MBUNGE WA TANGA MUSSA MBARUKU ATEMBELEA KITUO CHA TV CHA TANGA

August 20, 2017
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha Television cha Jiji la Tanga (Tanga TV) akiwa na wajumbe wa kamati ya Mfuko wa Jimbo kuangalia fedha za mfuko wa Jimbo zilivyotumika kulia ni Meneja wa kituo hicho,Mussa Labani
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akimsikiliza Afisa Mipango na Uchumi wa Jiji la Tanga ambaye pia ni Katibu wa Mfuko wa Jimbo,Ramadhani Possi mara baada ya kusaini kitabu hicho
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akiwa na wajumbe wa kamati hiyo wakiorozesha baadhi ya vitu wakati wa ziara hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika akimsikiliza Meneja wa kituo hicho,Mussa Labani kushoto
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku wa pili kutoka kushoro akipewa maelekezo na Meneja wa Kituo cha Tanga TV Mussa Labani

 Afisa Mipango na Uchumi wa Jiji la Tanga ambaye pia ni Katibu wa Mfuko wa Jimbo,Ramadhani Possi wa pili kutoka kushoto akimuonyesha jambo  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
Picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara hiyo

Tanzania rated Africa's best safari country of 2017

August 20, 2017
THE NETHERLANDS – SafariBookings.com has conducted an in-depth analysis of reviews from safari tourists and acclaimed Africa experts to determine the continent’s best country for safaris. And the winner? Tanzania came out on top – the country is the clear winner and has been awarded our best safari country for 2017.
More than 2,500 reviews were used in this comprehensive research. Contributions came from safari-goers all over the world. And 22 reputable guidebook authors – working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint, who make-up the SafariBookings expert panel – also contributed reviews.

MICHUANO YA "IKUNGI ELIMU CUP 2017" YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI IKUNGI

August 20, 2017
Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt.Angeline Lutambi, akizungumza kwenye ufunguzi wa michuano ya soka ya "Ikungi Elimu Cup 2017" kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.

Michuano hiyo ilizinduliwa jana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Ikungi, lengo ikiwa ni kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za elimu wilayani Ikungi ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, nyumba za waalimu pamoja na vyoo.

Wazo hilo liliibuwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu ambaye ni mlezi wa mfuko wa elimu Ikungi ulioanzishwa ulioanzishwa kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa changamoto za kielimu wilayani humo.


BMG Habari
Michuano ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” imezinduliwa kwa kishindo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida baada ya mamia ya wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na kuendeshwa na Chama cha Soka wilayani Ikungi, ilizinduliwa jana Agosti 19,2017 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi huku ikitarajiwa kushirikisha timu 69 wilayani humo.

Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt.Angeline Lutambi, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye alipongeza wazo la kuanzishwa kwa michuano hiyo inayolenga kuhamasisha wananchi pamoja wadau mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Ikungi ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu ambaye ni mlezi wa mfuko wa elimu Ikungi, alisema michuano hiyo itasaidia upatikanaji wa shilingi bilioni tatu kupitia mfuko wa elimu Ikungi katika kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa kero za elimu wilayani huo.

Uzinduzi wa michuano hiyo, ulikwenda sambamba na uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara uliokwama tangu mwaka 2009 katika shule ya sekondari Ikungi hii ikiwa ni uzinduzi rasmi wa zoezi kama hilo kwenye kata zote wilayani Ikungi ambapo kila Kata imepewa jukumu la kufyatua matofali elfu kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.

Katika zoezi hilo, walijitokeza wadau pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wenyeviti wa halmashauri, jeshi la polisi, Tanesco na wanachi ambao walimuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Mtaturu aliyekabidhi mifuko 100 ya simenti na wao wakachangia fedha taslimu zaidi ya shilingi 800,000 na ahadi zaidi ya shilingi 1,900,000, ahadi za simenti mifuko 194 na mchanga wa moramu malori matano kutoka kwa mdau wa maendeleo wilayani Ikungi Hussein Sungita.

