WANAFUNZI 1,044 WAHITIMU CHUO KIKUU ARDHI

December 07, 2014

Wahitimu wa digrii ya  elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa  digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu “Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania.” PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu (Doctor of Phylosophy Degree), Deusdedit Kibassa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.Mada ya utafiti aliyoifanya inahusu: “Umuhimu wa kutumia maeneo ya kijani kupunguza athari zitokanazo na kuongezeka kwa hali ya joto katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam.”
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Dawah Mushi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mada  ya utafiti aliyoifanya Mushi  inahusu: “Uhamishwaji wa makazi ya watu wengi waliobomolewa makazi yao katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam.”
Daniel Mbisso akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Joel Msami akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Eliwaha Msangi akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Margareth Ntiyakunze akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Sara Phoya akitunukiwa digriii ya uzamifu
Baadhi ya wahitimu wakipiga picha wakati wa mahafali hayo
Bendi ya JKT ikiongoza maandamano ya viongozi na wahadhili wa chuo hicho kuingia ukumbini
Wahadhiri na viongozi wakiingia kwa maandamano kwenye ukumbi
baadhi ya wahitimu wakisubiri kutunukiwa digrii
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi, Tabitha Siwale akihutubia katika mahafali hayo
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Mshoro akihutubia wakati wa mahafali hayo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakiweka kofia kichwani ikiwa ni ishara ya kutunukiwa digrii ya uzamili ya sayansi ya usimamizi na uchumi ujenzi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam
Ni furaha iliyoje baada ya kutunukiwa
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
Waziri Mkuu wa zamani, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha ARU, Cleopa Msuya akitoka baada ya mahafali hayo kumalizika leo
Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika

MASHINDANO YA MICHEZO YA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI YAANZA JIJINI ARUSHA

December 07, 2014

SAM_0436
Maandamano ya mashindano ya michezo ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),jijini Arusha ambayo yanatimua vumbi Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha kwanzia tarehe 6 hadi 12 mwezi huu
SAM_0464
Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakifwatilia ufunguzi rasmi wa bonanza la mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kulia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania Idd Azan katikati ni Mh.mbunge Stevin Ngonyani a.k.a Maji marefu
SAM_0493
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akifurahia ushindi baada ya kushinda nafasi ya kwanza kupeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuibuka mshindi  mbio za mita 100 akifuatiwa na Isaac Melley wa Kenya na Tom Aza wa Uganda aliyeshika nafasi ya tatu.
SAM_0514
Wabunge wa Tanzania Halima Mdee na Ester Matiko waliendeleza ubabe wa bunge la Tanzania dhidi ya wenzao baada ya kushika nafasi ya kwanza na pili katika mbio za mita 1,500 na kuwaacha wenzao kutoka Uganda, Kiiza Winfred na Kangi Elizabeth wakishikilia nafasi za tatu na nne.
SAM_0498
Mbunge Ester Matiko wa Tanzania  akijiandaa kukimbia mbio za mita 400,ambapo aliwatimulia vumbi wabunge wenzake kutoka Kenya, Uganda na bunge la Afrika Mashariki (Eala).
SAM_0469
Kaimu Spika wa bunge la EALA Chris Opoka akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo
SAM_0470
Mkuu wa wilaya Arumeru Mhe Nyirembe Munasa afungua mashindano ya michezo kwa wabunge ambapo aliwataka wachezaji kuacha kuamini imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mungu kwani michezo ni kazi kama ajira nyingine
SAM_0440SAM_0452
SAM_0495
Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Anna Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na EALA(East African Legislative Assembly)
SAM_0508
Katikati Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Barbra Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na EALA(East African Legislative Assembly)
SAM_0559
Aliyevalia t-shart ya njano ni designer mkuu wa kampuni ya KeyMedia Agency Limited Bahati Masawe akiwa na waheshimiwa Wabunge
SAM_0553
Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama akiwa anavuta kamba wakati wa mashindano ya hayo
SAM_0489
Mbunge wa Kenya akiwa amebebwa juju baada ya kushinda katika mbio za mita 100
SAM_0494
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya akiwa anashangilia kwa furaha katika mashindano hayo

UTATA MTUPU! WEMA APOSTI PICHA ZAKE NA DIAMOND WALIZOPIGA PAMOJA!

December 07, 2014


Diamond, Wema & Mama Naseeb
Inaonekana Wema Sepetu wadhungu wanasema 'Never Over it' yaani bado ajamaliza ishuyake na mpenzi wake wa zamani Diamond Platnumzambaye juzi juzi alimwita kaka kwa ku-share kwenye Official blog yake ya Bestizzo kwa kuweka picha mpya za mchumba wake huyo wa zamani na kushare kwenye Social Network,haijajulikana sababu hasa ya Wema Ku-share picha hiyo wakati event hiyo ilishafanyika kitambo tu tena hata kabla ya msimu mpya wa "In My Shoes" akiwa tayari ameshaachana na Diamond.

Ile StizzoFlava unayoipata kwenye macho yako kupia picha za Bestizzo ndo hii hapa, nimekuwekea picha za Birthday ya Diamond Platnumz zenye #StizzoFlava

Wema #MakeupTime

Wema Sepetu

Wema #Selfie…
Wema #Selfie…

Diamond & Wema…

KAMA ULIKOSA KUSOMA STORI HII KUHUSU TAHARUKI ILIYOJITOKEZA JENGO ALA BANDARI TANGA IPATE HAPA.

December 07, 2014

HUDUMA  za Kijamii Katika  Ofisi mbalimbali zilizopo kwenye Jengo la Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga zimesimama kwa masaa matatu  baada ya kutokea hali ya taharuki ya kishindo na kupasuka sakafu katika chumba kimoja kilichopo kwenye Jengo hilo.

