February 28, 2014
MAJANGA.....BASI LAGONGANA NA TRENI MANYONI!!!!
Basi la Bunda Express likiwa eneo la ajali Manyoni, Singida.
Basi la Bunda Express likitokea Dodoma-Mwanza, limegongana na treni eneo la Manyoni ambapo inadaiwa watu wanne wamepoteza maisha. Majeruhi tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
February 28, 2014

UONGOZI WA SIMBA WAWEKA WAZI SUALA LA KUMUONGEZEA MKATABA KOCHA WAO

Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi kuwa suala la kumuongezea mkataba kocha wake mkuu wa sasa, Zdravko Logarusic limewekwa pembeni kwa kuwa wanasubiri kuona mwelekeo wa timu yao ambayo imekuwa haina matokeo mazuri hivi karibuni.
Loga raia wa Croatia alisaini mkataba wa miezi sita wakati alipotua klabuni hapo mwishoni mwa mwaka jana, ambapo mkataba huo unatarajiwa kufikia tamati Juni mosi, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, aliweka wazi kuwa matokeo ya timu katika mechi zilizosalia ndiyo yatapa picha uongozi juu ya kuongeza au kutoongeza mkataba huo.

DR.MAGUFULI AKAGUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM

February 28, 2014
Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuli Kituo cha BRT kivukoni jijini Dar es salaam leo akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyekaa kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe (katikati) pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale (aliyesimama) wakisafiri kwa basi kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
February 28, 2014

Wanafunzi wa Tanzania Thailand Waizungumzia sekta ya Madini.

1Kamishna Msaidizi wa Madini  Mhandisi Hamis Komba katikati akiwa pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand. Wa kwanza kulia ni Agatha Mwinuka, anayefuata ni Emmanuel Minja na wa kwanza kushoto ni Doricas Moshi. 2Wanafunzi wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea  banda la Tanzania. 3 (2)Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.
……………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na  mchango wake kiuchumi.
Aidha, wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.
February 28, 2014
February 28, 2014

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA MEYA WA JIMBO LA CALIFONIA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meya wa Jimbo la Califonia nchini Marekani Mstahiki  Osby Davis,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na  Meya wa Jimbo la Califonia nchini Marekani Mstahiki  Osby Davis,leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao .Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
February 28, 2014
*MALINZI AUNDA KAMATI YA MIAKA 50 FIFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.