RAIS SAMIA AZUNGUMZA KATIKA JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA NORWAY JIJINI OSLO

February 13, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia jambo katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Viongozi, Wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.

TBS YAFANYA UKAGUZI NA KUTOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA KUOKWA KANDA YA KASKAZINI

February 13, 2024


Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kaskazini limefanya ukaguzi na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa bidhaa za kuokwa (mikate, mandazi, nk) mkoani Arusha ili kuhakikiza wanazalisha bidhaa hizo kwa kufuata taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika ukaguzi huo na utoaji elimu mkoani hapa, Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara, Joseph Mwaipaja, alisema ukaguzi na elimu hiyo ilitolewa kwa wananchi na wajasiriamali wanaozalisha bidhaa hizo ili bidhaa zao zinapoingia sokoni ziwe zinakidhi matakwa ya viwango.

"Tulianza kwa kutoa elimu kwa kuwaelezea njia sahihi za kuzalisha bidhaa za kuokwa ili wajue kwamba sio halali kwao kuendeleza kuuza bidhaa ambazo hazijakidhi matakwa ya ubora," alisema Mwaipaja.

Alifafanua kwamba ukaguzi huo unaenda mbali zaidi hadi kwenye maduka wanakouza bidhaa hizo kwa sababu kwa mamlaka waliyopewa na sheria, TBS inasajili maghala, maduka na supermakert, hivyo wahusika wanatakiwa kuruhusu kuingia bidhaa ambazo zimethibitishwa na shirika hilo.

Kwa mujibu wa Mwaipaja endapo watabaini bidhaa za kuokwa ambazo hazijakidhi matakwa ubora wataziondoa na kuziharibu kwa gharama za hao wafanyabiashara wanaoendelea kuzalisha bidhaa ambazo hazina ubora.

Aliwahimiza wazalishaji hao kuthibitisha ubora wa bidhaa zao, kwani kufanya hivyo kuna faida nyingi.

Alitaja baadhi ya faida hizo, akisema kwanza Arusha ni mkoa wa wa kitalii hivyo wanataka hata bidhaa ambazo watalii na Watanzania kwa ujumla wanazitumia ziwe ni zile zilizothibitishwa ubora na TBS.

"Kwa hiyo wakithibitisha bidhaa zao wataweza kuuza kwenye supermakert, pili kuwafanya wanunuzi kujiamini kwamba bidhaa husika ni salama kwa afya ya mlaji baada ya kuwa zimethibitishwa na shirika letu," alisema Mwaipaja na kuongeza;

"Kwa kufanya hivyo wanaongeza wigo wa bidhaa zao kwa sababu zinakuwa zinatambulika."

Alitaja faida nyingine za kuuza bidhaa zenye ubora kuwa ni pamoja na kuwa na biashara ambazo ni endelevu, kwani taasisi za kifedha zinamuelewa mfanyabiashara mwenye biashara endelevu, hivyo inakuwa ni rahisi kwake kwenda kuomba mkopo ili kuweza kutanua biashara yake.

Kwa mujibu wa Mwaipaja ukaguzi wa bidhaa za kuokwa na utoaji kwa mikoa ya kanda ya kaskazini litakuwa endelevu na kwa miezi miwili iliyopita wamekuwa wakifanya ukaguzi wa bidhaa ambazo hazina ubora.

"Lakini kwa sasa hivi tumeanza na mikate kwa sababu kuna watu wanaona ni haki kwao kuuza bidhaa ambazo hazina nembo ya TBS.

Kwa hiyo kwa mikoa yote ya kanda ya kaskazini wajue kwamba TBS tupo kazini tutaenda kila mkoa na tukibaini hizo bidhaa tutaziharibu," alisema.

Alitoa wito kwa wazalishaji kufika TBS kuanza mchakato wa uthibitishaji ubora wa bidhaa.





WAGANGA WAFAWIDHI WATAKIWA KUTENGA BAJETI KUNUNUA MAFUTA YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.

February 13, 2024

 Na Janeth Raphael - MichuziTv DODOMA.


