UNESCO IMEAHIDI KUWASAIDIA WATANZANIA KUKABILI DHULUMA DHIDI YA WANAOISHI NA ALBINISM

UNESCO IMEAHIDI KUWASAIDIA WATANZANIA KUKABILI DHULUMA DHIDI YA WANAOISHI NA ALBINISM

May 20, 2015
DSC_0349
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Mwanza
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeahidi kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.
Mwakilishi huyo wa Unesco amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa mkoa kumsalimia na kumweleza hatua zinazochukuliwana Unesco katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism.
Akifafanua zaidi alisema kwamba UNESCO haijatenga fedha zitakazotumika kuendesha kampeni mahsusi bali itatumia uwezo wa kiufundi uliopo kwa wataalamu walionao na kwamba wanakusudia kuona kwamba miaka 15 ijayo watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa huru pasipo na viashiria vya kuhatarisha maisha vinavyosababishwa na mauaji ya watu wenye albinism.
Akimkaribisha Bi Zulmira ofisini kwake, Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo alisema kwamba ingawa kuna utulivu katika kipindi hiki mkoani Mwanza, bado mkoa wake unaendelea kukabiliana na viashiria vinavyosababisha ukatili kwa watu wenye albinism na wazee.
Bwana Magesa alisema imani potofu zilizopo zinazosadikika kufanikisha biashara za uvuvi wa samaki, uchimbaji wa madini na wanasiasa kuendelea na madaraka ni miongoni mwa sababu kubwa za mauaji hayo yaliyoitia doa jeusi jamii ya kitanzania nje ya mipaka.
Alisema kwamba jitihada zinafanywa kukabiliana na imani hizo potofu kwa kuihamasisha jamii kutoziamini na kwamba madaraka na utajiri unatokana na juhudi, kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.
Aidha amesema mkoa wake umekuwa ukihakikisha kwamba makundi yanayotumika kuua watu wengine kwa kushirikisha jamii yanavunjwa na pia kuwachukulia hatua kali wote wanaobainika kushiriki kwa njia moja au nyingine.
Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa alisema kwamba hali ya amani itatawala pale tu watu watakapobaini kwamba kuua ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kosa la jinai.
Alisema pindi binadamu watakapokiri kwamba binadamu wote ni sawa na kuishi na albinism sio ‘mzimu’ watabadili mwelekeo mzima wa fikra potofu kimaisha na kuishi kwa amani na kuthaminiana.
Bi Zulmira alimwambia mkuu wa mkoa kwamba UNESCO kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha makongamano yenye lengo la kushirikisha jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayo changia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhuluma zinazofanya dhidi ya watu wenye albinism.
DSC_0373
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) akizungumza na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyeambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Mwaza, Faisal Issa.
Warsha hizo zitafanyika kwa wakati tofauti katika kipindi cha wiki mbili wilayani Sengerema, Misungwi, Msalala na Bariadi. Warsha hizo zilizoanzia Sengerema Jumatano na kumalizika Ijumaa zitafuatiwa na Misungwi Mei 25 hadi 27, Msalala Mei 28 hadi 30 na Bariadi kuanzia Mei 28-30.
Katika warsha hiyo pamoja na kujadili mada mbalimbali, mijadala itahusisha viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa kidini na kimila na hoja kubwa itakayojadiliwa ni dhana ya kisayansi ya albinism, mitazamo ya jamii kuhusu dhana hiyo, makundi mbalimbali ndani ya jamii, tofauti kati ya utamaduni na asili.
Pia watajadili kubainisha na kuanisha matatizo, changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism na kuchambua mambo yanayochangia uwepo wa changamoto na hatari kwa watu wenye alibinism.
Katika majadiliano hayo pia mikakati inayoweza kupunguza au kumaliza kabisa matatizo changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism katika jamii yetu itatazamwa.
Watoa mada wanatarajiwa kutoka katika halmashauri, vyama vinavyotetea maslahi ya albinism, mbunge anayetetea maslahi ya watu wenye albinism Al-Shaymaa Kwegyir na mwakilishi kutoka baraza la taifa la dawa asilia.
DSC_0357
DSC_0369
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiendelea na maongezi na ugeni huo ofisini kwake jijini Mwanza.
DSC_0377
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia), akielezea nia ya Shirika lake kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism nchini alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ofisini kwake jijini Mwanza.
DSC_0391 kawaida DSC_0349 Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog). Na Mwandishi wetu, Mwanza 