Aidha mgeni rasmi aliwakabidhi shilingi laki moja kila mmoja, jumla ya wanafunzi 16 wa kidato cha sita shule ya sekondari Ikungi waliopata daraja la kwanza kwenye mtihani wao ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu aliyoitoa wakati wa mahafali ya wanafunzi hao huku akiwaahidi walimu shilingi milioni moja kwa kila wanafunzi 10 wenye madaraja ya kwanza.

Nazo timu 69 zinazoshiriki michuano hiyo ya “Ikungi Elimu Cup 2017” zilipokea vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya michuano hiyo ambapo jana zilipigwa mechi mbili za kirafiki, ya kwanza ikiwa ni kati ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Ikungi ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare tasa.

Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Ikungi United dhidi ya Puma ukimalizika kwa puma kuwashangaza Ikungi waliokuwa wanaongoza kwa bao mbili hadi kipindi cha kwanza, baada ya kusawazisha na kujipatia bao la ushindi katika kipindi cha pili na hivyo matokeo kuwa Puma 3-2 Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mgeni rasmi akishiriki shughuli ya ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Ikungi ikiwa ni uzinduzi wa shughuli kama hiyo katika Kata zote wilayani Ikungi ambazo zitashiriki kufyatua tofali elfu kumi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe. Miraji Mtaturu akishiriki zoezi la ufyatuaji matofali
Matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2009
Mwenyekiti wa wa halmashauri ya Ikungi akishiriki zoezi hilo
Zoezi la ufyatuaji matofali ukiendelea ambapo viongozi mbalimbali walishiriki
Katibu wa CCM mkoa wa Singida akishiriki zoezi hilo
Mkuu wa wilaya ya Ikungi (kulia) akipokea michango ya papo kwa papo kutoka kwa viongozi mbalimbali waliojitokeza kumuunga mkono katika kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu wilayani humo kupitia mfuko wa elimu Ikungi
Mkuu wa wilaya ya Ikungi (wa pili kushoto) Miraji Mtaturu akikabidhi mifuko 100 ya simenti aliyoahidi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambapo wadau wengine walimuunga mkono kwa kuchangia mifumo mingine 194 na hivyo jumla ikapatikana mifuko 294
Msingi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Ikungi ambao ujenzi wake umekwama tangu mwaka 2009 huku mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Mhe.Tundu Lissu akilalamikiwa kukwamisha ujenzi huo baada ya kuwazuia wananchi kutoshiriki kwenye michango mbalimbali ya maendeleo
Mgeni rasmi akiwakabidhi wanafunzi 16 wa kidato cha sita waliopata daraja la kwanza katika shule ya sekondari Ikungi shilingi laki moja, ikiwa ni ahadi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi aliyoitoa kwa kila mwanafunzi atakayepata daraja hilo. Wanafunzi 16 walipata daraja la kwanza kwenye mtihani wao wa kidato cha sita. Pia waalimu waliahidiwa shilingi milioni moja kwa kila wanafunzi 10 wenye daraja la kwanza.
Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Ikungi akipokea shilingi laki moja baada ya kupata daraja la kwanza kwenye mtihani wake
Timu zote 69 zinazoshiriki michuano ya Ikungi Elimu Cup zilipatiwa vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira miwili
Timu shiriki za Ikungi Elimu Cup zikipatiwa jezi na mipira kwa ajili ya ligi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi (kulia) na mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi (kushoto) wakiingia uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki na timu ya Manispaa ya Singida
Mkuu wa wilaya ya Ikungi akipiga penati kama ishara ya ufunguzi wa michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017
Go Goo Goooooooo!
Mgeni rasmi akiwa na kikosi cha timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida kilichocheza na timu ya madiwani wa Halmashauri ya Ikungi kikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ikungi na matokeo yakawa ni suluhu ya bila kufungana
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi cha madiwani wa halmashauri ya Ikungi kilichocheza na kikosi cha madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida na matokeo yalikuwa ni suluhu ya bila kufungana
Baadaye kuliwa na mchezo kati ya timu zinazoshiriki ligi ya Ikungi Elimu Cup ambapo Ikungi United walicheza na Puma na Ikungi wakakubali kufungwa bao 3-2.
Ikungi United na Puma zikisalimia kabla ya kuanza kuchuana kwenye mchezo wa kirafiki kuelekea kwenye ligi ya Ikungi Elimu Cup 2017. Matoke yalikuwa ni Puma 3-2 Ikungi
Katibu wa CCM ikungi akifurahia ngoma ya asili iliyotumbuizwa na kikundi cha Nyota Njema
Kamanda wa polisi mkoani Singida, Debora Magirigimba aliwataka vijana kujikita kwenye michezo na kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya huku pia akiwaonya wanaowapa mimba wanafunzi na kwamba atakaebainika kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi atachukuliwa hatua kali za kisheria
Ikungi Elimu Cup-Changia, Boresha Elimu Ikungi
BMG Habari

