KOZI YA MAKOCHA WA MCHEZO WA WAVU NGAZI YA MKOA WA TANGA KUANZA MEI 11 MWAKA HUU

May 10, 2018
CHAMA cha mchezo wa Wavu Mkoani Tanga (Tareva) kinatarajiwa kuendesha mafunzo ya waamuzi na makocha yatakayoshirikisha washiriki kutoa wilaya zote mkoani Tanga na kufanyika kwenye shule ya Sekondari Tanga School.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Mei 11 hadi 15 mwaka huu yataendeshwa na Mwamuzi wa Kimataifa wa Mpira wa Wavu Saumu Agapa ambaye anatambuliwa na shirikisho la mpira wa wavu duniani (FIVB) ambaye atashirikiana na Salim Zuberi kocha mwenye levo ya pili.
Akizungumza jana na gazeti hili, Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Tanga Augustino Agapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ujuzi walimu wa shule za msingi na sekondari.
Alisema baada ya mafunzo hayo anaamini watafanya uamuzi sahihi kwenye shule zao kwa wale wa msingi na sekondari ambao wakati mwengine wanaweza kushindwa kufanya hivyo kutokana na kutokutambua sheria.
Hata hivyo alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha mchezo huo unachezwa kuanzia ngazi za chini ili vijana waweze kukua nao na baadae waweze kupatikana wachezaji wazuri ambao watakuwa chachu ya mafanikio.
Mafunzo hayo yatawashirikisha walimu wa shule za msingi na sekondari wanaofundisha michezo vikiwamo vilabu,wachezaji wa zamani ambao wapo mkoani Tanga.
“Kama unavyojua tumeamua kuanzia mashuleni kwa sababu huko ndio kisima cha mchezo kutokana na kuwepo kwa vipaji ambavyo vinaweza kuwa hazina kubwa mkoani hapa kwa siku zijazo”Alisema

DKT MAHIGA ATEMBELEA TAASISI YA SAVE THE CHILDREN HEART YA ISRAEL

May 10, 2018


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameshukuru Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuokoa maisha ya watu wengi nchini, hususan watoto.


Waziri Mahiga alitoa shukrani hizo leo alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu aliyoianza jana. "Zamani nilijua kuwa mtu akizaliwa na maradhi ya kurithi, mtu huyo hawezi kuishi lazima atakufa, lakini uwepo wa taasisi yenu kumenifanya niondoe itikadi hiyo" Dkt. Mahiga alisema.


Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart imeisifu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa ni moja ya Taasi bora kusini mwa Jangwa la Sahara na kwamba ina uwezo na wataalam wa kufanya upasuaji bila ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi. "Serikali inachotakiwa kufanya ni kuiboresha taasisi hiyo kwa kujenga majengo mapya na kuipatia vifaa zaidi na itakapofanya hivyo itaokoa maisha ya watu na fedha nyingi ambazo zingelitumika kugharamia matibabu nje ya nchi". Mkurugenzi wa taasisi hiyo alishauri.


Mkurugenzi wa Taasisi hiyo alimweleza Dkt. Mahiga kuwa taasisi ilianzishwa miaka ya 90 kwa madhumuni ya kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi ya moyo duniani kote, hususan katika nchi zinazoendelea. Hadi sasa imeshatoa matibabu kwa zaidi ya watoto 460,000 wenye maradhi ya moyo kutoka Afrika, Amerika, Asia na kwingineko.


Shughuli za taasisi hiyo inajumuisha kutibu wagonjwa, kutoa mafunzo kwa madaktari na wakufunzi na kusambaza madaktari katika nchi mbalimbali kuendesha upasuaji kwa kipindi maalum. Madaktari waliopewa mafunzo na taasisi hiyo wanaendelea kupata miongozo ya taasisi wanaporejea katika nchi zao kwa ajili ya kufanya matibabu.


