PICHA ZA MGOMO WA BODABODA AINA YA BAJAJI JIJINI TANGA JUZI.

August 17, 2014

 Bodaboda aina Bajaji zikiwa zimepaki kwenye barabara ya Mkwakwani jijini Tanga zikiashirikia mgomo wao kupinga agizo la mamlaka ya mapato nchini mkoa wa Tanga (TRA)kutaka walipe kodi ya mapato ya vyombo hivyo
 Msemaji wa waendesha Bodaboda aina ya Bajaji na Pikipiki wilaya ya Tanga,Misheto Jonas akieleza waandishi wa habari jijini Tanga dhamira yao ya kugoma kupiga agizo la mamlaka ya mapato nchini mkoa wa Tanga TRA kulipa kodi ya mapato ya vyombo hivyo
  Mwendesha bodaboda aina ya Bajaji Richard Leonard akilalamikia kupinga kodi ya mapato ya mamlaka ya mapato nchini TRA jana mara baada ya kuitisha mgomo wa waendesha bodaboda bajaji wilaya
ya Tanga,Picha 
Bodaboda aina ya bajaji zikiwa zimezagaa kwenye barabra ya mkwakwani mkoani Tanga zikkigoma kutoa huduma kutokana na kupiga agizo la mamlaka ya mapato mkoa wa Tanga TRA kuwataka kulipa kodi ya vyombo hivyo,

ABSAM MABINGWA WA POOL TABLE TANGA.

August 17, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
CLUB ya Absam Pool mwishoni mwa wiki walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mchezo wa Pool Table ngazi ya Mkoa wa Tanga na kukabidhiwa kitita cha sh.800, 000 baada ya kuibuka kidede kwenye mchezo wa fainali dhidi yao na Young Boys.

Fainali hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Fax Night Club uliopo jijini Tanga ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu hizo wachezaji wa timu zilizokuwa zikishiriki kuchukua vikali.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Club ya Young Boys ambao walizawadiwa kitita cha sh.400,000 wakati mshindi wa tatu Spider walikabidhiwa kitita cha sh.250,000 huku mshindi wanne Kange Brothers wakizawadiwa kitita cha 150,000 na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo Ofisa Utamaduni wa Jiji la Tanga Peter Semfuko.

Katika mshindi mmoja mmoja kwa upande wa wanaume, Abeid Juma kutoka Club ya Spider aliweza kuibuka kidedea na kufanikiwa kuondoka na kitita cha sh.400, 000 kwa kumshinda Ajinabi Baruti kwenye mchezo wa Fainali.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Ajinabi Baruti aliyazawadiwa 250,000, Nafasi ya tatu ikichukuliwa na Iddi Abasi Karonga ambaye alizawadiwa kitita cha sh.250,000 wakata nafasi ya nne ilichukuliwa na Tifu Abdallah aliyepata 100,000

Kwa upande wa wanawake bingwa alikuwa ni Neema Hamisi baada ya kumbwaga mpinzani wake Zainabu Kishingo kwenye mchezo wa fainali na kupata kitita cha sh.300,000,mshindi wa pili Zainabu Kishindo akizawadiwa 200,000,mshindi wa tatu alikuwa ni Halima Hamisi ambaye aliondoka na kitita cha sh.100,000 na nafasi ya nne ilichukuliwa na Mariam Raphael aliyejipatia 50,000

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Semfuko ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wachezaji wa mchezo wa Pool Table mkoani Tanga kuhakikisha wanauthamini mchezo huo ili waweza kupata fursa mbalimbali zinazotokana nazo lengo likiwa kujikwamua kiuchumi na maisha

Alisema wakitumia kucheza mchezo huo unaweza kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hiyo Ofisa Utamaduni huyo aliwataka kuacha kucheza kiholela holela badala yake wafuate taratibu zilizopo ikiwemo kuvisajili vilabu vyao ili viweze kutambulika.

