TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO DAR

May 28, 2015

 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Viongozi hao wakipongezana baada ya makabidhiano ya kisima hicho
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Kilindo akielezea mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya maji kutokana na faida ya mauzo ya vinywaji vyao.
 Herman Mkwizu ambaye Kampuni yake ya Winners inajishughulisha na uboreshaji wa miundombinu ya maji akielezea jinsi watakavyoendelea kuusimamia mradi huo wa maji.
 Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni akishukuru kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada wa kisima hicho kutoka TBL.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mshana akiishukuru  TBL kwa msaada huo wa kisima ambao ni muhimu mno hasa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa shule hiyo waliokuwa wakiteseka kutafuta maji.
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu  akizungmza wakati wa hafla hiyo
 Wanafunzi wakifurahia kukabidhiwa mradi huo
 Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Abisina Rashid (kulia) na Rozalia Polycarp (wa pili kulia), wakishiriki katika uzinduzi wa kisima cha maji kwa kufungua maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima hicho kwa shule hiyo Dar es Salaam jana. Kisima hicho kitakachohudumia pia Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ujenzi wake ulisimamiwa na Kampuni ya Winners. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho, Balozi mstaafu,Herman Mkwizu, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto),Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Zarina Kigoma baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana.Anayeshangilia kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.Kisima hicho kitakuwa kinahudumia pia Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akinywa maji ya bomba baada ya kukabidhi msaada wa kisima kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni na Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho.
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa kuona akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu kwao.
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YASAINI MKATABA WA KUBORESHA HUDUMA ZA UFUNDI WA VIFAA TIBA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YASAINI MKATABA WA KUBORESHA HUDUMA ZA UFUNDI WA VIFAA TIBA

May 28, 2015

af1

Dkt. Mmbando akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba huo  toka serikali ya korea ya kusini katika kutoa mafunzo kwa mafundi wa vifaa na vifaa tiba walioajiriwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya hapa nchini ili waweze kuongeza ujuzi katika matengenezo na kuboresha huduma ya ufundi.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowele
af2
Katibu mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na naibu meneja toka KOFIH wakisaini mkataba huo. Mkataba huo  utasaidia pia  kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba katika karakana za ufundi wa vifaa tiba zilizopo katika hospitali za rufaa za kanda, rufaa za mikoa na hospitali za wilaya.
af3
Dkt. Mmbado akikabidhiwa mkataba huo toka kwa Naibu Meneja Gong, In Jae .
…………………………………………………………..
Dkt. Mmbando amesema ,  serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya imeendelea kuboresha upatikanaji na uwepo wa huduma ya vifaa tiba na mashine mbalimbali za teknolojia za kisasa katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia zahanati hadi hospitali ya Taifa. Ili kusimamia matumizi bora na kutunza raslimali hii kumehitajika kuweka juhudi za maksudi kuandaa wataalam wa ufundi wa vifaa tiba kwa kuwajengea uwezo katika kufahamu wa namna ya matengenezo ya mashine zilizopo na zinazo endelea kununuliwa; Pia kuwapa  vitendea kazi(tools kits, measuring and calibration equipment) vyenye kuwezesha mafundi kuhakiki ubora wa ufanyaji kazi kwa baadhi ya vifaa tiba mara baada ya kufanyiwa matengenezo.
“Kwa ushirikiano huu kati yetu na Korea ya Kusini ikiwa ni nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na teknolojia au miundombinu kwa ujumla wake ninaimani tutajifunza mambo mengi na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini”.
Alisema kikubwa wamelenga kupata ujuzi zaidi kutoka kwao ingawa watagharimia masuala mengi katika mchakato mzima. Tunahitaji sisi wenyewe serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Manispaa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za Afya vinapatikana na vinatumika kutoa huduma kwa wagonjwa muda wote vinapohitajika.|” Hili litawezekana kama tutatenga bajeti za matengenezo kinga(Planned Preventive maintenance) na kutumia wataalam wa ufundi wa vifaa tiba wanaotambulika “.
Mzee mwenye umri wa miaka 75 ashikiliwa na polisi kwa tuhumza na bangi Pemba

