MBUNGE AOMBWA KUVISAIDIA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA ILI KUIPUNGUZIA MZIGO HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO

August 22, 2016
 Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) ambaye alikwenda kuitembelea hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kuangalia changamoto zinazowakabili
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita

 


 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
Ombi hilo lilitolewa jana na Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita wakati Mbunge huyo alipoitembelea hospitali ya alisema kuwa msongamano unaoikabili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika zahanati na vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika Hosptiali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na zahanati na vituo vya afya vingi Jijini Tanga kukakabiliwa na changamito nyingi zinazo sababisha kukosa ubora hali inayochangia kwa asilimia kubwa wananchi wengi kukimbilia katika hospital ya Rufaa ya Bombo na kuongeza msongamano wa wagonjwa.
Mahita alisema ipo haja ya kuvisaidia vituo hivyo ambavyo havina nyumba za watumishi, uzio, miundombinu mibovu na vingine kukosa umeme jambo ambalo linakuwa si rafiki kwa wahudumu na linakwamisha shughuli za kiafya hasa nyakati za usiku.
Alisema kuwa iwapo kutakuwepo na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali na wadau mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia Hospitali ya wilaya ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge Mussa Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
“Ndugu zangu huu si muda wa kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya ambalo ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo  lazima viongozi wajenge umoja na kutafuta njia ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema
Aidha alisema pamoja na changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo lazima Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya Wilaya iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya kukwama kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.
“Bado nashindwa kupa majibu ni kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa Hospitali ya Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa serikali inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali hiyo inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za matibabu.
Mbaruku alifanya mazungumzo hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.

JANET MBENE AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI ILEJE SEKONDARI

August 22, 2016
 Mbunge wa Ileje , Mh Janet Mbene,akiakabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Ileje Agrey Mwahihojo kwa ajaili ya ukarabati wa madarasa

 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akikagua Mabweni ya Wasichana  ya shule ya Sekondari ya Ileje
 Mbunge wa Ileje ,Janet Mbene akisalimiana na Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ileje , Hamidu Mwabulanga

FIFA YAONGEZEA UJUZI MAKOCHA TANZANIA

FIFA YAONGEZEA UJUZI MAKOCHA TANZANIA

August 22, 2016


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine limeipa nafasi Tanzania kwa kutoa kozi maalumu ya stamina (Physical fitness) kwa makocha wa Tanzania wenye leseni kiwango B inayoanza leo Agosti 22, 2016. Kozi hiyo inayoendeshwa na mkufunzi kutoka FIFA, Dk. Praddit Dutta, raia wa India itafikia ukomo Ijumaa wiki hii.
Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliishukuru FIFA kwa namna inavyoipa nafasi Tanzania katika kozi mbalimbali hususani za ukocha na uamuzi.

“Si kila nchi inapata privilege (fursa) kama hii. Bila shaka FIFA inatambua uwezo wa makocha wa Tanzania kwa sasa. Mjue kuwa FIFA ina watu wa kuwapa taarifa kila kona. Kama mngekuwa mnafanya vibaya, FIFA wangesema Tanzania bado, kwa hiyo kozi zisipelekwe… lakini inaonekana mnafanya vema, mngefanya vibaya msingefikiriwa,” alisema Mwesigwa aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Mwesigwa amesema kwa kuwa FIFA ina malengo chanya na Tanzania kwa kutoa kozi mbalimbali ikiwamo hiyo ya physical fitness inayolenga kuwapa ujuzi makocha hao kuwajengea uwezo wachezaji kuwa na stamina.
Hivyo akawataka makocha wanaohudhuria kozi hiyo kutumia fursa hiyo ya mafunzo si kwa ajili yao peke yao bali kuendeleza ujuzi huo kwa wengine ambao hawakubahatika kuwa sehemu ya wateule wa FIFA.
Naye, Mkufunzi wa kozi hiyo, Dk. Dutta alisema: “Bila shaka Tanzania inakwenda kufungua ukurasa mwingine wa soka la weledi kwa kuwa na wataalamu mbalimbali katika ukocha na uamuzi. Mnachotakiwa ni kujitahidi kufanya vema na kozi nyingine nyingi zinakuja.”
FIFA kwa kushirikiana na Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mkurugenzi Salum Madadi, imepitisha majina ya makocha 27 kuhudhuria kozi hiyo inayofanyika katika Hosteli ya TFF iliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Makocha wanashiriki kozi hiyo ni Mohammed Muza, Samwel Moja, Nassa Mohammed, Jemedari Said, Oscar Mirambo, Wane Mkisi, Cletus Mutauyawa, Shaweji Nawanda, Kizito Mbano, Dennis Kitambi, Sebastian Nkoma, Fikiri Mahiza, Nyamtimba Muga, Nassor Mwinchui, Alfred Itaeli, Henry Ngondo, John Tamba, Kidao Wilfred, Luhaga Makunja, Mohammed Tajdin, Mohammed Silima, Salum Ali Haji, James Joseph, Kessy Mziray, Daudi Sichinga, Bakari Shime na Salum Mayanga.