   “Michezo ni ajira ambayo inaweza kuwainua kimaisha hivyo nawasihi mzingatie michezo hasa mchezo wa Pool table kwani unaweza kuwainua kimaisha kama mtautilia mkazo “Alisema Ofisa Utamaduni Semfuko.
MSANII SHILOLE:HIZI NDIZO SABABU ZA KURUDIANA NA MZIWANDA

MSANII SHILOLE:HIZI NDIZO SABABU ZA KURUDIANA NA MZIWANDA

August 17, 2014

Staa wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema sababu kubwa ya yeye kurudiana na mpenzi wake waliyegombana, Nuhu Mziwanda ni kuombwa msamaha.

Staa wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Shilole alisema mpenzi wake huyo aligundua kwamba aliteswa na wivu na kusababisha wagombane hivyo alipotambua kosa lake, aliomba msamaha wakarudiana na mambo yakawa shwari.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema Shilole. Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake

COASTAL UNION YAIZIDI KETE SIMBA,YAMSAINISHA KIUNGO HATARI WA GORMAHIA YA KENYA.

August 17, 2014
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini Kenya,Rama Salum Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.

Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union  akitokea nchini Kenya
  na kusaini  mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Rama aliyewahi kuicheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa
  kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabu
  hiyo barabara 11,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta upinzani mkubwa sana.

Aidha amesema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwa

sababu tunamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili imara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile Obina,Shabani Kado Sued Tumba ,Bakari Mtama, na wengine wengi walipo kwenye kikosi cha timu hiyo

Amesema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha
  kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligikuu Tanzania bara msimu ujao.

DC MAKUNGA :SERIKALI WILAYANI HAI IMEJIPANGA KUONDOA KERO ZINAZOWAKABILI WANANCHI

August 17, 2014

Na Mwandishi Wetu,Hai

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga(Pichani) ameeleza kuwa serikali wilayani humo imejipanga kuondoa kero zote zinazoawakabili wananchi wanapoenda kutibiwa katika hospitali ya serikali ya wilaya hiyo zikiwemo lugha chafu za watumishi wa hospitali hiyo

Mhe.Novatus Makunga ametoa kauli hiyo katika mikutano yake ya hadhara na wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai Mjini.

Awali wananchi wa mitaa hiyo walieleza kuwa kero kubwa wanayokumbana nazo katika hospitali hiyo ni pamoja na lugha chafu katika eneo la mapokezi,ukosefu wa dawa pamoja na madaktari kutokaa katika vyumba vyao vya kuwahudumia wagonjwa.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kuanzisha mpango unaojulikana kama sauti ya jamii ambapo kupitia mpango huo wananchi wanaokumbana na kero katika hospitali hiyo wamekuwa wakitoa taarifa.

"Taarifa hizo zimekuwa zikijadiliwa na kamati ya uongozi ya hospitali hiyo kila mwezi na kuchukuwa hatua na baadaye mrejesho kutolewa kwa wananchi,hivyo zote kwa pamoja tupambane na uvunjaji wa maadili katika hospitali yetu" alisema Makunga

Aidha amewataka wananchi hao kutoa taarifa mara moja pale wanapokumbana na kero yoyote kwa mganga mkuu wa wilaya ama mganga mfawidhi ama muuguzi mkuu na hata yeye kama mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ambapo wote hao walitoa nambari zao za simu za mkononi.

“Tumeanza kuchukuwa hatua na itakuwa vyema pale unapokumbana na kero kutuletea taarifa hapo hapo bila ya kuchelewa,sasa wakati umefika wa kuambiana ukweli,kama mtu anaona kuhudumia umma kunampotezea wakati basi akaanzishe zahanati yake ambapo huko atakuwa huru kutumia lugha chafu,”aliongeza Makunga

Ameeleza maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika hospitali hiyo hayatakuwa na maana endapo kero hizo zitaendelea kudumu na kusababisha wananchi kupata huduma kwa mateso makubwa.

