Katikati
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina,
Mbele yake ni Bw. George Mratibu wa Kiwanda cha Ngozi Morogoro , cha ACE LATHER
TANZANIA LTD, wakiwa katika ukaguzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka
kiwandani hapo ambapo Mpina yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya ukaguzi wa
utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake, kufuatia maagizo aliyoatoa
awali katika ziara ya viwanda hivyo.
Naibu Waziri Mpina akikagua mabwawa hayo kama inayoonekana |
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, Luhaga Mpina Amekipongeza kiwanda cha nguo cha 21st century
na kiwanda cha ngozi cha ACE LEATHER TANZANIA LTD kwa kutekeleza sheria
ya mazingira kwa kujenga mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka
katika viwanda hivyo.
Akiwa katika Ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa Sheria ya mazingira Mkoani Morogoro leo, Mpina aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC pamoja na Bonde la Wami Ruvu, kuchukua Sampuli za maji hayo yanayotibiwa katika viwanda hivyo kwa ajili ya vipimo ili kujiridhisha kuwa hayana madhara kwa mazingira na viumbe hai wengine.
Katika ziara hiyo Mpina, Aliagiza NEMC kumuandikia Barua msajili wa hazina ili kujua ukweli wa mmiliki halali wa mabwawa ya majitaka yaliyotelekezwa katika maeneo ya kilimahewa, ili mmiliki halali wa mabwawa hayo kama ni mamlaka ya majitaka iweze kuyahudumia kwa kuyajengea miundombinu ya kisasa na kuyatibu ili kunususu mazingira, awali ilielezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuwa wakati wa msimu wa mvua maji hayo yamekuwa ni kero kwa wakazi hao kwa kutoa harufu kali.
Naibu Waziri Mpina anaendela na ziara yake ya ukaguzi wa mazingira na utekelezaaji wa shieria ya mazingira mkoani Morogoro.