzania mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Wahasibu

February 05, 2015

Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu mkutano utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12  mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile jana jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika nchini.
Mhasibu Mkuu wa Serikali Mwanaidi alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Katika mkutano huo, mada mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa zikilenga kwa lengo la kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika masuala ya hesabu za serikali na kutoa fursa ya kuwa na jukwaa kwa ajili ya washiriki ili kufanya tathmini kwa kujadiliana na kushirikishana uzoefu mbali mbali.
Aidha, mkutano huo unalenga kuhamasisha maendeleo ya watendaji wahasibu wa Serikali na kutoa mafunzo stahiki kupitia utekelezaji wa program shirikishi kwa kujifunza uzoefu wa masuala mbali mbali ndani ya nchi wanachama.
Mkutano wa wahasibu hao unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1000 wakiwemo Wahasibu wakuu 14 kutoka nchi wanachama na wadau wengine.
Ujio wa wageni hao pamoja na ushiriki wao katika mkutano wa siku tano utakuwa wa tija na fursa muhimu katika utoaji wa huduma za jamii wakati wote watakapokuwa nchini.
Aidha, katika mahitaji yao ya malazi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi, makadirio ni kwamba kila mgeni anaweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja, hivyo basi kwa hesabu za haraka haraka kutakuwa na matumizi ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano katika muda wa siku tano tu.
“Wito wangu kwa watanzania, nawaomba wajitokeze kushiriki katika mkutano huu wa ESAAG wa 2015, hivyo natoa rai kwa wataalam, wahasibu na wadau wetu wote kwa ujumla wao ili tuweze kushirikiana kuufanikisha mkutano huu wa kimataifa unaofanyika nyumbani, Tanzania” alisema Mwanaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile amesema kuwa nchi washiriki zinazounda umoja huo ni Botswana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
Azizi aliwahakikishia washiriki wote kuwa maandalizi ya mkutano huo katika masuala ya usafiri, usalama na malazi yapo katika hatua nzuri na kamati yake imejipanga vema ili mkutano huo uwe wa mfano wa kuigwa kwa nchi zote wanachama watakapopata fursa ya kuandaa mkutano wa mwaka katika nchi zao.
ni wa serikali wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika,Kwa bahati nzuri chama hiki kikiwa na malengo yafuatayo
ESAAG ni chama cha wahasibu wakuu ambacho kilizaliwa miaka 20 iliypoita Arusha hapa nchini mwaka 1995 na mkutano wa mwaka huu wa 22 wa ESAAG unaongozwa na kauli mbiu “Uimarishaji na usimamizi wa fedha kwa ajili ya Maendeleo ya kijamii na Kiuchumi katika kanda’’.
RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN

February 05, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akimlaki na kisha kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake
Ikulu jijini Dar es salaam jana, Jumatano, Februari 4, 2015. PICHA NA
IKULU ir2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Mambo ya Nje
wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake
baada ya kufanya mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jana, Jumatano, Februari 4, 2015. PICHA NA
 
ir3 
………………………………………………………………………………………………..
Tanzania imesema kuwa dhamira yake ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi inavyoruhusu. Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka maendeleo ya watu bila usumbufu na matishio ya ugaidi. Mambo hayo mawili yamejadiliwa leo, Jumatano, Februari 4, 2015 katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif. Mheshimiwa Zarif amewasili nchini leo akitokea Burundi katika ziara ambayo pia imemfikisha Kenya, Uganda na Rwanda akifuatana na maofisa wa Serikali na kundi kubwa la wafanyabiashara wa Iran. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif kuwa Tanzania bado inakusudia kufungua ubalozi mjini Teheran, mji mkuu wa Iran, kama ilivyoahidi na kuwa itafanya hivyo hali ya kifedha na kiuchumi itakaporuhusu. Rais ametoa maelezo hayo kufuatia ombi la Waziri Zarif kukumbushia umuhimu wa kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania katika Iran. “Tunakusudia kufungua balozi katika nchi marafiki ambako kwa sasa hakuna balozi ikiwamo Jamhuri ya Kiislam ya Iran. Katika Afrika, kwa mfano, tunapanga kufungua balozi katika Namibia, Angola, Algeria na Ghana. Hizi ni nchi rafiki ambazo baadhi yake zimekuwa na balozi katika Tanzania tokea uhuru wetu. Mbali na Iran katika Asia, tunaangalia nchi kama Uturuki, Qatar na Kuwait na nyingine marafiki,” Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif. Kuhusu mapambano dhidi ya magaidi, Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania na Iran kuwa na msimamo ulio sawa wa jinsi ya kukabiliana na ugaidi. “Wakati wote, sote tunakabiliwa na matishio ya ugaidi na hivyo tunalazimika wakati wote kuwa macho na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi. Sisi Tanzania bado tunakumbuka shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani hapa nchini. Ulishambuliwa Ubalozi wa Marekani lakini watu wote waliopoteza maisha yao ni Watanzania.” Rais Kikwete na Mheshimiwa Zarif pia wamejadili jinsi gani Tanzania na Iran zinavyoweza kuongeza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika maeneo mbali mbali ya uchumi na Rais Kikwete amemweleza Waziri fursa zilizoko katika sekta za nishati na reli. Waziri Zarif pia amemkumbusha Rais Kikwete mwaliko wa kumwomba Rais Kikwete kutembelea Iran kwa ziara ya Kiserikali. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.
4 Februari, 2015