Afya ya Maranda sasa yatetereka, alazwa Moi

March 04, 2014
Dar es Salaam. Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda, anayetumikia kifungo cha miaka 18 gerezani kwa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la mgongo.
Msemaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI), Jumaa Almasi aliliambia gazeti hili jana kuwa Maranda alifikishwa hospitalini hapo Februari 16, mwaka huu.
“Ni kweli Maranda yupo hapa tangu Februari 16 na alifanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mgongo wiki tatu zilizopita na hali yake inaendelea vizuri ingawa hawezi kuamka kitandani,” alisema Almasi.
March 04, 2014

Ridhiwani ashinda Kura za maoni CCM kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Chalinze

Matokeo:
Ridhiwani Kikwete kashinda kwa kupata kura 758 kati ya kura 1321,
Ilikuwa hivi:_
1.Ridhiwani Kikwete kura 758
2.Shaban Iman Madega kura 335
3.Athuman Ramadhan Maneno kura 206
4.Changwa Mohamed mkwazu kura 12
Kura zilikuwa 1363 zilizo Haribika 5 na Halali ni kura 1316
Wagombea wa Ubunge Chalinze kwa tiketi ya ccm walikuwa ni:-
1.Ndg.Ridhiwani Kikwete,
2.Shaban Iman Madega,
3.Athuman Ramadhan Maneno
4.Changwa Mohamed mkwazu
Tarehe 9/3/2014 KUCHUKUA FOMU
Tarehe 11/3/2014 KURUDISHA
Tarehe 15/3/2014
UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CC
Kwa hisani ya http://www.jamiiforums.com




Ndg.Ridhiwani Kikwete Mgombea wa ubunge katika Kura za Maoni za CCM jimbo la Chalinze akijipigia Kura muda huu , pia akipanga mstari katika uwakilishi wa Kata anayotoka ya Msoga..Zoezi la upigaji kura linaendelea hapa Msata (Chalinze).
March 04, 2014

Matukio Bunge la Katiba Leo

IMG_3125 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Jenista Mhagama (Kushoto) ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bi. Christowaja Mtinda wakiwasili katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. IMG_3137 
Wajumbe wa bunge maalum la Katiba Jumanne Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Maji akiwa na Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. IMG_3156 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira( Kulia). Leo Mjini Dodoma. Chini yao ni wajumbe wa Bunge Hilo Seif Khatibu( Kushoto) na Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
March 04, 2014

JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO

·        ARIDHISHWA NA UTIMAMU WA VIKOSI HIVYO KIMAFUNZO NA ZANA
·        AAHIDI TATIZO LA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI NDANI YA MWAKA 2014
·        KIKOSI CHA UHANDISI WA MEDANI CHAAHIDIWA VIFAA ZAIDI ILI KUPAMBANA NA MAJANGA NCHINI
·        AAGIZA JWTZ KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAKAZI YA MUDA
Ziara hiyo ya siku moja ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa
Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
(Na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT)
1 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando 2 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro. 3 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake. 5 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha. 6Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake. 7 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani). 8Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
March 04, 2014

Muungano wa Tanzania ni kielelezo cha maendeleo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan akiongea na waandishi wa habari( Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa masuala ya Muungano wakati wa Mkutano leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Ofisi hiyo Bi. Siglinda Chipungaupi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan leo mjini Dodoma.
(PICHA NA HASSAN SILAYO)
Na Jovina Bujulu
Muungano wa Tanzania umeendelea kuwa nyenzo na utambulisho muhimu katika kuleta umoja na maendeleo katika taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mh. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.
“Miaka 50 ya Muungano imekuwa ni ya mafanikio makubwa ambayo yamewanufaisha wananchi katika nyaja mbalimbali kijamii, kiuchumi, na Kisiasa” alisema Waziri Suluhu.
Waziri Samia alisema kuwa muungano huo umeendelea kuwa kielelezo imara katika suala la ulinzi na usalama hali iliyowezesha kuwepo kwa amani na utulivu nchini.
Katika suala la haki za binadamu Waziri Samia alisema kuwa suala hilo limeendelea kupewa kipaumbele ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wananchi wameendelea kupata haki zao za msingi kupitia mahakama za Mwanzo hadi za Juu.
Akifafanua kuhusu suala la elimu Waziri Samia alibainisha kuwa wanafunzi wenye sifa Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa mikopo ili kukidhi gharama za Masomo, hali iliyosabisha uimarishwaji wa elimu ya juu kwani kuwekuwepo kwa ongezeko la vyuo vya elimu ya juu kutoka 25 mwaka 2015 hadi 63 vilivyopo sasa.
Aidha Waziri Samia alisema kuwa Serikali hizi mbili zinashirikiana katika kubuni na kuibua miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Serikali kwa Kushirikiana na Wahisanai wa Maendeleo.
“Serikali hizi zimekuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya mandeleo mfano Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF III, MACEMP, ASDPL na ASDP kwa ujumla imekuwa ni chachu kubwa ya Maendeleo ya wananchi katika pande zote za Muungano” Alisema Waziri Samia.
Waziri Samia aliongeza kuwa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa Zanzibar tarehe 1 Machi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein ambapo nembo ya Muungano ilizinduliwa na sherehe za Muungano zitafanyika Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Utanzania wetu ni Muungano wetu, Tuulinde, Tuumarishe na Kuudumisha.”

*ALLY CHOKI ALIZWA SAA YA DOLA 300 YA SILVERA

March 04, 2014
 Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi Extra Bongo 'Next Level' 'Kamarade' 'wazee wa Kimbembe' Ally Choki alijikuta akimwaga machozi baada ya watu wanaodhaniwa kuwa vibaka kujipenyeza wakati wa uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' iliyozinduliwa Februari 22 mwaka huu na kumuibia saa ya silva yenye thamani ya dola 300 sawa na sh.500,000.
Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon

Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon

March 04, 2014
01
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) wakishiriki mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro jana. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji.
02
Mmoja wa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Kilomita tano za Vodacom Fun Run, Tsadia Jessie Bercuvitz (5) raia wa Uingereza akipewa sponji lenye maji kwa ajili ya kupunguza joto na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Saruji Tanga, Mtanga Noor wakati wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
03
Waziri wa Habari  Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo ,Dkt Fenella Mukangara akimpa cheti Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Leslie Massawe (wa pili kulia)  kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yaliyomalizika juzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kushoto kwa Waziri Mukangara ni Waziri wa Mifugo, Dk Titus Kamani.
 
04
Wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, Changwa Mjella (kulia) na Mtanga Noor (katikati) wakimpa maji mmoja wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
05
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart (kulia) akimpa maji mmoija wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro juzi. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji . Wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.
March 04, 2014
Grassroot programme kusheheresha Siku ya wanawake Duniani
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  kwa kupitia kamati ya wanawake na chama cha mpira wa miguu kwa wanawake wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani.Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika kusheherekea  siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu wanawake  ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake
Mwenyekiti TWFA/WFC
Lina P. Kessy 
March 04, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 4, 2014

TFF KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.

Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.
March 04, 2014

JK AKAGUA MADARAJA YA KIJESHI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua madaraja ya kijeshi yakiwemo yale ya kuelea juu ya maji wakati alipokagua zana za kijeshi jana, Jumatatu, Machi 2, mwaka huu, 2014.
CHANZO:MROKI MROKI.
March 04, 2014

*VITA KALI YA MASAA MATANO CHATU NA MAMBA, MAMBA HOI ATOLEWA MAJINI NA KUMEZWA

Nyoka aina ya Chatu akipambana na Mamba ndani ya maji.
Nyoka huyo baadaye alifanikiwa kumzidi nguvu Mamba na kumuua na kisha kumtoa ndani ya maji hadi nchi kavu na kuanza kummeza.
******************************************
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotarajiwa na wengi, Nyoka mkubwa aina ya Chatu ameibuka na ushindi kwa kumsinda nguvu Mamba akiwa ndani ya maji na kisha kumtoa nchi kavu na kummeza, huko Kaskazini mwa mji wa Queens Land.
March 04, 2014

