MUHONGO AKABIDHI RASMI OFISI KWA SIMBACHAWENE

February 01, 2015

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo amekabidhi Ofisi kwa Waziri mpya wa wizara hiyo George Simbachawene.
Katika makabidhiano hayo, Prof Muhongo ameonya juu ya matumizi mabaya ya Ofisi yanayoambata na rushwa ili kuwasaidia watanzania masikini wanaoitegemea sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi wao.
Muhongo amemuasa Simbachawene juu ya umakini na kufanya kazi kwa kuzingatia mikataba inayoweza kuwanuifaisha watanzania na rasilimali zao.
Amemsifu Simbachawene kuwa hakuahi kuonesha ubinafsi wala tamaa na muda wote alikuwa akizungumzia juu ya kuwatumikia watanzania alipokuwa naibu waziri wa wizara hiyo, kwahiyo ana imani naye.
Amesema Tanzania ni lazima ilenge katika kujenga uchumi imara kupitia sekta ya Nishati na Madini inayokua kwa kasi ili watanzania pia waweze kukua kiuchumi.
Kwa upande wake Simbachawene amesema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika, kwani ofisi ya umma sio mali ya mtu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »