MATUNDA YA UWEKEZAJI BANDARI YA TANGA YAIWEZESHA MELI KUBWA YA MZIGO KUTOKA NCHINI URUSI KUTIA NANGA GATINI

February 27, 2023

 Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Tanga mapema leo

 Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Tanga mapema leo

Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha akizungumza na waandishi wa habari leo
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko akizungumza 




Na Oscar Assenga,TANGA.

Matunda ya uwekezaji wa Bandari ya Tanga yameanza kuonekana mara baada ya Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 kutia nanga katika Bandari hiyo

Hatua hiyo ni baada ya kukamilika kwa gati lenye urefu wa mita 300 ambao umeiwezesha meli hiyo kuweza kutia nanga gatini na kuandika historia kwa mara ya kwanza kupokea meli kubwa mpaka gatini na hivyo kuandika historia ya kipekee baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali.

Akizungumza leo wakati wa mapokezi ya meli hiyo ambayo ilikuwa imebaba shehena ya Mbolea kwa ajili ya viwanda ,Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema ujio wa meli hiyo ni matunda makubwa ya uwekezaji ambao umefanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwenye Bandari hiyo.

Alisema kwamba meli hiyo ilikuwa imebeba mzigo wa tani 6909 unaokwenda nchini Kongo ambapo utapakuliwa kwa muda wa siku mbili kuanzia leo Jumatatu.

Aidha Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara kwamba Bandari ya Tanga imeanza kufunguka kutokana na maboresho makubwa hali ambayo imepelekea huduma kuimarika zaidi.

Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko alisema kwamba matunda ya ujio wa meli hiyo ni kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Rais Samia Suluhu.

Alisema uwekezaji huo umewezesha kuandika histoiria katika Bandari hiyo kwa kuanza kuhudumia meli ya kichele gatini jambo ambalo awali lilikuwa halifanyiki.

Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika Bandari hiyo na matokeo yake yameanza kuonekana .

TCDC kuja na mkakati wa kukuza biashara kidijitali

February 27, 2023
Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini (TCDC) imeanza kutekeleza mpango ya kubadili namna ya kuendesha vyama vya ushirika na kuviwezesha kutumia teknolojia za kisasa katika kufanya shughuli zao

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini Abdulmajid Nsekela ametoa taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta ya hiyo hapa nchini

Nsekela amesema uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali itaongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika, pamoja na Mamlaka za Usimamizi wa sekta hiyo.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine lakini mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo yatasaidia kuuboresha mfumo wa ushirika kuwa wa kisasa zaidi na ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo kwa ustawi wao na wa Taifa kwa ujumla.

“Ni matumaini yangu kuwa Maazimio yatakayofikiwa kupitia Mkutano huu yatapaswa kutekelezwa ipasavyo na kila mdau na kwamba taarifa ya utekelezaji itakuwa inatolewa na kujadiliwa mara kwa mara”-amesema Nsekela.
 
Kwa upande wake Mrajisi wa Ushirika nchini Dkt. Benson Ndiege amesema lengo kubwa la mkutano huo wa wadau wa ushirika ni kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo hapa nchini.  

“Mkutano huu ni muhimu kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Ushirika hapa nchini, lakini pia tumekutana wadau wote ili kuja na mapendekezo ya pamoja ya kuendeleza sekta hii kwa maendeleo ya Taifa”- amesema Ndiege.
 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023. 
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya  Ushirika Tanzania (TFC), Charles Jishuri akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023.


Sehemu ya wadau wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), wakifatilia mkutano uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023.