MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA

November 30, 2014


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati  wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kifurahia jambo na Makamu wa Rais wa  Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2014

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Za EAC Wakamilika Nairobi

November 30, 2014

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (kulia) na Naibu Waiziri wa TAMISEMI (Elimu) Mh. Kassim Majaliwa wakizungumza nje ya Ukumbi wa Mkutano wa Kenyatta kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Miundombinu Nov 29, 2014,Nairobi
 Mkurugenzi wa Miundombinu na Sekta za Kijamii wa Wizara Bw. George Lauwo (kushoto) akifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu Nov 29, 2014 Nairobi, Kenya.
 Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Petro Lyatuu akifuatilia Mkutano wa Miundombinu wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Nov 29, 2014 Nairobi,
 Mfanyakazi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Edna Chuku akifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya kuhusu Miundombinu Nov 29, 2014 Nairobi, Kenya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya.

 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt Abdullah Juma Saadalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utawala Bora (katikati) Mh. George Mkuchika na Naibu Waziri wa TAMISEMI (Elimu) Bw. Kassim Majaliwa wakifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya
 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt Abdullah Juma Saadalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utawala Bora (katikati) Mh. George Mkuchika na Naibu Waziri wa TAMISEMI (Elimu) Bw. Kassim Majaliwa wakifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki Bw. Amantius Msole (kulia) na Naibu Mwanasheria Mkuu Mh. George Masaju walifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Makamu wa Rais wa Kenya Bw. William Ruto akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA TIMU YA VIJANA YA COASTAL UNION U-20 MABINGWA WA KOMBE LA UHAI LEO KOROGWE

November 30, 2014

KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA COASTAL UNION U-20 LEO KABLA YA KUANZA SAFARI KUELEKEA WILAYANI KOROGWE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOROGWE UNITED

KIKOSI CHA COASTAL UNION U-20 KILICHOANZA KWENYE MECHI HIYO YA LEO NA KOROGWE UNITED,AMBAPO KABLA YA KUANZA MTANANGE HUO KULINYESHA MVUA KUBWA AMBAYO ILIPELEKEA MCHEZO HUO KUSIMAMA KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA KUENDELEA

KUSHOTO NI MKURUGENZI WA UFUNDI WA KOROGWE UNITED,FILBERT MPENZIA AKIMUELEZA KITU MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION SALIMU BAWAZIR LEO WA KWANZA KULIA NI NAIBU KADHI MKUU WA TANZANIA,SHEIKH ABUBAKARI ZUBEIR.

KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIPASHA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO LEO



WALINDA MILANGO WA COASTAL UNION U-20 WAKIPASHA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO LEO



MKURUGENZI WA BENCHI LA UFUNDI LA COASTAL UNION,MOHAMED KAMPIRA AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO WAKATI WA MAPUMZIKO KUSHOTO NI MCHEZAJI WA ZAMANI WA COASTAL UNION NA MJUMBE WA KAMATI YA USAJILI RAZACK KAREKA LRO

MASHABIKI WA SOKA WALIOJITOKEZA KWENYE UWANJA WA SOKA CHUO CHA UALIMU KOROGWE WAKIFUATILIA MPAMBANO HUO LICHA YA KUNYESHA MVUA KUBWA

WAGENI KUTOKA NANJING CHINA WATEMBELEA OFISI ZA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

November 30, 2014

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel kushoto akizungumza na watu kutoka Jamhuri ya watu wa china (hawapo pichani) walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara  kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika  jioni yake. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Sanaa Bibi Leah Kihimbi.
Mkuu wa masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka
Nanjing China Bw. Yan Yiping kushoto akifafanua jambo walipofika katika ofisi za  Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano  kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Baadhi ya wageni kutoka Nanjing China wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yakiendelea walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya  Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni  yake. Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Mila Bibi Lily Beleko.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Wizara kutoka kwa Mkuu wa  masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka Nanjing China Bw.  Yan Yiping walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya  Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

MSICHANA WA KAZI ALIYEMPIGA MTOTO AFUNGUKA MAZITO!

November 30, 2014

Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambapo amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo baada ya jana kumuomba samahani mtoto huyo. Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.

Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo alikuwa akimpiga kama njia ya kumkanya. 

Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

KINANA APOKELEWA KWA SHANGWE MTWARA MJINI

November 30, 2014

 Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Wananchi wa Mikindani mkoani Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa vikundi vya Bodaboda zilizotolewa na Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji akihutubia wakazi wa Mikindani baada ya kuwakabidhi leseni madereva 70 wa boda boda na kuwakabidhi pikipiki tatu kama mtaji wa kuendeleza vikundi vyao.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ukarabati wa ofisi ya CCM kata ya Majengo iliyochomwa moto wakati wa vurugu za gesi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ukarabati wa ofisi ya CCM kata ya Majengo iliyochomwa moto wakati wa vurugu za gesi
 Katibu Mkuu wa CCM akiwasalimia wakazi wa kata ya Majengo alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa ofisi ya CCM .
 Wananchi wakishangilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyewasili mkoani Mtwara ambaye anategemewa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya Jumapili tarehe 30 Novemba 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji mama mmoja mkazi wa mtaa wa Mwera kata ya Chikongola baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia kazi za kikundi cha wakina Mama wa Matopeni ambao wapo zaidi ya 200 na wanajishughulisha na shughuli mbali mbali za ujasiriamali Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la mradi wa ufugaji kuku wa mayai wa kikundi cha akina mama cha Rahaleo.
 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia kuku wa mayai wanaofugwa na kikundi cha akina mama wa Rahaleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kushona viatu pamoja na fundi viatu Abeid Yusufu Likanga (ambaye ni mlemavu wa miguu) wa kata ya Rahaleo mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa chama wakiangalia maendeleo ya uchimbwaji wa mfereji unaopeleka maji baharini katika kata ya Shangani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikara utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la CCM Chuo cha Utumishi wa Umma kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akigutubia wanafunzi wa Chuo Cha Utumishi Mtwara mara baada ya kuzindua tawi lao la CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi Katiba ya CCM kwa Katibu wa Tawi la Chuo Cha Utumishi Mwamvua Patrick.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa wa halmashauri kuu ya wilaya ya Mtwara mjini kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa VETA
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa wa halmashauri kuu ya wilaya ya Mtwara mjini kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa VETA ambapo alisisitiza wajumbe wasahau yaliyopita na kusimama kukijenga chama