MKURUGENZI WA ILEJE HAJI MNASI ATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO

September 26, 2016

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotembele hivi karibu na kujifunza mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya hayati baba wa taifa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi nzima
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika kaburi la marehem Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Na fredy mgunda,musoma.

VIONGOZI wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Bw. Haji Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu mara baada  kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.


mimi kitaaluma ni mwalimu hivyo namuezi mwalimu kwa vitendo hata nilipokuwa afisa elimu iringa nilikuwa naingia darasani kufundi na sasa nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yakeAmesema Mnasi.

Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa  uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,  wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Mnasi.

Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi  kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Mnasi.

Bw. Mnasi amebainisha kuwa  serikali itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa  wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Mnasi.

Bw. Mnasi amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.

Kwa upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa  watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.

Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.

“Ninyi mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania”

SUMATRA KUPAMBANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA YA BAHARI

September 26, 2016
 Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo  kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud
mziray1
  Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa leo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
 Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari leo
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA)Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga  
…………………………………………………………………..
MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.
Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.
Ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.
Aidha alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa mazingira uliopitiliza unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua samaki katika bahari na viumbe vingine vilivyomo baharini.
Alisema Tanzania imeingia katika shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya bahari hali ambayo inalazimika kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda
mazingira ya bahari.
“Hakuna vyombo vinavyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya baharini hivyo imetulazimu kuanzisha mpango maalumu ambao tunategemea kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na
uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.
 Hamza alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya maadhimisho hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia katika mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya usafirishaji wa Majini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho hayo lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani na nje ya nchi.
Alisema Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu ya kitovu cha biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari na hata nchi kavu ikiwa itawekewa mipango madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.

WANANCHI WAILALAMIKIA TAZARA KWA KUFUNGA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM

September 26, 2016
 Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
 Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
 Pikipiki ikivushwa.
 Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa  Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale


MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.

Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.

"Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini" alisema Gedion Robert.

Robert  alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.

Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.



'PANYA ROAD' WAIBUKA UPYA NA KUTESA WANANCHI MOSHI BAA JIJINI DAR ES SALAAM

September 26, 2016
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar. Simon Sirro


Na Dotto Mwaibale

KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaa leo hii mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina  la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.

"Tayari vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira  huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo" alisema Abubakar.

Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni  lazima wampige na kumpora.

"Wenye maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.

Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.

"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote tuna wahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo " alisema Kamanda Hamdan.

Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

September 26, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wafanyakazi waliokuwa wakimshangilia wakati akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa mapendekezo  kwa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozwa na Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu akikagua mtambo wa  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  chumba cha mitambo ya  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimlaki kwa furaha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Bandarini Bw.  Mashaka Karume akieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimsikiliza   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga  wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga  na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016