SIKU ZA WANAOAGIZA NYAMA MAZIWA NA SAMAKI KUTOKA NJE YA NCHI ZINAHESABIKA - ULEGA

SIKU ZA WANAOAGIZA NYAMA MAZIWA NA SAMAKI KUTOKA NJE YA NCHI ZINAHESABIKA - ULEGA

March 20, 2018

picha no 2
Kushoto Dkt. Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma akimuonyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega katikati, kizimba cha kufugia samaki kilichopo katika maji ya ziwa Tanganyika hakipo pichani, alipotembelea kituo hicho mjini kigoma jana. Kulia ni Afisa Mifugo wa Mkoa Bw. Noel Byamungu.
Picha no 3
Aliyesimama ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, akiongea na watumishi wa kituo cha  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, pamoja na watafiti hawapo pichani, alipotembelea kituo hicho, kulia ni Dkt Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, na kushoto ni  Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo katika chuo cha mafunzo ya uvuvi FETA Kigoma, Bw. Simtie Ambakisye, Naibu Waziri Ulega alifanya ziara katika kituo cha TAFIRI Kigoma pamoja na kutembelea mialo ya Muyobozi na Kibiri.
Picha no 1
Kulia Dkt. Emmanuel Sweke Kaimu Mkurugenzi wa kituo wa kituo cha  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega aliyekaa katikati  wakiwa katika boat wakielekea kuangalia kizimba cha kufugia samaki katika maji ya ziwa Tanganyika, kushoto ni Afisa Mifugo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Noel Byamungu.
……………….
KIGOMA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifigo ya kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa kama Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza mazao hayo ya mifugo na uvuvi kutoka nje ya nchi.
Naibu waziri Ulega aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa Samaki wa Muyobozi Uliyopo Wilayani Uvinza,Mwalo wa Kibirizi na kituo cha Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.
“Sioni kwanini tuagize nyama na maziwa  toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama, maziwa na hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za ndani  katika mifugo na samaki na kuongeza pato la taifa? “Aliuliza Ulega.
Ulega  aliongeza kwa kusema kuwa Wizara yake haitawavumilia  waafanyabiashara wanaoagiza nyama, maziwa na mazao ya samaki  toka nje ya nchi kwani sekya ya mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.
Tarkibani “tani elfu 20 za samaki zinaingizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka, samaki ambao wanafugwa katika maeneo mengine duniani, lakini sisi hapa nchini tunao katika mazingira ya asili.” Alisema
Na hapa Mhe. Ulega aliitaka TAFIRI kuhakikisha wanawafikia wafugaji wa samaki kwa kufanya tafiti zao ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kujua namna ya kuzitatua, akitolea mfano wa chakula sahihi kinachotakiwa kupewa masamki wanaofugwa na kuangalia miundombinu ya kufugia.
Akizungumzia suala la zana za uvuvi katika ziwa Tanganyika alipokuwa akiongea na watafiti na watumishi wa TAFIRI, Ulega alisema “TAFIRI mfanye tafiti ya aina ya nyavu zinazotumiwa kwa kiasi kikubwa na wavuvi  ili kuona kama zinafaa kuendelea kutumika, maana kumekuwa na malalamiko toka kwa wavuvi yanayopelekea kushuka kwa kiwango cha upatikanaji wa samaki na dagaa katika ziwa hili kutokana na matumizi ya nyavu hizo.” Alisema
Sambamba na hilo Ulega alisema Wizara yake ina mpango wa kuimarisha eneo la tafiti kwa kuongeza rasilimali fedha kwa kukarabati miundombinu na kuongeza rasilimali watu.
“Kila Mwaka TAFIRI itakuwa inafanya tafiti kuhusu mambo ambayo Wizara itakuwa imeyaelekeza ili kuondokana na suala la watafiti hawa kufanya kazi za watu wengine.” Alisema
Akizungumzia swala la mafanikio ya soko la nyama la nje ya nchi, Ulega alisema, “Hatuwezi kusafirisha nyama nje ya nchi kama mkakati wetu wa chanjo ya mifugo hauko sawa, lazima tuwe na mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo, soko la kimataifa linaangalia sana swala hili, Sisi kama Wizara tunaenda kusema kuwa kwa yoyote anayetaka kufuga swala la chanjo ni lazima.” Alisisiza Ulega.
Ulega aliendelea kusema kuwa ni lazima wizara kutengeneza mikakati ambayo itamfanya mfugaji asitaabike wazo wambalo amesema kama litaridhiwa litafanyiwa kazi.
“kuna watu wanaona mifugo ni balaa, mifugo siyo balaa mifugo na neema.” Alisisitiza.
Aidha Ulega alisisitiza suala la uwekezaji kwa ufugaji wa samaki kama njia ya kusaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uvuvi haramu wa samaki katika maeneo mbalimbali nchini, huku akipongeza jitihada za taasisi ya utafiti wa samaki TAFIRI kushirikiana na wananchi na kuonesha mfano wa namna ya ufugaji bora wa samaki unaowaonesha wafugaji wa samaki kuitumia ili kufikia malengo waliyokusudia.
Naibu Waziri Ulega pia alisema Serikali imepanga kuongeza makusanyo katika sekta ya mifugo kutoka bilioni kumi na sita hadi bilioni hamsini baada ya kuifanya mifugo ya ndani kuwa bora na kuwa ya kiushindani katika soko la kimataifa, hivyo suala la chanjo litakuwa la lazima.