Waganga Wafawidhi wa vituo vya huduma za Afya msingi Nchini wametakiwa kutenga Bajeti ya ya fedha,katika kila mwaka wa fedha kwaajili ya kununua mafuta ya kuwasaidia watu wenye Ulemavu wa ngozi(Albino)

Maagizo hayo yametolewa Jijini Dodoma na Naibu waziri TAMISEMI anayeshughulikia mambo ya afya DKt Festo Ndugange katika Mkutano wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutokea huduma za Afya ngazi ya msingi uliofanyika Jijini hapa.

Na kuongeza katika miaka mitatu ni Halmashauri 47 tu zilizotenga Bajeti hiyo kwa huduma ya mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

"Ndugu zangu Waganga Wafawidhi utengaji wa Fedha ya mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi ni maelekezo ya Serikali na ni muhimu Sana, katika kipindi cha miaka mitatu ni Halmashauri 47 tu zilitenga fedha za mafuta kwa ajili ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (ualbino),kwahiyo niwaombe tuhakikishe kwenye vituo vyetu tunawatambua watu wenye Ulemavu wa ngozi".

" Ndugu Waganga Wafawidhi tengeni Bajeti kwaajili ya vifaa saidizi kwa watu wenye mahitaji maalum na mafuta kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi,pia kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya jinsi ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum".

Aidha Naibu Waziri amewataka Waganga Wafawidhi hao kujitathmini na kujiuliza maswali kama wanatatua changamoto zinazowakabili wanachi ipasavyo,kwa weledi na kwa wakati.

"Kuna Malalamiko ya wananchi wanakuja kulalamika kuwa kuna Watumishi wanatoa lugha ambazo sio mzuri ,au kasema hakuna dawa na dawa zinapatikana au alitakiwa kuwa kazini na hayupo hivyo Maswali ambayo tunapaswa kujiuliza ni Je tunatatua changamoto za wananchi ipasavyo,kwa weledi na kwa wakati. Hapa tupate majawabu na kuondoka na maazimio ya kwenda kuboresha mapungufu na Malalamiko yaliyopo".

Sambamba na hayo yote pia hakuacha kuwa kumbusha Waganga Wafawidhi katika suala la utunzaji wa vifaa Tiba ambavyo Serikali inanunua na kupeleka katika vituo vya Afya kwani Serikali inatumia mabilioni ya fedha.

"Wakati mwingine unakuta vifaa Tiba vimewekwa katika sehemu isiyo salama na yenye vumbi wakati vifaa hivyo ni vya mabilioni, na sisi Waganga Wafawidhi tumepewa dhamana hiyo ya kutunza vifaa hivyo kila Mmoja akasimamie suala la utunzaji wa vifaa".

Naibu Waziri amesisitiza pia kuwa Serikali haita sita kumchukulia hatua Kali au hata kumfutia leseni ya Kazi yeyote atakaye kiuka Maadili ya Kazi yake.

Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Waganga Wafawidhi, Dkt Florence Hilari Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya msingi Tanzania Bara ameahidi kuyatekeleza maagizo yote ikiwemo kutenga Bajeti kwaajili ya wenye mahitaji maalum, yaliyotolewa na Serikali kupitia Naibu Waziri.

"Kwa niaba ya Waganga Wafawidhi wenzangu tunakushuruku na tunakuahidi kuyatekeleza haya na kuyasimamia kwa weledi mkubwa kama ilivyo kauli mbiu yetu".

Hii ni moja Kati ya mikutano ya Waganga Wafawidhi ambayo hufanyika kwaajili ya kukumbushana na kujengeana uwezo ili kuleta ufanisi na tija katika Kazi.
 

Naibu Waziri TAMISEMI anayeshughulikia mambo ya Afya Dkt. Festo Dugange akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.
 

Dkt. Florence Hilari Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.
 

NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Dkt.Wilson Mahera, akizungumza na Waganga Wafawidhi wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati  wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
 

MGANGA Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


 

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange (hayupo pichani), akizungumza wakati  akifungua  Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi nchini unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi” unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

RAIS SAMIA AWASILI OSLO, NORWAY KWA AJILI YA ZIARA YA KITAIFA

February 13, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya mapokezi yake katika Kasri la Kifalme, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mfalme Harald V wa Norway pamoja na Malkia Sonja mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo kwa ajili ya ziara ya Kitaifa tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kukabidhiana zawadi katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Malkia Sonja mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme, Norway wakati wa ziara yake ya Kitaifa tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.