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeahidi kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism. Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo. Mwakilishi huyo wa Unesco amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa mkoa kumsalimia na kumweleza hatua zinazochukuliwana Unesco katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism. Akifafanua zaidi alisema kwamba UNESCO haijatenga fedha zitakazotumika kuendesha kampeni mahsusi bali itatumia uwezo wa kiufundi uliopo kwa wataalamu walionao na kwamba wanakusudia kuona kwamba miaka 15 ijayo watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa huru pasipo na viashiria vya kuhatarisha maisha vinavyosababishwa na mauaji ya watu wenye albinism. Akimkaribisha Bi Zulmira ofisini kwake, Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo alisema kwamba ingawa kuna utulivu katika kipindi hiki mkoani Mwanza, bado mkoa wake unaendelea kukabiliana na viashiria vinavyosababisha ukatili kwa watu wenye albinism na wazee. Bwana Magesa alisema imani potofu zilizopo zinazosadikika kufanikisha biashara za uvuvi wa samaki, uchimbaji wa madini na wanasiasa kuendelea na madaraka ni miongoni mwa sababu kubwa za mauaji hayo yaliyoitia doa jeusi jamii ya kitanzania nje ya mipaka. Alisema kwamba jitihada zinafanywa kukabiliana na imani hizo potofu kwa kuihamasisha jamii kutoziamini na kwamba madaraka na utajiri unatokana na juhudi, kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo. Aidha amesema mkoa wake umekuwa ukihakikisha kwamba makundi yanayotumika kuua watu wengine kwa kushirikisha jamii yanavunjwa na pia kuwachukulia hatua kali wote wanaobainika kushiriki kwa njia moja au nyingine. Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa alisema kwamba hali ya amani itatawala pale tu watu watakapobaini kwamba kuua ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kosa la jinai. Alisema pindi binadamu watakapokiri kwamba binadamu wote ni sawa na kuishi na albinism sio ‘mzimu’ watabadili mwelekeo mzima wa fikra potofu kimaisha na kuishi kwa amani na kuthaminiana. Bi Zulmira alimwambia mkuu wa mkoa kwamba UNESCO kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha makongamano yenye lengo la kushirikisha jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayo changia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhuluma zinazofanya dhidi ya watu wenye albinism. DSC_0373 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) akizungumza na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyeambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru (wa tatu kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Mwaza, Faisal Issa. Warsha hizo zitafanyika kwa wakati tofauti katika kipindi cha wiki mbili wilayani Sengerema, Misungwi, Msalala na Bariadi. Warsha hizo zilizoanzia Sengerema Jumatano na kumalizika Ijumaa zitafuatiwa na Misungwi Mei 25 hadi 27, Msalala Mei 28 hadi 30 na Bariadi kuanzia Mei 28-30. Katika warsha hiyo pamoja na kujadili mada mbalimbali, mijadala itahusisha viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa kidini na kimila na hoja kubwa itakayojadiliwa ni dhana ya kisayansi ya albinism, mitazamo ya jamii kuhusu dhana hiyo, makundi mbalimbali ndani ya jamii, tofauti kati ya utamaduni na asili. Pia watajadili kubainisha na kuanisha matatizo, changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism na kuchambua mambo yanayochangia uwepo wa changamoto na hatari kwa watu wenye alibinism. Katika majadiliano hayo pia mikakati inayoweza kupunguza au kumaliza kabisa matatizo changamoto na hatari zinazowakabili watu wenye alibinism katika jamii yetu itatazamwa. Watoa mada wanatarajiwa kutoka katika halmashauri, vyama vinavyotetea maslahi ya albinism, mbunge anayetetea maslahi ya watu wenye albinism Al-Shaymaa Kwegyir na mwakilishi kutoka baraza la taifa la dawa asilia.