Makunga amezitaja huduma zilizoboresha kuwa ni pamoja na upasuaji mkubwa kwa kuwa na chumba cha kisasa,ukamilishaji wa wote ya upasuaji pamoja na kukamilishwa kwa huduma za X-Ray ambayo itafunguliwa rasmi na mwenge wa uhuru mnamo tarehe 22 ya mwezi huu

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa wilaya ya Hai,Dk Fanuel Mollel alikiri kwamba huko nyuma kulikuwa na tatizo kubwa la madaktari wa hospitali hiyo kutumia muda mrefu kwenda kunywa chai kwa kutoka pamoja kwa makundi na hivyo kusababisha wagonjwa kusota kwa muda mrefu.

Amesema hatua za kudhibiti tabia hiyo zimeshachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kantini eneo la hospitali hiyo.

Kuhusiana na upungufu wa dawa ameeleza hali hiyo inatokana na taratibu za serikali ambapo kwa sasa zinataka dawa ziagizwe kutoka katika bohari kuu ya madawa(MSD) ambapo mara nyingine ukumbwa na upungufu wa dawa

POPPE ATUA KIGALI BAADA YA TFF KUONGEZA MUDA WA USAJILI…AHAHA KUSAKA UNDANI WA VIFAA VIWILI VYA APR

August 17, 2014
Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa siku 10, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameibukia Kigali, Rwanda ambako michuano ya Kombe la Kagame inaendelea.

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), yupo Kigali kwa siku tatu sasa na amekuwa akihudhuria mechi za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Uwanja wa Nyamirambo.

Hakuonekana kabisa uwanjani jana wakati Azam FC ikimenyana na Adama City ya Ethiopia na kushinda 4-1, lakini juzi na leo amefika Nyamirambo.

Akiwa kwenye eneo la ‘watu wazito’ maarufu kama VIP Uwanja wa Nyamirambo, Poppe ameonekana kudadisi wachezaji kadhaa wanaomvutia.
Mawindoni; Hans Poppe wa pili kulia akiwa Uwanja wa Nyamirambo APR na KCC zikimenyana

Katika mchezo wa leo kati ya APR na KCC, Poppe aliinuka na kwenda kuulizia zaidi kwa mtu juu ya wachezaji Mwiseneza Djamal na Mugiraneza Baptiste wa timu ya jeshi la Rwanda.

Poppe aliulizia umri wa Djamal na baada ya hapo akatulia na kuendelea kuangalia mchezo- huku akionyesha dalili zote za kuwapiga hesabu wachezaji hao. 

TFF imeongeza kwa siku kumi muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL)  kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Soka Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja.
Poppe akiwa bize Uwanja wa Nyamirambo leo

Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani.

Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo. Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba.

Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu.

Hata hivyo, Simba SC tayari ina wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, ambao ni mabeki Mganda, Joseph Owino, Mkenya, Donald Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera na Amisi Tambwe pamoja na mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera  

Pamoja na hayo, kumekuwa na tetesi kwamba idadi ya wachezaji wa kigeni itaongezwa kutoka watano hadi saba.
Mwanafunzi wa Tanzania Aibuka mshindi wa Kwanza Tuzo ya Isha SADC

Mwanafunzi wa Tanzania Aibuka mshindi wa Kwanza Tuzo ya Isha SADC

August 17, 2014


D92A4879 D92A4896 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
D92A5209 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe(picha na Freddy Maro)
RAIS MUGABE AMTUNUKU BRIGEDIA JENERALI(MSTAAFU) HASHIM MBITA

RAIS MUGABE AMTUNUKU BRIGEDIA JENERALI(MSTAAFU) HASHIM MBITA

August 17, 2014


D92A5153[1]
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe akimkabidhi Bi. Sheila Hashim Mbita, binti yake Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita Tuzo ya Juu ya Taifa la Zimbabwe ya Nishani ya Royal Order Of Mwanamutapa kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa Taifa la Zimbabwe na nchi nyingine kusini mwa Afrika.Rais Mugabe alikabidhi tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe.(pictha na Freddy Maro)
D92A5154[1]

