WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA BOMBO WAPEWA MKONO WA SIKUU YA CHRISTMAS

December 22, 2023

 


MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Naima Yusuf kushoto akigawa zawadi za sikukuu ya christmas kwa Muuguzi wa Hospitali hiyo Mwanakombo Hassani mapema leo ikiwa ni utamaduni wao wa kila sikuu kubwa kufanya hivyo.

MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Naima Yusuf kushoto akigawa zawadi za sikukuu ya christmas kwa Muuguzi wa Hospitali hiyo Mwanakombo Hassani mapema leo ikiwa ni utamaduni wao wa kila sikuu kubwa kufanya hivyo.
MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Naima Yusuf kushoto akigawa zawadi za sikukuu ya christmas kwa Afisa Takwimu wa Hospitali hiyo Rashid Lukumbuja mapema leo ikiwa ni utamaduni wao wa kila sikuu kubwa kufanya hivyo.
Mmoja wa watumishi akitoka kuchukua zawadi za sikuu ya Christmas mapema leo ambazo zimetolewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo




Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wakiwa na zawadi zao za sikuu ya Christmas mapema leo ambao zimetolewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo

Mmoja wa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo akiwa na zawadi zake za sikuu ya Christmas mapema leo ambao zimetolewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo

Sehemu ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wakiwa za zawadi zao za sikuuu ya Christmas ambazo zimetolewa na Uongozi wa Hospitali hiyo
Sehemu ya watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo wakiwa kwenye foleni kuchukua zawadi za sikuu ya Christmas mapema leo ambazo zimetolewa na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo




Na Oscar Assenga,Tanga

UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo umetoa zawadi za sikuu ya Krismas kwa wafanyakazi wake ikiwa ni utamaduni wao wa kila sikuu kubwa kufanya hivyo.

Zoezi la Ugawaji huo lilifanywa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Naima Yusuf ambaye alisema ni muhimu wafanyakazi kusherehekea sikuuu kwa amani na utulivu.

Alisema ugawaji wa zawadi hizo ni zoezi ambalo limekuwa likifanyika katika sikuu za Eid na Krismas lengo likiwa ni kutoa motisha kwa watumishi katika Hospitali hiyo.

Aidha aliwataka kuendelea kuchapa kazi kwa waledi na uaminifu mkubwa katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupataa huduma mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali hiyo Salvatory Lyimo alisema wana mshukuru Mganga Mfawidhi Dkt Naima Yusuf kwa zawadi hiyo aliyowapa wafanyakazi sikuu zitaenda kuwa nzuri endelee kuwa na moyo huo huo kuwajali.

Alisema aliushukuru uongozi kwa zawadi hizo ambazo wamekuwa wakizitoa kila sikuuu wanawalisha Mungu awabariki na kuwapa maisha mazuri.

Kilimanjaro Warejea, Wafanikisha Utoaji Huduma Ya Miamala Kupitia Mashine Ya POS Kileleni.

December 22, 2023

 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hii leo imewapokea wafanyakazi wake na wadau mbalimbali wa utalii wakiwemo waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro ambao wameshuka kutoka kwenye kilele cha Mlima mrefu zaidi duniani (uliosimama peke yake), Mlima Kilimanjaro. Wafanyakazi hao walipanda mlima huo kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima huo.


Hatua hiyo mbali na kusogeza huduma za benki ya NBC wateja wake wanaotembelea mlima huo pia ililenga kudhihirisha umahiri wa teknolojia ya benki ya NBC katika utoaji wa huduma zake kwa wateja hususani kupitia mashine hiyo ya kisasa.

Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao waliopanda mlima huo Disemba 16 wakiongozwa na Bw Dickson Busagaga ambae ni mdau wa habari mkoani Kilimanjaro ilifanyika kwenye eneo la geti la lango la Marangu ikiongozwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi sambamba na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru, wafanyakazi wa benki ya NBC, baadhi ya wadau wa utalii pamoja na wateja wa benki hiyo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Bi Ngu’umbi pamoja na kuwapongeza wafanyakazi na wadau hao kwa kufanikisha zoezi hilo, pia aliipongeza benki hiyo kwa kuutumia mlima huo kama kigezo cha kuthibitisha ubora na ufanisi wa mashine hiyo ya miamala pamoja na kusogeza huduma hiyo kwenye kivutio hicho cha kimataifa, hatua aliyoitaja kuwa itasaidia sana kurahisisha huduma za malipo mbambali yanayofanywa na wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.

‘’Kwetu sisi kama wadau wa utalii ujio wa huduma hii ni mkombozi dhidi ya changamoto ya huduma ya malipo iliyokuwa ikiwakabili wadau mbalimbali hususani wasindikiza wageni. Baadhi yao walikuwa wanalazimika kuwafuata watalii hadi nje ya hifadhi huko ili tu kufuata malipo yao.’’

