Mara Paaap! Tigo Fiesta TAMADUNIKA 2017 ndani ya Tabora

September 27, 2017

Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Hekima mkoani Tabora kikionesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye maonesho ya kucheza ngoma za utamaduni za Tigo Fiesta Tumekusoma ‘TAMADUNIKA’ kwenye viwanja vya Taasisi(sanamu ya Mwl.Nyerere) Tabora mapema jana.

Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Hekima mkoani Tabora kikionesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye maonesho ya kucheza ngoma za utamaduni za Tigo Fiesta Tumekusoma ‘TAMADUNIKA’ kwenye viwanja vya Taasisi(sanamu ya Mwl.Nyerere) Tabora mapema jana.


Mshehereshaji  wa Tigo Fiesta ‘TAMADUNIKA’  Mc Kicheko akifanya yake.



Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Mapambano mkoani Tabora kikionesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye maonesho ya kucheza ngoma za utamaduni za Tigo Fiesta Tumekusoma ‘TAMADUNIKA’ kwenye viwanja vya Taasisi(sanamu ya Mwl.Nyerere) Tabora leo.





A-Z YA MSHINDI WA SHINDA NYUMBA ALIVYOPATIKANA (VIDEO)

September 27, 2017
Diwani ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi. Mheshimiwa diwani akiwa kwenye rundo la kuponi Mheshimiwa diwani akichanganya kuponi. Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi. Mheshimiwa diwani akiwa ameiinua kuponi juu. Diwani Lema akisoma jina la mshindi wa nyumba, aliyemshikia kipaza sauti ni MC Chaku. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba. Meneja Mrisho akipeana mikono na Diwani Lema Diwani Lema akizungumza na watu waliofika kushuhudia droo hiyo.

PROF. MAGHEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA 87 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

September 27, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.
Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

NSSF ARUSHA KUWASHTAKI WAAJIRI 126 KWA KOSA LA KUTOWASILISHA MICHANGO YA WAAJIRIWA INAYOFIKIA SHILINGI BILIONI

September 27, 2017
Meneja kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha katikati  Dr. Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwapeleka waajiri 126 mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango ya waajiriwa inayofikia kiasi cha shilingi bilioni moja nukta tano kwa kipindi cha miezi sita sasa. 
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Jumla ya Kampuni 126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa NSSF mkoani Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo yamegawanyika kati ya waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi milioni 50  na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia milioni 5 hadi 49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi elfu ishirini  hadi milioni  4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.

“Waajiri wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za kimahakama zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017 mtawajua ni waajiri gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi gani wanadaiwa kila mmoja wao” alisema dokta Maduga

Amesema kuwa Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita, kitendo hicho kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi wao kwa kukosa huduma za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya wanachama taarifa zao za kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda ule ambao michango haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwa wafanyakazi husika.

Mwanachama ana haki ya kulipwa michango yake yote akiacha kazi au kampuni ikifa na kuacha kuendesha biashara hulazimika kulipa fedha zote za michango ya wanachama na wao kama taasisi inayosimamia haki za waajiriwa huhakikisha malipo yote yanalipwa na kutolea mfano kampuni za snowcrest na mukidoma zilizositisha shughuli zake na kutangaza kufilisika  walihakikisha kuwa kila mfanyakazi anapata mafao yake bila wasiwasi wowote.

Amesisitiza kuwa mwanachama akishaacha kazi atasubiri kwa kipindi cha miezi sita ndiyo aweze kupewa fao la kustaafu na kipindi hiki huwekwa ili kumpa nafasi mwanachama kuweza kutafuta kazi na ama kuajiriwa na kampuni nyingine na changamoto inayowakabili ni kuwa baadhi ya wanachama hufoji barua za kuacha kazi ili waweze kupewa mafao yao huku bado wanafantya kazi jambo ambalo halikubaliki kwa mwanachama kulipwa fao lake huku anafanya kazi.

