WANANCHI KIJIJI CHA MKALAMA WAUNGA MKONO KAMPENI ZA MKUU WA WILAYA YA HAI ZA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

November 04, 2016

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkalama waliojitokeza kuunga mkono kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa iliyozinduliwa hivi karibuni wilayani humo.
Baadhi ya Kina mama wakishiriki shughuli ya usombaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa madarasa katika shule mpya ya Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai.
Afisa tawala wa wilaya ya Hai,Julieth Mushi akishiriki katika zoezi la ubebaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wela akishiriki katika usombaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule mppya ya Kilima Mswaki.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mkalama wilayani Hai wakishiriki kuvunja na kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa madarasa katika shule mya ya Kilima Mswaki iliopo kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa amebeba jiwe kubwa ikiwa ni kuonesha kwa vitendo namna viongozi wa serikali wameamua kushirikiana kwa vitendo na wananchi katika kujiletea maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki katika kuchimba msingi katika shule mpya ya Kilima Mswaki wakati wa kuanza kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wela akishiriki kuchimba msingi katika shule hiyo.
Sehemu ya Msingi ulianza kuchimbwa katika shule mpya ya Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama.
Sehemu ya Mawe yaliyokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule ya Kilima Mswaki .
Moja ya Madarasa yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi katika eneo la Kilima Mswaki kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata shule moja pekee ya Mkalama iliyopo katka kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizunumza katika kikao na wanachi wa kijiji cha Mkalama mara baada ya kushiriki zoezi la uchimbaji na ujenzi wa msingi kwa ajili ya madarasa katika shule ya msingi ya Kilima Mswaki.
Baadhi ya wnachi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu kuchangia katika ujenzi wa madarasa katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Uoendo Wela akizungumza wakati wa kikao hicho.kulia ni mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Bakanwa.
Baaadhi ya Wananchi.
Baadhi ya wananchi wakicahngia fedha katika harambee ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai                             Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

TAASISI YA ANSAF YAWANOA WADAU WA KILIMO KANDA YA ZIWA.

November 04, 2016

Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.

Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuhakikisha kunakuwa na kilimo chenye tija katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili familia ziweze kujikimu kiuchumi na kichakula.
Na BMG
Wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Meneja Mradi wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Diana Lugano, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Wadau wa kilimo wakimsikiliza Meneja mradi wa ANSAF wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Jimmy Luhende ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza, akijitambulisha.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
Picha ya pamoja
************************************************
Upungufu wa maafisa kilimo pamoja na uuzaji wa mbegu zisizo na ubora katika mikoa ya kanda ya ziwa umeelezwa kusababishwa sekta ya kilimo katika mikoa hiyo kuzorota.

Hayo yalibainishwa jana Jijini Mwanza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo uliolenga kujadili namna bora ya kuboresha sekta hiyo.

Walisema baadhi ya maafisa kilimo waliopo katika mikoa ya kanda ya ziwa kushindwa kuwafikia wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo husababisha kilimo kisicho na tisha huku uuzaji wa mbegu za kilimo zisizoota ukikwamisha kabisa juhudi za wakulima kulima zao hilo.

Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la wadau wa kilimo nchini ANSAF na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima, viongozi wa serikali pamoja na taasisi binafsi ambapo pamoja na mambo mengine umeadhimia kufikisha elimu kwa wakulima ili kulima kilimo chenye tija.

SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA MRADI WAKE WA SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI.

November 04, 2016
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTE SAWA lililopo Jijini Mwanza, Angela Benedicto, akizungumza hii leo wakati wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Na BMG

Benedicto amesema Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa nyumbani umelenga kuhamasisha jamii kuondoa aina zote za unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo wanajamii watajengewa uelewa juu ya vitendo vyote vya unyanyasaji na unyonyaji vinavyomuathiri mtoto mfanyakazi wa nyumbani ili kushiriki katika kuvitokomeza.

Aidha ameongeza kwamba mradi huo utaongeza ushiriki wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani katika kujilinda dhidi ya aina zote za unyanyasaji na unyonyaji ambapo unaambatana na ujumbe usemao "Saidia kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani".

Katika mradi huo ambao ni wa muda wa miezi sita, wananchi wataweza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu nambari 0800 71 00 60 bure kabisa.

Wadau waliohudhuria kwenye utambulisho wa mradi huo ni pamoja na Madiwani, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa mitaa, maafisa maendeleo ya jamii, waajiri wa watoto wa nyumbani, watoto waajiriwa wa nyumbani, mawakili, maafisa kazi, maafisa elimu kata, wawakilishi wa dawati la jinsia kutoka vyombo vya ulinzi pamoja na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto ambapo wameahidi kutoa ushirikiano wao ipasavyo ili kufikia malengo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTE SAWA lililopo Jijini Mwanza, Angela Benedicto, akizungumza hii leo wakati wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Zubeda Kimaro, akifungua mkutano wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.

Amelipongeza shirika la WOTESAWA kwa kazi nzuri ya kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani na kuhakikisha kwamba ukatili dhidi yao unatokomezwa kabisa.
Washiriki wa mkutano wa utambulisho wa Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani wakimsikiliza Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Zubeda Kimaro, wakati akifungua mkutano huo.
Jaqueline Ngalo ambaye ni Mwanasheria kutoka shirika la WOTESAWA akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Miradi ya Shirika la WOTESAWA
Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani umefadhiriwa na Taasisi ya The Foundation For Civil Society.

Katika mradi huo ambao ni wa muda wa miezi sita, wananchi wataweza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu nambari 0800 71 00 60 bure kabisa.

NYUKI WAZUA KIZAA ZAA KATIKA MCHEZO WA RUVU SHOOTING NA AFRICAN LYON

November 04, 2016
 Wachezaji wa timu za Ruvu Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon wakiwa wamelala chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo yalikuwa yanapita uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya wachezaji wa akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru kutokana na hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
 'Ni kama wanasema 'Nyuki hao bado wapo tuendelee kujificha chini ya viti"

 Watu wazima chini ya viti 'Chezea nyuki wewe'