MAKATIBU UENEZI WA CCM WA KATA 90 MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATIWA SEMINA ELEKEZI

August 17, 2014

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu waenezi 90 wa CCM wakati akifungua semina elekezi ya siku moja kwa makatibu hao kutoka Kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba na Katibu Muenezi Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Athuman Salum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu hao.
Makatibu Uenezi hao wakishangilia hutuba ya mgeni rasmi, Ramadhani Madabida.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Temeke wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Ilala wakipitia taarifa yao ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa chama chao.
Makatibu uenezi wa Wilaya ya Ilala wakiwa kwenye semina hiyo.
Hapa makatibu hao wakiwa kwenye majadiliano.
Makatibu hao kutoka Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hutuba ya mgeni Rasmi Ramadhani Madabida.
Makatibu uenezi hao wakiwa kwenye semina hiyo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 
Dotto Mwaibale
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amewataka makatibu waenezi wa chama hicho kumtetea Rais Jakaya Kikwete na chama hicho ili aendelee kuaminiwa na wananchi.
 
Madabida alitoa mwito huo wakati akifungua semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa mahususi kwa makatibu waenezi 90 wa chama hicho kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika leo ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala.
 
“Ninyi ni kama maofisa mawasiliano na masoko hivyo mnawajibu wa kukiuza na kukitangaza chama chetu kwa wananchi ili waendelee kuwa na imani nacho na serikali kwa ujumla” alisema Madabida.
 
Alisema kazi yenu kubwa ni kumtetea rais ambaye ni Mwenyekiti wetu wa chama taifa na ili aendelee kuheshimika kwa wananchi hasa pale anapochafuliwa na wapinzani.
 
Katika hatua nyingine Madabida aliwataka makatibu ueneze hao kuwa wamoja na kuacha kuwachukia viongozi waliopo madaraka baada ya chaguzi kuisha na akatoa onyo kuwa hata kuwa na mswalia mtume kwa mtu atakayebainika kuendeleza chuki hicho.
 
“Kumekuwa na tabia ya watu kuendeleza chuki baada ya kukosa nafasi katika uchaguzi hivyo kutufanya tushindwe kusonga mbele nasema katika hilo mtaniita majina mengi mabaya kwani siqwezi kumvumilia mtu” aliongeza Madabida.
 
Madabida aliwataka makatibu uenezi hao kufanya mikutano ya hadhara ili kukinadi chama chao kwani wenye wajibu wa kutekeleza ilani ya chama ni wao na si mtu mwingine.
WAZEE WA KUPANGUA WAONGEZA SIKU KUMI ZA USAJILI VPL, FDL

WAZEE WA KUPANGUA WAONGEZA SIKU KUMI ZA USAJILI VPL, FDL

August 17, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza kwa siku kumi muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja.
Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani.
Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo. Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba.

Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu.

WAGOSI WA KAYA COASTAL UNION KUTUA PEMBA JUMANNE

August 17, 2014

Na Mwandishi Wetu, Tanga

TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kundoka mkoani hapa Jumanne kuelekea Kisiwani Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
 Akizungumza wa waandishi wa habari leo katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kuwa kambi hiyo itawekwa visiwani humo pamoja na kufanyia mazoezi kwenye uwanja wa Migombani kila siku.
 El Siagi amesema kuwa kikosi cha wachezaji wapatao 25 ikiwemo Benchi la Ufundi litakuwa na watu watano ambao wataelekea visiwani humo wakiwa na lengo la kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.
 Amesema katika benchi la ufundi litakuwa na Kocha mkuu Yusuph Chipoo,Kocha Msaidizi Benard Mwalala na Kocha wa makipa Razack Siwa,Daktari wa timu pamaoja na Kiti meneja.
 