WANAFUNZI MVOMERO WATAKIWA KUJIKITA ZAIDI KATIKA MASOMO YA SAYANSI ILI WAWE WATAFITI

March 20, 2018


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Milama, iliyopo mkoani Morogoro baada ya kukabidhi mbegu bora ya mahindi ya Wema 2109 kwa ajili ya shamba darasa. Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani humo leo.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli  (katikati) mbegu ya Wema 2109 kwa ajili ya kuwakabidhi wakulima wa wilaya yake ili waanzishe mashamba darasa. Wengine kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mvomero, Hilali Focus Riddy, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mvomero, Daina Muywanga na kulia ni Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Mvomero wakiandaa shamba kwa ajili ya kupanda mbegu ya Wema katika shamba darasa.
 Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakikabidhiwa mbegu hiyo ya Wema.
 Mkulima Yacob Patrick, akikabidhiwa mbegu hiyo.
 Mkulima Mohamed Maungo, akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima Tatu Mbonde, akikabidhiwa mbegu.
 Walimu wa Shule ya Msingi Mvomero wakikabidhiwa mbegu.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero.
 Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu ambao ndio waliofanya utafiti wa mbegu hiyo, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
 Uzinduzi wa shamba darasa katika shule ya msingi Mvomero.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero wakiwa katika upandaji wa mbegu hizo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli akizindua shamba darasa kwa kupanda mbegu hiyo ya Wema 2109



 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utalli, akizungumza na wakulima wanaounda kikundi cha Tupendane kilichopo Kijiji cha Didamba.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Kijiji cha Didamba,  Mwanahamisi Omari (kushoto), akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima  Maulid Adamu kutoka Kikundi cha Kazibanza kilichopo Kijiji cha Milama akikabidhiwa mbegu.

Na Dotto Mwaibale, Mvomero-Morogoro.

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi ya Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi ili waweze kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti.

Mwito huo umetolewa wilayani humo leo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi ya Wema E2109 inayostahimili ukame iliyotolewa na COSTECH kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

"Ninyi wanafunzi nawaomba someni sana masomo ya sayansi ili hapo baadae muweze kuwa watafiti wa masuala mbalimbali jambo litakalosaidia taifa" alisema Hussein.

Alisema tafiti zozote zinafanywa na wataalamu waliobobea katika masomo sayansi hivyo aliwataka wanafunzi hao kujifunza kwa bidii masomo hayo ya sayansi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mohamed Utalli aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kupeleka mradi huo katika wilaya yake ambapo amewataka wananchi kuzichangamkia mbegu hizo.

"Tuna bahati sana katika mkoa wetu kwani katika mikoa tisa ambayo mradi huo utafanyika na sisi tupo hivyo ni fursa kwetu tusiiache ikapotea bure" alisema Utalli.

Utalli aliwataka wakulima wilayani humo ulimopita mradira huo kuhakikisha wanayatunza mashamba hayo ili kuleta tija katika zao la mahindi.

Alisema mradi huo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kufanya kazi kwa bidii wakati taifa likiingia katika uchumi wa kati wa viwanda.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel  alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.






MNEC MWAKA RAMADHAN AMEVUNA WANACHAMA WAPYA (80) KATA YA MKWAWA MANISPAA YA IRINGA

March 20, 2018
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiongea na wanawake waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza kwenye ziara ya UWT taifa mkoani Iringa katika Kata ya Mkwawa
Baadhi ya wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT katika kata ya Mkwawa wakatika wa ziara ya viongozi wa kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa katika kitendo cha kula kiapo pamoja na wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT kata ya Mkwawa
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo Pamoja katibu wa UWT manispaa ya Iringa


Na Fredy Mgunda,Iringa

MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan amevuna wanachama wapya zaidi ya themanini (80) katika kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.

Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo MNEC Ramadhan alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa kata ya Mkwawa ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa MNEC huyo.

