WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA

September 29, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)


Na Kahema Emanuel,Mbeya
Wito umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.
Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 
Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi octobar.
Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.
Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
Mwisho.

Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.




Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG


Daniel Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .




Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.



HIVI NDIVYO WANANCHI WALIVYOKUWA WAKIMPA MKONGOTO KIBAKA LEO BARABARA 15

September 29, 2015




FASTJET YAONGEZA SAFARI ZAKE KWENDA JOHANNESBURG SASA NI KILA SIKU

September 29, 2015

 Mkuu wa Biashara wa Fastjet Lan Petrie (kulia), akizungumza katika semina hiyo.
 Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia), akizungumza katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, iliyohusu kuongezeka kwa safari za ndege za shirika hilo kila siku kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.
 Ofisa Mtendaji wa Masula ya Biashara wa Fastjet, David Chacha, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari katika semina hiyo.
 Ofisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza kwenye semina hiyo.
Hapa semina ikiendelea.
MAMA SAMIA SULUHU :MGOMBEA MWENZA ALIYEPANGA KUWAPIGANIA WANAWAKE

MAMA SAMIA SULUHU :MGOMBEA MWENZA ALIYEPANGA KUWAPIGANIA WANAWAKE

September 29, 2015
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
 MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe. 
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa. Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT).Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.[/caption] Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. Kwa sasa kiongozi huyu anazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kuinadi ilani ya CCM. Bi. Suluhu anasema ilani ya CCM imepanga kufanya mengi mazuri kwa Watanzania, lakini pamoja na hayo amejitolea kuhakikisha anawapigania akinamama endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto anuai ambazo zimekuwa kero na kikwazo kwao. Anazitaja changamoto hizo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi ambapo akinamama wengi na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha katika eneo hilo. Anasema licha ya ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kufafanua zaidi itakavyo boresha huduma za afya kiujumla, lakini atalisimamia na kuongeza nguvu za ziada kuhakikisha akinamama wanapata huduma za kuridhisha maeneo wanapopata huduma za afya ya uzazi. Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mbulu Mjini anasema endapo CCM itashinda uchaguzi huu imepanga kuajiri watumishi 15,000 wa sekta ya afya wakiwemo madaktari 2020 ndani ya kipindi kifupi ili kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya maeneo mbalimbali nchini hasa huduma za akinamama na watoto. Bi. Suluhu anasema hatua hiyo ni mpango maalumu wa kuboresha huduma za afya kiujumla na hasa huduma za akinamama wajawazito na watoto ambapo wamekuwa na changamoto katika huduma hizo. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.
Aidha anaongeza kuwa mpango mwingine ni kuwawezesha akinamama na vijana kiuchumi kupitia vikundi vyao. Anabainisha kuwa eneo hili Serikali ya CCM kupitia ilani yake imetenga shilimi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo zitakuwa zikikopeshwa makundi hayo kwa masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Anasema eneo hilo pia halmashauri zitasimamiwa kutoa asilimia tano ya mapato kuwaunga mkono akinamama na vijana ili kuchochea maendeleo yao. Ili kukuza biashara zao Bi. Suluhu anasema Serikali itasimamia kuhakikisha asilimia 30 ya tenda ndogondogo za halmashauri mbalimbali zipewe vikundi vya akinamama na vijana. Anaeleza kuwa ili kuongeza thamani kwa mazao yatakaokuwa yakizalishwa na vikundi hivyo kupitia miradi ya kilimo imepanga kujenga viwanda vingi maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vitayaongezea thamani mazao na pia kuzalisha ajira kwa asilimia 40, jambo ambalo pia litakuza uchumia wa akinamama na vijana. Mwanamama huyo shupavu anabainisha kuwa kutokana na suala la kero ya maji pia kuwaumiza zaidi akinamama ilani ya chama chake imedhamiria kumalizia miradi ya maji na kuanzisha mingine anuai ili kukabiliana na changamoto ya kero ya maji safi na salama iliyopo maeneo mbalimbali ya nchini vijijini ama mjini. Bi. Suluhu anasema Serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi. Lakini ili kumaliza kabisa kero hiyo anasema Serikali itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama. Anasema migogoro yoyote inayosababisha mapigano idadi kuwa inayoathirika ni wanawake na watoto, hivyo Serikali itakayoundwa na CCM itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na Wilaya na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi inayochangia mapigano ya wakulima na wafugaji baadhi ya maeneo ya Tanzania mara kwa mara.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
Anasema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro. Hata hivyo katika kampeni zake mara zote amemalizia kwa kuwaomba wananchi kutunza amani iliyoasisiwa na viongozi wetu wa taifa kwa kutokubali kuyumbishwa na kushawishia kuvuruga amani ya nchi. "...Tusikubali kuchokozwa na kuchokoseka na kuvuruga amani...bila amani hakuna maendeleo," alisema Bi. Suluhu. Anawataka viongozi wa siasa kuacha kutoa vitisho kwa wapiga kura kwani hali hiyo ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye. Miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kulingana na taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni pamoja na CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NCCR- Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, TADEA, TLP, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, CHAUSTA, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

ASHIKILIWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA MAUAJI

September 29, 2015
Na Mwandishi Wetu,Muheza

JESHI la Polisi mkoa wa Tanga linamshikilia mkulima mmoja na mkazi wa Kijiji cha Machemba wilayani Muheza John Dastan (30) kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Abdi Godatha (54) kwa kumpiga fimbo kichwani.

Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake jana,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Zuberi Mwombeji alisema lilitokea Septemkba 28 mwaka huu majira ya saa 5.00 usiku huko kwenye kilabu cha pombe katika kijiji cha Machemba Kata ya Mkanyageni.

Kamanda Mwombeji alisema kwamba indaiwa siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa akinywa na mtuhumiwa waliingia katika ubishani na ndipo Dastan alipochukua fimbo na kuanza kumpiga nazo maeneo ya kichwani.

“Chanzo kiuu cha mauaji hayo kwa uchunguzi wetu wa awali ni kutokana na ulevi huyu mtuhumiwa alikuwa amelewa na waliingia ubishani na marehemu na ndipo Dastan alipochukua fimbo na kumpiga nazo marehemu kichwani na kusababisha kifo chake”,alisema Mwombeji.

Hata hivyo alisema kuwa Polisi inaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Mwombeji alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kitendo cha kupigana hadharani ni makosa kwa mujibu wa sheria.


BREAKIN NEWZZZ!! - AJALI YA LORI SINZA MORI SASA HIVI JIJINI DAR ES SALAAM!

September 29, 2015

Ajali ya roli imetokea Sinza Mori mida hii baada ya roli hilo kuchomoka tairi ya nyuma lakini hakuna mtu aliyepata madhara katika ajari hiyo pamoja na tairi kwenda mbali zaidi na eneo la tukio,
hata hivyo dereva wa roli hilo amesema alikuwa anaenda kubadilisha ekseli iliyochomoka.CHANZO OTHMAN MICHUZI
Roli lenye namba za usajili T 245 DEZ  limechomoka taili ya nyuma maeneo la Sinza Mori leo barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.. 
 Roli likiwa barabarani ya Shekilango barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.
 Hapo ndipo taili lilipochomoka wakati gari likiendelea kutembea.

MGOMBEA ubunge CCM -Namelock Sokoine AHIDI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI MONDULI