 
 Aidha amesema msafara wa timu hiyo utaondoka mapema mkoani hapa siku hiyo kwa ajili ya kwenda kuanza kambi mpya ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
MAJI YAFIKA SHINGONI! TFF KUREJESHA OFISI ZAKE KARUME

MAJI YAFIKA SHINGONI! TFF KUREJESHA OFISI ZAKE KARUME

August 17, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kurejesha ofisi zake Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa vile mipango ya uendelezaji wa eneo hilo bado haijakwenda kama ilivyopangwa awali.

Uamuzi huo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliokuwepo nchini kwa wiki nzima kwa ajili ya kufanya mapitio (review) ya uendeshaji wa TFF.

Akizungumza Dar es Salaam leo (Agosti 17 mwaka huu), kiongozi wa ujumbe huo wa FIFA uliokuwa na maofisa sita, Zelkifli Ngoufonja amesema wamepitia maeneo mbalimbali ya uendeshaji wa TFF na mpira wa miguu kwa ujumla na kukubaliana kufanya uboreshaji kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Ngoufonja ambaye ni Meneja Mwandamizi wa FIFA anayeshughulikia Programu za Maendeleo Afrika amesema kabla walikutana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kwa lengo la kuangalia jinsi watakavyochangia katika uendelezaji mpira wa miguu nchini.

Amesema wamekubaliana na TFF katika mpango wa utekelezaji (Action Plan) na maazimio waliyokubaliana ikiwemo na muda wa utekelezaji wake, hivyo FIFA watafuatilia na kutoa msaada ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kama ilivyopangwa.

Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni utawala bora (Governance), Maendeleo ya Ufundi (Technical Development), timu za Taifa (National teams), Mashindano na Vitendea Kazi (Competitions and Facilities), na Utawala na Uongozi (Administration and Management).


Maofisa wengine wa FIFA waliofuatana na Ngoufonja ambaye ni raia wa Cameroon ni Meneja wa Programu za Ustawi (Performance), Marco Schuepp, Ofisa Maendeleo, Ashford Mamelodi, Ofisa Maendeleo wa Ufundi, Govinden Thondoo, Mkufunzi wa Makocha, John Peacock na Mshauri wa Programu za Ustawi, Ian Riley.

KLABU 12 ZA TIMU ZA MAVETERAN KUSHIRIKI TAMASHA MAALUMU SEPTEMBA 6.

August 17, 2014
Na Elias Kimaro
KLABU 12 za timu za soka za maveterani zinazooundwa na nyota wa zamani nchini zinatarajiwa kuchuana katika michezo maalum ya Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym, itakayofanyika Septemba 6 kwenye uwanja wa Mwenge, Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango, klabu zilizothibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo litapambwa na burudani ya muziki na michezo mingine kama ya kufukuza kuku, mbio za kwenye magunia na kuvuta kamba ni pamoja na Mbagala Veterani, Boko, 501, Break Point, Survey, Mwenge na Msasani.
 
Mangomango alizitaja nyingine kuwa ni Biafra Veterani, Meeda, Mikocheni, Mbezi, Mabenzi, Segerea na Ukonga Veterani ambazo zinaundwa na nyota wa zamani wa kandanda waliowahi kutamba na timu za Simba, Yanga na Taifa Stars.
 
Mratibu huyo aliongeza kuwa, siku hiyo klabu zaidi ya 30 za Jogging toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam nazo zitashiriki tamasha hilo kabla ya baadaye washiriki wote kujumuika pamoja kuwatembelea yatima wanaolelewa kituo cha Chakuhama kwa ajili ya kuwapeleka misaada mbalimbali.
 
"Mbali na soka la maveterani, siku hiyo pia kutakuwa na michezo ya netiboli, kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, kuvuta kamba na shoo za watunisha misuli, wanyanyua vitu vizito, mabondia na watu wa karate, pia burudani ya muziki itakuwapo japo mpaka sasa hatujajua tutasindikizwa na bendi gani," alisema Mangomango.
 