BILIONI 1.6 KULIPA KIFUTA JASHO/ MACHOZI

February 13, 2024

 Na Mwandishi wetu Bungeni-Dodoma


Wizara ya Maliasili na Utalii imekamilisha mchakato wa kufanya tathmini ya malipo ya kifuta jasho/ machozi ambapo kiasi cha shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Sita zinatakiwa kulipwa kupitia Wizara ya Fedha.

Haya yamebainika wakati Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula akijibu swali la Mhe. Dkt. David Mathayo David(Mb) aliyetaka kujua lini Serikali itafanya mapitio ya Sheria na Kanuni za fidia kwa waathirika wa wanyamapori ili kulipa fidia ya gharama halisi tofauti na sasa.

Aidha, Wizara imekamilisha mapitio ya Kanuni za Kifuta Jasho/Machozi na kuiwasilisha Wizara ya Fedha ili kuona uwezekano wa kuongeza viwango hivyo.

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa kwa sasa Wizara ya Fedha inafanya tathmini ili kuona athari za kiuchumi na uwezo wa nchi kutekeleza suala hilo.

"Wizara imekuwa ikilipa kifuta jasho/ machozi kama mkono wa pole au faraja kwa wananchi wanaopata madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu. Malipo hayo yamekuwa yakifanyika kwa mujibu wa Kanuni za Kifuta Jasho/Machozi za mwaka 2011 na kwa kadri ya upatikanaji wa fedha" alisema Mhe. Kitandula.

Pia, Mhe. Kitandula aliongeza kuwa wizara inafahamu kumekuwa na changamoto ya ucheleweshaji wa malipo hayo,  sababu kubwa ikiwa ni ulazima wa kufanyika kwa tathimini ya kina inayolazimu kwenda uwandani ili kuhakiki na kujiridhisha kiwango cha uharibifu au madhara yaliyojitokeza na fidia stahiki inayopaswa kutolewa.


BUNGE LASHAURI SERIKALI KUPELEKA FEDHA ZA KUTOSHA TARURA

February 13, 2024

 Na Mwandishi wetu Bungeni-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeishauri Serikali kuona umuhimu wa kuipelekea fedha za kutosha TARURA   kwa kadiri ya bajeti  ilivyoainishwa  ili iweze kukabiliana  na hali mbaya ya miundombinu  nchini.

Ushauri huo umetolewa Bungeni leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Mikumi Mheshimiwa Dennis Londo wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2023 hadi Januari, 2024

Amesema kamati haijaridhishwa na hali ya upelekaji wa fedha za bajeti kwa TARURA, ikizingatiwa kuwa katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini uliotokana  na mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu kubwa ya nchi.

“Ikumbukwe kuwa Serikali iliahidi ndani ya Bunge lako kuwa pamoja na bajeti ya Bilioni 808.02 Serikali ingetoa Bilioni 350 za ziada kwa TARURA. Kamati inasikitika kwamba, hata fedha hizi pia hazijapokelewa, hivyo tunaiomba Serikali iweze kutoa fedha kwa wakati ili kutatua changamoto za miundombinu nchini “ amesisitiza Mheshimiwa Londo.

Aidha, amesema Kamati imeiomba Serikali  kuhakikisha inaiongezea  bajeti TARURA  kufikia shilingi  trilioni 1.64 kutoka shilingi  bilioni 710 kwa miaka minne mfululizo ili kufikia malengo  ya asilimia 70 ya barabara  kuwa za changarawe, asilimia 3 kuwa  barabara za lami.

Pia, imeitaka  Serikali kuhakikisha inasimamia kwa umakini taratibu za manunuzi kulingana na uwezo wa wakandarasi wanaoomba kazi na utekelezaji wa miradi husika.