Mhe. Waziri alipokuwa katika taasisi hiyo alipata fursa ya kuonana na Watanzania wanaosoma na wengine wanaopata matibabu ya maradhi ya moyo katika taasisi hiyo. Aidha, alioneshwa watoto wawili wanaougua maradhi ya moyo kutoka Nymmar na Romania ambao kwa mujibu wa Mkurugenzi alisema ndio wa kwanza kupokelewa kutoka nchi hizo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Israel
10 Mei 2017

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akiongea na wawakilishi wa Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo kujionea namna inavyoendesha shughuli zao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimjulia hali mmoja wa watoto kutoka Tanzania anayepata tiba ya maradhi ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel

Kutoka kulia, mtu wa kwanza na wa pili ni Watanzania wanaosomea fani za tiba za maradhi ya moyo katika taasisi ya Save the Children Haert wakiongea na Mhe. Waziri wakati alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel leo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Save the Children Heart ya Israel akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri hayupo pichani namna taasisi hiyo inavyofanya kazi.

Wanne kutoka kushoto ni wanafunzi kutoka Tanzania wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya Moyo wakimsikiliza Mkurugenzi wao hayupo pichani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Save the Children Heart/

Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akibadilishana mawasiliano na wanafunzi wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya moyo kutoka Tanzania.

Ulinzi wa Mpaka kwenye Ukanda wa Ghaza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Afisa Usalama kutoka Kitengo cha Protection Unit alipowasili katika eneo la Netiv Haasara lililopo Ghaza ambapo ni mpakani na eneo la Palestina linalotawaliwa na Hamas.

Mkazi wa eneo la Netiv Haasara, Ghaza, Bibi Hila Fenton akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri na wajumbe wengine kuhusu madhila wanayokutana nayo wananchi wa Israel wanaoishi karibu na mpaka wa Ghaza.

Bibi Hila Fenton akionesha mabaki ya gruneti la kwanza kabisa kurushwa kutoka Palestina na kuangukia kwenye eneo wanaloishi mwaka 2001/

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akipokea maelekezo alipowasili eneo la mpaka katika ukanda wa Ghaza lililojengwa ukuta/

Wageni wanaofika katika eneo la mpaka huu wanaombwa kuandika ujumbe wa matumaini katika mawe yaliyotengenezwa kwa sanaa ya aina yake na kuyabandika kwenye ukuta unaozuia maguruneti kupita. Hapo Mhe, Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima wakibandika vijiwe vyenye ujumbe wa kuleta matumaini kwenye ukanda wa Ghaza.

Bi. Kisa Mwaseba naye akibandika ujumbe wake

Sehemu ya ukuta wa sengenge unaotenganisha mpaka wa Israel na Palestina katika Ukanda wa Ghaza.

Sehemu ya ukuta uliojengwa imara kuzuia vijiji vya Israel vilivyo mipakani visifikiwe na mashumbulizi ya magruneti.


Eneo la Ukaguzi wa Malori ya mizigo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipata maeleozo kutoka kwa Meneja wa Usalama wa ukaguzi wa malori ya mizigo yanayokwenda Palestina kutoka Israel na kinyume chake.

Meneja wa Usalama anatoa maelezo namna kazi ya kukagua malori ya mizigo inavyofanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia uwezekano wowote wa kupitisha vilipuzi au vifaa vya kuundia vilipuzi.

Baadhi ya Malori ya mizigo

baadhi ya mizigo ambayo imekamilika kukaguliwa inasubiri kusafirishwa

Eneo la ukaguzi wa maslori ya mizigo ambalo pia limejengewa ukuta kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya maguruneti.

Scanner inayotumika kukagua malori ya mizigo ambayo ina nguvu kubwa ya kubaini vifaa vilivyobebwa katika lori kimoja baada ya kingine. kutokana na nguvu ya scanner hiyo harusiwi mtu kukaa karibu inapofanya kazi.

Waziri Mahiga akionesha moja ya mitambo iliyofungwa kwa ajili ya kuzuia bomu lisilipuke kabla halijasababisha madhara.

WAZIRI UMMY ATOA TAARIFA KUHUSU UGONJWA WA EBOLA LEO JIJINI DODOMA

May 10, 2018





Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu Ugonjwa wa Ebola leo Jijini Dodoma,kulia ni Mkurugenzi wa Tiba dkt. Dorothy Gwajima

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu Ugonjwa wa Ebola leo Jijini Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi huduma za Kinga dkt.Leonard Subi (Chanzo MichuziBlog)

WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA,AVUTIWA NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

May 10, 2018



Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kulia)akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia juu ya miradi ya upanuzi wa Chuo hicho inayoendelea kazi ziara ya siku moja aliyoifanya Mei 9,2018
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(katikati)akiwa na watumishi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) akikagua moja ya Karakana ya Mitambo inayofanyiwa ukarabati.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(katikati)akiwa pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Dk Erick Mgaya katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya upanuzi wa Chuo hicho.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia)akikagua moja ya makontena yenye vifaa mbalimbali kwaajili ya mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto)akiangalia kiungo cha bomba kwenye Karakana ya wanafunzi wanaosoma kozi fupi kwaajili ya kuwa sehemu ya mafundi watakaojenga Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kulia)akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia katika ziara aliyoifanya kwenye Chuo hicho kukagua shughuli mbalimbali zinazoendelea.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika moja ya Maabara ya Chuo hicho.



Wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha wakimsikiliza Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako.

TATU MZUKA YATANGAZA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA NA WEMA SEPETU

May 10, 2018
Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, leo imetangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu.

Ushirikiano huu ni mwendelezo wa mpango mkakakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania katika kuboresha maisha yao. Kusudi hasa la Tatu Mzuka kama ilivyoelezwa ni kusambaza fursa kwa watu wengi kadri inavyowezekana ili kubadilisha maisha yao.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alisema kwamba ushirikiano huu ni mmojawapo kati ya nyingi ambazo Tatu Mzuka wanajihusisha nazo.‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.‘Ninawashukuru sana Tatu Mzuka kwa ushirikiano huu, ambao hakika sio tu utanigusa mimi bali mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla wao katika kujitengenezea fursa za kuboresha maisha yao’ alisema Wema.

Wema alisema kwa kuanza, anaomba mashabiki zake wachangamkie fursa ya kucheza Tatu Mzuka, ambapo kama unatumia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, unaingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111 na baada ya hapo unaweka namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na jina langu WEMA na baada ya hapo ingiza kiasi unachotaka kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000.

‘Pamoja na kujiongezea nafasi za kushinda za kawaida za Tatu Mzuka kila saa hadi milioni 6, kila siku unaweza kushinda milioni 10 pamoja na zaidi ya milioni 140 kila Jumapili, utapata fursa zaidi ya zawadi mbalimbali kutoka kwa Wema’ alisema Wema. Pamoja na utambulisho wa Wema, Tatu Mzuka pia ilitangaza kwamba Jumapili hii ya tarehe 13 ambayo ni siku ya mama duniani kuna milioni 140 ambayo lazima itolewe kwa mtu mmoja pamoja na mama yake.

‘Hii ni fursa kwa kila mtanzania ambaye kwa namna moja ama nyingine angependa kumshukuru mama yake au mlezi wake kwa kazi kubwa aliyofanya, na hivyo ukicheza sasa, unaingia kwenye Mzuka Deile ambayo inafanyika kila siku Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo milioni 10 lazima itoke kwa mtanzania mmoja na yeye atamgawia mama yake milioni 3, wakati Jumapili hii kwenye Mzuka Jackpot yeyote atakayeshinda milioni 140 atambusti mama yake kwa milioni 30’ alihitimisha Maganga
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu pichani kushoto.

‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.

Bi Wema Sepetu akizungumza mbele ya waanidishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano nae wa kibiashara .

Wema Sepetu akifurahia jambo mara baada ya kutangazwa ushirikiano wake na kampuni ya The Netwek-ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.