Ummy Mwalimu atoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano Mapitio ya Sera ya Afya.

August 22, 2016




 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya wizara anayoiongoza alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na wataalam wanaofanya  Mapitio ya Sera ya Afya kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA.

MAPITIO YA SERA YA AFYA YA MWAKA 2007.
Utoaji wa huduma za afya nchini una simamiwa na Sera ya Afya ya mwaka 2007. Dhumuni kuu la Sera hii ya Afya ya Mwaka2007, ni kuinua hali ya afya ya wananchi wote na hasa wale walioko kwenye hatari zaidi, kwa kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa Watanzania. Mpaka sasa, Wizara yangu inaendelea kutekeleza Sera hii katika kusimamia utoaji na upatikanaji wa huduma za afya nchini. Katika utekelezaji wa Sera hii, Wizara na Sekta ya Afya kwa ujumla imepata mafanikio mbalimbali. Mafanikio haya ni pamoja na:

  • Ongezeko la Vituo vya kutolea Huduma: Wizara imeendelea kuboresha huduma za tiba kwa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM). Katika utekelezaji wa Mpango huo,vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015, sawa na ongezeko la vituo 2,075. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini, Vituo 5,072 ni vya Serikali na 2,175 nivyataasisibinafsi.

  • Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka112 kwa kila vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi 81 kwa vizazi hai 1000 mwaka 2010. Aidha, Taarifa ya Kimataifa ya Septemba 2013, imeonesha kuwa Tanzania tumeweza kufikia Lengo la millennia namba 5, la angalau kuwa na vifo 54 kwa kila vizazi hai 1000, Tanzania iliweza kufikia lengo hilo kabla ya mwaka 2015..

  • VifovitokanavyonamatatizoyaUzazivimepunguakutoka 578 kwakilavizazihai 100,000 mwaka 2005 hadivifo 432 kwavizazihai 100,000 mwaka 2012 navifo 410 kwavizazihai 100,000 mwaka 2014. PiamatumiziyaUzaziwampangoyameongezekakutokaasilimia 20 mwaka 2005 hadiasilimia 27 mwaka 2010.

  •   Huduma za Chanjo: Serikali imefanikiwa katika kupanua wigo wa huduma za chanjo ambapo, kiwango cha chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2005 hadi asilimia 97 mwaka 2014. Kutokana na mafanikio katika chanjo, Wizara imefikia viwango vya kimataifa vya kutokomeza pepopunda kwa watoto wachanga mwaka 2012 na pia imeweza kudhibiti ugonjwa wa Polio.
  •   Katika kipindi hiki cha kutekeleza sera hii, Wizara imeanzisha huduma mpya za kibingwa na uchunguzi hapa nchini na kuwawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa hazitolewi hapa nchini. Huduma hizo ni pamoja na upasuaji mkubwa wa moyo, upasuaji wa mifupa,mishipa ya fahamu na ubongo, kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na uanzishaji wa huduma za dharura.

  •   Udhibiti wa Malaria: kiwango cha maambukizi ya malaria kimeshuka kutoka asilimia 18 mwaka 2008 na kufikia asilimia 10 mwaka 2012 (THMIS).
  •   Udhibiti wa UKIMWISerikali imepata mafanikio katika kudhibiti UKIMWI, kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI(VVU) kimepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/12. Vituo vya tiba kwa watu wanaoishi na VVU vimeongezeka kutoka 91 mwaka 2005 hadi 1,463 mwaka 2015. Hadi Juni 2015, jumla ya watu 703,589 wanapatiwa ARV ikilinganishwa na Mwaka 2005, ambapo watu wanaoishi na VVU 16,199 walipatiwa huduma hii.