Naye Straton Simon Afisa msimamizi wa fao la matibabu NSSF kanda ya kaskazini inayowakilisha mikoa ya ARUSHA,KILIMANJARO, TANGA na MANYARA amesema kuwa fao la matibabu hutolewa bure na mfuko huo kwa kila mwanachama anayekuwa amewekewa michango yake kwa miezi mitatu  na kuendelea na fao hili halihusiani na kukatwa akiba yako siku utakayostafu kazi au kampuni yako kusimama kufanya kazi hivyo amewataka wanachama wasiwe waoga kutumia fao hili kwani lina faida kwa mwanachama na wategemezi wake wane ambao ni mke au mume na watoto wane.

Amesema kwa Arusha pekee NSSF ina mkataba wa matibabu kwa wanchama wake na hospitali 34 zinazotibu wanachama wote wa hiari na wale waajiriwa ambao mpaka sasa wanafikia 18,400  na kwa kanda nzima ya kaskazini wanafikia wanachama 34000 wanaopata fao hilo la matibabu na kuwasihi wanachama wengine wote wahakikishe wanajaza fomu na kuchagua moja ya hospital ambayo ungependa kutibiwa kati ya hizo hospitali 34 ili wanufaike na fao hilo muhimu kwa maisha ya mwanachama.

DC MTATURU AKUBALI KUWA MLEZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA AMINIKA NA KUCHANGIA MILIONI 1

September 27, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu pamoja na viongozi wengine wakifatilia taarifa ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya wachimbaji wadogo wadogo ya AMINIKA Ndg Hamisi A. Nkingi akisoma taarifa ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi hiyo kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekubali ombi la viongozi wa Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA la kuwa mlezi wao Sambamba na kuchangia Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kusaidia Kupunguza ukali wa changamoto zinazowakabili.

Chama hicho Cha USHIRIKA wa wachimbaji wadogo (AMINIKA GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) chenye jumla ya wanachama 193 Ni muungano wa vikundi vitano vya Uchimbaji mdogo wa Madini ya dhahabu vinavyotokana na vikundi vya Elimika-Sambaru, Amka-Sambaru, Amani-Sambaru, Aminifu-Mang'onyi na Muungano-Mlumbi.

Akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya AMINIKA Mhe Mtaturu alimuagiza Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha E. Msemo kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu mwenendo wa Chama hicho.

Alisema kuwa Uongozi wa Wilaya unatambua umuhimu wa Chama hicho kutokana na umahiri wake na muelekeo wa kuwakomboa wachimbaji wadodo katika Wilaya ya Ikungi.

Alisema ili Chama hicho kuwa na Ushirika mzuri na mafanikio makubwa Ni vyema viongozi watakaochaguliwa kutanguliza maslahi ya wananchi mbele kwa kusoma taarifa kwa uwazi na ukweli.

Mhe Mtaturu alisema mafanikio ya Chama Cha Ushirika Cha AMINIKA Ni pamoja na kuchagua viongozi Bora watakaokuwa na mikakati makini kea ajili ya kukikomboa Chama na kuwa na mbinu zenye manufaa kwa ustawi wa Chama.

"Wapo watu wanaodhani kuwa kuzaliwa kwenye eneo la Madini Basi inakufanya kuwa mtaalamu wa Madini, nataka niwaeleze kuwa Madini yanataka utaalamu, mtaji na teknolojia hivyo sisi Kama serikali tunawahakikishia kuwa tutashirikiana nanyi bega kwa bega" Alisema Mtaturu

Aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli anawathamini wachimbaji wadogo endapo watakuwa na mipango Bora ya maendeleo katika uchimbaji.

Akizungumza kwa niaba ya mwanachama menzake wa Chama hicho Cha Ushirika Cha wachimbaji wadogo wadogo Bi Elizabeth Shango alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwa kukubali ombi la kuwa mlezi wa Chama hicho Cha Ushirika ambapo alipongeza pia namna ambavyo Dc Mtaturu Ameanza malezi ya Chama hicho kwa kuchangia Shilingi Milioni Moja.

Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi ya Chama hicho Cha USHIRIKA Cha wachimbaji wadogo (AMINIKA GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) kinafanya uchaguzi wa awamu ya Pili kwa kipindi Cha miaka mitatu 2017/2020 mara Baada ya Uongozi uliopo madaraka kumaliza muda wake kwa kipindi Cha awamu ya kwanza Mwaka 2014/2017.