Rais Kikwete afungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) jijini Dar es salaam leo

May 20, 2015

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielezea jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of  thanks baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
 Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of  thanks baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
 Mshereheshaji wa mkutano huo Mhe. Maria Sarungi-Tsehai akitoa maelezo baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkaribisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kupokea tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
   Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkabidhi  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akishukuru kwa kupewa tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
 Rais Kikwete akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini ambaye ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
  Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
 Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa mabalozi ambaye  ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
  Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Kikwete na viongozi wengine wakijiandaa kupata picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete akiagana mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.

WAFUGAJI WALIOVAMIA ENEO LA LOLIONDO WATAKIWA KUONDOA MIFUGO YAO

May 20, 2015

  Waziri  wa Maliasili  na  Utalii  Lazaro  Nyalandu  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tatu kulia), wengine ni wawakilishi kutoka balozi huo. (Picha  zote na Loveness  Bernard)
Waziri  wa Maliasili  na  Utalii  Lazaro  Nyalandu  akiwa  amebeba  ndoo  ya maji  kichwani  alipokuwa  akikabidhiwa  visima  33 vilivyochimbwa kwa msaada  wa Watu  wa Falme  za Kiarabu  na Balozi  wa Falme  hizo.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Olosokwani, Loliondo wilayani Ngorongoro, juzi. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imewekeza wilayani humo. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijindaa kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kata ya Olosokwani, ambako alizindua mradi mkubwa wa maji ya visima virefu wilayani Ngorongoro, juzi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa  Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifurahia jambo na wakazi wa kijiji Olosokwani, baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima virefu wilayani Ngorongoro juzi. Kushoto ni Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.

Na Loveness Bernard

Wafugaji kutoka nchi za jirani  waliovamia katika eneo la Loliondo  wametakiwa kuondoa mifugo yao mara moja ili kuliacha eneo hilo kubaki na amani.

Akizungumza na wananchi na wafugaji wa kijiji cha Ololosokwani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema wakazi wa Loliondo wanauwezo wa kutatua migogoro yao wenyewe ila wanaosababisha migogoro hiyo isiishe na kuibuka mara kwa mara ni wageni wanaoingia katika eneo hilo na kuchungia mifugo yao.

“Ninatoa tahadhali kwa wageni wanaoitazama loliondo kwa jicho la husda waache kufugia mifugo yao loliondo, kila mmoja afugie kwao ardhi ya loliondo ni ya wana loliondo na sio wageni” alisema Nyalandu.

Alisema changamoto kubwa inayoikabili eneo hilo la Loliondo ni ongezeko la watu na mifugo wakati ardhi ikibaki kuwa ile ile.

Nyalandu alisema kuna haja ya kuendeleza uhifadhi ili eneo la Loliondo liendelee kustawi na wageni waendelee kuja Loliondo ambapo watachangia utalii endelevu katika shughuli kama za utalii wa picha na uwindaji.

Akizungumzia kuhusu miradi ya maji aliyoikabidhi kwa wananchi wa loliondo jana kutoka kwa Balozi wa Falme za Kiarabu waliofadhiri ujenzi wa miradi hiyo iliyogharimu sh bilioni 1.6 Waziri Nyalandu alisema hayo ni matunda  ya ushirikiano mzuri baina ya Rais Jakaya Kikwete na Mfalme wa Dubai Shekh Makthum na Jumuiya  ya falme za kiarabu.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni ahadi ya Rais Kikwete kwa maeneo ya wafugaji ambapo alisema azma yake ni kuona tatizo la maji katika maeneo ya wafugaji linamazika na kuona mifugo na wafugaji wakinenepa.

Aliwataka wananchi wa Loliondo kuitunza miradi hiyo kwa faida yao na mifugo yao huku wakitumia muda mwingi kwa kazi za maendeleo ya loliondo.

