RC MAKONDA AMWAPISHA MKUU WA WILAYA MPYA WA KINONDONI ALLY SALUM HAPI JIJINI DAR ES SALAAM

April 21, 2016

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akijiandaa kuapa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwa tayari kumwapisha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisaini hati ya kiapo wakati alipomwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akisaini hati ya kiapo chake, mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akionesha Katiba ya Jamhuri ya Muungano (kushoto) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambavyo alikuwa tayari kumkabidhi Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mara baada ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akiabidhiwa maua na Katibu Tawala Msaidizi (Utawala) wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elly Mcha. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.  
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akiabidhiwa maua na Katibu Tawala Msaidizi (Utawala) wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elly Mcha. 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akisoma salamu za Mkoa kwa Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akimkabidhi kadi yenye salamu za Mkoa Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi. 
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi, akizungumza mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akizungumza wakati akielezea kuhusu hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (wa pili kushoto), jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wa nne ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waalikwa, wafanyakazi wa Manispaa za jijini la Dar es Salaam na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza wakati wa kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kulia), jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kulia), akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Wakuu wa Wilaya za Ilala, Raymond Mushi (kushoto) na wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, wakiwa katika hafla hiyo ya kumwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akielezea kuhusu utaratibu wa kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (katikati), wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla hiyo. 
Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya. 
Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya.  
Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Adrofina Ndandakizye, akichukua habari wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

TIGO YATANGAZA VIDEO ZA YOU TUBE KUPATIKANA BURE USIKU KWA WATU WOTE

April 21, 2016
 Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia  (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu huduma iliyoanzishwa na kampuni hiyo ya kutiririsha  video za YouTube bure  ambayo itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Kulia ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.
 Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo. 

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Kampuni  inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania imetangaza upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za YouTube nyakati za usiku  kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu  kutoa huduma hiyo  kwenye mitandao ya kijamii  bila tozo hapa nchini.

Akitangaza tukio hilo jijini Dar es Salaam leo,  Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia  aliviambia vyombo vya habari kuwa  huduma ya kutiririsha  video za YouTube bure  itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. 

Tigo ina wateja  zaidi ya milioni 10. Ikiwa imezinduliwa Mei 2005, YouTube ni utiririshaji wa video  ambao uunatumiwa na wafuasi zaidi ya bilioni  1 duniani kote, takribani theluthi moja yake  wakiwa wanatumia intaneti. 

Huduma hiyo inawapa fursa ya kuangalia video za YouTube kwa muda wa saa nyingi yakiwawo pia mabilioni ya maoni.  Aidha inaruhusu mabilioni ya watu kugundua, kuangalia na kushirikiana  video ambazo awali zilibuniwa  na kubuni jukwaa na kuunganisha, kuhabarisha na kuvutia  wengine sehemu mbalimbali duniani.

“Kitu pekee kinachohitajika ili kuweza kupata data za bure katika kutiririsha  video za YouTube ni kuwa na aina ya simu itakachoweza data hizo. Tunaamini  huduma hii mpya itaendelea  kuonesha kujituma kwetu  kwenye kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na kuongoza  kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubinifu kwa wateja wetu,” alisema Zacharia.

Pamoja na utriririshaji huo watumiaji wa YouTube  pia wateja watakuwa na njia mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu ya simu  inayojulikana kama YouTube Offline  inayomwezesha mtumiaji  kuongeza video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadaye wakati ambapo muunganisho na itaneti  unakuwa haupo au upo chini.

Kwa video ambazo  pale ambapo  zinapatikana watumiaji wanaweza  kuchagua  kuongeza video kwa  kuzitiririsha  na kwa ajili ya kuangalia hapo baadaye  kwa kutumia  kitufe cha ‘offline’. 

Ikiwa  imeshachukuliwa kwa njia hiyo  video hiyo inaweza kuchezeshwa  bila kuunganishwa na intaneti kwa muda wa hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za YouTube  bila hofu ya maunganisho na intaneti kuwa yapo chini.

Zacharia aliongeza kwamba  kuzifikia data  bure kutakuwa  kunapatikana kwa wateja wa Tigo wa huduma ya malipo kabla  bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika  kuifurahia huduma hiyo. 

Upatikanaji bure wa data za huduma ya kutiririsha video za YouTube umefanyika baada ya kampuni hiyo ya simu  kutangaza huduma nyingine ya bure ya WhatsApps kwa wateja wake mwanzoni mwa mwaka huu ambako pia kulitamnguliwa na  kiuzinduliwa kwa huduma ya Facebook ya Kiswahili mwaka 2014.

Tigo inayofuraha  kujumuisha  majkuwaa ya video kwenye ofa hii. Kama wewe ni  msambazaji wa huduma ya video unaweza kuwasiliana nasi  kupitia customercare@tigo.co.tz

WANANCHI WA JIMBO LA HANDENI WAMLILIA WAZIRI WA MAJI

April 21, 2016

WAZIRI  wa maji  Mhandisi  Gerson Lwenge pichani )kushoto ameombwa  kuingilia kati  na  kushughulikia  kwa haraka  utata  uliogubika  utekelezaji  wa mradi  wa  Bwawa  la maji  la malezi  lilipo kata  ya Malezi ,Mjini Handeni  ambao  haujaanza  licha  ya Benk ya Dunia  kutoa shs. 740  kwa  ajili  ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo, wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji  katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni sababau ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo ambao  unatarajiwa  uwanufaishe Wakazi Zaidi  ya 6000. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880.
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha zilizoingizwa kaikamakauntinkuwa shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa nini mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.


(Pichani kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini,Omari Kigoda)
Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi ammepokea wataalamu ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizw kwenye mradi huo waache kulima.
“Tunapata lawama kwa wananchi kwa sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,” alisema.
 Naye Cecilia Ibrahimu wa Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu wote.
“Sina cha kusema nataka maji tu. Cha ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi. Cecilia.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah Kigoda.

Tigo wakabidhi madawati 400 kwa wilaya ya Mwanga katika shule 8

April 21, 2016







Inline image 2

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mwanga Theresia Msuya(katikati) Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.



Aprili 20 2016 Mwanga: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Lugata.

Lugata amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro  na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Kilimanjaro. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki

Madawati hayo yametolewa kwa shule za msingi  nane kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.



photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"