September 29, 2015

Na Mahmoud Ahmad,Monduli
Mgombea ubunge wa jimbo  Monduli Bi,Namelock Sokoine kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi (ccm)  amewaahidi wananchi pindi watakapo mpa ridhaa ya kuwa mgunge wao atahakikisha anamaliza kabisa migogoro ya ardhi katika jimbo hilo ambayo imekuwa kero ya muda mrefu na hata kupelekea  hata mifugo kuwa kutokana na hali hiyo na kupunguza jitihada za za waanchi kujiletea maendeleo yao kupitia kilimona ufugaji.
Hayo ameyasema jana katika uzinduzi wa kampeni ya ubunge katika jimbo la Monduli  iliyofanyika katika viwanbja vya soko la Nanja katika kata ya Nanja iliyoko wilaya ya Monduli ,mkoani Arushana kuhudhuriwa na maelfuya watu katika viwanja hivyo.
Hata hivyo aliongeza kuwa endapo wananchi watamchagua atataua matatizo yao yote kwa ikiwemo viwanja vyote vya monduli vitapimwa ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima ambayo imekuwa ikiwagharimu wananchi wake na kusababisha matatizo mbalimbali ameahidi kuyatatu kwa kipindi kifupi mara baada ya kuapiushwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Bi,Namelock alisema  jimbo la monduli limekuwa na tatizo loa uhaba wa maji ambayo ameahidi kulitatua kwa kiindi kifupi na suala la maji kulipa kipaumbele ili kuweza kuondoa kero ya maji katika jimbo hilo ili kuweza kuongeza shughuli za uzalishaji mali ili kuweza kuwaongezea kipato wananchi wake na kupambana na adui umaskini uliopo.
Mbali na hayo mgombea huyo ameahidi neema kwa wakazi na monduli na viunga vyake na ataweza kujenga kiwanda cha ngozi ili kuweza kuwanufaisha wafugaji pindi wanapovuna mifugoyao kwa matumizi mbalimbali kuweza kutumia kiwanda hicho kwa kuongeza ngozi thamani ili kuweza kupata bei kubwa ya ngozi kwa viwanda vya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza kipato cha mfugaji na kujiongezea kipato kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Mbunge Namelock ameahidi kutoa kipaumbele kwa vijana  kupewa viwanja katika jimbo hilo ili kuweza kuwawezesha kujiendeleza na kupata  makazi bora na yakisasa ili kuwarahisishia ugumu wa maisha ya sasa na badae kwa vcizazi vyao sambamba na kuboresha sekta ya afya na elimu ili kumkwamua katika maisha ya sasa.
Awali akizindua kampeni hiyo ya mbunge huyo,Waziri wa Katiba na sheria Bi,Asharose Migiro  aliwataka wapiga kura kuweza kuchagua wagombea wa chama cha mapinduzi iliuweza kuletewa maendeleo yao kuanzia ngazi ya kata hadi jimbo ili kuweza kutataua changamoto mbalimbali katiuka eneo hilo ikiwemo uhaba wa chakula,mikopo kwa akina mama na vijana hususani a boda boda ili kuweza kuwapatia mikopo ya haraka ili kuwezaq kujiletea maendeleo yao kwa kuzalisha mali na kufanya biashara mbalimbali na kuweza kujiajiri kupambana na ukosefu wa ajira ulioko sasa.
Ambapo alisema kuwa wagombea wa ccm anatekeleza iolani ya chama chao kwa kuwaletea maendeleo ya haraka kulingana na mahitaji yao na changamoto zilizoko katika maeneo yao na hata kuendeleza ilani hiyopale ilipofikia kwa kuwaletea maendeleo yao.
Ambapo alitolea mfano ndchi nyingi za Afrika hajizamaliza kutatua matatizo katika jamiii zao lakini kinachofanyika nimuendleo na mikakakati thabiti ya ushirikiano wa kutatua matatizo ya wananchi wao  na mbali ya hivyo azma ya Serikali ya Tanzania nikurejesha mashamba yote kwa wananchi hasa maeneo ya wafugaji ili kuweza kulisha mifugo yao na kuongeza jitihada za dhati katika kuzalisha mifugo yao na kuondoa migogoro isiyo ya lazima baina ya wafugaji na wakulima iliyoko sasa.
Pia amewataka wananchi kuweza kchagua Namelock siku ya uchaguzi kwani yy ndie mbunge pekee ambae anaweza kutekeleza ahadi zake kwa makini kwa kushirikaina na Serikali na viongozi wake na kuweza kutafuta vyanzo mbadala vya umeme ili kuweza kuwaletea wananchi maedneleo na kuweza kuendnakarne ya sayansi na teknolojia iliyokosasa.
Kwa upande wake mmoja wa kada wa ccm Bi,Vaileth Mfuko  wakiwa wanamnadi mbunge huyo aliwataka wapiga kura kuweza kumchagua mbunge huyo kwani ni kiongozi bora ambae atawaletea mabadiliko na maendeleo ya kweli katika jimbo hilo kwani awali alishatoa vifaa vya kisasa vya hospitali katika jimbo hilo na kuboresha sekta ya Afya na wananchi hao kupata huduma kwa wakati na ambazo wanahitaji.
MKUTANO WA WADAU WA MADAWA ZANZIBAR WAFANYAIKA ZANZIBAR BEACH RESORT