Ramadhan alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia  mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.

“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisema Ramadhan

Aidha Ramadhan aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.

“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisema Ramadhan

Ramadhan alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.

“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Ramadhan

Ramadhan alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.

“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Ramadhan

Kwa upande wake mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.

“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Kabati

WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DC NA JUMUIYA MPYA 2018

March 20, 2018
Siku ya Jumapili March 18, katika ukumbi wa Mount rainier, Maryland, Team Libe walifanikisha azama juu ya mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Jumuiya Mpya ya Watanzania waishio DMV utakaofanyika siku ya Jumapili March 24, 2018

MAWAKALA WA TIGO PESA NCHI NZIMA WAENDELEA KUJISHINDIA ZAWADI

March 20, 2018
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo ,Kanda ya Kaskazin,Henry Kinabo akimkabidhi wakala wa Tigo Moshi mjini ,Hassan ,mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Mbili kwa kuibuka mshindi wa pili wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini. Promosheni hii inawahusu Mawakala zaidi ya 73000 wa Tigo Pesa nchi nzima huku zawadi za Shilingi za kitanzania Milioni 144 zikishindaniwa. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo ,Kanda ya Kaskazin,Henry Kinabo akimkabidhi wakala wa Tigo wilaya ya Same Real Stationary ,mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni tatu  kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini. Promosheni hii inawahusu Mawakala zaidi ya 73000 wa Tigo Pesa nchi nzima huku zawadi za Shilingi za kitanzania Milioni 144 
zikishindaniwa. 


Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni ,mbili kwa Juliana Shilatu aliyeibuka kama wakala wa pili bora wa kanda ya Ziwa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa. Zawadi zenye thamani ya TZS 88 milioni zimetolewa na Tigo pesa kwa mawakala wake 73,000 nchini kote walioshiriki katika promosheni hiyo.

Meneja wa Tigo Mkoa Iringa Davis Kisamo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi millioni 3/- kwa wakala wa Tigo Pesa, Gibson Chaula wa Songea mwishoni mwa wiki mkoani Iringa.

Meneja wa Tigo Mkoa Iringa Davis Kisamo (kushoto) na Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa Iringa, Samuel Chanay (kulia) wakimkabidhi mfano wa hundi wakala wa Tigo pesa Asha Ramadhani aliyeshindia zawadi ya shilingi millioni 2/-  kwenye hafla iliyofanyika mkoani Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.


MBEGU BORA YA MAHINDI YA WEMA 2109 KUWAONGEZEA TIJA WAKULIMA CHALINZE

March 20, 2018

Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein Rajab (kulia), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata ya Msoga mkoani Pwani. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani Kapilima George. Mbegu hiyo imetolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).

Mkulima wa  kutoka Kikundi cha Gezaulole kilichopo Msoga, Shabani Mbogo akielezea changamoto za kilimo katika eneo hilo.
Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la Kikundi cha Gezaulole katika Kata ya Msoga.

 Mkulima Ally Mhenga akichangia jambo kuhusu changamoto za kilimo zinazowakabili.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein akiangalia mbegu ya Wema.
 Mkulima akisubiri majibu ya maswali yake kuhusu mbegu 
ya Wema.


 Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu (wa nne kushoto), akielekeza namna ya kupanda mbegu hiyo kwa wanakikundi cha Gezaulole.
 Hapa akielekeza vipimo vya upandaji wa mbegu hiyo.
 Zoezi la upandaji wa mbegu hiyo likiendelea.
 Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibindu, Juma Athumani (kushoto), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata hiyo Mbwewe mkoani Pwani. Wengine kutoka kulia ni ni Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George. 
 Wanawake wa Kata ya Kibinda wakiwa kwenye uzinduzi wa mbegu hiyo.
 Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, akitoa maelezo ya upandaji wa mbegu hiyo kwa wakulima wa Kata ya Kibindu.
 Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya , akichangia jambo.
Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.

Na Dotto Mwaibale, Chalinze

WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani wa Pwani wamefurahia kupokea mbegu bora ya mahindi aina ya Wema 2109 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa katika halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hiyo kwenye uzinduzi wa mashamba darasa katika vijiji vya Diozile na Kibindu vilivyopo Kata ya Msoga mkoani humo Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George alisema mbegu hiyo itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi katika halmshauri hiyo hivyo amewataka wakulima kuichangamkia.

"Tuwashukuru COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hii ambayo kwetu itakuwa ni mkombozi mkubwa katika mkoa wetu hasa kwa wakulima wa Kata ya Kibindu ambao ni vinara kwa kilimo cha mahindi katika mkoa wetu" alisema George.

