BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

July 19, 2016


Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mbele) akitoka kukagua eneo lililoathirika na mmomonyoko wa ardhi eneo la Lukumburu Mkoani Njombe. 
Muonekano wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. 

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe alipotembelea kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotoa taarifa ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akisalimiana na Wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.


Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimbeba mtoto aliyehudhuria kikao cha Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akicheza na wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe waliokuwa na furaha mara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Iringa Bi. Elikael Manase akitoa maelezo kwa Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari ya mmomonyoko wa ardhi unavyoathiri sehemu ambayo Mkongo wa Taifa umepita eneo la Lukumburu Mkoani Njombe. 




Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe. Wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

……………………………………………………………………………………………

Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 109.4 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Njombe ili kurahisisha huduma ya usafiri wa barabara kwa wakazi wa mikoa hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo mkoani Njombe wakati akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, kata ya Ulembwe, wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua barabara hiyo.Profesa Mbarawa amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo imetenga kiasi cha sh.bilioni 19 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

“Tumejipanga na tuna nia dhabiti kuhakikisha barabara hii tutaijenga kwa kiwango cha lami na katika kuharakisha kazi hii tutatafuta makandarasi wawili ili ujenzi huu ukamilike kwa haraka”, amesema Prof. Mbarawa.Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewataka wananchi kushirikiana na Makandarasi watakapoanza ujenzi huo ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kulete tija kwa wananchi wa Mikoa ya kanda ya kati.

Amesema kuwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Njombe upo katika hatua za kutangaza zabuni ili kupata Makandarasi wenye uwezo wa kujenga barabara hiyo kwa kuzingatia viwango kulingana na mkataba.Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Eng. Yusuph Mazana amesema kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makaete yenye urefu wa KM 109.4 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umekamilika na Mhandisi mshauri M/s Crown Teach Consult Ltd ameshawasilisha taarifa ya usanifu wa kina.

“Tumepokea taarifa ya usanifu wa kina kutoka kwa Mhandisi Mshauri hivyo tunahaidi kusimamia utekelezaji wa mradi huu kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani”,amesisitiza Eng. Mazana.Waziri Prof. Mbarawa ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo Mkoani Njombe.

JUST IN: TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MSD JUU YA UAMUZI WA BODI YA WADHAMINI KUHUSU WAKURUGENZI WALIOSIMAMISHWA

July 19, 2016

SBL yazindua bomba la 470m/- kudhibiti majitaka

July 19, 2016


Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie  wakiongozana kuelekea kwenye  bomba la kudhibiti wa majitaka  ambalo linalenga  kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira  na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo kwa wageni waalikwa katika hafla   ya uzinduzi wa bomba la majitaka  ambalo lilizinduliwa na  Mhe. Luhaga Mpina Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira mapema leo katika kiwandani hapo mapema leo.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini jinsi mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akifurahi jambo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie mara baada ya kukata utepe katika mtambo kusafirisha majitaka katika hafla iliyofanyika mapema leo kiwandani hapo,


Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiwasha mtambo wa kusafirisha majitaka  kiwandani hapo mara baada ya kuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika kiwanda hicho Temeke Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda cha bia cha serengeti wakifuatilia kwa makini

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia ya serengeti mara baada ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda hicho Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Julai 19, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imezindua  bomba la kudhibiti wa majitaka  ambalo linalenga  kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira  na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.


Bomba hilo  limejengwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Maji Safi na Taka  ya Dar es Salaam (Dawasco), Mamlaka ya Barabara (Tanroads) na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke  likihusisha takribani  kilometa mbili kuanzia katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichpo Temeke  hadi Kurasini ambako ndip ulipo mfumo wa majitaka wa Dawasco.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie, alisema kwamba  mradi huo wa aina yake na wa kwanza nchini unadhihirisha juhudi zisizo na ukomo za kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira.


“Ubora wa maji ni jambo lililo mstari wa mbele katika utengenezaji wa bia  lakini suala la usafi kutokana na kuzalishwa kwa majitaka ni sehemu kubwa inayotujengea hisia za kimazingira katika shughuli za kutengeneza bia. Kwa hiyo uzinduzi wa bomba hili ni moja ya hatua ya kusonga mbele  katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira safi kiafya,” alisema Weesie.


Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha kwamba majitaka yanayotolewa na bomba hilo yatakuwa yanafanyiwa tiba kwanza ili kuondoa aina yoyote ya sumu kabla ya kuachiwa ili kuingia katika mfumo wa majitaka wa Dawasco.


 Alisema kuwa uzinduzi huyo uko katika mkondo  mmoja na sera ya Kampuni ya Serengeti ya kujikita katika ustawi wa jamii ambayo imeainishwa katika maeneo manne ya vipaumbele ambavyo vinajumuisha, Utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuboresha Unywaji wa Kistaarabu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Masuala ya Muungano na Mazingira, Mh. Luhanga Mpina aliipongeza Serengeti kwa kuzindua bomba hilo  akibainisha kwamba  ujenzi  unaendana na ajenda ya serikali  ya uhifadhi wa mazingira.

Mpina alibainisha kwamba uchafuzi wa mazingira katika miji na maeneo ya pembezoni unaathiri afya za watu wengi na kupunguza tija inayotokana na mazingira na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga  kazi nzuri ya Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kuhifadhi mazingira. photo ab Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com : www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ashiriki maadhimisho miaka 59 ya Aga Khan kuongoza Ismailia

July 19, 2016


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba (Mb.), akizungumza katika maadhimisho ya Miaka 59 ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Shia Ismailia, Mtukufu Aga Khan tangu aliposhika nafasi hiyo.Katika hotuba yake Dkt. Kolimba alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mtukufu Aga khan kwa mafanikio katika kipindi cha uongozi wake na kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo iliyochini ya Taasisi yake. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Ismailia hapa nchini, Bw. Amin Kurji. 
Mkurugenzi wa masuala ya kidiplomasia katika Taasisi ya Aga Khan, Balozi Arif Lalani pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Mhe. Kolimba (hayupo pichani) alipokuwa akiendelea kuzungumza kwenye maadhimisho hayo. 
Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara(Kulia) akifuatilia hotuba ya Mhe. Kolimba pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Hellen Mgeta. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Ramla Khamis (wa pili kutoka kushoto), akiwa pamoja na Maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa hafla hiyo. 
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo nao wakimsikiliza Dkt. Kolimba, wa pili kutoka kulia ni Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshinda. 
Wageni waalikwa . 
Mhe. Dkt. Kolimba na Bw. Kurji wakiwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mtukufu Aga Khan wakati wa hafla hiyo. 
Dkt. Kolimba akitambulishwa kwa wageni waalikwa na Bw. Kurji 
Dkt. Susan Kolimba akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam aliyebuni mchoro waa Chuo Kikuu cha Aga Khan kitakachojengwa Jijini Arusha. 
Picha na Reginald Philip

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB YAIPIGA JEKI TANZANIA DOLA MILIONI 200

July 19, 2016


 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero, alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto), akimsikiliza kwa makini  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Kushoto) akibadilishana "Business Card"  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), (Katikati), akiwa katika mazungumzo maalumu na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake Jijini Dar es slaam, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
 Kaimu Kamisha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta Mtagwaba akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani), ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akibadilishana "Business Card"  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa katika mazungumzo maalumu na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto) akizungumza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.


Na Benny Mwaipaja-WFM 

BENKI ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, imeahidi kuchangia Dola Milioni 200, sawa na Shilingi 433.6b, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2016/2017. 

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es salaam 

Makamu huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia Dola Milioni 150. "Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa serikali ya Tanzania imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa" Alieleza Dkt. Kacou 

Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahili ya maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo. "Tuna malengo matano ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula, kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla" aliongeza Dkt. Kacou 

Amepongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi. Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS). 

Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga. 

"Vilevile tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini" Aliongeza Dkt. Mpango 

Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. "Mpango huo utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda vitapata malighafi ya kutosha" alisisitiza Dkt. Mpango 

Amerejea msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada inayoambatana na masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta maendeleo. 

"Hatutakubali misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe" alieleza Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii. 

Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

KIWANDA CHA KUTENGENEZA SODA AINA YA PEPSI CHAPIGWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

July 19, 2016
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (Kulia) akifurahia Jambo na Meneja Mahusiano wa kiwanda cha Pepsi bw,Alexander Nyirenda alipotembelea kiwanda hicho kilichopo kiwalani Temeke Jijini Dar es salaaam mapema hii leo.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa ameambatana na Maafisa wa Mazingira kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira Nchini( NEMC)akikagua mfereji unaotiririsha maji machafu kutoka katika kiwanda hicho na kusababisha madhara kwa wanainchi wanaozunguka eneo hilo.   
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha pepsi kilichopo kiwalani,temeke jijini dar es salaam

                                                          EVELYN MKOKOI
                                 AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
                                        KIWALANI-DAR ES SALAAM
                                                         19/7/2016

Kiwanda cha kutengeneza kinywaji cha soda aina ya Pepsi kilichopo Kiwalani jijini jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni 25 na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku kumi na nne kwa kosa la uchafuzi wa mazingira, kwa kutiririsha maji machafu yenye kemikali katika mtaro wa maji ya mvua ya mtaa wa kiwalani.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa adhabu hiyo ya ukiukwaji wa sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kupitia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ya kukagua mazingira ya jiji la Dar es Salaam na mitaa ya viwanda.
Naibu Waziri Mpina alisema kuwa wawekezaji wenye viwanda wanapaswa kuelewa kuwa NEMC huwa inapita mara kwa mara na kutoa mwongozo, wa utekelezaji wa sheria ya mazingira na kuwataka wawekezaji waache dharau ya kuthaminisha maisha ya wananchi kwa gharama ndogo, na kuwaasa wawe serious na sheria ya mazingira, na kuwaonya wamiliki wa kiwanda cha SBC Tanzania Limited. kuacha kabisa kutiririsha maji machafu, pamoja na kuelekeza kila kiwanda kiwe na Afisa Mazingira ambae ndiyo mshauri mkuu wa masuala ya mazingira.
Aidha Mhe. Mpina aliwataka wawekezaji pia wapeleke kwake malalamiko ya watendaji wa NEMC ambao wanaona hawawatendei haki.
Awali akitamka adhabu hiyo  Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Jaffari Chimgege alisema kuwa  pamoja na adhabu hiyo kiwanda hicho cha Pepsi pia kimekuwa na kosa la kutiririsha maji hayo machafu bila kuyatibu na kwa mujibu wa sheria ya wenye viwanda walitakiwa kukusanya taarifa ya ukaguzi kwa baraza, ili kuona kama wanatekeleza sheria ya mazingira na hawakufanya hivyo.
“Wafanyie kazi haraka taarifa ya ukaguzi.”
Kwa upande wake, Afisa Mauhusiano wa kiwanda hicho Bw. Alexandra Nyirenda aliliomba Baraza (NEMC) kuelekeza wenye viwanda zaidi ya mara mbili kabla ya kutoa adhabu, ili waweze kwenda sawa na  utekelezaji wa Sheria ya mazingira na kanuni zake kwani kujisahau ni ubinadamu.
Wakati huo huo; Mhe Naibu Waziri Mpina amezindua bomba lenye urefu wa kilometa mbili la, utoaji maji taka katika kiwanda cha bia cha Serengeti. (SBL) cha Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

Dk. Kigwangalla asimikwa Uchifu wa Wanyamwezi wa Tanzania, aahidi makubwa

July 19, 2016
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepewa heshima ya Uchifu wa Watanzania wa Kabila la Wanyamwezi na Wazee wa Kijiji cha Isalalo katika Kata ya Utwigu iliyopo katika Jimbo hilo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho,
Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.
Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.
Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.
“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.
Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.
Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.
Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
DSC_2015 DSC_2023 DSC_2030Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wanakijiji cha Isalalo
DSC_2032
Wazee wa Mila
DSC_2037
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni
DSC_2038
Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum
DSC_2043
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akivishwa shuka katika hatua ya kusimikwa uchifu huo
DSC_2044 DSC_2047
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale
DSC_2050 DSC_2051 DSC_2054 DSC_2059
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipewa baraka na wazee hao
DSC_2083 DSC_2062 DSC_2066 DSC_2073 DSC_2073 DSC_2083 DSC_2084 DSC_2088
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akirejea kukaa baada ya kukabidhiwa Uchifu wa Wanyamwezi
DSC_2089
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akinyanyua juu mkuki ishara ya Kijana shujaa wa Wanyamwezi..
DSC_2095
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Diwani wa Kata Utwigu
DSC_2104 DSC_2123
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa shukrani zake kwa wananchi
DSC_2174
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kijiji
DSC_2186
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea salamu kutoka kwa watoto
DSC_2201 DSC_2212 DSC_2217
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
DSC_2219
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
DSC_2224
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).