MKUTANO WA WADAU WA MADAWA ZANZIBAR WAFANYAIKA ZANZIBAR BEACH RESORT

September 29, 2015

???????????????????????????????????? 
NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
………………………………
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeandaa miongozo ya utoaji huduma bora katika kufanikisha  Mpango wa uwiano wa Itifaki ya pamoja kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa ZFDB  Dkt. Burhani Othman Simai ameeleza hayo katika Mkutano wa wadau wa Madawa Zanzibar ulioandaliwa na Mpango wa Udhibiti wa bidhaa za Chakula na Dawa wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema kuanzia sasa bidhaa zote za chakula na madawa za  Zanzibar na zinazotoka nje  zitasajiliwa na Bodi yake na Viwanda vinavyotengeneza bidhaa hizo vitafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa  bidhaa hizo.
Aliongeza kuwa katika kufanikisha mpango huo,  Zanzibar inategemea kupata ithibati ya Kimataifa (ISO Certification) mwezi Disemba na kuanzia Januari 2016 maombi na kazi zote za udhibiti wa bidhaa za chakula na madawa zitafanywa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya ZFDB.
Dkt. Burhani  aliwataka wadau wa bidhaa za chakula na madawa kutoa ushirikiano kwa  Bodi kwa kujisajili  katika Ofisi  yao  iliyopo Mombasa kwa Mchina na kuandaa utaratibu mzuri wa kurahisisha ukaguzi wa  bidhaa na viwanda vyao.
Alisema taratibu hizo zinazochukuliwa na ZFDB zinalengo la kulinda afya za wananchi wa Zanzibar na Nchi wa wananchama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mwakilishi kutoka Sekriteriati ya Jumuia ya Afrika Mashariki Mjini Arusha Mwesige John Patrick aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha Mpango wa uwiano wa Nchi wanachama wa Jumuia hiyo.
Alikumbusha  kuwa Mpango huo ulioanza mwaka 2012 kwa awamu ya kwanza ya miaka mitatu, ukizishirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Ruwanda  umeanza kuleta mafanikio makubwa kwa nchi zote  wanachama na mwaka huu umeanza awamu ya pili ya miaka miwili.
Akifungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulid ameitaka ZFDB kuendelea kusimamia mpango wa uwiano wa Udhibiti wa Bidhaa za chakula na dawa  na kuhakikisha zinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu.
Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwafahamisha wadau wa Zanzibar miongozo mipya iliyoandaliwa kwa pamoja na wataalamu wa Mamlaka za udhibiti wa Chakula na Dawa wa Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
WADAU WAWEKA MIKAKATI KUUPA HADHI MUZIKI WA REGGAE