Mzee mwenye umri wa miaka 75 ashikiliwa na polisi kwa tuhumza na bangi Pemba

May 28, 2015

downloadNa Masanja Mabula -Pemba 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 75 akikabiliwa na tuhuma ya kupatikana na majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja mzee huyo kuwa ni Hamad Hamad Bakar Mkaazi wa Mchangamdogo Wilaya ya Wete .
Amesema kuwa mzee huyo amepatikana akiwa na nyongo 75 na mafurushi mawili ya majani makavu yanayo sadikiwa kuwa ni bangi baada ya kufanyiwa upekuzi ndani ya nyumba yake .
Ameeleza kwamba tukio hilo limetokea juzi  na kuongeza kuwa walipokea taarifa juu ya uwepo kwa bangi katika nyumba ya mzee huyo kutoka kwa Polisi Jamii ambao waliambatana nao kufanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo .
Aidha Kamanda Shekhan amesema kuwa jeshi hilo kwa sasa linaendelea kumhoji mzee huyo na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamlika kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili .
“Ni kweli kwamba jeshi la Polisi linamshikilia mzee Hamad Hamad Bakar baada ya kukamatwa akiwa na nyongo 75 pamoja na mafurushi mawili ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi na tutamfikisha mahakamani upelelezi utakapo kamilika ” alifahamisha Kamanda .
 Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi polisi Jamii katika Shehia hiyo wamesema kuwa bado vyombo vya sheria ikiwemo Mahakama hazijakuwa tayari kushirikiana na polisi kwani mzee huyo ameshakamatwa mara nyingi lakini kesi zake hazipatiwa hukumu stahili
Wamesema kuwa mzee huyo anaugonjwa wa Ukoma  ni mzoefu wa biashara hiyo na kwamba amewahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani zaidi ya mara moja lakini hakuna adhabu iliyochukuliwa dhidi yake .
“Hatuwezi kufanikisha udhibiti na utumiaji wa dawa za kulevya iwapo watuhumiwa wanashindwa kuchukuliwa hatua kwani huyu mzee si mara ya kwanza kukamatwa na bangi lakini hakuna adhabu iliochukuliwa dhidi yake ” alifahamisha Kiongozi wa Polisi Jamii .
Hivyo wameviomba vyombo vya sheria kuhakikisha kwamba wanachukua hatua inayostahili ili kukomesha biashara hii haramu ya madawa ya kulevya kwa lengo la kuwalinda vijana dhidi ya majanga mbali mbali .

WAZIRI KOMBANI AIPA SOMO MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI.

May 28, 2015


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ( kati kati) akisisitiza jambo.
 Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe ( kushoto ) akiwa na mwezeshaji wa mafunzi, Patrick Ngwila.
Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kuelekeza nguvu zao vijijini kwenye idadi kubwa ya  wananchi na wazalishaji wa mali wanaohitaji huduma zao badala ya kung’ang’ania mijini pekee.
Kombani alitoa changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku nne yaliyoanza Mei 25 hadi kufikia 28, 2015 mjini Morogoro ya  kuwajengea uwezo na ufahamu wafanyakazi wanaunda Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) kutoka katika mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PPF,NSSF,LAPF,GEPF,NHIF na ZSSF.
Hata hivyo alisema,  mifuko hiyo imekuwa ikikimbilia kutafuta wanachama katika maeneo ya mijini na kushindwa kubuni mbinu mbadala za kuwafikia wananchi wengi wanaoishi vijijini.
Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa, dhana iliyojengeka kutoka kwa Mifuko hiyo kuwa vijijini hakuna watu wenye vipato sasa imepitwa na wakati kwa kuwa wananchi wanaishi vijijini  ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara ndogo ndogo ambao  wanaouwezo mkubwa wa kuchangia mifuko hiyo.
Waziri Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki(CCM) alisema , kutokana na mifuko hiyo kujikita katika maeneo ya mjini imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa asilimia 4 na endapo itajitoa kuwafikia  watu wa maeneo ya vijijini inaweza kutoka hapo ilipo na kufikia asilimia 10 na zaidi.
“ Wilaya ya Ulanga pekee kuwa kuna kundi kubwa la wakulima,wafugaji na waendesha bodaboda” alisema na kuongeza kusema.
“ Mfano mfuko wa bima ya afya wao wamejitoa kwenda  kuhamasisha na wananchi wengi wameweza kujiunga na kuchangia huduma za matibabu na sasa  mifuko mingine ya hifadhi ya jamii inafaa  kufuata nyayo hizo za kubuni  mbinu mpya za kwenda maeneo ya vijijini kupata wanachama wengi” alisema Waziri Kombani.
Awali , Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshack Bandawe, alisema  malengo ya kuanzisha Jumuiya hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja.
Hata hivyo alisisitiza kuwa lengo moja ili kuhakikisha sekta ya Hifadhi ya jamii inaimarishwa ili kuingiza Watanzania katika mifuko hiyo ili waweze kunufaika nayo katika maisha yao.
“ Tunayo mifuko saba ya Hifadhi ya Jamii na imewafikia watu asilimia 4.5 ...lengo ni kutoka hapo angalao kufikia wastani wa asilimia 10 “ alisema Bandawe.
Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa alisema, kupitia Jumuiya hiyo sasa wataanza kuwaelimisha wananchi wote walioko rasmi katika soko ajira na wale wasio rasmi waweze kukingwa na mifuko ya hifadhi ya jamii .
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, Patrick Ngwila,alisema kwa sasa  wanaangalia namna ya kuiboresha mifuko hiyo kwa kupata uzoefu wa namna ya mifuko hiyo inavyofanya kazi katika nchi hizo ambayo imekuwa ikisaidia wananchi hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini.
Kwa mujibu wa Mwezeshaji huyo kuwa,  kupitia mafunzo hayo wanaangalia namna ya kupata wanachama ambao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza  kuchangia kwenye mifuko hiyo wakiwa huko na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.