Ofisi iliyotokea na kishindo hicho na kupelekea kupasuka iliyopo
ghorofa ya tatu iliyokuwa imepangishwa na kampuni ya mizingo ya Cargo Stars.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG ,Meneja wa Kampuni ya Cargo Stars  Tawi la Tanga,Godlisen  Mushi alisema kuwa wao walishtushwa sana na hali hiyo kutokana na kuwa kitendo hicho hakijawahi kuwakuta tokea wapipopoangisha ofisi hiyo.

  “Nilikuwa nimekaa ofisini nikiendelea na kazi zangu lakini ghafla nikasikia tetemeko kwa chini hali ambayo ilinilazimu kuacha kufanya kazi kwa muda mpaka wafanyakazi wenzangu na wengine tulipokutana na baadae tukarudi kwenye ofisi zetu “alisema Mushi.

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mkoa wa Tanga,Bertha Mwambela alisema kuwa wao walipokea tukio hilo kwa mshukto mkubwa hali ambayo iliwalazimu kutoka nje ya ofisi yao mpaka hapo hali hiyo ilipotulia na kurejea ofisini kwake.

Mwambela aliishauri mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga,kuangalia uwezekano wa kuangalia namya ya kuvifanyia ukaguzi mara kwa mara nyumba viliyopo kwenye jengo hilo.

Akizungumzia tukio hilo,Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga,Fredy Liundi alisema kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi ambapon tails zilizopo kwenye chumba hicho kilipasuka na kunyanyuka juu kutokana na uzito wa vitu vilivyokuwepo kwenye chumba hicho.

   “Kutokana na taharuki hiyo asilimi 60 ya wafanyakazi kwenye ofisi zilizopo kwenye jengo letu walitoka nje kwa ajili ya kujihami “Alisema Kaimu Meneja Fredy Liundi

Tamasha la Handeni Kwetu lasogezwa mbele, sasa kufanyika Desemba 20

December 07, 2014
Na Mwandishi Wetu, Handeni
TAMASHA la Utamaduni la NSSF Handeni Kwetu, sasa litafanyika Desemba 20, badala ya Desemba 13, kama ilivyotangazwa hapo awali, huku sababu kubwa ikiwa ni kuwaachia Watanzania washiriki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, utakaofanyika Jumapili ya Desemba 14 nchini kote.
Mratibu Mkuu wa Tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014, pichani akizungumza jambo katika tamasha la mwaka jana lililofanyika kwa mafanikio makubwa wilayani Handeni, mkoani Tanga.
 
Akizungumzia hilo leo mjini Handeni, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kwamba hatua ya kusogeza mbele kwa wiki moja, ni kutokana na mguso wa tukio lenyewe na nia ya kuwashirikisha Watanzania wote ili kuliweka tamasha lao katika kiwango cha juu.
 
Alisema kuwa Desemba 13 ni siku ya mwisho kwa kampeni za ugombea uenyekiti wa serikali za mitaa, vitongoji na mitaa, hivyo kwa kushauriana na jeshi la Polisi wilayani Handeni, wamekubaliana kulifanya Desemba 20.
 
“Tumeangalia mambo mengi sana hadi kukubaliana lifanyike Desemba 20, ikiwa ni kukosekana kwa wengi, wakiwamo Wakurugenzi ambao kimsingi wao ndio wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mengi.
 
“Tunaamini kwa kufanyika Desemba 20, tamasha litakuwa kwenye mvuto pamoja na kukwepa malalamiko kwa baadhi ya wanasiasa ambao huenda wangelalamika endapo lolote lingetokea huku wao kushindwa uchaguzi wao,” alisema Mbwana.
 
Mbwana alitumia muda huo kuwaomba radhi wadau wote, wakiwamo wasanii, wadhamini na wale waliokuwa wamepanga kutembelea Handeni Desemba 13, huku akiwataka safari yao ifanyike kwa ajili ya Desemba 20, ukizingatia kuwa wote wanaweza kushiriki chaguzi zao na kupata muda mkubwa wa kutembelea wilayani Handeni na mkoa mzima wa Tanga kumaliza mwaka wao vizuri.
 
 Wadhamini tamasha hilo ni Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.
 

*MOSES IYOBO, RAMA TONSA NA DJ ROMY JONES WAWASILI WASHINGTON, DC, DIAMOND KUWASILI LEO

December 07, 2014

 Kutoka (kushoto) ni Dj Romy Jones, Moses Iyobo na Rama Tonsa wakisubili usafiri na huku wakijaribu kupata mawasiliano mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia tayari kwa kuwasha moto leo kwenye sherehe ya Uhuru itakayofanyika Sheraton ya Downtown Silver Spring.
 Moses Iyobo, Dj Romy Jones wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa mara tu baada ya kuwasili siku ya Ijumaa Desemba 5, 2014 kwa ajili ya sherehe ya Uhuru itakayofanyika leo Jumamosi Sheraton ya Downtown Silver Spring, Maryland.
 Moses Iyobo na Rama Tonsa wakiwasili hotelini mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege.
 Dj Romy Jones (Dj wa Diamond) akiendelea na mawasiliano akiwa hotelini.
 kushoto ni Inno na watatu toka kushoto ni Phanuel ambao ni waratibu na waliomleta Diamond wakishirikiana na DMK (hayupo pichani wakiwa katika picha ya pamoja na Dj Romy Jones, Moses Iyobo
 Saada Wadau kutoka Michigan wakiwasili tayari kwa show ya Diamond. Picha na Vijimambo.