“Kupitia mashine hii sasa malipo yao yanaweza kufanyika huko huko kwenye kilele wakiwa wanajipongeza’’ alibainisha Bi Ngu’umbi kauli ambayo iliungwa mkono na Bw Hillary Kombe na Godlisten Mkonyi wanaotoa huduma za kusindikiza wageni kwenye mlima huo.

Kwa upande wake Bw Ndunguru alisema hatua hiyo sio tu njia ya kuangazia sifa na kutangaza mashine hiyo ya POS bali pia kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza utalii wa ndani na nje kwa kuutangaza mlima huo mrefu zaidi barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

“Tunatabasamu siyo tu kama washindi ila kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa usalama na afya kufanikisha zoezi la kufikisha tabasamu hadi kilele cha mlima Kilimanjaro ambapo POS za NBC sio tu zimefika kilele cha mlima Kilimanjaro, bali pia zimewaka na kufanya miamala.’’

“Tunajivunia kuwa waanzilishi wa uzinduzi wa kwanza wa mashine ya POS katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. POS zetu zimeweza kufanya miamala katika vituo vyote, Mandara, Horombo, Kibo, Gilmans Point, Stella na hadi Uhuru Kileleni. Hii ni kuwahakikishia wateja wetu kuwa Mashine za POS ni imara, za uhakika na zinafanya kazi wakati wowote, kwenye mazingira yoyote na hali ya hewa yoyote. “ alibainisha Ndunguru.

Zaidi alisisitiza kuwa : ‘Sababu ya uzinduzi wa mshine hii katika kilele cha Mlima wa Kilimanjaro pia inatokana na sifa kuu tano zinazoendana na alama na maana ya vituo tunavyokutana navyo katika kupanda mlima huu. Tunaamini kila kituo kimeoana na sifa za mashine zetu za POS za NBC ambazo ni Urahisi, Haraka au Kasi, Teknolojia ya hali ya juu, Mahiri (Smart) na Uhuru wa malipo. Hatua hii inafuingua rasmi pazia la kuruhusu malipo kwa chaguzi mbalimbali za kidigitali kama vile Apple Pay , Google Pay, Amazon Pay, Samsung Pay na kadi yoyote ya benki. au hata kwa kutumia saa ya kidigitali''. alitaja.

Jitihada hizo ni muendelezo wa kampeni yetu mpya ya "Tabasamu Tukupe Mashavu," ya benki hiyo inayolenga kutoa fursa kwa wateja kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki katika Sikukuu za mwisho wa mwaka kupitia miamala iliyorahishwa kupitia benki ya NBC.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi waliopanda mlima huo Bi Florence Ng’wavi ambae ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Barabara ya Meru alisema mafanikio hayo yanawasilisha adhima ya pamoja ya wafanyakazi wa benki hiyo katika kuthibitisha na kutetea ubora wa huduma wanazozitoa kwa wateja wa benki hiyo.

“Pamoja na changamoto mbalimbali tulizokumbana nazo wakati wa zoezi hili, bado tuliona ni rahisi zaidi kwasababu kila kituo tulichokuwa tunapanda kilikuwa kinathibitisha sifa moja wapo muhimu kwenye mashine hii. Kwa kuamini hivyo ikawa ni rahisi kwetu kwa kuwa tuliongozwa na dhamira ya kuthibitisha kile tunachokiamini yaani ufanisi na ubora wa huduma hii muhimu,’’ alisema Bi Florence.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wa saba kushoto)sambamba na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (wa saba kushoto)   wakionesha  mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao  hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Maafisa waandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), akiwemo Afisa Uhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gladys Ngu’umbi (wa pili kushoto) wakiwapongeza baadhi ya baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na wadau wa utalii mkoani humo wakiwemo waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo.Anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wan ne kulia). Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (Kushoto) akimpongeza baadhi ya baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na wadau wa utalii mkoani humo wakiwemo waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.


Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao waliopanda mlima huo Disemba 16 wakiongozwa na Bw Dickson Busagaga (wa tatu kushoto) ambae ni mdau wa habari mkoani Kilimanjaro ilifanyika kwenye eneo la geti la lango la Marangu ikiongozwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (wanne kushoto)  sambamba na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (wa tano kushoto) wafanyakazi wa benki ya NBC, baadhi ya wadau wa utalii pamoja na wateja wa benki hiyo mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC mkoani Kilimanjaro na Arusha wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (kushoto)  wakiwapongeza wenzao muda mfupi baada ya kurejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya kufanyia miamala (POS Machine)  ya benki hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Afisa Uhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Gladys Ngu’umbi (katikati)   akionesha  mashine ya kufanyia miamala (POS Machine) ya benki ya NBC ikiwa ni ishara ya kutambulisha huduma hiyo kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na maeneo mengine nchini wakati wa hafla ya kuwapokea wafanyakazi wa benki hiyo pamoja wadau wa utalii mkoani Kilimanjaro wakiwemo Waandishi wa habari waliorejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo. Wanaoshuhusia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC Bw. Elvis Ndunguru (kushoto)  na Ofisa Mwandamizi wa benki hiyo Bi Dogo Ramadhani (Kulia).Hafla ya kuwapokea wafanyakazi hao  hao imefanyika hii leo kwenye eneo la geti la lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.




