LUSHOTO YAWEKA MIKAKATI YA KUWAADHIBU WACHAFUZI WA MAZINGIRA.

November 20, 2014
      
                               NA BURHAN YAKUB,LUSHOTO.
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga imeagizwa
kuanza utekelezaji wa utozaji wa faini ya papo kwa papo ya sh 50,000 kwa wale watakabainika kuchafua mazingira.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Magid Mwanga wakati wa  kongamano la kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira lililoandaliwa na Shirika la Wanawake la Utunzaji wa Mazingira nchini (YWCA),kupitia mradi wake wa ‘wajibika’.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na afisa tarafa ya
Lushoto,Asha Hazali,mkuu huyo wa Wilaya alisema  pamoja na jitihada zinazochukuliwa ikiwemo kampeni ya usafi wa kila mwisho wa mwezi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi wakati wote,bado wako baadhi ya watu ambao kwa makusudi wanakwamisa jitihada hizo.

 "Umefika sasa wa sheria kuanza kufanyakazi kwani kama ni suala la elimu limekuwa likitolewa sana na viongozi wa serikali na wanaharakati mbalimbali hivyo kuna kila sababu kwa adhabu kuanza kutolewa"alisema Mwanga .

Akizungumzia kuhusu mpango huo,afisa wa mradi wa
‘wajibika’nchini.Carloline Biseko,alisema kuwa  unawahusisha zaidi vijana, ili waweze kujitambua na kushiriki kikamilifukatika kutunza mazingira.

Kwa mujibu wa Biseko ni kuwa sanjari na masuala ya mazingira vijana pia wana elimishwa juu ya masuala ya ujasirialimali ili waweze ili waweze kutumia fursa zilizopo  kuzalisha mali nakuondokana na umaskini.

Kongamano  hilo liliwashirikisha wasanii na wanafunzi kutoka shule za sekondai za Magamba na Lushoto,ambao walifanya  kazi za kusafisha mazingira ya mji na kupanda miti.

KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL YAISHUSHIA KIPIGO VILLA SQUAD YAIPIGA MABAO 2-0,MKWAKWANI LEO

November 20, 2014
KIKOSI CHA KMC AMBACHO KIMEIFUNGA VILLA SQUAD MABAO 2-0,MKWAKWANI LEO


WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI WAKISALIMIANA LEO
Na Mwandishi Wetu,Tanga.

TIMU ya Soka ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam(KMC) leo imeifunga timu ya Villa Squad "Watoto wa Magomeni"mabao 2-0 kwenye mechi ya Ligi daraja la kwanza iliyochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.

Mabao ya washindi hao yalipatikana kunako dakika za 38 na 67 kupitia kwa wafungaji wake Camara Jongo aliyatumia uzembe wa mabeki wa Villa Squad na kupachika wavuni bao hilo.

Kwenye mechi hiyo bao la pili la lilifungwa na Mohamed Ndonga kwenye dakika ya 67 ambaye alipiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Villa Squad Fadhili Saidi na kujaa wavuni.

MAALIM SEIF ATEMBELEA ENEO LA JENGO LILILOANGUKA JANA MJI MKONGWE ZANZIBAR

November 20, 2014
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Kamanda Ame Ali ambaye ni kiongozi wa shughuli za usafishaji wa eneo lilipoanguka jengo la ghorofa huko Shangani mjini Zanzibar.
 
Na Khamis Haji , OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amezitaka Mamlaka zinazosimamia majengo katika enelo la Mji Mkongwe Zanzibar kuwa na utaratibu mzuri wa kuyakagua ili kuhakikisha uimara wake na kuepusha maafa kwa watumiaji na jamii nzima.
Maalim Seif amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua shughuli za uondoaji kifusi katika jengo lililoanguka jana katika eneo la Shangani mjini Zanzibar, zoezi linalofanywa na askari wa Kikosi cha Zimamoto, Manispaa pamoja na wananchi wa Mji Mkongwe.
Makamu wa Kwanza wa Rais amesema nyumba zilizopo katika Mji Mkongwe zinasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mji Mkongwe au Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, hivyo taasisi hizo ni jukumu lao kuzigagua uimara wake na kuhakikisha ni madhuti.