MISS KANDA YA ZIWA KUTOKA NA VITZ

August 17, 2014
Na Elias Kimaro
MREMBO wa Kanda ya Ziwa 2014, ‘Miss Lake Zone 2014’, anataibuka na zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya Sh.10,000,000, katika shindano litakalofanyika Agosti 30 CCM Kirumba.
 
Akizungumza na TANGA RAHA BLOG, muandaaji wa shindano hilo, Flora Lauwo, alisema jumla ya warembo 18 wanatarajiwa kuchuana kuwania zawadi hiyo iliyotolewa na Lenny wa Geita.
 
“Shindano hili limedhaminiwa na kampuni ya bia TBL kupitia kinywaji cha Redd’s na Pepsi…shindano hili litafanyika Kirumba baada ya lile la Miss Talent kufanyika Agosti 23 mkoani Geita,” alisema Lauwo.
 
Aidha, Lauwo alisema washindi watano wa awali watapewa ving’amuzi, na mshindi wa tatu wa Miss talent atapata Bajaj yenye thamani ya Sh.3,000,000.
 
Awali, meneja wa matukio wa TBL kanda ya ziwa, Erick Mwayela, alisema kampuni yake imekuwa mstari wa mble kudhamini vipaji vya warembo kwa miaka mingi.
 
“Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza vipaji vya warembo na mavazi nchini,” alisema Mwayela.
 
Warembo watakaowania zawadi hiyo ya kwanza ni Christina William, Moshi Shaban na Doreen Robert wote wa Mwanza, Cecilia Kibanda, Evelyne Charles, Chritine John (Simiyu), Winfrida Nashon, Elinaja Nnko na Martha John wote toka Mara.
 
Wengine ni Mary Emanuel, Nicole Sarakyika na Recho Judica toka Shinyanga, Jackline Kimanbo, Nyangi Warioba na Faudhia Haruna (Kagera), wakati toka Geita ni Recho Clavery, Farida Ramadhani na Rose Msuya.

NCHI NANE KUCHUANA MICHUANO YA KIMATAIFA YA MCHEZO WA WUSHU DAR ES SALAAM.

August 17, 2014
NA ELIAS KIMARO,DAR ES SALAAM.
NCHI nane zikiwamo za China, Kenya, Iran na wenyeji Tanzania inatarajiwa kuchuana katika michuano ya kimataifa ya mchezo wa Wushu itakayofanyika kati ya Agosti 30-31 jijini Dar es Salaam.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Wushu Tanzania (TWA), Sempai Golla Kapipi ameiambia TANGA RAHA kuwa, michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na Tanzania kuanzia saa 4 asubuhi.

Sempai Kapipi alisema wenyeji Tanzania itawakilishwa na klabu 23 na wachezaji wengine mmoja mmoja dhidi ya wawakilishi wa nchi za Kenya, Uganda, Iran, China, Libya, Nigeria na Zimbabwe.

"Nchi zilizothibitisha mpaka sasa kushiriki michuano hiyo ni majirani zetu wa Kenya na Uganda, Iran, China, Zimbabwe, Nigeria na Libya na wenyeji Tanzania itakayowakilishwa na klabu 23," alisema.

Katibu huyo alifafanua kuwa katika michuano hiyo kutakuwa na mitindo miwili itakayoonyeshwa kupitia mchezo huo maarufu kama Kungfu ya Sanda na Tai-ru itakayohusisha mapigano ya mapanga.

Sempai Kapipi alisema kuwa wapo katika mipango ya kuwaalika wanamichezo wa judo, karate na ngumi ili kuonyesha manjonjo yao.

Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuandaa michuano mikubwa ya mchezo huo baada ya awali kuandaa michuano ya taifa iliyohusisha klabu pekee za Tanzania iliyofanyika Ufukwe wa Coco mwaka 2011.

Naye Mkurugenzi wa mashindano wa chama hicho, Karama Masoud 'Karapina' alisema maandalizi yanaendelea vyema na wawakilishi wa nje ya nchi na klabu za mikoa mbalimbali wataanza kuwasili wiki ijayo.

"Kila kitu kimekaa vema na tutaanza kupokea wageni ndani ya wiki ijayo, hadi siku ya kuanza kwa michuano tunaamini wawakilishi wote watakuwa wameshawasili jijini Dar es Salaam," alisema Kalipina.

MIFUGO NI MALI - UZALISHAJI WA BIDHAA ZITOKANAZO NA MIFUGO

August 17, 2014

PEMBE ZA NG'OMBE AINA YA ANKOLE ZILIZOONGEZWA THAMANI 

Pembe hizi hupatikana zaidi maeneo ya Magharibi mwa Tanzania ambapo Ng'ombe aina ya Ankole wanafugwa, "Tembelea maeneo ya Machinjio na Minada" zinapatika








Picha zinazoonekana ni pembe za ng'ombe zilizoongezwa thamani kwa kutumika kama kishikia taa au kwa kingereza Lamp Holder  




Urembo ni kitu muhimu kwa Mwanamke Bangili na Hereni zitokanazo na pembe za Ng'ombe Wajasiriamali Mpo''''''''''''''''''''''''''' mawasiiano Deo Kagera 0767894492                  kwa 

WAZIRI KAMANI ATEMBELEA MKOA WA TANGA KUJIONEA MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

August 17, 2014


JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA KAMA VINAVYOONEKANA KATIKA PICHA

KUSHOTO NI WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI,MHE DKT TITUS KAMANI AKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI TANGA KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI

KUSHOTO NI WAZIIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI,MHE:DKT TITUS KAMANI KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA TANGA ,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIMSIKILI KAIMU OFISA UVUVI WA MKOA WA TANGA AMBAYE HAYUPO PICHANI KULIA NI KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA,BENEDICT NJAU

WA NNE KUSHOTO NI WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA UVUVI NA MIFUGO MHE: DKT TITUS KAMANI AKIWA NA MAAFISA KUTOKA WIZARA HIYO WALIOTEMBELEA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA MWISHONI MWA WIKI KUZUNGUMZA NA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA ALIYEKAA KATIKATI.

DAKTARI WA MIFUGO MKOA WA TANGA ZODIAC LYIMBO AKITOA TAARIFA YA HALI YA SEKTA YA MIFUGO MKOA WA TANGA KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI  MHE:DKT TITUS KAMANI AMBAYE HAYUPO PICHANI WAKATI ALIPOTEMBELEA MKOA WA TANGA.


WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI  MHE:DKT TITUS KAMANI  KUSHOTO AKIMPA ZAWADI MSHINDI WA KWANZA WA SHINDANO LA MAZIWA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA JUKWAA LA MAZIWA TANZANIA
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI  MHE:DKT TAITUS KAMANI AKIKABIDHIWA ZAWADI MSHINDI WA PILI KATIKA SHINDANO HILO

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI AKIMKABIDHI ZAWADI MSHINDI WA TATU ALIYEIBUKA MSHINDI KATIKA SHINDANO HILO
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI KUSHOTO AKIANGALIA JINSI MAZIWA YANAVYOKAMULIWA KWA KUTUMIA NJIA SAHIHI ZA KUKAMUA MODULI YA KIWELE CHA NG'OMBE
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI AKIANGALIA KWA UMAKINI MAZIWA YANAVYOKAMULIWA KWA KUTUMIA NJIA SAHIHI ZA KUKAMUA MODULI YA KIWELE CHA NG'OMBE

 WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI KUSHOTO AKIPATA MAELEZO JINSI YA MITAMBA BORA ILIYOZALISHWA KWENYE SHAMBA LAILA AGRO FARM LILILOPO PONGWE JIJINI TANGA.
WAZIRI WA  MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI AKIANGALIA MASHINE INAYOTUMIA UMEME YA  MFUMO WA UKAMUAJI MAZIWA KATIKA KAMPASI YA MAFUNZO YA VYUO VYA MIFUGO(BUHURI) ANAYETOA MAELEZO NI MKURUGENZI WA KAMPASI HIYO PAUL SHEMPEMBA.
WAZIRI WA  MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI AKIANGALIA MASHINE INAYOTUMIA UMEME YA  MFUMO WA UKAMUAJI MAZIWA KAMPASI YABUHURI ANAYETOA MAELEZO NI MKURUGENZI WA KAMPASI HIYO PAUL SHEMPEMBA

 WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA KAMPASI YA BUHURI MKOANI TANGA MARA BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI HAPA
WAFANYAKAZI WA KAMPASI YA BUHURI WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI  MHE.DKT TITUS KAMANI AMBAYE HAYUPO PICHANI.
 
MKURUGENZI WA KAMPASI YA BUHURI PAUL SHEMPEMBA KATIKATI AKITOA MAELEZO YA MAJANI AINA YA MIKUNDE AMBAYO NI MALISHO BORA KWA MIFUGO KUSHOTO NI WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI,MHE.DKT TITUS KAMANI AKIPANDA MITI WA KUMBUKUMBU KATIKA KAMPASI YA WAKALA WA MAFUNZO YA VYUO VYA MIFUGO NCHINI BUHURI MARA BAADA YA KUITEMBELEA WAKATI AKIWA KWENYE ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI TANGA.
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI KWA KWANZA KULIA AKIPATA MAELEZO KUTOKA MENEJA  WA SHAMBA LA HOLLAND DIARIES BWANA LUT ZYLSTRA  KUHUSU UMILIKI WA ENEO HILO
WAZIRI WA MAENDELEO YA UVUVI NA MIFUGO KULIA MHE:DKT TITUS KAMANI AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIZUNGUMZA NA MENEJA WA SHAMBA LA HOLLAND DIARIES BWANA LUT ZYLSTRA WA TATU KUTOKA KUSHOTO.
MENEJA WA SHAMBA LA HOLLAND DIARIES BWANA LUT ZYLSTRA WA TANO KUSHOTO AKIMUELEZA JAMBO WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TAITUS KAMANI WAKATI WAZIRI HUYO ALIPOFANYA ZIARA KWENYE SHAMBA HILO.
MSAIDIIZI WA MENEJA WA SHAMBA HILO MR.MTUNGUJA AKIMKABIDHI TAARIFA YA SHAMBA HILO WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI AKIPEWA MAELEZO NA DAKTARI WA SHAMBA LA UZALISHAJI WA MITAMBA LA MRUAZI DKT ALLY SAIDI MAJANI.
MTAALAMU WA MIFUGO WA KUPANDISHA NG'OMBE,MBEGU BORA  AINA YA KIKE KATIKA SHAMBA LA MITAMBA LA MRUAZI BWANA WILIAM MGUNYA AKITOA MAELEZO KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI.
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI,MHE:DKT TITUS KAMANI AKIANGALIA NDAMA BORA WALIOZALISHWA KUTOKA KWA MAJIKE YA ASILI.
DKT.ALLY SAIDI MARIJANI KUTOKA SHAMBA LA MITAMBA LA MRUAZI KATIKATI AKIONYESHA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI NG'OME WAZAZI WANAOHAMILISHWA KWA KUTUMIA MBEGU BORA ZA MADUME ZA KIKE
             MFUGAJI WA NGO"MBE WA MAZIWA KUTOKA USHIRIKA WA CHAMA CHA MSINGI WAKO WILAYANI KOROGWE BWANA AMIRI MOHAMED SHEKILANGO AKITOA KERO YAKE KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE:DKT TITUS KAMANI

            AFISA USHIRIKA WA WILAYA YA KOROGWE BIBI JACKLINE AKIFUATILIA KWA MAKINI MAJIBU YA KERO ZA WAFUGAJI KUTOKA KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE.DKT TITUS KAMANI AMBAYE HAYUPO PICHANI.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA BLOG YA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI.
www.habarimfugouvuvi.blogspot.com