 Pamoja mafanikio mbalimbali yaliyopatika katika utekelezaji wa Sera hii, Sekta ya Afya imekuwa na changamoto mbalimbali na kusababisha madhumuni ya Sera kutofikiwa. Changamoto hizo ni pamoja na:
  1.   Upungufu wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya,
  2.  Uhaba wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini hasa, zahanati, vituo vya afya na hospitali,
  3.  Uwezo mdogo wa viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini,
  4.    Upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya katika ngazi zote za kutolea huduma
  5.  Maendeleo madogo ya upunguzaji wa Vifo vya wakinamama vinavyotokana na Ujauzito.
  6.    Maendeleo na mabadiliko ya tabia na mwenendo wa maisha vimebadili sura ya magonjwa. Aidha, hali hii imesababisha kuanza kujitokeza kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na yanayotokana na ajali na majanga, ambayo kwa huduma zilizopo haziwezi kukidhi.
  7.  Kuendelea kupungua kwa Rasilimali fedha katika  Sekta ya Afya na kusababisha kuendelea kushuka kwa ubora wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma.
  8.  Kuwalinda wananchi hasa wenye kipato cha chini katika katika kupata huduma za afya wakati wanazihitaji.

  1. Uwepo wa vituo vya kutosha vya kutolea huduma na kudumisha upatikanaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya.
  2. Ongezeko la idadi ya watu ambalo linapelekea ongezeko la mahitaji ya huduma za afya.
Aidha, changamoto hizo na Mabadiliko mbalimbali ambayo yatatokea yamepelekea serikali kutoa maagizo na kutayarisha mikakati mbali mbali ya Serikali kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo kwa umma. Mikakati na maagizo hayo ni pamoja:

  • Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya 2015-2020 ( HSSP IV)
  • Utekelezaji wa Mkakati wa Ugharamiaji wa Huduma za Afya
  • Utekelezaji katika mfumo wa malipo kwa matokeo.
  • Mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa
  • Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, inayobadilisha namna huduma za Afya      zinavyotolewa
  • Ongezeko la Magonjwa sugu, hasa magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo yana gharama kubwa na yanaweza kuzuilika.
  Mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa

   Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, inayobadilisha namna huduma za Afya zinavyotolewa
  Ongezeko la Magonjwa sugu, hasa magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo yana gharama kubwa na yanaweza kuzuilika.

Kutokana na changamoto zilizojitokeza na utekelezaji wa mikakati na maagizo hayo , ni muhimu kufanya mapitio ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 ili utekelezaji wa matamko ya kukidhi  Lengo na  Madhumuni yaliyokusudiwa kufikiwa na Sera.

Mapitio haya, yanafanywa na Wizara yangu kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

Nawaomba wananchi wote kutoa ushirikiano wakutosha kwa Wizara na Wataalam wa timu hii katika kuhakikisha kuwa mnatoa maoni yenu kwa uwazi kwa ajili ya kusaidia maendeleo a Sekta ya Afya nchini. 

Wananchi wote mnaweza kutoa maoni yenu kupiti Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) au kuwasilisha maoni yenu pia Kupitia anuanimaoni.sera@moh.go.tz. Mwisho wa kutoa maoni ni tarehe 30 Oktoba 2016.

Nawashukuru sana.

Ummy A. Mwalimu (mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto

MCHUNGAJI DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AKIHUDUMU NCHINI MAREKANI.

August 22, 2016
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani) yuko nchini Marekani kwa huduma ya kiroho tangu jumanne iliyopita Agost 16,2016 ambapo alianza kuhudumu ijumaa Agost 19,2016 katika Kanisa la "Assemblies Of God Agape Church" lililopo Boston Marekani.

Huduma ya Mchungaji Dkt.Kulola inaendelea katika majimbo mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Dallas, Texas, Houston na Arizona.