Diamond Platinumz aibukia programu ya Mziiki

May 28, 2015


Nyota wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia kama vile Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ili ziweze kuwafikia watu wengi na kwa wakati huohuo wanamuziki pia kunufaika na jasho lao.

Diamond anasema kuwa  ameamua kazi zake kuziingiza sokoni tofauti na kazi zake za nyuma ambapo baada ya  kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ameamua aingie sokoni kwa njia ya kidigitali kupitia programu ya Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza.

Anasema Tanzania ina wanamuziki wengi wenye vipaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wasifike mbali zaidi ya muziki wao kusikika hapa nchini na wengi wao kutamba kwa muda mfupi na kupotea katika ulimwengu wa muziki huku wakiwa hawajanufaika na kitu chochote kimaisha na kushauri kuwa  wasibaki nyuma kiteknolojia hasa wakati wa kupeleka kazi zao sokoni iwapo watataka kujikwamua.

“Licha ya kuwepo na changamoto kubwa kama vile kutokuwepo sheria ya hakimiliki inayopelekea wasanii kuibiwa kazi zao na kazi za muziki kutumiwa na vyombo vya habari kama redio na televisheni  bila kuwalipa wahusika chochote. Tatizo lingine linalodumaza muziki wa Tanzania ni uoga wa wanamuziki kubadilika na  kuogopa teknolojia za kisasa kama  hii programu ya kupakua muziki kwenye simu kwa kupitia Mziiki” Alisema.

 Amesema  sababu kubwa iliyopelekea kuamua kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia washabiki wake popote na muda wowote kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato tofauti na kama zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani.

“Duniani kwa sasa hivi kuna ushindani  mkali katika nyanja zote. Sisi kama wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu na kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ndani na ya nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii kama ilivyo program hii ya Mziiki. Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa” anasema Diamond Platinumz

Aliwaomba wapenzi wa muziki nchini kuwaunga mkono wanamuziki wa hapa nchini kwa kupakua nyimbo zao kwenye Mziiki  kwa kuwa njia hii iko wazi na inamuwezesha mwanamuziki kujua kirahisi  jinsi kazi zake zinavyokubalika sokoni na inamuwezesha kujua mapato yake tofauti na njia nyingine kama uuzaji wa CD kwenye maduka na mitaani.

Programu ya Mziiki ambayo ilizinduliwa na Vodacom kwa kushirikiana na  Spice VAS Africa  imeanza kufanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini na nje ya nchi na katika  kipindi cha muda mfupi tayari imesajili wanamuziki wapatao 1,000  ambao kazi zao  hususani zile mpya zitasambazwa kwa njia ya kidigitali na malengo yake makubwa ni kuhakikisha wanamuziki wanapeleka kazi zao sokoni kwa haraka na kunufaika na jasho lao hususan pale ambapo wananchi wengi watatumia mtandao kwenye simu zao kupakua nyimbo wazipendazo za wanamuziki ambao wamejiunga kwenye tovuti ya kampuni hiyo ambayo inapatikana kwa kubofya tovuti ya www.mziiki.com.