Thanda: Kisiwa kinachopatikana Tanzania ambapo kulala usiku mmoja inagharimu zaidi ya shilingi milioni 22!

August 20, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Inawezekana usiamini kwamba kuna sehemu zinagharimu zaidi ya shilingi milioni 22 za kitanzania kulala kwa usiku mmoja tu! Amini au usiamini sehemu hizo zipo, tena hapa hapa nchini kwetu Tanzania.

Jumia Travel ingependa kukujulisha kwamba kupitia shughuli za kitalii, hakuna kinachoshindikana. Linapokuja suala la kujionea mazingira adimu na ya kuvutia au wanyama wa aina mbalimbali, gharama au umbali wa kuyafanikisha hayo huwa siyo masuala ya msingi.

DKT ANGELINE LUTAMBI AZINDUA “IKUNGI ELIMU CUP 2017” AMFAGILIA DC MTATURU KWA UBUNIFU

August 20, 2017
Na Mathias Canal, Singida
 
SERIKALI imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, Nyumba za walimu, Maabara, Matundu ya vyoo na mabweni.

Ili kunusuru kadhia hiyo imeelezwa kuwa moja ya mikakati ni pamoja na wakuu wa Wilaya kuwashirikisha wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi wawe na furaha na amani. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu yanayojulikana kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017” itakayofanyika katika vijiji vyote 101 vilivyopo katika wilaya ya Ikungi.

Mashindano hayo yaliyoanza leo Agosti 19, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi yanataraji kufika ukomo siku ya Jumanne Septemba 19, 2017 kwa matazamio ya kuwafikia zaidi ya wanachi 5000 katika Wilaya hiyo.

Dkt Lutambi alisema kuwa Mashindano hayo yenye kauli mbiu isemayo “CHANGIA, BORESHA ELIMU IKUNGI” yamebeba mtazamo chanya wa elimu wenye manufaa kwa wananchi katika kizazi cha sasa kuelimika na kizazi kijacho.

Alitumia nafasi hiyo pia kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku akiwaeleza wananchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alichagua mtu muhimu kumuwakilisha katika Wilaya hiyo kwani ubunifu wake katika utendaji una manufaa makubwa kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Awali akisoma taarifa ya uzinduzi wa Mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa mashindano hayo ambayo yatakuwa yanalenga kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia vitu mbalimbali kwa ajili ya kuboresha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, maabara ya masomo ya sayansi kwa shule za sekondari, Madarasa kwa shule za msingi pamoja na vifaa vya kujifunzia.

Sambamba na mashindano hayo ya mpira wa miguu lakini pia umezinduliwa ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya masomo ya Sayansi ambazo zipo katika hatua za msingi kwa muda mrefu.

Aidha, zimetolewa zawadi kwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza (Division One) katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka huu 2017 na walimu wao ikiwa ni ahadi iliytolwa na mkuu wa wilaya hiyo.

Mhe Mtaturu aliahidi kutoa shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayepata Daraja la Kwanza na shilingi milioni moja kwa walimu kwa wanafunzi 10 watakaopata Daraja la Kwanza.