Alisema mkoa wa Pwani kwa mwaka jana ulizalisha tani 110 za mahindi huku tani 65 zikizalishwa na Kata ya Kibindu jambo la kuwapongeza wakulima wa kata hiyo.

Alisema mbegu hiyo itaongeza msukumo wa kilimo ilimo cha mahindi kwenye halmashauri hiyo hivyo kujikwamua kupata baa la njaa na ziada kuuza. 

Aliwaomba wakulima hasa kwa wanavikundi waliopata mbegu hizo kuhakikisha wanayatunza mashamba darasa hayo kwa manufaa ya wakulima wote wa wilaya hiyo.  

Akizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu  hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein alisema 
kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.

Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kwa mkoa huo wametoa mbegu kilo 58 kwa ajili ya mashamba darasa katika wilaya ya Bagamoyo na Chalinze ambapo kwa wakulima mmoja mmoja wametoa kilo 42 pamoja na mbolea ya kupandia.




SBL yatangaza mpango Kabambe wa kuwasaidia wakulima nchini

March 20, 2018

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha, akiwasilisha mada ya utendaji na changamoto za kampuni hiyo kwa wajumbe wa  Kamati ya kudumu ya Bajeti, walipotembelea kiwanda cha Mwanza jana.



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia(katikati) akiongozwa na mwenyeji wake  Mwanzilishi wa kiwanda cha bia Serengeti tawi la Mwanza Christopher Gachuma(kushoto), walipotembelea kujionea utendaji na changamoto,jana, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Albert Obama.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof Elisante Ole Gabriel(katikati) akifurahia jambo na Mwanzilishi wa kiwanda cha bia Serengeti tawi la Mwanza Christopher Gachuma(kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bajeti Albert Obama, wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kiwanda cha bia cha Setrengeti  jijini Mwanza jana kujionea utendaji mapema wikiendi hii.



Mwanza Machi 17, 2018 – Mpango maridhawa wa kuwasaidia wakulima unaoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL), umeiwezesha kampuni hiyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa malighafi kutoka vyanzo vya ndani ya nchi kufikia tani 15,000, sawa na asilimia 80 ya mahitaji ya kampuni hiyo kwa mwaka.
Mpango huo unaojulikana kama Kilimo-biashara, unatekelezwa katika mikoa mbali mbali  hapa nchini ambapo wakulima wanaolima mazao kama mahindi, mtama na ulezi hupewa misaada inayowawezesha kuongeza uzalishaji.
Akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti iliyotembelea kiwanda cha SBL kilichopo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha alisema, SBL inawasaidia wakulima 300 waliopo sehemu mbali mbambali nchini huku lengo likiwa ni  kuongeza idadi na kufikia 450 katika kipindi cha miaka 2 ijayo.
Mpango wa kuwasidia wakulima unahusisha kuwapatia bure mbegu bora, kuwaunganisha na taasisi za fedha ili kupata mitaji kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wao pamoja na kuwapatia huduma za pembejeo. SBL hununua mazao yao na kuwawezesha kulipa mikopo pamoja na kuboresha masha yao kupitiua kipato wanachokipata.
Ili mpango huo uweze kuendelea kuwa endelevu na kuiwezesha SBL kuwafikia wakulima wengi zaidi, kampuni hiyo imeiomba Serikali kuendelea kuacha kiwango cha ushuru wa bidhaa kwa bia zinazozalishwa na malighafi za ndani kubakia asilimia 40 ambacho ni chini ukilinganisha na zile zisizotumia malighafi za ndani.
“Zaidi ya nusu ya vinywaji vinavyozalishwa na SBL zikiwamo bia kama Pilsner Lager, Kibo Gold, Kick Lager, Pilsner King and Senator Lager, zinazalishwa kwa asilia 100 na malighafi zinazotoka hapa nchini,” alisema Wanyancha
SBL pia imeishauri Serikali kutoongeza ushuru kwenye bia na pombe kali katika bajeti ijayo. Wanyancha alisema, kutoongezwa kwa ushuru kutasaidia kutafanya bei za bidhaa hizo zibaki kama zilivyo kwa sasa.
“Kwa kutobadilika kwa bei za vinywaji, Serikali itakuwa na uhakika wa mapato Zaidi kutokana na watumiaji kumudu kununua Zaidi,” alisema
Mkurugenzi huyo alitahadharisha kuwa, ongezeko la ushuru litasababisha ongezeko la bei huku likiathiri mauzo, jambo ambalo litapelekea kushuka kwa mapato ya serikali na kuongezeka kwa biashara ya pombe haramu.  

Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel ambaye alisema Serikali itaendelea na dhamira yake ya kuiwezesha sekta binafsi kukuwa na kustawi