Amesema pale ambapo taasisi hizo zitabaini kuna nyumba ambazo zimechakaa zinazoweza kuanguka na kuhatarisha maisha ya watu na mali zao ni vyema kuwataka watumiaji wake wahame, ili kuepusha kuangukiwa na nyumba hizo na kuhatarisha maisha yao.
Katika ziara hiyo, ambapo alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jusa Ladhu alivipongeza vikosi vinavyoendesha shughuli za Uokoaji na wananchi wa Mji Mkongwe kwa kazi kubwa ya uokozi wanayoifanya.
Naye Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi Makao Makuu, Ame Ali ambaye anaongoza shughuli za uokozi na usafishaji wa eneo hilo amesema kazi hiyo inaendelea vizuri na walitarajia kuikamilisha leo.
Amesema jengo hilo lililoanguka jana asubuhi lilikuwa halikaliwi na watu kutokana nakukabiliwa na uchakavu na hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa kufuatia tukio hilo
 crdtblog ya wananchi.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE YAENDELEA NDANI YA WILAYA YA NACHINGWEA

November 20, 2014

 Kikundi cha Wakulima cha Umoja Rika wakiinua majembe juu kama ishara ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyefika kwenye shamba hilo la ushirika la Mkotokuyana wilaya ya Nachingwea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wa kikundi cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana ,Nachingwea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakulima wa kikundi cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana,Nachingwea mkoani Lindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha treka kulima shamba la ushirika la Mkotokuyana huku akiwa amempakia Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Ngugu Mathias Chikawe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la Mkotokuyana  wilayani Nachingwea.

 Sehemu ya shehena ya Korosho.  

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia korosho kwenye ghala ambalo hapo awali ilikuwa kiwanda cha korosho cha Nachingwea .
 Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta Ilulu Nachingwea ambacho sasa kinatumika kama ghala ya kuhifadhia vifaa vya umeme.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mandai ambao walieleza shida ya maji,zahanati pamoja na ofisi ya Serikali .

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jiko la kisasa la shule ya sekondari ya Nachingwea High School .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majiko ya kisasa ya shule ya sekondari ya Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Naipanga ambapo alikagua na kushiriki ujenzi , Katibu mkuu wa CCM aliwaambia wananchi wawe mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani Ndugu Mathias Chikawe (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea Ndugu Albert Mnari kuelekea kwenye shamba la ushirika Mkotokuyana  wilaya ya Lindi Vijijini tayari kwa kushiriki shughuli za kilimo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Naipanga Nachingwea.
 Wananchi wa Nachingwea wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha chama mkoani Lindi.


 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia upinzani umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao kushabikia
 Wananchi wakifurahia hotuba ya Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Mama akichukua matukio kwa simu yake wakati mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Soweto wilaya ya Nachingwea.
 Wananchi wakifuatilia mkutano nje ya senyenge ya uwanja wa mikutano wa Soweto wilayani Nachingwea.
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani akielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010  katika jimbo lake kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, Nachingwea.
 Bibi Esha Kanduru mwenye umri wa 89 ambaye alishiriki harakati za uhuru na kujiunga na TANU mwaka 1957 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Soweto, Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali inapokosea mambo na kuchelewa kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso wanapata wananchi, akizungumzia kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa maghala na hakuna mtu serikalini amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Ndugu Mathias Chikawe wakati wa mkutano wa CCM mjini Nachingwea kwenye viwanja vya Soweto.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachma kutoka CUF waliojiunga rasmi na CCM wilayani Nachingwea.
 MKWAJA FC MABINGWA WAPYA WA MWIDAU CUP 2014

