NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA

September 26, 2017
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kulia) akizungumza jambo na Mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili mkoani singida tayari kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Mwenye suti nyeusi) akielekea kujionea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuk.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe alipotembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akikagua ujenzi wa eneo maalamu litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhi umeme kwa ajili ya kusafirisha maji kuelekea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Manyoni katika eneo la Mitoo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe kukagua utekelezaji wa ilani uchaguzi ya CCM 2015-2020
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akisisitiza jambo mbele ya wananchi, Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kulia) akisalimiana na wananchi wa Kitongoji cha Kaloleni mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kujionea hali ya upatikanaji wa maji.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuka (Kulia) akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya vyanzo vya maji.
Mfereji wa Skimu ya Umwagiliaji kijijini Itagata ukiwa katika hatua nzuri za ujenzi
Bwala la Skimu ya Umwagiliaji lililogomewa na wananchi wa kijiji cha Itagata mara baada ya kubaini kuwa linavuja kutokana na mashimo yaliyopo yanayopelekea upotevu wa maji.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itagata, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuhusu namna bora ya kukamilisha Mradi wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji.
 
Na Mathias Canal, Singida

Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi Mkoani Singida ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji upatikanaji wa maji.

Naibu Waziri Mhe Kamwelwe amepokelewa na Mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Ambaye Ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni.

Mara Baada ya mapokezi hayo Mhe Naibu Waziri alianza shughuli ya kukagua Mradi wa chanzo cha maji Kintinku/Lusilile ambapo amewasihi wananchi kutunza mazingira hususani misitu ya asili kwani ndio chanzo cha upatikanaji wa maji.

Mhe Kamwelwe ameelekeza wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji Sambamba na kutoa taarifa za uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji ovyo wa miti na uharibifu wa mazingira.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kufikia Mwaka 2020 wananchi waweze kupata maji kwa urahisi katika maeneo wanayoishi tofauti na hali ya upatikanaji wa maji kwa hivi Sasa kwa wananchi wanaotumia umbali mrefu kutafuta maji.

Aliwasihi wananchi kuvitunza vyanzo hivyo vya maji kwani pindi vitakapoanza kufanya kazi vitapunguza ukali wa uhaba wa upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

Alisema kuwa katika Bajeti ya kipindi Cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Vijijini imetengewa shilingi Milioni 611 huku eneo la Mamlaka ya Mji wa Manyoni ikiwa imetengewa zaidi ya Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya upatikanaji wa maji utakaopelekea Wilaya ya Manyoni kufikia 50% ya upatikanaji wa maji.

Mhe Kamwelwe aliwataka wakurugenzi kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa ukarabati wa miradi ya maji, Uchimbaji wa visima virefu, na Ukarabati wa pampu zinazotumia upepo (Windmill).

Sambamba na hayo pia Mhe Naibu Waziri alikiri kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazosababisha kutopatikana kwa maji ya kutosha ambapo ameahidi kuzifanyia kazi kwa haraka ambazo Ni pamoja na uchakavu wa miundombinu ya mabomba hasa eneo la usambazaji, Taasisi nyingi za serikali kutolipa Ankara zao za za maji, Kupandana kwa gharama za uendeshaji na Mamlaka kutokuwa na vyanzo vyake vya fedha.

Akiwa Kijijini Itagata, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Bwawa na Skimu ya Umwagiliaji, Mhe Naibu Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe aliagiza Uongozi wa Umwagiliaji Kanda ya Kati Dodoma kufika Mjini Singida ndani ya siku mbili ili kubaini changamoto ya kukwama kwa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Itagata lililokataliwa na wananchi kutokana na kuvuja kwake mnamo Septemba 2015 mara Baada ya kukamilika.

Mradi wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji Cha Itagata ukikamilika utaweza kuhudumia Hekta zipatazo 160 katika eneo tambarare kwa ajili ya Kilimo Cha Umwagiliaji hususani zao la mpunga, Mazao ya Bustani na Vitalu vya kuoteshea Miche ya Tumbaku kwani eneo Hilo Lina udongo rafiki kwa Kilimo hicho.

