WAFANYAKAZI sekta mbalimbali nchini watakiwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwenye maeneo yao.

July 16, 2013
Na Elizaberth Kilindi,Tanga
 
WAFANYAKAZI wa sekta mbalimbali nchini wametakiwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi na hivyo waondokane na imani kuwa vyama hivyo avitatui migogoro ya wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tucta mkoani Tanga Hemed Ngereza wakati akifanya mahojiano na blog hii,ofisini kwake na kusema kuwa na vyama vya wafanyakazikatika eneo la kazi ni vema vikawepo kwani tatizo linapotokea wapate kiongozi wa kuweza kuwaesemea katika mahali husika.

Aidha kusema kuwa kila sekta inapaswa kuwa na chama cha
wafanyakazi ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo kwa wafanyakazi wao sanjari na kuboresha maslah pamoja na kutetea haki za wafanyakazi wao ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi na ufanisi wa utendaji kazi.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa bado Elimu inahitajika kwa
wafanyakazi wa maeneo mbalimbali kwani wengi wao hawaelewa umuhimu wa vyama hivyo katika sehem zao zakazi hivyo ni jukumu la kila mmoja kujitambua na kubadilika.

Ngereza alisema kuwa serikali pia inapaswa kuwapatia wafanyakazi wa sekta zote mikopo endelevu sambamba na kupunguza ukali wa sheria za mikopo ya kibenki ili waweze kutumia mikopo hiyo kwa kujiendeleza.

mwisho