Balozi Seif Ali Idd akagua ujenzi wa Jengo jipya la Abiria wa usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar

May 20, 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka kushoto akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Abiria { Terminal 11 } katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar wa Abeid Amani Karume akiwa pamoja na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio na Msimamizi wa ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De Costa.
Msimamizi wa ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De Costa akimpatiamaelezo Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi huo.
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa Mhandisi Guillaume Verna akifafanua hatua zilizochukuliwa katika utaalamu utaotumika katika ujenzi wa mikonga kwenye jengo hilo jipya la abiria.
Eneo litakalotumika kwa huduma mbali mbali ikiwemo maduka na katika jengo jipya la abiria linaloendelea kujengwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Eneo la Nje ya jengo la Abiria litakalotumiwa na abiria wanaosafiri na kuingia Nchini kwa kutumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume uliopo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Harakati za ujenzi wa Jengo jipya la Abiria wa usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa   Abeid Amani Karume  ulipo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar  zimekuwa zikiendelea kama kawaida kufuatia marekebisho ya ujenzi wa jengo hilo  utaozingatia kiwango cha Kimataifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua harakati za ujenzi huo unaofanywa na wahandisi wa  Kampuni ya Kimataifa ya Beijing Construction Engineering  Group { GCEG } ya Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Chini ya Usimamizi uelekezi wa Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa.

Msimamizi wa ujenzi wa Mradi huo kwa  upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De Costa alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi huo hivi sasa uko katika hatua za uwezekaji paa na baadaye kuwekwa vioo.

Nd. Costa alisema Jengo hilo kubwa litakuwa  na lango kuu kwa ajili ya abiria wote wa ndege za kimataifa na Kitaifa ambapo baadaye watajigawa kwa mujibu wa safari za abiria hao katika huduma za ndani.

Alieleza kwamba mizigo ya abiria itafanyiwa ukaguzi mbara mbili kabla ya kuingizwa ndani ya ndege utaratibu ambao utathibitisha usalama wa abiria, mizigo na eneo lote la uwanja wa ndege.

Msimamizi huyo wa mradi wa ujenzi wa Jengo la abiria wa Serikali alifahamisha kwamba abiria wapatao 500 watakuwa wakihudumiwa ndani ya saa moja katika eneo la jengo hilo la abiria.

Naye mshauri wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa  Mhandisi Guillaume Verna alisema kwamba ujenzi wa Mikonga itakayohudumia ndege kubwa katika jengo hilo imezingatiwa katika kiwango kikubwa.

Mhandisi Guillaume alisema utafiti wa kina umefanywa katika kuona mikonga itakayopjengwa haiathiri jengo hilo kwa mujibu wa vipimo vinavyokubalika Kimataifa.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Maiundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio alisema Serikali ya Jamuhuri ya China ambayo ndio mfadhili wa Ujenzi huo Kupitia Benki ya Exim imeridhia kuendelea kutekelezwa kwa mradi huo.

Dr. Malik alisema Wizara ya Miundombinu na Mawasliano kwa kushirikiana na wadau wa Mradi huo wanaandaa utaratibu wa kumaliza ujenzi huo kwa mujibu wa ushauri wa Kitaalamu.

Alisema  mategemeo ya mradi wa ujenzi huo yalipangwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu lakini kutokana na kusita kwa muda ujenzi huo unatazamiwa kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu.

Alieleza kwamba  mategemeo ya mradi wa ujenzi wa jengo hilo yalipangwa kukamikia mwezi oktoba mwaka huu lakini kutokana na kusita kwa muda ujenzi huo unatazamiwa kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na kuendelea kwa  ujenzi wa jengo hilo  ambao uko katika hatua inayoridhisha.

Balozi Seif aliwapongeza wahandisi wa ujenzi huo pamoja na usimamizi mahiri wa mshauri muelekezi wa mradi huo hatua ambayo kumalizika kwake kutatoa faraja kwa abiria wanaotumia uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Balozi Seif alifahamisha kwamba matarajio ya abiria wanaotumia uwanja huo wataondokana na  usumbufu wa kushuka au kufuata ndege masafa marefu kwa miguu hasa wakati wa mvua.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/5/2015.
Mkutano wa tatu wa Shirikisho la Vyama vya Wataalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe Afrika

Mkutano wa tatu wa Shirikisho la Vyama vya Wataalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe Afrika

May 20, 2015


VY2
Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam, kuhusu Mkutano wa tatu wa Shirikisho la Vyama vya Wataalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe Afrika ambao unalenga kutoa fursa kwa wanasansi wa masuala ya lishe ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda na Afisa Mawasiliano wa taasisi hiyo Herbert Gowelle (kushoto).
VY3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia umuhimu wa lishe nchini kama moja ya masuala muhimu ya kimaendeleo. Kushoto ni Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo.
VY4
Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu kupunguza viwango vya ukondefu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa asilimia 50 mwishoni mwa mwaka huu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt. Joyceline Kaganda.
VY1
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa taasisi ya chakula na lishe uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu.

Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu.

May 20, 2015

images 
Na Lorietha Laurence-Maelezo
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) itaadhimisha wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bw. Assah Mwambene ,amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe. katika ufunguzi huo, Mkurugenzi ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na uzinduzi wa Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania (TAHAP) ikiambatana na maonyesho ya picha ya kumbukumbu mbalimbali zinazoelezea ukombozi wa bara hilo. “Mradi wa nyaraka za urithi wa Tanzania unatarajia kuweka na kutunza kumbukumbu mbalimbali zinazohusu ushiriki wa Tanzania katika harakati za zinazohusu ukombozi wa nchi za Bara la Afrika” alisema Bw.Mwambene. Naye Mshauri Mkuu wa masuala ya Uhifadhi wa Nyaraka kutoka UNESCO, Bw.Philippe Roisse ameeleza namna shirika hilo lilivyojidhatiti katika kuhakikisha kumbukumbu hizo zitakavyohifadhiwa kwa usahihi na manufaa ya kizazi kijacho. “UNESCO imeazimia kusimamia suala hili la uhifadhi wa nyaraka za kumbukumbu Barani Afrika kuhusu harakati za ukombozi na hasa ukizingatia shirika hili limefikisha miaka 17 katika kutoa huduma” Alisema Bw. Roisse. Kwa Upande wa Mshauri Mwelekezi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Dkt. Dinah Mbaga ameeleza kuwa mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa, na kuongeza kuwa ni muhimu kukumbushana. Aidha, Mshauri kutoka UNESCO Bw. Daniel Ndagala, ameongeza kwa kueleza kuwa mradi wa uhifadhi wa kumbukumbu mbalimbali na nyaraka za urithi ni chombo muhimu sana katika utekelezaji wa utambuzi wa juhudi za Tanzania kwa nchi za Bara la Afrika. Wiki ya maadhimisho ya Ukombozi wa Bara la Afrika utaenda sambamba na midahalo mbalimbali ikiwemo, mdahalo wa mchango wa vyama vya siasa katika harakati za ukombozi, Mchango wa wanajeshi katika harakati za ukombozi Mingine ni mchango wa wanawake katika harakati za ukombozi, mchango wa wasanii na watunzi na mchango wa vyombo vya habari yote ikilenga suala zima la harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni naMichezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
 PPRA YAIKABIDHI UTUMISHI TUZO YA UTENDAJI ULIOTUKUKA KATIKA ENEO LA UNUNUZI WA UMMA

PPRA YAIKABIDHI UTUMISHI TUZO YA UTENDAJI ULIOTUKUKA KATIKA ENEO LA UNUNUZI WA UMMA

May 20, 2015


Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (kushoto) akikabidhi tuzo ya utendaji uliotukuka katika eneo la ununuzi wa umma kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Samson Akyoo (kulia) katika Maadhimisho ya  miaka 10 ya PPRA yaliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jana.Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA Balozi Martin Lumbanga (wa pili kutoka kushoto) na Mtendaji Mkuu Mstaafu wa PPRA Dkt. Ramadhani Mlinga (wa pili kutoka kulia). mi2
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Samson Akyoo (wa tatu kutoka kulia) akionyesha tuzo ya utendaji uliotukuka katika eneo la ununuzi wa umma kwa watumishi wa ofisi yake.Tuzo hiyo alikabidhiwa na PPRA katika Maadhimisho ya miaka 10 ya PPRA  yaliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jana.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YABUNI MRADI KABAMBE KUENDELEZA MJI MDOGO WA KISARAWE

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YABUNI MRADI KABAMBE KUENDELEZA MJI MDOGO WA KISARAWE

May 20, 2015

Baadhi ya maofisa na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa katika mkutano huo. k6Baadhi ya madiwani na wanakamati wa mradi huo wakiwa kwenye mkutano huo. k7 (2) 
Mkutano huo ukiendelea
K8
Kitabu kinachouelezea mradi huo