MWISHO


Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisoma taarifa ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017” mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akibeba tofali lililofyatuliwa na Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Ndg Jimson Mhagama akibeba tofali lililofyatuliwa wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Kikosi cha Timu ya Ikungi United
 Kikosi cha Timu ya Puma Combine kilichoshinda goli 3 kwa 2 dhidi ya Ikungi United
Moja ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kwa kupata Daraja la kwanza akipokea shilingi 100,000 ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu
Matofali ambayo yamefyatuliwa na wadau wakati wa ufunguzi wa ufyatuaji matofali Wilayani Ikungi

Mipira iliyotolewa kwa jili ya timu zote washiriki wa “Ikungi Elimu Cup 2017”


SHAKA ASIFU UZALISHAJI WA ZAO LA KARAFUU, ASEMA SERIKALI ILINDE ASILI YA ZAO HILO

August 20, 2017
Zao la Karafuu
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akipanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza Mazingira wakati wa ziara yake katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwasili katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya kujionea hali ya upandaji miti aina ya Mikoko unavyoendelea.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo na Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Zao la Karafuu likiwa limehifadhiwa ghalani chini ya Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar
Vijana wakijishughulisha na shughuli za ubabeji mizigo katika ghala la kuhifadhia zao la Karafuu, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza maelezo mbalimbali ya Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Na Mathias Canal, Pemba

Zanzibar ni maarufu kwa uzalishaji wa karafuu ulimwenguni kwa zaidi ya  karne mbili sasa. Uzalishaji huo ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia tani 35,000 mwaka 1830 na kumiliki soko la karafuu duniani kwa asilimia 90.

Iliongoza katika uzalishaji wa zao hilo kuanzia mwaka 1830 hadi 1940 kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Indonesia.Tathmini iliyofanywa hivi karibuni ya Sensa ya Miti (Woody Biomass Survey 2013) imeonesha kwamba Zanzibar kwa sasa ina idadi ya mikarafuu 4,131,783, ambapo Unguja pekee ina zaidi ya mikarafuu 277,196 na Pemba zaidi ya mikarafuu 3,854,587.

Tathmini ya mwaka 1997 ilionesha idadi ya mikarafuu 790,400 kwa  Unguja na mikarafuu 5,042,700 kwa upande wa Pemba, ikifanya idadi ya mikarafuu yote kuwa ni 5,833,100

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amelitaja zao la karafuu kuwa ni zao muhimu kwa uchumi wa taifa ambalo huongeza kwa kiasi kikubwa kipato kwa wananchi.

Alisema katika kuimarisha zao la karafuu Zanzibar, pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kuna haja ya kupandwa mikarafuu na minazi maskulini, ili wanafunzi waweze kupata uwelewa zaidi wa kutunza na kulienzi zao hilo, kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Shaka alisema hayo wakati alipotembelea na kupanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza Mazingira ili kuhuisha uoto wa asili na kuepuka mmomonyoko wa ardhi katika eneo la Mwambe lenye asili ya Watumbatu Wilaya ya Mkoani na Mkoa Ni Kusini PEMBA .

Pia aliwasisitiza wananchi kuhusu kupanda miche ya mikarafuu na minazi na kutotupa taka ovyo ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

Alisema kuwa serikali inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa inaandaa sheria kali itakayokuwa maalumu kwa kuwachukulia hatua wananchi wanaokata miti ovyo kinyume na utaratibu.

Katika hatua nyingine Shaka alitembelea shirika la Taifa la Biashara Zanzibar kujionea hali ya ununuzi wa zao la karafuu ambapo alimpongeza Mdhamini wa wa shirika hilo Ndg Seif Suleiman Kassim kutokana na kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa zao hilo ambapo katika msimu huu hadi kufikia Mwezi Julai 13, 2017 tayari 2203 sawa na Kilogramu 99180.0 zilikuwa zimehifadhiwa kwa ajili ya kupelekwa Unguja.

Alisema uzalishaji wa zao la karafuu, katika Wilaya ya Mkoani unaongoza kwa zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji wa zao hilo kwa zanzibar, na amewataka wananchi kuendelea kutunza mikarafuu, kwani ndio pato la Taifa.

Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.

Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.