WADAU WAWEKA MIKAKATI KUUPA HADHI MUZIKI WA REGGAE

September 29, 2015

1
 Msanii mkongwe wa muziki wa reggae na Mkurugenzi wa Reggae Production House Innocent Nganyagwa akiongea na wadau wa muziki huo mapema wiki hii kwenye programu maalum ya kujadili hatma ya muziki wa reggae iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame na Katibu wa chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli .
2
 Katibu wa chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa muziki wa reggae (hawako pichani) kwenye programu maalum ya kujadili hatma ya muziki huo. Kushoto kwake ni Msanii mkongwe wa Reggae Innocent Nganyagwa.
3
 Ras Bumijah Zinyongwa ambaye pia ni kiongozi wa Tanzania Rastafarai Movement (TARAMO) akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyoibuka kwenye programu hiyo.
4
Msanii mkongwe wa muziki wa Band John Kitime akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kuhusu umuhimu wa Wasanii kujiunga na Shirika la Bima la Taifa (NHIF) ili kujihakikishia matibabu na kuepuka kuombaomba wakati wanapougua.
5
Msanii mkongwe wa reggae Innocent Nganyagwa akionesha makali yake ya muziki wa Reggae wakati akitoa burudani kwa wadau wa Sanaa waliohudhuria programu mahsusi ya kujadili hatma ya muziki huo nchini.
6
Sehemu ya wadau waliohudhuria programu hiyo wakifuatilia mjadala.
……………………………………………………………………………….
New Picture  
Wadau wa muziki wa reggae nchini kwa kujengewa mazingira na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wameweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha wanaurudisha jukwaani muziki huo na kuainisha changamoto mbalimbali zinazoukabili. Akizungumza mapema wiki hii kwenye programu maalum iliyolenga kuujadili muziki wa reggae na kuja na mikakati ya kuurudishia hadhi iliyoandaliwa na BASATA, Msanii mkongwe wa muziki huo Innocent Nganyagwa alisema kwamba wasanii wa muziki huo kwa sasa wamejipanga kuurudisha jukwaani muziki huo kupitia kufanya maonesho maeneo mbalimbali nchini. “Tumejipanga kufanya maonesho ya muziki wa reggae katika mikoa mbalimbali nchini, tutakuwa na kundi la wasanii ambao kazi yao itakuwa kufanya maonesho ya hisani na kuurudisha jukwaani muziki huu ambao kihistoria ni muziki mama” alisema Innocent Nganyagwa. Aliitaja mikoa ambayo maonesho hayo ya reggae yatafanyika kuwa ni pamoja na Mbeya, Ruvuma, Iringa, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na mingine ambayo maandalizi bado yanaendelea ili kuhakikisha wanawafikia wapenzi wengi zaidi wa muziki huu ambao huko nyuma ulipata kuwa na mvuto mkubwa. Mikakati mingine iliyowekwa ukiacha kufanya maonesho mbalimbali nchini ni pamoja na wasanii wa reggae kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika kujitangaza, kuanza kuuza kazi zao kupitia mitandaoni, kubuni kazi zenye ujumbe unaoendana na soko na kuacha kuganda na falsafa ya reggae ni muziki wa ukombozi. Awali wakibainisha changamoto mbalimbali zinazoukabili muziki huo, wadau wengi walisema kwamba muziki huu unasuasua kutokana na vituo vingi vya radio kuupa kisogo, watanzania wengi kuuhusisha na imani za urasta kitu ambacho si sahihi na zaidi wadau muhimu hasa makampuni ya biashara kutoujali katika ufadhili. “Muziki huu wa reggae si wa marasta pekee, bahati mbaya watu wengi wamekuwa wakiuhusisha na imani za kirasta. Hapana. Muziki huu unafanywa na mtu yeyote na ni muziki kama ilivyo miziki mingine” alisema Ras Bumijah Zinyongwa ambaye pia ni kiongozi wa taasisi ya Tanzania Rastafarai Movement (TARAMO)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA HAFLA YA UCHANGISHAJI FEDHA KWA AJILI YA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI KATIKA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME YA MTERA, KIHANSI, KIDATU, NYUMBA YA MUNGU NA PANGANI

September 29, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani. Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa Mabibo Beer, Wines & Spirits na Mkurugenzi wa VIP Engineering Marketing Ltd, Benedicta Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPTL, Parthiban Chandrasakaran,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala wa REA, George Nchwale,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.




  Picha na OMR