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AFUNGA MKUTANO WA MABALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JIJINI DAR

May 28, 2015

Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini Dar es Salaam.Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ. 
---
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa tofauti Duniani wanapaswa kuitekeleza vilivyo Sera ya Mambo ya Nje inayolenga katika Diplomasia ya uchumi ambayo ndiyo muongozo wao katika utekelezaji wa jukumu lao la msingi.
Alisema Sera hiyo ni vyema ikatumika vizuri wakati huu ambao Taifa la Tanzania linatekeleza Dira ya kuelekea uchumi wa Kati na kati ifikapo mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar na Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara.
Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.
Alisema katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye kuweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania imepiga hatua kubwa vikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
Dr. Shein alifahamisha kwamba matunda ya Sera hii yanadhihirisha wazi ukuaji wa sekta ya Utalii, miradi mengine ya kiuchumi ikiwemo pia ile mikubwa inayotekelezwa na wahisani kwa upande wa Zanzibar.
“ Mikakati mipya ya muda mfupi na mrefu mliowekeana katika Mkutano huu ni msingi mzuri kabisa kufuatana na mabadiliko ya uchumi yanayotokea Duniani na kufikia malengo ya Dira ya 2020 na 2025 “. Alisema Dr. Shein.
“ Nina hakika kuwa katika Mkutano huu mmeweza kuziba nyufa zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi ambayo ndio muongozo wetu katika utekelezaji wake na ni jukumu letu la msingi “. Alisisitiza Dr. Shein.
Rais wa Zanzibar alieleza kwamba licha ya mafanikio makubwa ya kiuchumi na maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa kwa upande wa Zanzibar lakini bado iko haja kwa Mabalozi hao wa Tanzania kuongeza juhudi za kuitangaza Zanzibar katika Mataifa waliyopangiwa kutekeleza majukumu yao ya Kidiplomasia.
Alisema mafanikio ya Zanzibar katika kukuza sekta ya Utalii , uwekezaji na utekelezaji wa mipango mengine ya maendeleo hutegemea sana juhudi za Ofisi za Kibalozi katika kuitangaza Zanzibar nchi za Nje.
Dr. Shein alifahamisha kwamba baadhi ya wakati Serikali imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wawekezaji, watalii na wageni wanaofika Zanzibar juu ya ukosefu wa taarifa za kutosha kuhusu Zanzibar katika Ofisi za Kibalozi za Tanzania.
Aliwakumbusha Mabalozi hao kwamba katika kutekeleza majukumu yao ni vyema kila wakati wakazingatia kuwa Ofisi zao zinaweka taarifa za kutosha juu ya sekta zote muhimu za kiuchumi na kijamii za pande zote mbili za Jamuhuri hasa zile fursa za uwekezaji vivutio vya utalii.
“ Suala hili nimekuwa nikilikumbusha kila ninapopata fursa ya kuzungumza nanyi, hasa wakatia mbao Mabalozi huja kunitembelea na kuniaga kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi “. Alifafanua Dr. Shein.
Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kupokea mawazo ya Mabalozi hao ili kupata fursa nzuri ya nini Wanadipomasia hao wakitangaze kuhusu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alihimiza kwamba katika kipindi hichi ambapo Nchi mbali mbali Duniani zimekumbwa na misukosuko ya kutetereka kwa hali ya amani na utulivu Mbalozi hao wanapaswa kuzitangaza fursa ya kiuchumi zilizopo Nchini na kuzihusisha na hali ya amani na utulivu uliopo Nchini Tanzania.
Alieleza kuwa amani na utulivu ni miongoni mwa vigezo muhimu vya awali vinavyozingatiwa na wawekezaji pamoja na wageni wanaotaka kwenda nje ya nchi zao kwa nia ya kuwekeza na kufanya biashara.
Mapema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Bernard Membe alisema utekelezaji wa sera ya mambo ya nje inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi umeleta faida kubwa katika uchumi wa Taifa ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Waziri Membe alisema ipo miradi kadhaa ya kiuchumi iliyotokana na sera hiyo kufuatiwa kutanganzwa na Ofisi za Kibalozi za Tanzania akiitaja kuwa ni pamoja na misaada ya maendeleo iliyofadhiliwa na mpango wa Milenia wa Marekani MCC na mradi wa chuma wa Mchuchuma.
Mh. Membe alisisitiza pia kuwa ipo miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Tanzania kusamehewa mikopo tofauti kutoka kwa baadhi ya wafadhili, mradi wa huduma za maji safi unafadhiiwa na Serikali ya Japan pamoja na mradi wa Kilimo kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar.
Alisisitiza kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya nje itahakikisha kwamba inaendelea kuchangia vikosi vya kulinda amani Barani Afrika.
Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania Nchi Mbali mbali Duniani Dini wa Mabalozi hao Balozi Kijazi alisema Maalozi hao wakirudi vituoni mwao watakuwa na kazi moja tu ya kutekeleza yale waliyoyajadili na kukuibaliana katika Mkutano huo.
Balozi Kijazi alilihakikishia Taifa kwamba Mabalozi hao wana nia safi ya kutekeleza majukumu yao kwa ufasini uliotukuka, lakini lakuzingatia zaidi ni uwezeshwaji wao ili kutekeleza vyema kazi yao hiyo ya Kidiplomasia.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA

TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA

May 28, 2015
DSC_0009
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Kigoma
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Tanzania itatoa nafasi zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka wakimbizi wa Burundi wanaoingia nchini katika mazingira ya kuishi maisha ya kawaida.
Kauli hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali ilivyo akiambatana na watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini.
Alisema kama taifa wameona uwingi wa Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili kuwezesha Wakimbizi hao kupata mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi.
Alisema katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi wanaomiminika kwa sasa serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.
“Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa kama wananchi wa Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi zaidi na tunashukuru msaada tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo hili …,” alisema.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa unatiwa shaka na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema kuyumba kwa hali ya kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.
Alisema kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini Burundi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.
Rodriguez alisema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa unaangalia hali inayojitokeza Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania isilemewe na Wakimbizi.
Aidha alisema kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kutoa nafasi zaidi ya kuwezesha kusiwepo na msongamano wa Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha ushirika wa kweli kati ya serikali ya Tanzania na jumuiya ya Kimataifa katika kushughulikia matatizo ya Wakimbizi.
Alisema hata hivyo kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya.
Aidha alisema kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika moja, chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia wanavyostahili pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo.
DSC_0014
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akisamiana na Waziri wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui (kulia) pamoja na viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
Changamnoto hizo ni pamoja na uwingi wa Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali uliopo wa kambi ya Kagunga ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi wakiwa wanawake na watoto.
Alisema hata hivyo UNHCR walifanikiwa kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa mazingira ya ukazi wao katika kambi ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga hadi Kigoma.
Pia alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo jirani ambako Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo walivyotakiwa kuwepo.
Pia UNICEF waliweza kusaidia maji na vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao walihakikisha chakula kinafikishwa hasa biskuti za kuongeza nguvu.
Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu.
Aidha UNFPA walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Mratibu huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa kama si kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Mratibu huyo alisema kuwa Mashriika ya Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha za kusaidia katika shughuli zao na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani milioni 12.
Alisema kwamba Umoja wa Mataifa umeona kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao kumeleta hali ngumu kwa serikali ya Tanzania na wakazi wa Kigoma.
Alisema wanatambua changamoto zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la Wakimbizi lakini wataendelea kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika kipindi hiki kigumu.
DSC_0016
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma.
DSC_0019
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada ya kuwasili akiwa amefuatana na Waziri Chikawe (hayupo pichani).
DSC_0018
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma mara tu baada ya kuwasili.
DSC_0024
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia) mara tu baada ya kuwasili mjini Kigoma tayari kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
DSC_0027
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akifafanua jambo kwa viongozi wenzake mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux.
DSC_0036
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea chumba maalum cha mapumziko mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma.
DSC_0049
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko.
DSC_0071
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi mkoani Kigoma.
DSC_0099
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Kigoma.
DSC_0113
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
DSC_0128
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
DSC_0134
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
DSC_0146
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
DSC_0163
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.
YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN LEO

YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN LEO

May 28, 2015


KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
 
Wasanii wa yamoto band.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’.
Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.