Hafla hiyo ilihusisha utoaji wa vyeti wa utambuzi na pongezi kwa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja wadau wa utalii mkoani Kilimanjaro wakiwemo Waandishi wa habari waliorejea kutoka safari ya kihistoria ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kufikisha mashine ya hiyo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kusogeza huduma za benki hiyo kwa wateja wake wanaotembelea mlima huo.

MAKONDA AWATAKA VIONGOZI KUJITATHMINI KWA NAFASI WALIZOPEWA

December 22, 2023


KATIBU wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Paul Makonda amewataka watendaji wa serikali kujitathmini kwa nafasi walizopewa kwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo pasipokumuangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kumuwakilisha kwenye kuhudumia wananchi.

Ameyasema hayo leo Desemba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa tathmini ya ziara mbalimbali zilizofanywa na viongozi wa Chama hicho ili kuzungumza na wananchi na kujua changamoto zinazowakabili.

Amesema katika ziara hizo wameweza kuibua kero mbalimbali ambazo wanakutana nazo wananchi katika maeneo yao.

“Hizi ziara tumezifanya kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na tumepata kero nyingi sasa niwaombe watendaji ambao mmewekwa kumsaidia Rais mjitathmini Je? mnafaa kuwepo mlipo na Je? mnatimiza matakwa ya Rais wetu katika kuwahudumia wananchi”. Amesema Makonda.

Sambamba na hayo Makonda amewataka watendaji wa shirikia la umeme TANESCO kutoa taarifa ya changamoto ya umeme wakiwa site na sio ofisini ili wananchi waweze kuelewa nini wanachozungumza.

Aidha makonda amewataka wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kwenye dira ya maendeleo ya mwaka 2025-2050 ili iweze kutoa dira kwa serikali katika kupanga maendeleo na sera zake.





Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2023 katika Ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba Jijini Dar es Salaam


Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2023 katika Ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba Jijini Dar es Salaam

WAZIRI UMMY AITAKA OCEAN ROAD NDANI YA MWEZI MMOJA KUANZA KUTUMIA PET-CT SCAN

December 22, 2023

 Na. WAF -  Dar es Salaam 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road hadi kufikia Fubruari Mosi, 2024 mashine ya Pet-CT Scan iwe imeanza kutoa huduma kwa Watanzania ili rufaa za kwenda nje ya nchi zipungue. 

Waziri Ummy ametoa tamko hilo Disemba 21, 2023 baada ya kufanya ziara ya kujionea huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam. 

“Mmeniambia tarehe 26, Disemba mtafanya majaribio ya mashine hii sasa nataka nikija tena hapa tarehe 01-02-2024 nione mashine ya Pet-CT Sacan iwe imeanza kufanya kazi Ili Watanzania waweze kupata huduma za Pet-Ct Scan hapa nchini.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali Afya za  Watanzania kwa kuipa fedha Sekta ya Afya kwa ajili ya matibabu ikiwemo ya Saratani Pamoja na Vifaa Tiba. 

Amesema, kwa sasa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa udhamini wa Serikali ni wagonjwa  42 wakiwemo wa Saratani wagonjwa 15 kwa muda wa miezi Mitatu kuanzia Julai hadi September Mwaka huu. 

“Tunataka kupunguza Rufaa za nje ya nchi ili kusogeza huduma kwa Watanzania lakini pia kuokoa fedha za Serikali na tutaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za Saratani nchini.” Amesema Waziri Ummy 

Pia, Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road kwenda kuwajengea uwezo wataalamu waliyopo katika Hospitali za Rufaa za Kanda pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa hususan huduma za mkoba kwa kuwa Taasisi hiyo ni kituo cha umahiri wa Masuala ya Saratani nchini Tanzania. 

Vilevile, ameitaka Taasisi hiyo kuharakisha harakati za kufungua vituo katika Mkoa wa Mbeya na Dodoma ili watu wanaotaka kupata huduma za mionzi wazipate kwa haraka. 

Waziri Ummy ameipongeza Taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za Saratani kwa Watanzania na amewahakikishia kuwa Serikali itatimiza wajibu wake ili wafanye kazi katika mazingira rafiki.

Mwisho Ametoa wito kwa Watanzania kuwa na tabia ya kupima Afya zao mara kwa mara ili kujua hali zao za kiafya mapema na kuanza kupata huduma mapema kama umekutwa na ugonjwa ikiwemo Saratani.