Vilevile, wameielekeza Serikali kutekeleza mchakato wa kuanzisha Hati Fungani (TARURA SAMIA INFRASTRUCTURE BOND) kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara pamoja na kutafuta vyanzo vya fedha mbadala ikiwemo kushirikisha sekta binafsi ili kuiwezesha TARURA kuwa na fedha za uhakika za kutekeleza miradi ya barabara.


WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUFANYA UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO MARA KWA MARA

February 13, 2024

 


Na Oscar Assenga, TANGA.

DAKTARI Mwandamizi wa Magonjwa ya Kinywa na Meno katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Dkt Onesmo Ezekiel amewashauri wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa kinywa na meno mara bili kwa mwaka ili kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kukutana nayo ikiwemo ya kung’oa jino

Dkt Onesmo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Kinywa na Meno Katika Hospitali hiyo aliyasema hayo leo wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema uchunguzi huo wanaweza kufanya bila hata kuumwa kwa sababu magonjwa ya kinywa na meno katika hatua za awali hayana dalili zozote.

Alisema ila dalili zinaanza kujitokeza wakati ugonjwa unakuwa tayari upo kwenye hatua za mbele zaidi hivyo unapokwenda daktari ukiwa na maumivu na kukuangalia kama kuna uwezekano wa kuzuia magonjwa ya kinywa na meno unakuta tayari umeshaathiri eneo kubwa na hivyo kuwa na uchaguzi mmoja wa kung’oa jino.

“Lakini niwaambie kwamba dalili za meno ukiziwahi kwenye hatua za awali inakuwa rahisi kufanya matibabu na gharama zake zinakuwa ni rahisi vyenginevyo utakwenda kwa daktari ukiwa na maumivu makubwa zaidi na hivyo kuwa na uchaguzi wa kungo’a jino”Alisema

Hata hivyo Dkt Onesmo alisema kwamba magonjwa hayo yanaathiri watoto na watu wazima hivyo kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanazingatia suala la usafi wa kinywa na meno vizuri wasimamiwe watumie dawa ya mswaki yenye madini ya floride,calcium na karafuu .

“Lakini mswaki wanaoutumia usizidi zaidi ya miezi mitatu kwa sababu baada ya miezi hiyo unashindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi huku asisisitiza umuhimu wa jamii kuhakikisha wanatunza vinywa vyao kwa kuzingatia kufanya usafi mara kwa mara”Alisema

Akizungumza kuhusu kitengo cha huduma ya Afya ya Kinywa na Meno katika Hospitali hiyo Dkt Onesmo alisema wanatoa huduma zinazohusiana na magonjwa ya kinywa na meno kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu mpaka saa tisa na nusu mchana.

“Pia wakati mwengine tunatoa huduma siku za wikiendi linapokuwa limejitokeza suala la uhitaji na kitengo chetu kina vitengo kadhaa ndani yake ambapo tunatoa huduma za meno bandia,kuziba meno,kusafisha meno,kufanya matibabu ya mzizi wa jino na kungarisha jino “Alisema

Alisema pia wakati mwengine wanalazimika kwenda chumba cha upasuaji inatpokea kuna mahitaji mfano wanapotokea wagonjwa wenye uvimbe ambao unahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa au wagonjwa wa ajali ambao matibabu yao ili kuweza kuwatibu wanapaswa kwenda chumba cha upasuaji.

“Tunafanya upasuaji mdogo ambao hauhitaji mgonjwa kulazwa bali isipokuwa ikiwekewa ganzi katika eneo husika anaweza kufanyiwa huduma hizo na kuruhusiwa“Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba hospitali hiyo inapokea inapokea wagonjwa kutoka wilaya zote za mkoa huo na wanapata matibabu hapo na wachache wanalazimika kuwapa rufaa kwendfa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumzia magonjwa yanayowatesa wananchi wengi,Dkt Onesmo alisema magonjwa hayo ni kutoboka kwa meno ambao zaidi ya nusu ya wagonjwa ni tatizo kubwa na wengine ni fizi kutoka damu na yamekuwa yakiathiri watu wa umri zote.