CANADA, UNICEF, TIGO WAWEZESHA KASI UANDIKISHAJI VYETI VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

September 26, 2017
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kutumia fursa waliyoipata ya usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano kufanya hivyo kwa maslahi ya watoto na taifa.
Dkt. Mwakyembe alisema hayo wakati akizundua  mpango huo wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.
Alisema uandikishaji wa watoto utasaidia kuwa na rekodi sahihi ya idadi ya vizazi na vifo ambapo inasaidia serikali katika kuangalia mipango yake na mahitaji ya wananchi katika masuala ya afya, jamii na uchumi.
Aidha vyeti vinavyopatikana pamoja na kuonesha utambuzi wa mtoto, pia vinamsaidia kumpatia haki zake nyingine kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya pama) akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakati wa uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Akihutubia katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo kauli mbiu yake ni Mtoto anastahili cheti za kuzaliwa, mpe haki yake ya kuzaliwa, Waziri Mwakyembe alisema kwamba kampeni hiyo kwa mikoa ya Mtwara na Lindi inatarajia kuwanufaisha watoto zaidi ya 290,000 wenye umri chini ya miaka mitano.
Akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ambaye shughuli hiyo iko katika mkono ya ofisi yake alisema kwamba wananchi wa Lindi na Mtwara walikuwa nyuma katika usajili kama walivyokuwa watu wa Njombe na kutumaini watafanya vyema kama wananchi wenzao walivyofanya.
Wananchi wa Njombe kabla ya kampeni walikuwa wameandikisha kwa asilimia 8.9 toka Uhuru upatikane lakini baada ya kuanza kwa kampeni  katika kipindi cha miezi mitatu wamefikia asilimia 99.
Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman akisalimia wakazi wa wilaya ya Tandahimba (hawapo pichani) wakati wa zoezi la utambulisho kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Kampeni ya kuandikisha vyeti watoto chini ya miaka mitano imelenga kuondoa kero za uandikishaji na kuweka sawa mfumo wa uandikishaji wa vizazi na vifo hivyo kusaidia mipango ya serikali kwa kuwa na takwimu halisi na hivyo kupanga maendeleo halisi.
Mpango huo uliozinduliwa jana unafikisha huduma ya usajili karibu na wananchi kwa kuanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya ambavyo pia ndio vinavyosaidia  elimu ya afya ya uzazi, kiliniki na uzazi.
Pia vituo hivyo vya usajili vitakuwepo katika ofisi za kata, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya taifa ya ugatuaji madaraka.
Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga

Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga

September 26, 2017
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.

Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo. 
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikata utepe wakati wa kukaabidhi gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
 
Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya. 

Awali wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa uangalifu wa hali juu huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika kusaidia wananchi wake. 

“Nimesikia kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine ya X-Ray na na vifaa vingine muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na tunawaomba muwe na imani na Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya jambo hilo. Hospitali ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa vifaa ikiwemo mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali katika tukio hilo.
 MIPANGO YA TIMU ZA TAIFA ZA VIJANA

MIPANGO YA TIMU ZA TAIFA ZA VIJANA

September 26, 2017

Kocha Mkuu wa timu za vijana Tanzania, Kim Paulsen, amevutiwa na uwezo wa vijana wanaoibuka kila mwaka katika soka nchini na kusema tuna hazina ya wachezaji wenye uwezo wa kucheza mahala popote duniani.
Poulsen amewaambia waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 26, 2017 jijini Dar es Salaam kwamba wamefanikiwa kuona uwezo wa vijana kwa wakati wote, lakini umahiri umekuwa ukiongezeka kwa kila timu mpya inapoitwa.

Kwa takribani mwezi mmoja, Kocha Poulsen akishirikiana na Oscar Mirambo walikuwa kwenye programu ya kuinoa Serengeti Boys mpya.

“Hii Serengeti mpya inayokuja, nayo ni bora kama ilivyo kwa wale waliopita. Bado naona kuna vipaji vikubwa sana. Ni kulea tu hawa vijana kazi ambayo tutaendelea nayo.”

Poulsen - Raia wa Denmark amesema kambi ya vijana 57 walioripoti na kufundishwa na makocha hao, wameonesha uwezo mkubwa, lakini kiufundi wamepunguza hadi hadi kubaki 27.

Amesema hao waliobaki watapangiwa kambi nyingine itakayoanza Novemba 19, 2017 na itafikia mwisho Desemba 19, mwaka huu  baada ya kuivunja kambi ya muda jana Septemba 25, mwaka huu.

Katika programu ya kambi hiyo mpya ya Novemba na Desemba, Kocha Kim ametaka angalau mechi moja ya kirafiki ya kimataifa huku akisisitiza apate timu ya nchi iliyowekeza hasa katika soka la vijana: “Ikiwezekana hata mbili.”

Akizungumzia kuhusu ujio mpya wa timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 - Ngorongoro Heroes, Kocha Kim amesema itaitwa kambini wakati wowote kuanzia Oktoba mwanzoni kwa kambi ya wiki tatu.

“Timu ya Serengeti Boys iliyopita ilifanya vizuri sana. Ni matarajio yetu hata hii itafanya vizuri, lakini hapa nataka nizungumzie ile iliyoshiriki fainali za AFCON u17 nchini Gabon…

“…kwa hiyo kambi itakayoitwa ya Ngorongoro Heroes, tutaita wale wote waliounda Serengeti Boys iliyopita. Hata wale ambao hawakubahatika kwenda Gabon tutawajumuisha kwa ajili ya kambi ya wiki tatu mwezi Oktoba,” amesema Poulsen.

Amesema kwamba sababu za kuita nyota wale wa Serengeti Boys katika Ngorongoro Heroes ni kuwapa nafasi ya kwanza wao kuonekana kama wangali na uwezo wa kupambana kama ilivyokuwa zamani na kwa wale wenye uwezo tu, ndio watakaochukuliwa,” amesisitiza.