Waziri Mkuu awataka wajumbe wa bunge la katiba kuwa na staha na matumizi ya lugha sahihi

IMG_3007 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiongea na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na kuwataka kuzingatia maadili na lugha fasaha katika kikao hichi ili kufikia lengo linalotazamiwa kwa maslahi ya Taifa.Wakati wa semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. IMG_3014 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi(Kushoto) leo mjini Dodoma. IMG_3059 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Vuai ally Vuai akiongea leo katika semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kuwataka wajumbe kufuata yale aliyoyasema Waziri Mkuu ya kuzingatia Staha ya Lugha katika Vikao vya Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma. IMG_3099 
Baadhi ya wa Bunge Maalum la Katiba waliohudhuria katika semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO
March 04, 2014

WAANDISHI NA WADAU WA HABARI WAJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PPF HAPO JANA KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE, JIJINI DAR ES SALAAM

Mwandishi wa Habari Ndg Elias Mnonjera Daudi akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF jana mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF ulilenga Kuwapa elimu waandishi na wadau wa habari nchini juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF.
 Mwandishi wa habari, Ndg Francis Dande (wa kwanza kulia) akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa pensheni wa PPF jana  mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF ulilenga Kuwapa elimu waandishi na wadau wa habari nchini juu ya huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF.
Mwandishi wa Habari wa Kituo Cha Runinga cha ITV, Bi Fatma Almasi Nyangasa akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF jana mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF.

CHADEMA TANGA YAMKALIA KOONI MWEKEZAJI.

March 04, 2014
KULE HIPI NAPO WALIHARIBU MASHAMBA YENU:HII NI KAULI YA KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAWEJE KATIKA AKIONYOOSHA VIDOLE AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA HICHO NGAZI YA WILAYA NA KATA WILAYA YA KOROGWE WALIOPOKWENDA KUANGALIA UHARIBIFU ULIOFANYWA NA MWEKEZAJI KWENYE MASHAMBA WALIOLIMA WANANCHI WA VIJIJI VILIVYO ENEO LA SHAMBA LA MKONGE LA KWASHEMSHI ESTATE.

KOROGWE.
KATIBU wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Tanga(Chadema) Jonathan Bawehje amemuagiza Katibu wa Chama hicho Jimbo la Korogwe Vijijini,Salim Sempori kumuandikia barua Mwekezaji wa Shamba la Mkonge la Kwashemshi Estate awalipe fidia wakazi wa kijiji cha Kwashemshi walioharibiwa mazao yao waliokuwa wamepanda kwenye shamba hilo ndani ya siku saba la sivyo watakwenda kumshtaki mahakamani.

ATHUMANI RASHID MMOJA WA WAKAZI WA KIJIJI CHA KWASHEMSHI AKIMUONYESHA KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAWEJE JINSI MWEKEZAJI WA SHAMBA HILO ALIVYOFANYA UHARIBIFU KWENYE MASHAMBA WALIOPANDA MAHINDI.
 Lakini viongozi hao walifika mbali zaidi na kutaka pia kumshtaki Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Vijijini ,Diwani wa kata hiyo Rasuli Semahombwe na  Mtendaji wa Kata hiyo Kimweri Magogo kwa madai ya kushindwa kulipatia suala hilo ufumbuzi suala hilo.
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAWEJE KUSHOTO AKIMSIKILIZA MMOJA WA VIONGOZI WA CHAMA HICHO WILAYA YA KOROGWE KWENYE MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATA YA KWESHEMSHI WILAYANI HUMO.

MUHEZA WAANZISHA DORIA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

March 04, 2014


MUHEZA.
MKUU wa wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu amesema wilaya hiyo imeanzisha doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya misitu na ukanda wa bahari kwenye kata za Kigombe ili kuweza kukabiliana na wimbi la uharibifu wa mazingira hususani ukataji wa miti.

Mgalu alitoa kauli hiyo wakati akisoma taarifa fupi ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kwa kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.