“Kuanzia vijana,watoto hadi wazee wa jinsia zote wanakaribiana huku kundi jingine ni wale wanaopata ajali za kuvunjika taya la chini na la juu au yote mawili pamoja au kung’oka meno kwa ajili ya ajali ambazo zinahusisha bodaboda ambao wamekuwa wamelewa”Alisema

TUTAFUTE FEDHA ZAIDI KATIKA MAJI-MHANDISI MWAJUMA

February 13, 2024

 NAIBU  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wadau wa Sekta Mtambuka kuongeza nguvu zaidi katika kupata fedha na kushirikiana na Serikali katika kufanikisha masuala anuai yahusuyo huduma ya maji kwa Watanzania.


Amesema hayo wakati akifunga Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji Jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza umuhimu wa kuongeza wadau wa Jukwaa ili kuyafikia makundi mengi katika jamii pia kuongeza nguvu ya ushirikishwaji.

Ameongeza  ni muhimu kuwa nabmipango inayotekelezeka ya kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubalika na jamii.

Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam likiwa limebeba kaulimbiu  isemayo; Majanga ya Mafuriko na Ukame:  Uwekezaji katika Usalama wa Maji ni Jambo la Haraka.

Mhandisi Mwajuma ni mmoja kati ya vinara wanawake katika masuala ya uhandisi na huduma kwa jamii hapa nchini.


ASILIMIA 10 YA WANAOTOA MIMBA KWA NJIA ZISIZO SALAMA HUFARIKI

February 13, 2024

 Naibu Waziri wa afya DKT Godwin Mollel amesema kuwa jumla ya asilimia 10 ya wanawake wanaotoa mimba wanafariki kwa utoaji mimba usio salama.


Akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Conjesta  Rwamlaza lililohoji kuhusu vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama vina ukubwa na madhara gani naibu waziri alisema kuwa tafiti zilizofanywa matatizo yatokanayo na utoaji wa mimba ni moja ya sababu inayochangia vifo vitakokanavyo na uzazi kwa asilimia 10.

Pia alihoji serikali imejipangaje kupunguza vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama?

“Serikali mlisaini Mkataba wa Maputo ‘Maputo Protocol’ kutetea haki za wanawake na uzazi salama, makubalino hayo yalilenga mimba zitolewe zile za kubakwa, shambulio la ngono, mimba maharimu, serikali haioni umuhimu wa kuweka makubaliano hayo katika sheria za nchi yetu ili kuwasaidia wamama wanaopata mimba za namna hii waweze kuzitoa kwa usalama bila kuhatarisha maisha yao? alihoji Conjesta.

Amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na uambukizo mkali wa mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi maisha.


MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA LOWASA KARIMJEE, WAKO PIA VIONGOZI WA DINI

February 13, 2024

 MAMIA ya watu wamejitokeza katika Viwanja vya Karimejee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, huku zoezi hilo likitarajiwa kuongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango.


Leo Jumanne, Februari 12, 2024, mwili wa Lowassa unatarajiwa kuagwa katika Viwanja hivyo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mawaziri wengine wamehudhuria.

Mbali na mawaziri wa Tanzania Bara, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman na mawaziri kadhaa wa visiwa hivyo, wamehudhuria kwa ajili ya kushiriki hafla hiyo ya mwisho kwa Lowasa.

Viongozi wengine wa vyama vya siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na viongozi wa dini, wamehudhuria shughuli hiyo.

Jeneza lililobeba mwili wa Lowassa huku likiwa limefunikwa na bendera ya Tanzania, limeingia uwanjani hapo majira ya 10.20.

Shughuli hiyo inatanguliwa na ibada fupi inayoongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Azania Front.

Lowassa anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Monduli jijini Arusha, Jumamosi ya Februari 17 mwaka huu.


VIONGOZI WA UWT TAIFA MSIBANI KWA LOWASSA-KARIMJEE DAR ES SALAAM.

VIONGOZI WA UWT TAIFA MSIBANI KWA LOWASSA-KARIMJEE DAR ES SALAAM.

February 13, 2024




Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda wamewasili katika Viwanja vya Karimjee,Posta Jijini Dar es Salaam tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndg. Zainab Khamis Shomari,Katibu Mkuu Ndg. Jokate Urban Mwegelo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa Ndg. Hawa Ghasia.