MKWAJA FC MABINGWA WAPYA WA MWIDAU CUP 2014

November 20, 2014
Mabigwa wa Mwidau CUF 2014, Timu ya Mkwaja FC wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe. unnamed1 
Mdhamini wa Kombe la Mwidau CUF, Amina Mwidau akiwa na wabunge wenzake, Yussuf Salim (Chambani) na Khatib Said Haji (Konde) unnamed2 
Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timu ya Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake. unnamed3 
Kombe la likiwa mezani huku mchezo wa fainali ukiendelea. Na mpigapicha Wetu
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Pangani
Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza.
Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko . 
 Hata hivyo kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli la pili la timu hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga bao la nne.
Akikabishi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa, medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku mshindi wa pili ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba, seti moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16 zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya soka  katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini.
Katika mchezo huo wa fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.

WATATU WAKAMATWA TANGA KUHUSISHWA NA BIASHARA YA UUZAJI WA NOTI BANDIA

November 20, 2014
KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,FRESSER KASHAI AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI DOLA ZA KIMAREKANA FEKI ZILIZOKAMATWA NAZO WATUHUMIWA HAO



WATU watatu wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa noti bandia mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakiwa na dola za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Kitanzania .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17 mwaka huu saa saba na nusu eneo la barabara ya kumi na sita Kata ya Ngamiani wilayani Tanga  wakati kwenye harakati za kuziingiza kwenye mzunguko.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Polisi wakiwa kwenye gari lenye Chasis namba JLg 100037726 ambazo ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa na noti hizo bandia ambazo walikuwa wamezificha

Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kuwa ni Julius Kanza(30),kabila Mchaga na Mkazi wa Ubungo,Kenedy Binagi(35) mkazi wa Sinza na wa tatu ni Ramadhani  Saddy(33) kabila Muha na mkazi wa Mwenge

Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kukamatwa walikiri kuhusika na biashara hiyo ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelekezi wa awali kukamilika.

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linaendesha msako mkali wa kuwatafuta wahusika wa matukio ya mauaji ya Mkulima mmoja yaliyotokea Kijiji cha Nyadigwa Kata na Tarafa ya Kimbe wilayani Kilindi.

Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo la mauaji hayo lilitokea Novemba 18 mwaka huu majira ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano katika eneo la kijiji cha Vyadigwa Kata ya Kimbe wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo,Kamanda Kashai alisema mkulima wa Vyadigwa alikutwa porini akiwa amejeruhiwa maeneo ya utosini kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana hali iliyomsababishia kifo chake.

Alisema kuwa mkulima huyo alifariki dunia saa kumi jioni wakati akiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Kilindi(KKT) ambapo chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa .

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LEO

November 20, 2014
Release No. 179

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Novemba 20, 2014
 
SDL SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6.
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.

Mechi hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.

 MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA

Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yanayoshirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30 mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.

Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza Desemba 6 mwaka huu, lakini yamelazimika kuyasogeza ili kutoa fursa ya kukamilika kwa matengenezo ya viwanja vitatu ambayo vitatumika.

Kila timu ya mkoa inatakiwa kuwa na ujumbe wa watu 16, wakiwemo wachezaji 14 na makocha wawili katika mashindano hayo ya timu yenye wachezaji saba (7 aside).

Timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu tayari kwa ajili ya uhakiki wa umri na taratibu nyingine za mashindano. Timu zote zitafikia katika shule ya Alliance (Alliance Schools).

Wachezaji wanaotakiwa kushiriki mashindano hayo ni wenye umri chini ya miaka 12, hivyo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 2003 na kuendelea.

 RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Innocent Munyuku na Baraka Karashani vilivyotokea jana (Novemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

 Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu, na tasnia ya habari nchini kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa waliotoa katika ustawi wa mpira wa miguu nchini kupitia kalamu zao.

Munyuku alikuwa mmoja wa waandishi waanzilishi wa gazeti la Mwanaspoti wakati Karashani kwa nyakati tofauti alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kampuni ya New Habari 1996 akiripoti habari za mpira wa miguu.

 Tunatoa pole kwa familia za marehemu, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kampuni ya New Habari 1996 na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

 Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)