Aidha Mchungaji Kulola ametoa shukurani zake za dhati kwa familia yake, Kanisa la EAGT Lumala Mpya, ndugu, jamaa pamoja na marafiki kwa kuendelea kumuombea kwa huduma anayoifanya nchini Marekani ambapo watu wengi wanaokoka na kuponywa.
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akihudumu nchini Marekani.
Picha ya pamoja baada ya huduma katika jimbo la Boston
Mchungaji Kulola (katikati) na familia yake
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola(kulia).
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

HONGERA BWANA DAVID MANOTI KWA KUUAGA UKAPERA

August 22, 2016
Bwana Harusi David Saire Manoti akiwa na Mke wake mpenzi Nezia Manumbu  Baada ya Kufunga Pingu za Maisha katika Kanisa la St. Peters Jijini Dar
Maharusi wakiwa katika Ibada ya ndoa yao Takatifu
 Bwana na Bibi David Saire Manoti wakipata Picha za ukumbusho katika Ufukwe wa Bahari ya Hindi
 Maharusi wakipata Picha ya pamoja na Wasimamizi wao
Maharusi wakipata picha  na wasimamizi wao pamoja na wasindikizaji walionogesha Harusi hiyo 
 Bwana na Bibi Harusi David na Nezia wakiingia ndani ya ukumbi wa Law School
Bwana harusi David Manoti akiwa na shangwe wakati anaingia ukumbini 
 Kamati kuu ya Maandalizi wakitangaza zawadi yao kwa Maharusi
Ulifika muda wa kuzifungua Champagne, huku kila mmoja aliyekuwa nayo mkononi akifungua kwa mbwembwe zake 
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kumiminiwa Champagne kabla ya kufanya Cheers ili kutakiana heri
 Maharusi wakipeleka Keki upande wa Bibi Harusi Familia ya akina Manumbu ikiwa ni  ishara ya shukurani
 Maharusi wakipeleka keki katika familia ya Bwana Harusi Saire Manoti ikiwa ni ishara ya Shukurani
 Maharusi wakilishana keki
 Wazazi upande wa Bibi Harusi wakiongozwa na mama mzazi wa Nezia kutoa zawadi ya Familia
Wazazi upande wa Bwana Harusi wakiongozwa na Mama Mzazi wa David wakitangaza zawadi yao
Wageni waalikwa wakiwa katika Harusi ya Bwana na Bibi David Manoti
 Baadhi ya Marafiki wakiwa katika harusi ya David na Nezia
Burudani ikiiendelea ...
Picha zote na Fredy Njeje.
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com

KISHINDO CHA UZINDUZI WA MSIMU WA TIGOFIESTA 2016 CHAZIZIMA JIJINI MWANZA USIKU WA JANA

August 22, 2016
Mkali wa singeli ManFongo na Shilole wakilivamia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika tamasha hilo kubwa liliofanyika usiku wa  jana jijini Mwanza na kukutanisha wasanii nguli katika muziki wa kizazi kipya na Msanii wa kimataifa  toka Nijeria Wizkid 


Umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza wakitoa shangwe wakati burudani mbalimbali zikiendelea katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016  viwanja vya CCM Kirumba hapo usiku wa jana`.

IMOOOOOOOOOOO

Alikiba alikuwa kivutio kwa mashabiki wengi mara baada ya kufanya suprize na kutoa burudani ya kukata na shoka huku mashabiki zake wakifuatisha nyimbo zake moja baada ya nyingine katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 katika viwanja vya Kirumba Jijini Mwanza


Benpol akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 lilifnayika jana katika viwanja vya CCM kirumba Jijini Mwanza.
Msanii wa kizazi kipya Dayna Nyange akitumbuiza umati uliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta 2016 jijini Mwanza hapo usiku wa jana.

Mkali wa Singeli anayetamba na nyimbo yake "HAINAGA USHEMEJi"  akitumbuiza jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza.


Aika na Nahreel (Navykenzo ) nao walifanikiwa kuteka jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza

Wasanii toka kikundi cha TipTop connections Tundaman na Madee Ali wakitumbuiza mashabiki katika jukwaa la Tigo Fiesta 2016  katika viwanja vya CCM kirumba hapo usiku wa jana .

Weusi wakilishambulia vilivyo  jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza hapo usiku wa jana

Msanii wa  kimataifa toka Nigeria Ayodeji Balogun(Wizkid) akitumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta 2016 liliofanyika hapo jana Jijini Mwanza  katika viwanja vya CCM Kirumba

Baadhi ya waandishi wa Habari wakichukua matukio katika tamasha la Tigo Fiesta 2016 wakazi msanii wa kimataifa toka Naijeria Wizkid akitumbuiza katika viwanja vya CCM kirumba usiku wa jana .

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia wakati burudani mbalimbali zikitolewa na wasanii waliotikisa jukwaaa la Tigo Fiesta 2016 hapo usiku wa jana katika viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza 

photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com