RAIS AMTEUA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI (TPDC)

December 18, 2014

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.
Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
• Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
• PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
• MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
• BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994
UZOEFU WA KAZI:-
• Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
• 2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
• 2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
• 1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
• 1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.
Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.
​Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014

POLISI TANGA YAFANIKIWA KUOKOA NYAYA ZA UMEME ZENYE THAMANI YA SH.MILIONI 7 ZILIZOKUWA ZIMEFICHWA

December 18, 2014

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kuokoa nyaya za umeme zenye thamani ya sh milioni 7 zilizokuwa zimefichwa porini kwenye Kijiji cha Magoma wilayani Korogwe ambazo zilikuwa kwenye mchakato wa kusafirishwa kwa ajili ya kuziuza kwenye maeneo mengine.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki ameimbia Tanga Raha Blog Ofisi kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi ambapo nyaya hizo ziliibiwa na watu wasiofahamika na kwenda kuzihifadhi kwenye eneo hilo ambazo zilionekana .

Alisema kuwa ugunduzi wa nyaya hizo uligunduliwa na Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Suleimani Kalulu mkazi wa Kwamkole ambaye alibaini kuwepo kwa kasora ya waya wenye urefu wa mita 1080 ambazo zilikuwa zimeibiwa.
 
Kaimu Kamanda huyo alisema baada ya kugundua kasoro hiyo walianza msako wakishirikiana na askari ndipo walipobaini zilikuwa zimefuchwa porini .

Aidha alisema kutokana na tukio hilo hakuna mtu yoyote ambaye anashikiliwa Jeshi hilo wakati askari wakiendelea na msako mkali ili kuweza kuwabaini wahusika wake ili waweze kuchukulia hatua.

  “Kama ujavyojua sisi tulipata taarifa hizo na tunajipanga vilivyo kuhakikisha tunafanikisha kupatikana na kwa bahati nzuri kwenye msako wetu tulifanikiwa kuzikuta zimetelekeza porini “Alisema Kaimu Kamanda Ndaki.
 
Hata hivyo,Kaimu Kamanda Ndaki aliwataka wananchi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapowabaini wezi wa miundombinu ya umeme ikiwemo nyaya ambazo hupelekea kuliingiza shirika hilo kwenye hasara ili waweze kuchukua hatua .

COASTAL UNION YACHEZA SOKA SAFI,MWADUI YAILAZIMISHA SARE MKWAKWANI LEO

December 18, 2014
KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOLAZIMISHWA SARE NA MWADUI YA SHINYANGA LEO 

WAGOSI WA KAYA WAKIPIGA DUA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO.
KIKOSI CHA TIMU YA MWADUI YA SHINYANGA KILICHOCHEZA NA COASTAL UNION LEO

KUSHOTO NI KOCHA MKUU WA COASTAL UNION  JAMES NANDWA AKIBADILISHANA MAWAZO NA MKURUGENZI WA BENCHI LA UFUNDI COASTAL UNION MOHAMED KAMPIRA KABLA YA KUANZA MECHI YA KIRAFIKI KATI YA COASTAL UNION NA MWADUI YA SHINYANGA.
KUTOKA KULIA NI MENEJA WA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI,KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI WAKIFUATILIA MCHEZO WA LEO WAKIWA SAMBAMBA NA MASHABIKI WENGINE WA SOKA MKOANI TANGA.

KOCHA WA COASTAL UNION JAMES NANDWA AKITOA MAWAIDHA KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO LEO

 KOCHA MKUU WA COASTAL UNION,JAMES NANDWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO MARA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YAKE NI MWADUI YA SHINYANGA.

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA AFUNGUA SEMINA YA WAENDESHA MAGARI LEO TANGA BEACH RESORT.

December 18, 2014
KUSHOTO NI MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI AKIINGIA UKUMBINI AKIWA NA Rais wa Chama cha mashindano ya mbio
za Magari Tanzania (AAT), Nizar Jivan

WASHIRIKI WAKIWA WAMESIMAMA WAKATI MGENI RASMI AKIINGIA UKUMBINI.

MEZA KUU






Rais wa Chama cha mashindano ya mbio za Magari Tanzania (AAT), Nizar Jivan akimkabidhi cheti Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort ,Joseph Ngoyo ikiwa ni kutambua mchango wa hotel hiyo mara baada ya kufunguliwa semina ya mashindano ya magari ambayo iliwahusisha maofisa wa vilabu kutoka mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro,Arusha,Dar es Salaam,
Rais wa Chama cha mashindano ya mbio za Magari Tanzania (AAT), Nizar Jivan akimkabidhi cheti Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort ,Joseph Ngoyo ikiwa ni kutambua mchango wa hotel hiyo mara baada ya kufunguliwa semina ya mashindano ya magari ambayo iliwahusisha maofisa wa vilabu kutoka mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro,Arusha,Dar es Salaam,


Mwenyekiti wa Chama cha Magari Mkoani

Tanga (TSM)  Mstaafu ,Hussein Noor (Makoroboi) kushoto akipokea cheti Rais wa
Chama cha mashindano ya mbio za Magari Tanzania (AAT), Nizar Jivan
ikiwa ni kutambua mchango mara baada ya kufungua semina ya mashindano
ya magari ambayo iliwahusisha maofisa wa vilabu kutoka mikoa ya
Morogoro, Kilimanjaro ,Arusha,Dar es Salaam iliyofanyika kwenye Hotel
ya Tanga Beach Resort mjini hapa,
wa kwanza kushoto  ni Mwenyekiti wa Chama cha Magari Mkoani Tanga,Akida Machai akiwa sambamba Meneja Mkuu wa Hotel ya Tanga Beach Resort leo wakati wa semina ya waendesha magari iliyofanuyika hotel ya Tanga Beach Resort leo

TUME YA MIPANGO WATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA

December 18, 2014


Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Bandari ya Bukoba, walipofika kujionea bandari hiyo kongwe iliyopo kwenye fukwe za Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wengine ni baadhi ya wajumbe wa msafara huo kutoka kushoto ni Bw. Omary Abdallah, Bibi Zena Hussein (Wapili kushoto) na Bw. Julius Edward (Kulia).
Madhari ya gati la Bandari ya Bukoba.
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye ngazi za kupandia kwenye meli zinazotia nanga kwenye Bandari ya Bukoba.
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye Ofisi za Bandari ya Bukoba. Jengo la Ofisi hiyo limejengwa takriban miaka 70 iliyopita.
Sehemu ya kupumzikia abiria ya Bandari ya Bukoba.
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye moja ya maghala ya kuhifadhia mizigo kwenye Bandari ya Bukoba. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

ZIARA YA KIKAZI YA WANAHABARI KATIKA UJENZI WA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI GEREZA IDETE MKOANI MOROGORO

December 18, 2014


Wafungwa wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama inavyoonekana katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na trekta wakiwa gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa nchini. Kwa wastani Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku.
Mkuu wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa.
Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifanya mahojiano na Mkuu wa Gereza Idete(hayupo pichani) walipofanya ziara yao ya kikazi Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
MAMA KIKWETE AWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA KUWEKA AKIBA NA KUKOPA ILI KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA

MAMA KIKWETE AWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA KUWEKA AKIBA NA KUKOPA ILI KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA

December 18, 2014
unnamed
Na Anna Nkinda – Maelezo
18/12/2014 Vijana wametakiwa kujiunga na vikundi vya kuweka akiba na kukopa  ili kuchangia mawazo yao  na ubunifu na wakati huo huo wanajitengenezea mazingira ya kujiajiri kwani wengi wao wana elimu na ujuzi walioupata  masomoni lakini wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Rai hiyo imetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua Umoja wa Vikundi vya kuweka Akiba vilivyopo chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI) katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Usafirishaji jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA alisema kupitia vikundi hivyo vijana wanaweza kupata mitaji midogomidogo pamoja na mafunzo ya kuwawezesha kuanzisha biashara na kujiajiri. Kwani mfumo huo wa vikundi na mafunzo ni moja ya njia za kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na hivyo kupunguza tatizo la ajira.
Kwa upande wa wanachama wa UWAMAKI aliwasisitiza  kutoridhika na mafanikio waliyoyapata bali waendelee kutafuta njia za kupiga hatua hususani kupata utaalamu wa kuboresha bidhaa zao , kutafuta masoko zaidi na kufanya ubunifu wa kuweza kuvumbua bidhaa na biashara nyingine tofauti ili kuepukana na ushindani wa soko.
“Mnapokuwa na bidhaa zinazofanana mtakuwa katika mazingira ya kushindania soko jambo ambalo litapunguza kiasi cha mauzo ambayo ndiyo pato lenu wajasiriamali. Jitihada ifanywe ili kuweza kutafuta watalaam ambao watawapa mafunzo ya kukuza biashara”, alisema Mama Kikwete.
Akisoma risala ya vikundi hivyo Katibu wa UWAMAKI , Mwajuma Waziri aliishukuru Taasisi ya WAMA kwa kuwawezesha  kuwa na vikundi na kupata mafunzo ya kuweka akiba, elimu ya kibenki, usindikaji wa vyakula na huduma ya bima ya afya.
Waziri alisema, “Kutokana na mafunzo hayo tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali kama vile kutengeneza sabuni za maji za kufulia, sabuni za kuoshea vyombo na kusafishia tairizi, siagi ya karanga na batiki na hatimaye tumeweza kufungua akaunti yetu ya Umoja katika benki ya wanawake (TWB)”.
Katibu huyo alisema walianza na kikundi kimoja kwa kujiwekea hisa moja kwa thamani ya shilingi 1000 pia waliweza kukopesha kiasi cha shilingi 6,300,000 mpaka mwisho wa mwaka walivuna shilingi 12,750,000.
“Hadi sasa tunavikundi 11 vyenye wanachama 274 kati ya hao wanaume ni wanane katika vikundi hivi  tumeweza kukopesha kiasi cha shilingi 47,500,000/= na kufikia mavuno ya shilingi 79,739,000 kwa mwaka”, alisema.
Alimalizia kwa kusema lengo la kuunda umoja huo ni kushirikiana katika matatizo ya kijamii, kuunda SACCOS na kutafuta masoko ya bidhaa zao.
Taasisi ya WAMA inasimamia mradi wa kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mafunzo kupitia vikundi katika mikoa ya Dar es Salaam Lindi na  Pwani hadi kufikia Septemba mwaka huu jumla ya watu 18,000 wamefikiwa kwa kupitia vikundi 688 vilivyoundwa na tayari shilingi milioni 227 zimekusanywa na kukopeshwa.

ZIDANE AMPA CASILLAS KIPA BORA DUNIANI, ATAJA KIKOSI CHAKE BORA, YAYA TOURE NDANI

December 18, 2014
ZIDANE (KULIA) AKISALIMIANA NA IKER CASILLAS.
Kocha wa timu ya vijana ya Real Madrid maarufu kama Zizou, amesema tayari kipa Iker Casillas amerejea kwenye ubora wake.

Kiungo huyo nyota wa zamani wa Real Madrid amesema Casillas amerudi katika kiwango chake cha juu.

Ingawa kipa wa Bayern Munich na Ujerumani Manuel Neuer ndiye anaonekana bora hadi kuingia kuwania FIFA Ballon d'Or  2014 akiwa na Cristiano Ronaldo na  Leo Messi, mkongwe huyo amesisitiza, Casillas sasa amerudi kwenye nafasi yake.

Akihojiwa na runinga ya Canal Plus ya Ufaransa, Zidane alisisitiza, Casillas ndiye kipa bora zaidi duniani kwa kipindi cha miaka kumi.

Wachezaji wengine aliowasifia ambao wanacheza katika kiwango cha juu ni mabeki wa Madrid, Sergio Ramos, Pepe na Marcelo pamoja na Dani Alves kutoka Barcelona.

Kwa upande wa kiungo, Zidane ameweka wazi kwamba anavutiwa na Mwafrika kutoka Ivory Coast, Yaya Touré anayekipiga Man City, pia Luka Modric wa Madrid kutokea Croatia.


Kwa upande wa washambuliaji, amewataja wanne ambao anaamini ni bora kuwa ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na Karim Benzema.

Ziara ya naibu waziri maji katika halmashauri ya Meru, kata ya Makiba leo

December 18, 2014
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiongozana na ujumbe wake kutembelea Kata ya Makiba iliopo kwenye kijiji cha Valeska Wilayani Arumeru akiwa katika ziara ya Kikazi leo.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akisikiliza maelezo ya mradi wa maji toka kwa mmoja wa watendaji katika Kata hiyo.Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makiba,Bi. Mwanaid Kimu.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiangalia kisima cha maji katika kijiji cha Majengo kata ya Makiba.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiwa katika ukaguzi wa tanki la maji kijiji cha Patanumbe Kata ya Makiba.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akivishwa vasi la kimila wakati alipokutana na wanakijiji wa Patanumbe Kata ya Makiba Wilayani Arumeru.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akijibu maswali mbalimbali yaliyokulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na maji leo.